YANGA YAMPA ULAJI MSHAMBULIAJI HUYU, ATUA CHINA KIBABE


MSHAMBULIAJI wa Stand United, Alex Kitenge raia wa Burundi ambaye alijizolea umaarufu baada ya kuwafunga Yanga mabao matatu 'hat trick' na kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kumtungua mabao hayo kipa namba mbili Klaus Kindoki amepata dili nchini China.

Kitenge ambaye amesema kwamba kwa sasa hana hesabu za kurejea bongo kuichezea Stand United mpaka watakapomkamilishia malipo yake, kwa sasa amepata fursa nchini China.

"Nimepata timu nchini China, inaitwa Maccau Club ambayo nitakuwa huko kwa muda wa mwezi mmoja kwa majaribio nikitafuta nafasi ya kusajiliwa moja kwa moja.

"Kuna wakala aliniona kupitia kanda ya video ambapo alinifuata na kunitafutia timu huko, hivyo nitafanya jitihada kupata nafasi ya kusajiliwa jumlajumla," alisema.

Kwa hatua hiyo ni kama amepata ulaji kupitia timu ya Yanga kwa kuwa ni mchezo mmoja tu alionyesh uwezo wake na baada ya hapo hajafanikiwa kufunga hata bao moja katika michezo yake mingine Ligi Kuu Bara.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA