Na Mwandishi Wetu, BIRMINGHAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza kwa dakika 67 tu, timu yake mpya, Aston Villa ikishinda 2-1 dhidi ya Leicester City Uwanja wa Villa Park, Jijini Birmingham na kuingia fainali ya Kombe la Ligi England. Samatta alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza kabisa baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 8.5 kutoka KRC Genk ya Ubelgiji, klabu yake ya kwanza Ulaya aliyojiunga nayo mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Pamoja na ugeni wake, Samatta, mchezaji wa zamani wa Mbagala Market, ambayo sasa inajulikana kama African Lyon na Simba, zote za Dar es Salaam, alicheza kwa kiwango kizuri na kukaribia kufunga kabla ya kocha Dean Smith kumpumzisha dakika ya 67, akimuingiza mshambuliaji kinda wa England, Keinan Davis. Mbwana Samatta akisikitika baada ya kukosa bao la wazi jana Uwanja wa Villa Park, Birmingham PICHA ZAIDI GONGA HAPA Katika mchezo huo, mabao ya Villa yalifungwa na Ma