MJUMBE YANGA SC AWA WA KWANZA KUJIUZUKU TUHUMA ZA KUUTILIA SHAKA UDHAMINI WA GSM
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Shijja Richard amejiuzulu wadhifa huo leo, kufuatia tuhuma za kuhusishwa katika orodha ya wajumbe wanne wa klabu wanaodaiwa kuutilia shaka udhamini wa kampuni ya GSM.
Shijja, Mwandishi wa habari za michezo wa zamani, amesema kwamba ameamua kwa hiari yake kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ya Yanga.
“Yanga ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote. Yamezungumzwa mengi lakini mimi sitazungumza chochote. Wakati utaongea. Ukweli hata usipousema, huwa una tabia ya kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele,”amesema Shijja katika taarifa yake.
Shijja aliyewahi kugombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliopita na kuangushwa na Wallace Karia ni mmoja kati ya Wajumbe wanne wanaodaiwa kumpinga mdhamini wa klabu, kampuni ya GSM.
Pamoja na kuwa na mkataba wa udhamini wa vifaa vya michezo, kampuni ya GSM imekuwa ikijitolea kufanya mambo zaidi kuisaidia Yanga, lakini inadaiwa baadhi ya Wajumbe akiwemo Shijja, Salum Rupia, Rodgers Gumbo na Frank Kamugisha wanadaiwa kutilia shaka hilo.

Comments
Post a Comment