Posts
Showing posts from February, 2020
ISMAILA SARR AWAZIMA LIVERPOOL VICARAGE, AWAPIGA MBILI JOGOO LAFA 3-0
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji wa umri wa miaka 22 Msenegal, Ismaila Sarr (katikati) amefunga mabao mawili dakika za 54 na 60 katika ushindi wa 3-0 wa Watford dhidi ya Liverpool, bao lingine la wenyeji likifungwa na Troy Deeney dakika ya 72 Uwanja wa Vicarage Road kikosi cha Jurgen Klopp kikipoteza mechi ya kwanza ya msimu katika Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
ALONSO AIPIGIA ZOTE MBILI CHELSEA YALAZIMSHA SARE 2-2 NA BOURNEMOUTH
- Get link
- X
- Other Apps
MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA JAFFAR ABBAS KATIKA SPORTS AM AZAM TV
- Get link
- X
- Other Apps
NCHIMBI ATOKEA BENCHI NA KUIFUNGIA YANGA MABAO YOTE IKIWAPIGA 2-0 ALLIANCE FC TAIFA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM YANGA SC imepata ushindi wa kwanza katika mechi tano za Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Alliance FC ya Mwanza mabao 2-0 usiku wa leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Ushindi huo unaofuatia sare nne mfululizo, unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 44 baada ya kucheza mechi 23, ingawa inabaki nafasi ya tatu sasa ikizidiwa pointi moja tu na Namungo FC inayoshika nafas ya tatu, ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi. Shujaa wa Yanga SC katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Omary Mdoe aliyesaidiwa na Mohamed Mkono na Arnord Bugado wote wa Tanga ni mshambuliaji wake mpya, Dtram Adrian Nchimbi aliyefunga mabao yote mawili baada ya kutokea benchi kipindi cha pili. Nchimbi aliyechukua nafasi ya mchezaji mwenzake mpya, Tariq Seif Kiakala alifunga mabao yake dakika ya 47 akimalizia pasi ya winga Mghana, Bernard Morrison na 78 baada ya kuuwahi mpira mrefu ulioanzishwa na kipa Metacha Boniphace Mnata. Hata hivyo, baada ya mabao hayo m
AZAM FC YAICHAPA JKT TANZANIA 1-0 DODOMA, NAMUNGO FC NAYO YAIPIGA 2-1 LIPULI SAMORA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DODOMA BAO la dakika ya 90 la mshambuliajii chipukizi, Andrew Simchimba limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Kwa ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na Mromania, Aristica Cioaba inafikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, hivyo kuendelea kushika nafas ya pilim, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 62 za mechi 24. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Namungo FC ikaibuka na ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya Lipuli FC Uwanja wa Samora mjini Iringa hivyo kufikisha pointi 46 katika mchezo wa 24 na kuendelea kukamata nafas ya tatu, mbele ya Yanga yenye pointi 41 za mechi 22. Nayo Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbao FC, mabao ya Graham Naftal na Baraka Mtuwi Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Mwadui FC imeshinda 2-0 dhidi ya Coastal Union, mabao ya Raphael Aloba dakika ya 19 na Mussa Chambega dakika y
SHIME ANAAMINI TANZANIA ITAICHAPA UGANDA KESHO KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U-17
- Get link
- X
- Other Apps
Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa timu ya wanawake u-17 ya Tanzania, Bakari Shime amesema kuwa kikosi kimejipanga kufanya vyema katika mechi dhidi ya Uganda. Timu hiyo ya wanawake inashuka dimbani Jumapili uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kuwakaribisha Uganda katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia nchini India, Julai mwaka huu. Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Shime amesema kuwa ana amini kuwa maandalizi yapo vizuri na wanahakikisha watafanya vyema katika mechi hiyo ya hapa nyumbani. Alisema kuwa wachezaji wote wapo vizuri na kikosi kina morali ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo. “Kwa mujibu wa ripoti ya daktari hakuna majeruhi wachezaji wote wapo fiti na kufikia siku ya mechi kikosi kitahakikisha kinafanya vyema katika mechi hiyo ambayo ni mechi muhimu kwa taifa" alisema Aliongeza kuwa maandalizi yapo vizuri na wamepanga kufanya vyema nyumbani na ugenini japo mechi utakuwa ngumu lakini atahakikisha kikosi kinafany
ARSENAL YATUPWA NJE EUROPA LEAGUE BAADA YA KUPIGWA 2-1 EMIRATES
- Get link
- X
- Other Apps
Youssef El-Arabi akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Olympiacos dakika ya 119 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Arsenal kwenye mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London. Olympiacos ilitangulia kwa bao la Pape Abou Cissé dakika ya 53, kabla ya Pierre-Emerick Aubameyang kuisawazshia Arsenal dakika ya 113, hivyo kufanya matokeo ya jumla kuw asare ya 2-2 na baada ya Washika Bunduki wa London kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini, lakini timu ya Ugiriki inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini PICHA ZAIDI GONGA HAPA
