Posts

Showing posts from July, 2021

AZAM FC YAMSAJILI MSHAMBULIAJI MKONGO, IDRIS MBOMBO KUTOKA EL GOUNAH YA MISRI KWA MKATABA WA MIAKA MIWILI

Image
KLABU ya Azam FC imemsainisha mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Idris Mbombo, kutoka El Gounah ya Misri. Mbombo amesaini mkataba huo mbele ya Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya kuhudumu ndani ya timu yetu hadi mwaka 2023. Mshambuliaji huyo hatari, aliyewahi kuzichezea kwa mafanikio timu za Nkana, Zesco United, Kabwe Warriors, zote za Zambia, anakuja kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo msimu uliopita ililtegemea zaidi Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo. Huyo anakuwa mchezaji mpya wa sita dirisha hili kubwa la usajili baada ya Mkenya, Kenneth Muguna, Wazambia watatu, Charles Zulu, Paul Katema,  mshambuliaji Rodgers Kola na beki wa kushoto mzawa, Edward Manyama.

KIKOSI CHA TANZANIA KILICHOTWAA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE U23 KUREJEA NCHINI KESHO MCHANA

Image
KIKOSI cha Tanzania kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Mafaifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 23, CECAFA Challenge U23 jana nchini Ethiopia kinatarajiwa kurejea nchini kesho mchana.

KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI YA TFF YAAGIZA UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA PWANI URUDIWE

Image
  KAMATI ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeagiza uchaguzi wa Chama cha Soka Pwani (COREFA) urudiwe.

TANZANIA PRISONS YAENDELEA KUIMARISHA KIKOSI KWA KUMSAJILI NYOTA ALIYEKUWA ANACHEZA KARIOBANGI SHARKS YA KENYA

Image
KLABU ya Tanzania Prisons imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kumsajili kiungo mshambuliaji Athanas Mdam aliyekuwa anachezea Kariobangi Sharks ya Kenya kwa mkataba wa miaka miwili. Pamoja na mchezaji huyo aliyeibukia akademi ya Alliance ya Jijini Mwanza, Prisons pia imemsajili tena mlinda mlango wake, Hassan Msham na kumpandisha beki wa kushoto wa  timu ya vijana U20, Ibrahim Abdallah Abraham.

AZAM FC YAMPONGEZA MTENDAJI WAKE MKUU WA ZAMANI KUTEULIWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU YA ZANZIBAR

Image
KLABU ya Azam FC imempongeza aliyekuwa Mtendaji wake Mkuu, Abdul Mohamed kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar. Uteuzi huo umefanywa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mh. Dk. Hussein Mwinyi.

NYOTA WA R&B NCHINI, BEN POL ATOA NYIMBO NNE MPYA KALI TUPU AZIITA KIFURUSHI CHA B, ZAWADI KWA MASHABIKI WAKE

Image
NYOTA wa Muziki wa R&B nchini, Behnam Paul maarufu kama Ben Pol  amewazawadia mashabiki zake kifurushi chenye nyimbo Nne mpya (4)  alichokiita “B”. Ben Pol ameachia nyimbo hizo leo ambapo mojawapo amemshirikisha Msanii Billinas aliyoiita Kisebusebu, nyingine ni Unaita, For You na Warira ambayo tayari alishaiachia mapema mwezi huu. Msanii huyo amesema, ameamua kuita B kwa sababu inabeba stori na hali tofauti tofauti katika mapenzi kupitia nyimbo hizo nne. “Naamini jumbe zitaeleweka kwa watu wengi kwa kuwa ni mambo ambayo tunayaishi kila siku,  Upendo ndio jibu, na muziki ndio njia, nami namshukuru kila mmoja kwa Upendo na support yake kwangu” amesema Ben Pol Amesema kuwa bado anaendelea kuwashukuru mashabiki wake kwa kupokea nyimbo na kuendelea kufanya vizuri na amewaahidi kuendelea kuwapa ladha tofauti kila siku. B inapatikana katika mitandao yote ya muziki na vituo vya redio ndani na nje ya nchi. Nyimbo hizo zimetayarishwa katika studio za Pizzey Records na watayarishaj

