Posts
Showing posts from December, 2019
SIMBA SC ‘YAWATISHA WATANI’, YAWACHAPA NDANDA FC 2-0 WAFUNGAJI KAHATA NA DEO KANDA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Ndanda FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Simba SC iliyo chini ya kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck anayesaidiwa na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, inafikisha pointi 34 katika mchezo wa 13, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 10 zaidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi. Katika mchezo wa leo ambao Simba SC ilimuacha benchi kwa muda wote kinara wake wa mabao, Mnyarwanda, Meddie Kagere – ilipata bao moja kila kipindi na yote yakifungwa na wachezaji wake wa kigeni. Aliyefungua shangwe za mabao leo Uwanja wa Taifa alikuwa ni kiungo wa kimataifa wa Kenya, Francis Kahata Nyambura aliyemtungua kipa wa zamani wa Simba SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ kwa kufunga bao la kwanza kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 13. Kiungo anayecheza kwa mkopo kutoka klabu ya TP
YANGA SC YAJISOGEZA NYUMA KABISA YA SIMBA SC LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM YANGA SC imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United ya Musoma mkoani Mara jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Shukrani kwa bao pekee la mshambuliaji mpya, Tariq Seif Kiakala dakika ya 84 akimalizia pasi ya Nahodha na kungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi kuiadhibu timu yake ya zamani. Na kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na gwiji wake, Charles Boniface Mkwasa inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 11 na kupanda hadi nafasi ya pili, ikiizidi wastani wa mabao tu Kagera Sugar na sasa inazidiwa pointi saba na mabingwa watetezi, Simba SC. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Coastal Union imeshinda 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Lipuli FC imeichapa Mbao FC 3-0 Uwanja wa Samora Iringa, Ruvu Shooting imeichapa Kagera Sugar 2-1 na Alliance FC wameshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa C
MSHAMBULAJI YIKPE GILSLAIN GNAMIEN KUTOKA IVORY COAST ASAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA YANGA SC
- Get link
- X
- Other Apps
DE BRUYNE ASETI MOJA, AFUNGA MOJA MAN CITY YAICHAPA SHEFFIELD 2-0 ETIHAD
- Get link
- X
- Other Apps
CHELSEA YAIKANYAGA ARSENAL 2-1 PALE PALE EMIRATES
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji Tammy Abraham akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la ushindi dakika ya 87 ikiwalaza wenyeji, Arsenal 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates, London. Arsenal ilitangulia kwa bao la Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 13, kabla ya Jorginho kuisawazishia Arsenal dakika ya 83 PICHA ZADI GONGA HAPA
MANE AFUNGA BAO PEKEE LIVERPOOL YAILAZA WOLVES 1-0 ANFIELD
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji Msenegal, Sadio Mane akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Liverpool dakika ya 49 ikiwalaza Wolverhampton Wanderers 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield. Ushindi huo unaifanya Liverpool ifikishe pointi 55 katika mchezo wa 19 na kuendelea kuongoza EPL kwa pointi 13 zaidi ya Leicester City na 17 zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TATIZO LA KMC NI KUJIKUNA KWENYE UNYAYO BADALA YA KICHWANI
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM IKIWA ni siku ya Jumatatu tulivu kabisa majira ya saa nne kamili za usiku nikiwa nipo katika moja ya Usafiri wa jumuiya nikiwa natoka kwenye mihangaiko yangu ya kila siku. Ilikuwa ni siku ambayo macho yangu yalihisi uzito saana na ilitokana na lepe kubwaa la usingizi kuniandama kichwani mwangu hata likapelekea macho kujihisi uzito usio kifani. Sikujua mda gani hasa usingizi ulinipitia lakini ninacho kumbuka ni kuwa wakati usingizi una nipitia nilikuwa nimeweka Headphone masikioni nikiwa nasikiliza moja ya kipindi cha michezo. Nikiwa katika usingizi huo mzito huku mwili mzima ukiwa umepumzika lakini Ubongo haukuacha kufanya kazi yake. Nikiwa katika hali hiyo ghafla ilinijia taswira ya Klabu ilijizolea umaarufu kwa mda mchache saana hapa nchini.hata ikawafanya watanzania waone ni kawaida kulitaja jina la Klabu hiyo kila lilipowajia. Ndani ya msimu mmoja tu ilitosha kuwafanya watoto hawa wa kinondoni kufikia lengo la kuandikwa kwenye ripoti za makam
NCHIMBI ANA HAMU NA KAZI, LAKINI YANGA ISHAWEKA MAMBO SAWA ACHEZE KESHO DHIDI YA BIASHARA?