FRED APIGA MBILI MANCHESTER UNITED YASHINDA 5-0 NA KUTNGA 16 BORA EUROPA LEAGUE
- Get link
- X
- Other Apps
Kiungo wa Manchester United, Frederico Rodrigues Santos 'Fred' akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili timu hiyo dakika za 82 na 90 katika ushindi wa 5-0 Uwanja wa Old Trafford usiku wa jana dhidi ya Club Brugge KV kwenye mchezo wa marudiano Hatua ya 32 Bora UEAFA Europa League. Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya 27, Odion Ighalo dakika ya 34 na Scott McTominay dakika ya 41 na kwa ushindi huo Mashetani Wekundu wanatinga 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 6-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Ubelgiji PICHA ZAIDI GONGA HAPA
RONALDO AKOSA 'BAO LA WAZI' JUVE YACHAPWA 1-0 NA LYON UFARANSA
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo akisikitika baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 80 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya wakichapwa 1-0 na wenyeji, Lyon usiku wa jana Uwanja wa Groupama, Decines-Charpieu bao pekee la Lucas Tousart dakika ya 31. Timu hizo zitarudiana Machi 17 Jijini Torino PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MANCHESTER CITY WAIKANDAMIZA REAL MADRID 2-1 PALE PALE BERNABEU
- Get link
- X
- Other Apps
Kevin De Bruyne (kulia) akishangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Manchester City kwa penalti dakika ya 83 ikiwalaza 2-1 wenyeji, Real Madrid usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu Jijini Madrid kwenye mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya. Real Madrid ilitangulia kwa bao la Isco dakika ya 60, kabla ya Gabriel Jesus kuisawazishia Man City dakika ya 78 na timu hizo zitarudiana Machi 17 Uwanja wa Etihad, Manchester PICHA ZAIDI GONGA HAPA
YANGA SC YAICHAPA 1-0 GWAMBINA FC NA KUTINGA ROBO FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION CUP
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM YANGA SC imeungana na mahasimu wao, Simba SC kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Gwambina FC jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Shujaa wa Yanga SC ni kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 45 na ushe kwa shuti la umbali wa mita 35. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Nassor Mwinchui wa Pwani, aliyesaidiwa na Rashid Zonga wa Iringa na Abdulaziz Ally wa Arusha, pamoja na kufungwa, Gwambina ya Daraja la Kwanza ilionyesha mchezo mzuri. Mechi nyingine za leo za Hatua ya 16 Bora ASFC, mabingwa watetezi Azam FC nao wamekwenda robo fainali kwa ushindi mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya wenyeji, Ihefu ya Daraja la Kwanza pia kufuata sare ya 0-0 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kagera Sugar pia imeshinda kwa penalti 2-0 dhidi ya KMC kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Kai
JONAS MKUDE AUNGANISHWA NA MORRISON KESI YA KUPIGA ‘VIWIKO’ KAMATI YA NIDHAMU TFF
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIUNGO wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Februari 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kwa Vyombo vya Habari leo mjini Dar es Salaam imesema kwamba Mkude alimpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United FC, Ally Kombo katika mchezo wa Ligi Kuu ambao timu yake, Simba SC ilishinda 3-1. Hata hivyo, kiungo huyo aliyecheza vizuri siku hiyo, Mkude alinaswa na picha za Televisheni akimpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United, Ally Kombo. Lakini kiungo huyo wa kimataifa wa Tanzania alikuwa mwenye bahati kwa sababu marefa hawakuona tukio hilo, hivyo kuepuka adhabu ya kadi mchezoni. Mkude anaungana na kiungo wa mahasimu wao wa jadi, Yanga SC, Mghana Bernard Morrison kwenda kusimama Kamati ya Nidhamu – wote kwa makosa yanayofanana
MAREFA WALIOKATAA BAO LA POLISI DHIDI YA YANGA MOSHI WAFUNGIWA MIEZI MITATU KILA MMOJA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MAREFA waliochezesha mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya wenyeji, Polisi Tanzania na Yanga SC ya Dar es Salaam Abel William na Martin Mwalyaje wamefungiwa miezi mitatu kila mmoja kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mchezo huo Februari 18, mwaka huu Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Polisi Tanzania walilazimishwa sare ya 1-1 na Yanga SC, lakini marefa hao walikataa bao moja zuri la wenyeji lililofungwa na mshambuliaji Matheo Anthony (pichani) . Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imesema kwamba William na Mwalyaje wamefungiwa kwa mujibu wa kanuni ya 39 (1A) ya Udhibiti wa Waamuzi.