ARSENAL YAMSAJILI BEN WHITE KWA ADA YA PAUNI MILIONI 50

Image
  KLABU ya Arsenal imemtambulisha beki wa kati Ben White kutoka Brighton aliyesaini mkataba wa miaka mitano kwa ada ya Pauni Milioni 50. Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 anatua The Gunners baada ya kufanya vizuri akiwa kwa mkopo Leeds msimu uliopita. Na huo unakuwa usajili wa tatu kwa kocha Mikel Arteta baada ya beki wa pembeni, Nuno Tavares kutoka Benfica na kiungo Albert Sambi Lokonga kutoka Anderlecht.

MORRISON AFUNGIWA MECHI TATU NA FAINI YA SH MILIONI 3 KWA KOSA LA KUVUA BUKTA NA KUBAKI NA KICHUPI KIGOMA, MUKOKO NA SHIKALO NAO WAADHIBIWA NA TFF KWA MAKOSA TOFAUTI

Image
WINGA Mghana wa Simba SC, Bernad Morrison amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh. Milioni 3 kwa kosa la kuvua bukta na kubaki na kichupi kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Cup (ASFC) dhidi ya Yanga SC Julai 25, mwaka huu Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Taarifa ya TFF leo imesema katika mchezo huo ambao Simba ilishinda 1-0 bao la kiungo Mganda, Thadeo Lwanga dakika ya 80, klabu zote mbili zimetozwa faini kwa makosa mbalimbali ha uvunjaji wa kanuni. Kiungo Mkongo wa Yanga, Tonombe Mukoko naye amefungiwa mechi tatu na faini ya Sh. 500,000 baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 45 kwa kosa la kumpiga kiwiko mshambuliaji wa Simba, John Bocco. Kipa Mkenya wa Yanga SC, Farouk Shikalo ametozwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kukwepa kusalimiana na waamuzi na wachezaji wa Simba SC.

TANZANIA YATWAA UBINGWA WA CECAFA CHALLENGE U23 BAADA YA KUIPIGA BURUNDI KWA PENALTI 6-5 KUFUATIA SARE YA 0-0 LEO ETHIOPIA

Image
TANZANIA imetwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 baada ya ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya 0-0 na Burundi leo Uwanja wa Bahir Dar, Jijini Bahir Dar, Ethiopia. Sudan Kusini imemaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Kenya jana hapo hapo Bahir Dar.

CECACA YABADILI MPANGILIO KOMBE LA KAGAME, SASA NI MAKUNDI MAWILI YANGA WAPO A, AZAM FC B

Image
BARAZA la Soka Afrika Mashariki na Kati limefanya marekebisho michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kamgame sasa kutakuwa na makundi mawili badala ya matafu. Kundi A sasa litaundwa na timu za Yanga SC. Nyasa Big Bullet ya Malawi, Express ya Uganda na Atlabara ya Sudan Kusini, wakati kuna Azam FC, KCCA ya Uganda,  Le Massager Ngozi ya Burundi na KMKM ya Zanzibar. Michuano hiyo itaanza Agosti 1 hadi Agosti 14 Jijini Dar es Salaam, ingawa mabingwa wa Tanzania kwa miaka minne mfululizo, Simba SC wamejitoa.

