Posts

Showing posts from October, 2020

OLEKSANDR USYK AMSHINDA CHISORA KWA POINTI WEMBELY

Image
Bondia Oleksandr Usyk wa Ukraine (kulia) amemshinda mwenyeji, Derek Chisora kwa pointi usiku wa jana katika pambano la ngumi za kulipwa uzito wa juu Uwanja wa Wembley, London, hivyo kujiweka katika nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia dhidi ya Muingereza mwingine, Anthony Joshua  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

BARCELONA YAAMBULIA SARE YA 1-1 KWA ALAVES LA LIGA

Image
Nahodha wa Barcelona, Muargentina Lionel Messi akitafuta maarifa ya kuwatoka wachezaji wa Deportivo Alavés kwenye mchezo wa La Liga timu hizo zikitoka sare ya 1-1 jana Uwanja wa Mendizorroza. Luis Rioja alianza kuifungia Alaves dakika ya  31, kabla ya Antoine Griezmann kuisawazishia Barcelona dakika ya 63   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

BENZEMA APIGA MBILI REAL MADRID YAICHAPA HUESCA 4-1 LA LIGA

Image
Mshambuliaji Karim Benzema akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Real Madrid dakika za 45 na 90 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Huesca kwenye mnchezo wa LaLiga jana Uwanja wa Alfredo Di Stéfano, Jijini Madrid. Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Eden Hazard dakika ya 40 na Federico Valverde dakika ya 54, wakati bao pekee la Huesca lilifungwa na David Ferreiro dakika ya  74   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

KYLE WALKER AIFUNGIA BAO PEKEE MAN CITY YASHINDA 1-0

Image
Kyle Walker akifumua shuti kuifungia bao pekee Manchester City dakika ya 28 akicheza mechi ya 100 ya Ligi Kuu ya England katika ushindi wa 1-0 dhidi ya timu yake ya zamani, Sheffield United Uwanja wa Bramall Lane   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

HAKIM ZIYECH AFUNGA LA KWANZA CHELSEA YAICHAPA BURNLEY 3-0

Image
Hakim Ziyech akishangilia baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 26 na la kwanza kwa Mmorocco huyo katika Ligi Kuu ya England kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Burnley jana Uwanja wa Turf Moor mabao mengine yakifungwa na Kurt Zouma dakika ya 63 na Timo Werner dakika ya 70   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

DIOGO JOTA ATOKEA BENCHI KUIFUNGIA BAO LA USHINDI LIVERPOOL

Image
Diogo Jota akishangilia baada ya kutokea benchi dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Roberto Firmino na kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya 85 ikiwalza West Ham United 2-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Anfield. Wagonga Nyundo wa London walitangulia kwa bao la Pablo Fornals dakika ya 10, kabla ya Mohamed Salah kuwasawazishia wenyeji kwa penalti dakika ya 42   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

YANGA SC YASHINDA MECHI YA SABA MFULULIZO LIGI KUU, YAIPIGA BIASHARA UNITED 1-0 MUSOMA

Image
Na Mwandishi Wetu, MUSOMA VIGOGO, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara. Ushindi huo wa saba mfululizo katika mchezo wa nane wa msimu, unaifanya Yanga SC inayofundishwa na kocha Mrundi, Cedric Kaze ifikishe pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa wastani wa mabao na Azam FC ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi. Bao pekee la Yanga SC leo limefungwa na mshambuliaji wake Mghana, Michael Sarpong dakika ya 68 akimalizia krosi ya Ditram Nchimbi kutoka upande wa kulia. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabingwa watetezi, Simba SC wamezinduka kutoka kwenye vipigo viwili mfululizo baada ya kuichapa Mwadui FC 5-0, mabao ya Nahodha na mshambuliaji, John Bocco na viungo Hassan Dilunga mawili kila mmoja na Said Ndemla moja. Namungo FC ikaibika na ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, bao pekee la Steven Sey dakika ya 66 Uwanja wa Majaliwa