RUVU SHOOTING YAPIGWA FAINI SH MILIONI 1, MASAU BWIRE APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Ruvu Shooting FC imetozwa faini ya Sh Milioni 1 kwa kosa la timu hiyo kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi na kusababisha kutokea kwa vurugu kwenye mchezo huo uliofanyika Februari 22, mwaka huu Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kwa Vyombo vya Habari leo mjini Dar es Salaam imesema kwamba vurugu hizo ziliongozwa na mwalimu wa timu hiyo Salum Mayanga pamoja na wachezaji wake, Shaaban Kisiga, Emmanuel Martin na Rajab Zahir na adhabu imetolewa kwa mujibu wa Kanuni 14(43) ya Ligi Kuu Kuhusu Taratibu za Mchezo. Taarifa ya Kamati pia imesema kwamba ilipitia tena shauri hilo Ruvu Shooting kuomba marejeo juu ya maamuzi ya kuwapa Tanzania Prison FC ushindi dhidi ya kutokana na kutofata Kanuni ya 14(2l) ya Ligi Kuu maamuzi kubaki kama yalivyokuwa. Naye Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kwenye vyombo
LUC EYMAEL NA TSHISHIMBI WAPIGWA FAINI KWA KUGOMA KUZUNGUMZA NA AZAM TV TANGA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA wa Yanga SC, Mbelgiji Luc Eymael ametozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na mdhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Azam Media Februari 23, mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga. Eymael alifanya kosa hilo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga na adhabu imetolewa kwa mujibu wa kanuni ya 41(2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha. Kosa kama hilo lilifanuywa pia na Nahodha wa Yanga SC, Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye yeye ametozwa faini ya Sh. 200,000. Tshishimbi naye alikataa kufanya mahojiano na Azam TV baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0 Uwanja wa Mkwakwani na adhabu yake imetolewa kwa mujibu wa kanuni 38(18) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
DEONTAY WILDER AMFUKUZA KOCHA WAKE ALIYERUSHA TAULO ULINGONI
- Get link
- X
- Other Apps
BONDIA Deontay Wilder atamfukuza kocha wake Mark Breland baada ya kukasirishwa na kitendo chake cha kurusha taulo ulingoni Jumapili katika pambano lake dhidi ya Tyson Fury. Mmarekani, Wilder alivuliwa taji la WBC uzito wa juu baada ya kuchapwa kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba na Fury ukumbi wa MGM Grand Jijini Las Vegas. Na hiyo ni baada ya Breland kurusha taulo ulingoni raundi ya saba kufuatia Wilder kuchapwa ngumi mfululizo bila majibu katika pambano ambalo tayari alikwishaangushwa mara mbili. Hata hivyo, mbabe wa Alabama, Wilder amesema aliwazuia watu wa kona yake kusalimu amri licha ya kuzidiwa na wamuache aendelee kwa sababu alikuwa ana raundi tano zaidi kuelekea mwisho wa pambano. Wilder na kocha wake mkuu, Jay Deas walizungumza na Waandishi wa Habari baada ya pambano na kusema hawakukubaliana na uamuzi wa kurusha taulo na kwa hilo atabomoa 'benchi lake la ufundi'. Wilder amesema ataanza kushughulikia pambano la marudiano na ataingia na kocha mpya.
