TAIFA STARS YAJIWEKA PAGUMU KUFUZU CHAN 2020 BAADA YA SARE YA 0-0 NYUMBANI NA KENYA
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Tanzania, Ettiene Ndayiragije amesema ataenda kufanyia kazi mapungufu yaliyojitojeza na kwenda kusaka ushindi katika michezo wa marudiano nchini Kenya.
Tanzania imeshindwa kupata matokeo katika mchezo wa leo dhidi ya Kenya kwa kutoa sare ya bila kufungana katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya CHAN kati ya Taifa umekamilika uwanja wa Taifa kwa sare ya bila kufungana.
Alisema ameona mapungufu ya kikosi chake na kufanyia kazi kwa lengo la vijana wake kupambana katika mchezo wa marudiano
Kipindi cha kwanza kwa timu zote mbili hakuna hata timu moja iliyopiga shuti lililolenga lango kwa mpinzani.
Dakika ya tatu beki wa Tanzania, Gardiel Michael alipiga krosi na mpira kutoka nje.
Dakika ya 34 Nahodha John Raphael Bocco alipiga shuti mpira ukatoka pembeni ya lango baada ya kupokea pasi kwa Ayubu lyanga
Kelvin John aliyeingia dakika 67 kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga alifanya kazi nzuri na Idd Seleman nusura aipatie Tanzania bao dakika ya 76 alipiga shuti na kipa wa Kenya kuzuia.
Sasa Stars italazimika kushinda ugenini kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Kenya Agosti 4.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Paul Godfrey, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Jonas Mkude, Hassan Dilunga/Kelvin John dk67, Salum Abubakar, John Bocco/Salim Aiyee dk85, Ayubu Lyanga/Ibrahim Ajibu dk54. na Idd Seleman.

Comments
Post a Comment