SIMBA SC WAZINDUKA KUTOKA KWENYE VIPIGO VIWILI MFULULIZO NA KUITANDIKA MWADUI FC 5-0

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA watetezi, Simba SC wamezinduka kutoka kwenye vipigo viwili mfululizo baada ya kuichapa Mwadui FC mabao 5-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Ushindi huo wa kwanza katika mechi tatu, unaifanya Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck ifikishe pointi 16 baada ya kucheza mechi nane na kurejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nyuma ya Azam FC na Yanga wenye pointi 22 kila mmoja. Nahodha na mshambuliaji, John Raphael Bocco leo amefunga mabao mawili katika ushindi huo, la kwanza dakika ya 25 akimalizia pasi ya kiungi Mzambia, Clatous Chama na la pili dakika ya 64 akimalizia kazi nzuri ya mtokea benchi Hassan Dilunga. Kiungo wa zamani wa Yanga SCm, Dilunga naye akafunga mabao mawili, la tatu dakika 81 akimalizia pasi ya mtokea benchi mwenzake, Ibrahim Ajibu na la nne dakika ya 86 akimalizia pasi ya Said Ndemla. Ndemla ambaye amerejea kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC msimu huu baada ya ku

TWAHA KIDUKU AMSHINDA BONDIA WA THAILAND TKO RAUNDI YA SABA

Image
BONDIA, Twaha Kassim Rubaha (kushoto), maarufu kwa jina la utani Twaha 'Kiduku usiku wa jana amesmhinda kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba, Mthailand Sirimongkhon Lamthuam katika pambano lililokuwa la raundi 10 uzito wa Super Welter lililofanyika ukumbi wa PTA, Saba Saba, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

SURE BOY AINUSURU AZAM FC KUFUNGWA NYUMBANI, YATOA SARE 1-1 NA JKT TANZANIA CHAMAZI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.  Pamoja na sare hiyo, Azam FC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 22 baada ya kucheza mechi tisa sasa, ikiwazidi pointi tatu mabingwa wa kihistoria, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi. Katika mchezo wa leo, Michael Aidan Pius alianza kuifungia JKT Tanzania dakika ya 43, kabla ya Nahodha na kiungo hodari, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kuisawazishia Azam FC dakika ya 78. Baada ya mwanzo mzuri ikishinda mechi saba mfululizo, Azam FC ilipunguzwa kasi wiki iliyopita kwa kuchapwa 1-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo, Morogoro na leo imetoa sare nyumbani.  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, KMC imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Gwambina FC Uwanja wa Gwambina, Misungwi mkoani Mwanza, mabao ya Lusajo Mwaikenda dakika ya 43, Rell

KIKOSI CHA YANGA SC CHAZURU KABURI LA MWALIMU NYERERE NA KUMKABIDHI JEZI MAMA MARIA

Image
Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk Mshindo Msolla akimkabidhi jezi ya klabu hiyo, Mama Maria Nyerere, mjane wa baba taifa, marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo kijijini Mwitongo, Butiama mkoani Mara. Wachezaji na viongozi wa Yanga SC wakiwa mbele ya kaburi la marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo kijijini Mwitongo, Butiama mkoani Mara. Wachezaji wa Yanga SC wakipewa maelezo kuhusu eneo la Mwitongo, Butiama mkoani Mara Wachezaji wa Yanga SC wakiwa katika picha ya pamoja na mjane wa marehemu Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere leo Butiama

MORRISON KUWA NDUGU MTAZAMAJI SIMBA NA YANGA NOVEMBA 7, AFUNGIWA MECHI TATU KWA KULETA UBONDIA KWENYE SOKA

Image
WINGA Mghana wa Simba SC ataukosa mchezo dhidi ya mahasimu na timu yake ya zamani, Yanga SC Novemba 7 baada ya kufungiwa mechi tatu kwa kumpiga ngumi beki wa Ruvu Shooting, Juma Said Nyosso.

JUMA NYOSSO AFUNGIWA MECHI TATU KWA KUMKANYAGA MORRISON MECHI YA RUVU NA SIMBA SC

Image
BEKI wa Ruvu Shooting, Juma Said Nyosso amefungiwa mechi tatu kwa tuhuma za kumkanyaga kwa makusudi kiungo Mghana wa Simba SC, Bernard Morrison.  