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Ditram Nchimbi akiwa hoi baada ya mazoezi magumu gym mjini Dar es Salaam jana. Bado haifahamiki kama Ditram Nchimbi aliyesajiliwa kutoka Azam FC mwezi huu baada ya kufanya vizuri akicheza kwa mkopo Polisi Tanzania kama ataanza kucheza kesho, Yanga ikimenyana na Biashara United ya Musoma mkoani Mara kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
CHIRWA AING'ARISHA AZAM FC, YAICHAPA 1-0 POLISI TANZANIA LEO MOSHI, NAMUNGO NAYO YAIPIGA JKT
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji Mzambia wa Azam FC, Obrey Chirwa akishangilia baada ya kuifungia timu hiyo bao pekee dakika ya tisa ikiwalaza wenyeji, Polisi Tanzania 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Namungo FC wameshinda 1-0 ugenini dhidi ya JKT Tanzania bao pekee la Bgirimana Blaise dakika ya 90
MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA SAID MSHAMU, MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA MAJI MAJI
- Get link
- X
- Other Apps
DAVIS AMUANGUSHA MARA TATU GAMBOA NA KUMPIGA KWA TKO
- Get link
- X
- Other Apps
Bondia Mmarekani, Gervonta 'Tank' Davis (kushoto) akirejea kwenye kona yake baada ya kumuangusha Yuriorkis Gamboa (kulia) kwa mara ya tatu katika raundi ya 12 kabla ya refa Jack Reiss kumpa ushindi wa Technical Knockout (TKO) na kutwaa taji la WBA uzito wa Light Alfajiri ya leo ukumbi wa State Farm Arena Jijini Atlanta, Marekani PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MAN UNITED YAPANDA NAFASI YA TATU ENGLAND BAADA YA KUIPIGA BURNLEY 2-0
- Get link
- X
- Other Apps
Wachezaji wa Manchester United wakipongezana kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Burnley, mabao ya Anthony Martial dakika ya 44 na Marcus Rashford dakika ya 90 na ushei jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Turf Moor. United inapanda nafasi ya tano baada ya ushindi huo katika mchezo wa 20, ikifikisha pointi 31, ikizidiwa pointi moja na Chelsea na saba na Manchester City ambazo hata hivyo zina mechi moja moja mkononi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KIKOSI CHA SIGARA 1991 MWANGATA NA NYALUSI YEYOTE ANADAKA
- Get link
- X
- Other Apps
WACHEZAJI wa kikosi cha Sigara FC kabla ya moja ya mechi zake mwaka 1991 kutoka kulia waliosimama; Patrick Mwangata, Idd Nassoro ‘Cheche’, Michael Burton, Ladislaus Shawa (sasa marehemu), Abdallah Msamba (sasa marehemu), Shaaban Ramadhan, Ramadhan Kessy, Mahmoud Nyalusi na Muscat Subeiya. Kutoka kulia waliosimama ni Nahodha Mustapha Hoza, Abunu Issa, Abubakar Kombo, Peter Lucas, Hija Jamal (sasa marehemu), Iddi Msigala na Aziz Nyoni Njalambaya.
SIMBA SC YAZIDI ‘KUPOTELEA MBALI’ KILELENI LIGI KUU BARA BAADA YA KUIPIGA KMC 2-0 LEO
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA watetezi, Simba SC wameendelea kuwapa raha mashabiki wao baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Ushindi huo wa tatu mfululizo chini ya kocha mpya, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck unaifanya Simba SC ifikishe pointi 31 katika mchezo wa 12, ikiwazidi pointi saba sasa Kagera Sugar wanaofuatia nafasi ya pili ambao pia wamecheza mechi moja zaidi, wakati mahasimu wao wa jadi, Yanga SC ni wa tatu kwa pointi zao 21 za mechi 10. Katika mchezo huo uliochezeshwa na Mbaraka Rashid aliyesaidiwa na washika vibendera Hamisi Chang’walu na Shaffi Mohammed wote wa Dar es Salaam Simba SC ilipata mabao yake yote kipindi cha pili na kwa mara nyingine tena wafungaji wote wageni. Alianza Deogratius Kanda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwainua vitini mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kwa bao zuri dakika ya 46 akimalizia kazi nzuri ya kiungo mwenzake, Hass
EDERSON ALIMWA NYEKUNDU MAPEMA, MAN CITY YACHAPWA 3-2 NA WOLVES
- Get link
- X
- Other Apps
Refa Martin Atkinson akimuonyesha kadi nyekundu kipa wa Manchester City, Ederson dakika ya 12 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Wolverhampton jana Uwanja wa Molineux. Wolves ilishinda 3-2, mabao yake yakifungwa na Adama Traore dakika ya 55, Raul Jimenez dakika ya 82 na Matt Doherty dakika ya 89, baada ta Man City kutangulia kwa mabao ya Raheem Sterling dakika ya 25 na 50 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