HATIMAYE MO DEWJI AKABIDHI HUNDI YA SH BILIONI 20 KUNUNUA ASILIMIA 49 YA HISA NDANI YA KLABU YA SIMBA

Image
HATIMAYE mfanyabiashara, Mohamed Gulam Dewji amekabidhi hundi ya Sh. Bilioni 20 kununua hisa asilimia 49 za klabu ya Simba ya Dar es Salaam. Mo Dewji amemkabidhi hundi hiyo Mwenyekiti wa klabu, Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Ally Mangungu mchana wa leo katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Golden Jubilee Jijini Dar es Salaam. "Tumekamilisha mchakato wa mabadiliko. Tumepata hati kutoka FCC ya kuturuhusu kumalizia mchakato," amesema Mo Dewji na kuongeza; "Leo naweka hiyo Bilioni 20 ya hisa asilimia 49 mbele ya mdhamini wa klabu na mwenyekiti wa klabu,". Mo Dewji amesema ndani ya miaka minne tangu mchakato huo umeanza amekuwa akiihudumia Simba kwa kila kitu na katika kipindi hicho chote ametumia kiasi cha Sh. Bilioni 21.3, wastani wa Bilioni 5.3 kwa mwaka kwa ajili ya usajili wa wachezaji, makocha, maandalizi ya kabla ya msimu, mishahara na uendeshaji wa klabu,".  Mo amefurahi uwejezaji wake umekuwa na tija, kwani klabu imeshinda mataji manne ya Ligi

BODI YAAHIDI KUFANYIA MAREKEBISHO DOSARI ZILIZOJITOKEZA KATIKA MSIMU WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA ULIOMALIZIKA ILI MSIMU UJAO MAMBO YAWE TOFAUTI

Image
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika msimu uliomalizika wa ligi hiyo ili msimu ujao mambo yawe mazuri. Katika taarifa yao ya shukrani baada ya msimu wa Ligi Kuu wa 2020-2021, Bodi imetoa shukrani kwa wadau mbalimbali, wakiwemo wadhamini waliofanya msimu huo ukamilike vyema. "Kwa umuhimu wa kipekee, Bodi imezichukua changamoto zote zilizojitokeza kwenye msimu wa 2020-2021 na kuahidi kuzifanyia kazi ili kuhakikisha msimu wa 2021-2022 unakuwa bora zaidi ya msimu huu tuliomaliza," imesema taarifa ya Bodi.

JKT TANZANIA YATWAA UBINGWA WA LIGI YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 17 IKIZIACHA MBALI KABISA SIMBA NA YANGA

Image
TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), ikizipu Azam FC na Simba SC zilizomaliza nafasi ya pili na ya tatu. JKT Tanzania imemaliza na pointi 50, tano zaidi ya Azam na nane zaidi ya Simba, wakati vigogo wa soka nchini, Yanga SC U17 yao imemaliza nafasi ya sita baada ya kukusanya pointi 36.

YANGA SC YAACHANA RASMI NA BEKI WAKE MGHANA KWA MAKUBALIANO YA PANDE ZOTE MBILI

Image
KLABU ya Yanga SC imeachana na beki wake Mghana, Lamine Oumar Moro (pichani kulia)baada ya misimu miwili kwa makubaliano ya pande zote mbili.

YANGA SC YAPANGWA KUNDI MOJA NA BIG BULLET YA MALAWI NA EXPRESS FC YA UGANDA MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME

Image
 

EZEKIELKAMWAGA AREJESHWA SIMBA SC KUKAIMU NAFASI YA MANARA, HAJI AAGWA RASMI MSIMBAZI

Image
 

SPORTPESA YAWAZAWADIA SIMBA SC KITITA CHA SH MILIONI KWA KUTWAA KWA MARA NYINGINE TENA UBINGWA WA BARA

Image
MDHAMINI Mkuu wa klabu ya Simba, kampuni ya SportPesa leo imeikabidhi timu hiyo kiasi Sh. Milioni 100 kama zawadi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21.  GONGA HAPA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

WINGA MGHANA, BERNARD MORRISON ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MASHABIKI WA SIMBA SC MWEZI JUNI

Image
WINGA Mghana, Bernard Morrison amekabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Juni (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month). GONGA HAPA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

TANZANIA YATINGA FAINALI MICHUANO YA CECAFA CHALLENGE U23 BAADA YA KUICHAPA U23 SUDAN KUSINI 1-0 ETHIOPIA

Image
TANZANIA imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wamiaka 23 (CECAFA Challenge U23) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini mchana wa leo Uwanja wa Bahir dar nchini Ethiopia. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Kelvin Nashon Naftali dakika ya 64 na sasa Tanzania itamenyana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili inayoendelea hivi sasa baina ya Burundi na Kenya. Mechi za Fainali na ya kusaka mshindi wa tatu zote zitafanyika Jumamosi hapo hapo Bahir Dar.