KINGWENDU AWAPA NENO WANAOMZUSHIA KIFO
Muigizaji maarufu wa vichekesho Bongo, Rashidi Mwinshehe ‘Kingwendu’ ameyatolea ufafanuzi madai ya kuwa ni mgonjwa wa kufa wakati wowote huku wengine wakizusha kuwa amekufa.
Akizungumza na Showbiz, Kingwendu alisema yeye si mgonjwa kama watu wanavyomzushia kwani anaendelea vizuri na sanaa yake hasa ya muziki kwa sababu amekuwa akipiga shoo zake kama kawaida mikoani.
“Unajua watu wanaonizushia habari za ugonjwa, mara oo… nimekufa ni wale ambao hawajaniona muda mrefu kwani nafanya kazi zangu binafsi na shoo mbalimbali za muziki huko mikoani, ingawa mimi sishtuki kwani wananitabiria umri mrefu,” alisema Kingwendu.
Kingwendu alisema kuwa, ana miaka mingi hajaugua hata malaria na mpaka sasa anapiga shoo mkoani Mwanza katika kuufunga mwaka wa 2018.
CHANZO: SHOWBIZ - GLOBAL PUBLISHERS
Comments
Post a Comment