YANGA SC YASOGEA ‘ANGA ZAKE’ LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0 SAMORA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, IRINGA YANGA SC imepanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya jioni ya leo Uwanja wa Samora mjini Iringa. Ushindi huo, unawafanya mabingwa hao mara nyingi zaidi wa Ligi Kuu kufikisha pointi 21 katika mchezo wa 10 – na sasa wanazidiwa pointi tatu na Kagera Sugar inayoshika nafasi ya pili, japo imecheza mechi tatu zaidi, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wanaongoza kwa pointi zake 28 za mechi 11. Bao pekee la Yanga SC leo limefungwa na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana dakika ya tano tu akimalizia mpira wa kurushwa na kiungo Mzanzibari, Abdulaziz ‘Bui’ Makame kutoka upande wa kulia. Sifa zimuendee kipa wa Tanzania Prisons, Jeremiah Kisubi kwa kuokoa michomo kadhaa ya hatari kuizuia Yanga SC kupata mabao zaidi. Hata kipa wa Yanga, Metacha Boniphace Mnata naye alizuia majaribio mawili ya hatari mno ya Tanzania Prisons kipindi cha pili. Wachezaji wawili wa Yanga,
MSENGI WA KMC ASAINI MIAKA MITATU KUJIUNGA NA STELLENBOSCH YA LIGI KUU AFRIKA KUSINI
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIUNGO mkabaji chipupizi wa Tanzania, Ally Msengi amesajiliwa na klabu ya Stellenbosch ya Ligi Kuu Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Kinondoni Municipal Council (KMC) ya Dar es Salaam. Mratibu wa kampuni ya Siyavuma Sports Group, Michael Mwebe ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Msengi alizivutia klabu kadhaa za Afrika Kusini kabla ya kuamua kumwaga wino Stellenbosch baada ya kocha wa klabu hio kuonesha imani kubwa ya kumpa nafasi katika kikosi chake. Msengi ambaye amezichezea timu zote za vijana za taifa kuanzia U17 na 20 anatarajiwa kuanza rasmi maisha mapya Katika Ligi Kuu Afrika Kusini Jumapili ya keshokutwa. Kiungo Ally Msengi amesajiliwa na Stellenbosch ya Ligi Kuu Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu “Msengi anaanza ukurasa mpya baada ya kufanya vizuri akiwa na klabu ya KMC aliyoichezea kwa takriban msimu mmoja na nusu. Tunaushukuru uongozi wa KMC kwa ushirikiano mkubwa tangu alipotua hapo na pia kumpa ba
LIVERPOOL 'MOTO FIRE' YAILIPUA LEICESTER CITY 4-0 PALE PALE KING POWER
- Get link
- X
- Other Apps
Beki wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold akishangilia kibabe mbele ya mashabiki wao baada ya kufunga bao la nne dakika ya 78 akimalizia pasi ya Sadio Mane katika ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa King Power, Leicester, Leicestershire. Mabao mengne ya Liverpool yalfungwa na Roberto Firmino dakika ya 31 na 74 mara zote akimalizia pasi Alexander-Arnold, wakati bao la pili lilifungwa na James Milner kwa penalti dakika ya 71 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
ARSENAL YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA AFC BOURNEMOUTH
- Get link
- X
- Other Apps
Kiungo Mjerumani, Mesut Ozil akimtoka Mcolombia, Jefferson Lerma kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Vitality mjini AFC Bournemouth. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1, Dan Gosling akianza kuwafungia wenyeji, Bournemouth dakika ya 35 kabla ya Pierre-Emerick Aubameyang kuisawazishia Arsenal dakika ya 63 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
CHELSEA WAPIGWA 2-0 NA SOUTHAMPTON PALE PALE DARAJANI
- Get link
- X
- Other Apps
MARTIAL APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA NEWCASTLE 4-1
- Get link
- X
- Other Apps
Anthony Martial akishangilia baada ya kuifunga mabao mawili Manchester United dakika za 24 na 51 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford. Mabao mengine ya Man United yamefungwa na Mason Greenwood dakika ya 36 na Marcus Rashford dakika ya 41, wakati bao pekee la Newcastle United limefungwa na Matty Longstaff dakika ya 17 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
COASTAL UNION YAINYAMAZISHA AZAM FC, YAICHAPA 1-0 MKWAKWANI BAO PEKEE LA HAJI UGANDO
- Get link
- X
- Other Apps
MECHI YA YANGA NA TANZANIA PRISONS YAHAMISHIWA UWANJA WA SAMORA MJINI IRINGA KESHO
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Tanzania Prisons na Yanga SC ya Dar es Salaam uliokuwa ufanyike Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya sasa utafanyika kesho Uwanja wa Samora mjini Iringa. Hiyo ni baada ya Uwanja wa Sokoine kuharibika katika eneo la kuchezea kufuatia tamasha la muziki lililofanyika usiku wa kuamkia leo, hivyo Bodi ya Ligi kuamua kuuzuia uwanja huo kutumika kwa mechi zote za Ligi zinazotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Yanga SC ipo mjini Mbeya tangu Jumapili na Jumanne ilicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wengine na kutoa sare ya 0-0. Kikosi hicho chini ya kocha wake Mkuu, Charles Boniface Mkwasa kitaondoka leo usiku kwenda Iringa, umbali wa kilomita zisizopungua 278 tayari kwa mchezo wa kesho jioni. Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja tu, Coastal Union wakiikaribisha Azam FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kesho kutwa, mabingwa watetezi, Simba SC watameny