TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JUMAMOSI HOTELI YA WHITE SANDS MAANDALIZI YA AFCON
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaingia kambini Juni 1 katika hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam kujiandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baadaye mwezi huu nchini Misri.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwamba hoteli ya White Sands imejitolea kuisaidia Taifa Stars kambi ya awali ya wiki moja kwa maandalizi ya AFCON.
Karia amesema kwamba Taifa Stars itaingia kambini White Sands Juni 1 hadi 7 kwa maandalizi ya awali ya AFCON kabla ya kikosi kwenda Alexandria.
Amesema kikosi kitaondoka na wachezaji 32 baada ya kuchujwa saba kutoka 39 walioitwa na kati ya hao ni 23 tu watashiriki AFCON.
Karia amesema wachezaji wengine wataendelea kubaki kambini kwa maandalizi ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Kikosi cha kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kitaanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wa AFCON, Misri Juni 13, mwaka huu Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Baada ya hapo Taifa Stars itacheza mechi zake tatu za Kundi C mfululizo ikianza na Senegal Juni 23, Kenya Juni 27 na kumaliza na Algeria Julai 1 kuangalia matokeo yake kama yataipeleka hatua ya mtoano.
Kikosi kitakachoingia kambini Jumamosi kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC), Suleiman Salula (Malindi SC) na Aaron Lulambo (Tanzania Prisons).
Mabeki; Claryo Boniface (U20), Hassan Kessu (Nkana FC, Zambia), Vincent Philipo (Mbao FC), Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni (Simba SC), Kelvin Yondan, Gardiel Michael (Yanga SC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Ally Mtoni (Lipuli FC), David Mwantika, Aggrey Morris (Azam FC), Ally Ally (KMC) na Kennedy Wilson (Singida United).
Viungo ni Feisal Salum, Ibrahim Ajibu (Yanga SC), Himid Mao (Petrojet, Misri), Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Shiza Kichuya (ENNPI, Misri), Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi Morocco), Farid Mussa (Tenerife, Hispania) na Freddy Tangalu (Lipuli FC).
Washambuliaji ni Yahya Zayd (Ismailia, Misri), Shaaban Iddi Chilunda (Tenerife, Hispania), Rashid Mandawa (BDF, Botswana), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Khamis (Kagera Sugar), Miraj Athumani (Lipuli FC), Kelvin John (Serengeti Boys), Adi Yussuf (Solihull Moors, England), John Bocco (Simba SC), Thomas Ulimwengu (JS Saoura, ALgeria) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).
Mbali na Taifa Stars kupangwa Kundi C AFCON 2019 pamoja na jirani zao, Kenya, Algeria na Senegal – wenyeji, Misri wapo Kundi A pamoja na na Zimbabwe, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kundi B linaundwa na Burundi, Madagascar, Guinea na Nigeria, Kundi D linaundwa na Namibia, Afrika Kusini, Ivory Coast na Morocco, wakati Kundi E kuna Angola, Mauritania, Mali na Tunisia na Kundi F ni Guinea Bessau, Benin, Ghana na mabingwa watetezi, Cameroon.
Taifa Stars imefuzu AFCON ya mwaka huu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi L kwa pointi zake nane, nyuma ya jirani zao wa Afrika Mashariki, Uganda walioongoza kwa pointi zao 13 wakizipiku Lesotho iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.
Mwaka huu, Tanzania itashiriki AFCON kwa mara ya pili tu kihistoria baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria ambako ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji, Nigeria, Misri na Ivory Coast na kushika mkia.
Mwaka 1980 ilifungwa mechi mbili, 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast na kuishia Raundi ya kwanza tu, wakati timu nane tu zinashiriki michuano hiyo.
Michuano itaanza Juni 21 hadi Julai 19 na Taifa Stars itachezea mechi zake Uwanja wa Juni 30 na Al Salam mjini Cairo.
Na katika CHAN, Taifa Stars itaanzia nyumbani dhidi ya Sudan Julai 26 kabla ya kurudiana Agosti 2 na ikifuzu mtihani huo itamenyana na mshindi kati ya Kenya na Burundi.

Comments
Post a Comment