REFA SHOAMRI LAWI AFUNGIWA MWAKA MZIMA KWA KUBORONGA MECHI YA PRISONS NA SIMBA SUMBAWANGA

Image
REFA Shomary Lawi wa Kigoma amefungiwa mwaka mmoja kwa tuhuma za kushindwa kuumudu mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Tanzania Prisons na mabingwa watetezi, Simba SC. Mchezo huo ulifanyika wiki iliyopita na Tanzania Prisons wakaibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.     

ARSENAL YAWACHAPA DUNDALK 3-0 EMIRATES UEFA EUROPA LEAGUE

Image
Eddie Nketiah akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 42, kabla ya Joe Willock kufunga la pili dakika ya 44 na Nicolas Pépé la tatu dakika ya 46 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Dundalk kwenye mchezo wa Kundi B  UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Emirates, London   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

NEYMAR AUMIA, PSG YASHINDA 2-0 UTURUKI LIGI YA MABINGWA

Image
Mshambuliaji Neymar akitoka nje dakika ya 27 baada ya kuumia kwenye mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Paris Saint-Germain ikishinda 2-0 dhidi ya wenyeji, Istanbul Basaksehir, mabao ya Moise Kean dakika ya 64 na 79 Uwanja wa BaÅŸakÅŸehir Fatih Terim jijini Ä°stanbul   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MESSI APIGA LA PILI BARCELONA YAICHAPA JUVENTUS 2-0 TORINO

Image
Wachezaji wa Barcelona wakimpongeza Nahodha wao, Lionel Messi baada ya kufunga bao la pili dakika ya 90 na ushei kufuatia Ousmane Dembele kufunga la kwanza dakika ya 14 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Juventus kwenye mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Allianz Jijini Turin   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

CHELSEA YAWACHAPA KRASNODAR 4-0 KULE KULE KWAO URUSI

Image
Wachezaji wa Chelsea wakipongezana kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Krasnodar kwenye mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya mabao ya Callum Hudson-Odoi dakika ya 37, Timo Werner dakika ya 76 kwa penalti, Hakim Ziyech dakika ya 79 na Christian Pulisic dakika ya 90 usiku wa jana Uwanja wa FK Krasnodar, Jijini Krasnodar, Urusi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

RASHFORD APIGA HAT TRICK MAN UNITED YAIPIGA LEIPZIG 5-0 LIGI YA MABINGWA

Image
Mshambuliaji Marcus Rashford akishangilia baada ya kuifungia Manchester United mabao matatu dakika za 74, 78 na 90 na ushei katika ushindi wa 5-0 dhidi ya RB Leipzig kwenye mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford. Mabao mengine ya Man United yalifungwa na Mason Greenwood dakika ya na 21 Anthony Martial kwa penalti dakika ya 87   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

REAL CHUPUCHUPU KUPIGWA UJERUMANI, YATOA SARE 2-2

Image
Casemiro akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid bao la kusawazisha dakika ya 90 na ushei ikitoa sare ya 2-2 na wenyeji, Borussia Moenchengladbach kwenye mchezo wa Kundi B usiku wa jana Uwanja wa im BORUSSIA-PARK. Bao lingine la Real Madrid lilifungwa na Karim Benzema dakika ya 87, baada ya Borussia Moenchengladbach kutangulia kwa mabao ya Marcus Thuram, mtoto wa mchezaji wa zamani wa Ufaransa, Lilian Thuram dakika ya 33 na 58   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

BAYERN YAENDELEZA UBABE ULAYA, YAICHAPA LOKOMOTIV 2-1 MOSCOW

Image
Kiungo Joshua Kimmich akishangilia baada ya kuifungia Bayern Munich bao la ushindi dakika ya 79 ikiwalaza wenyeji, Lokomotiv Moscow 2-1 kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Arena. Bao la kwanza la Bayern Munich lilifungwa na Leon Goretzka dakika ya 13 kabla ya Anton Miranchuk kuisawazishia Lokomotiv Moscow   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MAN CITY YAWACHAPA MARSEILLE 3-0 PALE PALE UFARANSA

Image
Wachezaji wa Manchester City wakipongezana baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Marseille mabao ya Ferran Torres dakika ya 18 Ilkay Gundogan dakika ya 76 na Raheem Sterling dakika ya 81 kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Orange Velodrome   PICHA ZAIDI GONGA HAPA