SERGE GNABRY APIGA MBILI BAYERN MUNICH YAICHAPA CHELSEA 3-0 STAMFORD BRIDGE
- Get link
- X
- Other Apps
Serge Gnabry akishangilia baada ya kuifungia Bayern Munich mabao mawili dakika za 51 na 54 kabla ya Robert Lewandowski kufunga la tatu dakika ya 76 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Chelsea usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London, kwenye mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya. Timu hizo zitarudiana Machi 18 Jijini Munich PICHA ZAIDI GONGA HAPA
GRIEZMANN AISAWAZISHIA BARCELONA YATOA SARE YA 1-1 NA NAPOLI ITALIA
- Get link
- X
- Other Apps
Antoine Griezmann (kulia) akijiandaa kushangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Barcelona dakika ya 57 ikitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Napoli waliotangulia kwa bao la Dries Mertens dakika ya 30 katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa San Paolo Jijini Napoli. Timu hizo zitarudiana Machi 18 Camp Nou PICHA ZAIDI GONGA HAPA
STAND UNITED 1-1 (PENALTI 2-3) SIMBA SC (KOMBE LA TFF)
- Get link
- X
- Other Apps
SIMBA SC YAING’OA KWA MATUTA STAND UNITED NA KUTINGA ROBO FANALI MICHUANO YA ASFC
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA MABINGWA wa soka Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 na wenyeji, Stand United jioni ya leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere alikosa penalti ya pili katika mchezo wa pili mfululizo leo baada ya mkwaju wake kupanguliwa na kipa wa Stand United, Murtala Hamad ambao ndio ulifungua ngwe ya matuta leo. Kagere alikosa penalti pia kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ingawa Simba SC iliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Biashara United naye akifunga bao la pili siku hiyo. Waliofunga penalti za Simba SC leo ni viungo, Mzambia Clatous Chama, Mkongo Deogratius Kanda na mzawa, Hassan Dilunga, wakati Ibrahim Ajibu shuti lake liligonga mwamba wa juu na kupotelea nje. Kwa upade wa Stand United penalti
MANE APIGA BAO LA USHINDI DAKIKA ZA JIONI LIVERPOOL YAICHAPA WEST HAM 3-2
- Get link
- X
- Other Apps
Sadio Mane akitabasamu baada ya kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya 81 ikiichapa 3-2 West Ham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Anfield, Liverpool. Mabao mengine ya Liverpool yalifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya tisa na Mohamed Salah dakika ya 68, wakati ya West Ham United yalifungwa na Issa Diop dakika ya 12 na Pablo Fornals dakika ya 54 na kwa ushindi huo kikosi cha Jurgen Klopp kinafikisha pointi 79 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 22 zaidi ya Manchester City inayofuatia nafasi ya pili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TWIGA STARS WALIVYOWASILI DAR ES SALAAM LEO BAADA YA KUSHIKA NAFASI YA PILI MICHUANO YA UNAF TUNISIA
- Get link
- X
- Other Apps
MAZOEZI YA SIMBA SC LEO SHINYANGA KUJIANDAA NA MCHEZO DHIDI YA STAND UNITED KESHO MICHUANO YA ASFC
- Get link
- X
- Other Apps
Viungo wa Simba SC, Mbrazil Gerson Fraga 'Vieira' (kulia) na Jonas Mkude wakichuana mazoezini leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kujiandaa na mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya wenyeji, Stand United kesho mjini humo Viungo wengine wa Simba SC, Msudan Sharaf Eldin Shiboub (kulia) na Mkongo Deogratius Kanda wakionyeshana ufundi Hapa ni mchezaji wa zamani wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Deo Kanda akimpita beki wa zamani wa El Merreikh ya Sudan, Muivory Coast, Serge Wawa Pascal. Nyuma ni Shiza Kichuya