YANGA YATUA DAR, ZAHERA ATOA MAAGIZO KWA WACHEZAJI WAKE


Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Dar es Salaam kikitokea Mwaza ambako kilicheza mchezo wa robo fainali wa kombe la Azam Sports Federation Cup na kushinda kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Baada ya kurejea Kocha mkuu Mwinyi Zahera amewapa mapumziko wachezaji wake kwa leo na kesho asubuhi wataendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi kurasini.

Mazoezi hayi yataanza  kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC April 04 katika dimba la Nagwanda Sijaona Mtwara.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho jana na sasa itacheza dhidi ya Lipuli Fc kwenye mchezo ujao utakaopigwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA