Posts

Showing posts from September, 2021

KAGERA SUGAR 0-1 YANGA SC (LIGI KUU KAITABA)

Image
 

RONALDO AING’ARISHA MAN UNITED ULAYA

Image
WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Villarreal katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Wageni walitangulia kwa bao la Paco Alcácer dakika ya 53, kabla ya wenyeji kuzinduka kwa mabao ya Alex Telles dakika ya 60 na Cristiano Ronaldo dakika ya 90 na ushei. Ushindi huo unawafanya Mashetani Wekundu waokote pointi tatu za kwanza kwenye kundi hilo kufuatia kuchapwa 1-0 na Young Boys kwenye mchezo wa kwanza Uswisi.

LEWANDOWSKI APIGA MBILI, BAYERN YASHINDA 5-0

Image
WENYEJI, Bayern Munich wameibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Dynamo Kyiv katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani. Mabao ya Bayern Munich jana yalifungwa na Robert Lewandowski mawili, dakika ya 12 na 27 akimalizia pasi ya Thomas Müller, Serge Gnabry dakika ya 68, Leroy Sané dakika ya 74 na Erick Choupo-Moting dakika ya 87. Ushindi huo unawafanya Bayern Munich waendelee kuongoza Kundi E wakifikisha pointi sita, mbele ya Benfica wenye pointi nne, Dinamo Kiev pointi moja na Barcelona ambayo haina pointi.

BARCELONA YAPIGWA TENA LIGI YA MABINGWA

Image
WENYEJI, Benfica wamewatandika Barcelona mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Luz Jijini Lisbon, Ureno. Mabao ya Benfica jana yamefungwa na Darwin Núñez dakika ya tatu na 79  kwa penalti na Rafa Silva dakika ya 69 na kwa kipigo hicho cha pili mfululizo, Barcelona inashika mkia nyuma ya Dinamo Kiev yenye pointi moja. Bayern Munich wanaongoza sasa kwa pointi zao sita, wakifuatiwa na Benfica yenye pointi nne.

JUVENTUS YAICHAPA CHELSEA 1-0 TORINO

Image
WENYEJI Juventus jana wameutumia vizuri Uwanja wa nyumbani, Allianz Jijini Torino baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Kundi  H bao pekee la Federico Chiesa dakika ya 46. Ushindi huo unawapandisha kileleni Juve wakifikisha pointi sita,     wakati  Chelsea inabaki na pointi zake tatu sawa na Zenit, huku Malmö ambayo haina pointi ikiwa inashika mkia.

MWANAHAMISI ANG’ARA, TWIGA YASHINDA COSAFA

Image
MSHAMBULIAJI Mwanahamisi Omary Shaluwa leo amechaguliwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya Zimbabwe akiiwezesha Tanzania kushinda 3-0 katika mchezo wa Kundi B michuano ya COSAFA Uwanja wa Nelson Mandela Bay Jijini Port Elizabeth nchini Afrika Kusini. Mwanahamisi ‘Gaucho’ anayechezea klabu ya Chabab Atlas Khenifra ya Morocco leo ameifungia Twiga Stars bao la pili dakika ya 60, baada ya Deonisia Minja kufunga la kwanza dakika ya 41 na kabla ya Aisha Masaka kufunga la tatu dakika ya 90 na ushei. Twiga Stars itateremka tena dimbani Oktoba 2 kumenyana na Botswana kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kumenyana na Susan Kusini Oktoba 4.

YANGA YAANZA VYEMA LIGI KUU

Image
BAO pekee la kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 24 limeipa mwanzo mzuri Yanga SC katika Ligi a Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Kagera Sugar 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera. Fei Toto amefunga bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akimalizia mpira uliookolewa na kipa Issa Chalamanda kufuatia shuti la awali la mshambuliaji Mkongo, Fiston Mayele Kalala. Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabao ya mshambuliaji Vitalis Mayanga dakika ya tatu na 20 yameipa Polisi Tanzania ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha.

PACQUIAO AJIUZULU NGUMI BAADA YA MIAKA 26

Image
GWIJI  wa ngumi, Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo baada ya miaka 26 ulingoni akicheza mapambano 72 na kushinda mataji 12. Hatua hiyo inakuja mwezi mmoja tangu apoteze pambano mbele ya Mcuba, Yordenis Ugas kwa pointi Jijini Nevada Agosti 21, mwaka huu. Pacquiao ambaye ameshinda mapambano 62, kati ya hayo 39 kwa Knockouts (KO), akipigwa nane na kutoa sare mawili ni bondia pekee kihistoria kushinda mataji ya dunia katika madaraja nane tofauti. Seneta huyo wa Ufilipino, sasa anatarajiwa kuelekeza nguvu zake zaidi kwenye siasa baada ya kutangaza kuwania Urais wa nchi yake mwakani.

MO DEWJI AJIUZULU UENYEKITI SIMBA SC

Image
BILIONEA mwenye asili ya Kiasia, Mohamed ‘Mo Dewji’ ametangaza kujiuzulu Uenyekiti wa Bodi ya Simba SC na kubaki mwekezaji pekee kwa umiliki wa asilimia 49 ya hisa zenye thamani ya Sh. Bilioni 20. Akitangaza uamuzi wake huo leo, Dewji amesema kwamba nafasi yake itashikiliwa na aliyekuwa Makamu wake, Salum Abdallah Muhene ‘Try Again’. "Muda umefika mimi kama Mohamed, tumefanya mkutano tarehe 21 mwezi wa tisa, 2021 na tumekubaliana kwamba mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Simba Sports Club,".  "Naomba sana wana Simba msifikirie mimi nimeondoka kwenye Simba, bali bado ni mwekezaji kwenye Simba ni mwana hisa kwenye Simba, naipenda Simba na nitaendelea kuipenda Simba mpaka siku yangu ya mwisho," amesema Dewji leo Dares Salaam. Hatua hiyo inakuja siku moja tu baada ya timu kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Biashara United katika mchezo wake wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara huku Nahodha, John Bocco akikosa penal

BIASHARA UNITED 0-0 SIMBA SC (LIGI KUU MUSOMA)

Image
 

MESSI AWABAMIZA MAN CITY PARIS

Image
MABAO ya Idrissa Gueye dakika ya nane na Lionel Messi dakika ya 74 jana yamewapa wenyeji, Paris Saint-Germain ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa. Ushindi huo unaipeleka kileleni mwa Kundi hilo PSG ikifikisha pointi nne baada ya mechi mbili, sawa na Club Brugge, wakati Manchester City inabaki na pointi zake tatu katika nafasi ya tatu, mbele ya RB Leipzig ambayo haina pointi baada ya mechi mbili za awali.

LIVERPOOL YAICHAPA PORTO 5-1 URENO

Image
WENYEJI, FC Porto jana wamechapwa mabao 5-1 na Liverpool katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Do Dragão Jijini Porto, Ureno. Mabao ya Liverpool yalifungwa na Mohamed Salah mawili, dakika ya 18 na 60, Sasio Mané dakika ya 45 na Roberto Firmino mawili pia, dakika ya 77 na 81, wakati la Porto lilifungwa na M. Taremi dakika ya 74. Ushindi huo unaifanya Liverpool ifikishe pointi sita na kuendelea kuongoza kundi mbele ya Atletico Madrid yenye pointi nne, wakati Porto inabaki na pointi yake moja katika nafasi ya tatu mbele ya AC Milan ambayo haina pointi.

REAL MADRID YACHAPWA BERNABEU

Image
WENYEJI, Real Madrid wamechapwa 2-1 na FK Sheriff Tiraspol katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid nchini Hispania. Mabao ya FK Sheriff yalifungwa na  0 - 1 25' J. Yaxshiboyev dakika ya 25 na Thill dakika ya 89, wakati la Real lilifungwa na K. Benzema kwa penalti dakika ya 65. Sheriff inafikisha pointi sita baada ya ushindi huo na kupanda kileleni, ikifuatiwa na Real Madrid pointi tatu, Shakhtar Donetsk pointi moja sawa na Inter Milan baada ya mechi mbili za awali.

BOCCO AKOSA PENALTI, SIMBA YADROO MUSOMA

Image
MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara. Nahodha na mshambuliaji tegemeo, John Raphael Bocco  hatalala vizuri leo baada ya kuikosesha ushindi timu yake kufuatia mkwaju wake wa penalti kupanguliwa na kipa Mganda, Cleo James Ssetuba dakika ya 90. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, bao pekee la Cleophace Mkandala dakika ya 33 limewapa wenyeji, Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Na Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, bao la Peter Mapunda dakika ya 90 na ushei limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

NAMUNGO YAANZA VYEMA LIGI KUU

Image
TIMU ya Namungo FC imeanza vyema Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Geita Gold jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi. Mabao ya Namungo FC, timu kutoka Ruangwa yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 13 na Relliant Lusajo dakika ya 81. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wageni wakitangulia kwa bao la beki Mghana, Daniel Amoah dakika ya 49, kabla ya Hance Masoud kuwasawazishia wenyeji dakika ya 90. Na wageni wengine, Mbeya Kwanza wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar bao pekee la William Edgar dakika ya 50 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

YANGA WAWASILI KUIVAA KAGERA

Image
KIKOSI cha  Yanga kimewasili salama Bukoba mkoani Kagera leo baada ya kuondoka Dar es Salaam asubuhi ya leo, tayari kwa mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Jumatano Uwanja wa Kaitaba.

SIMBA WATUA MUSOMA KUIVAA BIASHARA

Image
KIKOSI cha Simba tayari kipo Musoma mkoani Mara baada ya safari ya ndege Dar-Mwanza na basi Mwanza- Musoma tayari kwa mchezo wake wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Biashara United kesho Saa 10:00 jioni Uwanja wa Karume.

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA SUNDAY MANARA

Image
 

POULSEN AMREJESHA MKUDE TAIFA STARS

Image
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wake wa tatu wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Benin Oktoba 7 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Katika kikosi hicho, Mdenmark huyo amemrejesha kiungo wa Simba SC, Jonas Gerlad Mkude na kumtema Salum Abubakr ‘Sure Boy’ wa Azam FC. Kikosi kamili kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Polisi), Wilbol Maseke (Azam), Ramadhani Kabwili (Yanga). Mabeki; Israel Mwenda (Simba), Kennedy Juma (Simba), Mohammed Hussein (Simba), Erasto Nyoni (Simba), Dickson Job (Yanga), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Edward Manyama (Azam FC) na Nickson Kibabage (KMC).  Viungo; Meshack Mwamita (kagera Sugar), Novatus Dismas (Maccabu Tel Aviv/Israel), Muzamil Yassin (Simba), Jonas Mkude (Simba) na Feisal Salum (Yanga Washambuliaji; John Bocco (Simba), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam), Abdul Suleiman (Coastal Union), Mbwana Samatta (Royal Antwerp/Ubelgiji), Relli

ARSENAL YAITANDIKA SPURS 3-1 EMIRATES

Image
WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumapili Uwanja wa Emirates Jijini London. Mabao ya The Gunners yamefungwa na Emile Smith Rowe dakika ya 12, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 27 na Bukayo Saka dakika ya 34, wakati la Spurs lilifungwa na Son Heung-Min dakika ya 79. Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mikel Arteta inafikisha pointi tisa na kupanda nafasi ya 10 ikilingana kila kitu na Spurs sasa baada ya wote kucheza mechi sita.

JOSHUA AVULIWA UBINGWA WA DUNIA

Image
BONDIA Anthony Joshua amevuliwa mataji yake ya ubingwa wa ngumi za kulipwa uzito wa juu baada ya kuchapwakwa poonti Oleksandr Usyk wa Ukraine usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London, Uingereza.  Joshua, mwenye umri wa miaka 31 alionekana kabisa kushindwa kummmudu Usyk ambaye majaji wote walima ushindi wa pointi 117-112, 116-112 na 115-113 na sasa huyo ndiye bingwa wa mataji ya WBO, WBA, IBF na IBO.

YANGA SC 1-0 SIMBA SC (NGAO YA JAMII)

Image
 

YANGA WAKIFURAHIA NA NGAO YAO LEO MKAPA

Image
WACHEZAJI wa Yanga wakifurahia na Ngao yao ya Jamii baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu, Yanga bao pekee la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

LIVERPOOL SARE 3-3 NA BRENTFORD

Image
TIMU ya Liverpool imelazimisha sare ya 3-3 na wenyeji, Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Brentford Community mjini Brentford, Middlesex. Mabao ya Brentford yamefungwa na Ethan Pinnock dakika ya 27, Vitaly Janelt dakika ya 63 na Yoane Wissa dakika ya 82, wakati ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya 31, Mohamed Salah dakika ya 54 na Curtis Jones dakika ya 67. Liverpool inafikisha pointi 14 baada ya mchezo huo na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani pointi moja tu zaidi ya Manchester City, Chelsea na Manchester United baada ya wote kucheza mechi sita.

RATIBA CHAMPIONSHIP YATOKA

Image
BODI ya Ligi Kuu imetoa ratiba ya Ligi ya Ubingwa,  ijulikanayo kama Championship kuwania kupanda Ligi Kuu ambayo itaanza Oktoba 2 nchini.

TANZANITE YAICHAPA ERITREA 3-0 ASMARA

Image
 TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Eritrea leo Uwanja wa Asmara Jijini Asmara katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani Costa Rica. Tanzanite inafunga safari kurejea Dar es Salaam kujipanga kwa mchezo wa marudiano Oktoba 9 nchini.