Posts

Showing posts from July, 2022

YANGA SC YASHINDA 9-0 MECHI YA KIRAFIKI LEO KIGAMBONI

Image
KLABU ya Yanga imeendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya baada ya leo kuichapa Friends Rangers mabao 9-0 leo Uwanja wa Avic Town, Somangira nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Khalid Aucho na chipukizi aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Clement Francis Mziza kila mmoja mawili, Fiston Kalala Mayele, Lazarous Kambole, Dennis Nkane, Jesus Moloko na Yacouba Sogne moja kila mmoja.

SIMBA KUCHEZA MECHI NYINGINE YA KIRAFIKI KESHO MISRI

Image
KLABU ya Simba kesho Jumatatu itacheza mchezo wa nne wa kirafiki katika kambi yake ya mjini Ismailia nchini Misri dhidi ya Al-Kholood FC. Mechi tatu za kwanza Simba ilitoa sare ya 1-1 na Ismailia,ikashinda 6-1 dhidi ya Abo Hamad na kufungwa 2-0 na Haras El Hodoud.

WAZIRI MCHENGERWA AKUTANA NA NYOTA WA ZAMANI WA COASTAL UNION ULAYA

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa akiwa na wachezaji wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Hussein Mwakuluzo (kushoto) na Abdallah Shamuni (kulia), walipokutana Jijini Leicester, England. Waziri Mchengerwa yupo Uingereza akiwa ameambatana na msafara wa Tanzania unaoshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola Jijini Birmingham, wakati Mwakuluzo aliyecheza pia timu ya taifa enzi zake miaka ya 1980, kama Shamuni ambaye ni baba wa mchezaji wa Taifa Stars, Adi Yusuf  wote kwa saaa wanaishi Uingereza.

ZUCHU KUTUMBUIZA SIMBA DAY AGOSTI 8

Image
MWANAMUZIKI nyota wa kike Tanzania, Zuhura Othman Soud atatumbuiza kwenye tamasha la Simba Day Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Leo klabu ya Simba imezindua rasmi Wiki ya Simba kuelekea Simba Day Jumatatu ya wiki ijayo, shughuli ambayo imefanyika viwanja vya Mbagala Zakheim Jijini Dar es Salaam.

BANGALA NA DJUMA SHABANI WAONGEZA MIKATABA YANGA HADI 2024

Image
MCHEZAJI Bora na kiungo Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita, Mkongo Yannick Bangala ameongeza mkataba wa kuendelea kufanya kazi Jangwani hadi mwaka 2024. Aidha, Mkongo mwenzake, beki Djuma Shabani naye ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea na majukumu Yanga hadi mwaka 2024. Katika Hatua nyingine, Yanga imeunda Kamati ya Wiki ya Mwananchi yenye wajumbe saba, akiwemo Meneja wa Idara ya Michezo ya Azam Media Limited, Tina Korosso.

SENZO MAZINGISA AAMUA KUONDOKA YANGA SC

Image
KLABU ya Yanga imekubali ombi la Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wake Mkuu, Senzo Mazingiza Mbatha kutoongeza mkataba mpya wa kuendelea na kazi Jangwani baada ya huu wa sasa kumalizika kesho Julai 31. Taarifa iliyotolewa na Yanga leo imesema kwamba,  Kamati ya Utendaji imemteua Wakili Simon Patrick kuwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo.

TAIFA STARS YASONGA MBELE KUFUZU CHAN

Image
TANZANIA imesonga mbele katika kuwania tiketi ya Fainali za CHAN mwakani baada ya ushindi wa 2-1 leo dhidi ya Somalia Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na Abdul Sopu dakika ya 34 na Dickson Job kwa penalti dakika ya 64, wakati la Somalia limefungwa na Farhan Ahmed dakika ya 47. Taifa Stars inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mechi ya kwanza hapo hapo Benjamin Mkapa.

SIMBU ASHINDA MEDALI YA FEDHA MARATHONI MADOLA

Image
MWANARIADHA Alphonse Simbu wa Tanzania ameshinda Medali ya Fedha kwenye mbio ndefu, Marathoni leo kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola Jijini, Birmingham, England. Simbu amemaliza nyuma ya Vincent Kiplangat ambaye ameipatia Medali ya kwanza kabisa ya Dhahabu Uganda, huku Michael Githae wa Kenya akichukua Medali ya Shaba.

MAYELE APIGA HAT TRICK YANGA YASHINDA 5-1 KIGAMBONI

Image
MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 5-1 katika mchezo wa Kirafiki dhidi ya Transit Camp Ijumaa Uwanja wa Avic Town, Somangira nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Yanga SC yamefungwa na washambuliaji wake Wakongo, Fiston Kalala Mayele matatu, Heritier Makambo na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki moja kila mmoja.

AZAM FC NAYO YAZINDUA JEZI ZA MSIMU MPYA

Image
KLABU ya Azam FC imezindua jezi zake mpya kuelekea msimu ujao ambazo ni nyumbani, ugenini na ya tatu ambayo ni ya ziada.

HIZI HAPA JEZI ZA MSIMU MPYA YANGA SC

Image
HIZI ndiyo jezi za msimu mpya za mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga SC zilizozinduliwa leo Jijini Dar es Salaam.

BARBARA ATUA NIGERIA KUKAMILISHA USAJILI WA KIUNGO MPYA

Image
MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez (kulia) akiwa na kiungo Mnigeria, Nelson Esor-Bulunwo Okwa (28) nchini Nigeria ambako amekwenda kukamilisha usajili wake ajiunge na Wekundu hao wa Msimbazi kutoka klabu ya Rivers United ya kwao.

YANGA WAPEWA SH MILIONI 100 KWA KUTWAA UBINGWA WA NCHI

Image
RAIS wa Yanga SC, Hersi Said, Mtendaji Mkuu, Senzo Mbatha na baadhi ya wachezaji wakipokea mfano wa hundi ya Sh. Milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa, Tarimba Abbas kama zawadi baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara  msimu wa 2021/22.

AZAM FC YACHAPWA 1-0 NA WADI DEGLA

Image
TIMU ya Azam FC imechapwa 1-0 na wenyeji, Wadi Degla katika mchezo wa kirafiki leo kwenye kambi yake ya kujiandaa na msimu ujao huko Gunna nchini Misri.

SIMBA YACHAPWA 2-0 NA HARAS EL HODOUD MISRI

Image
TIMU ya Simba leo imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Haras El Hodoud katika mchezo wa kirafiki kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya mjini Ismailia. Huo unakuwa mchezo wa tatu wa kujipima nguvu kwa Simba katika wiki ya pili ya kambi yao mjini humo, baada ya awali kutoka sare ya 1-1 na Ismailia kabla ya kushinda 6-0 dhidi ya Abo Hamad.

SPORTS PESA YAMWAGA. NEEMA NZITO YANGA SC

Image
KLABU ya Yanga imesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya Sport Pesa Tanzania wenye thamani ya Sh. Bilioni 12.335 kwa miaka mitatu.

BEKI WA SIMBA QUEENS AJIUNGA NA KLABU YA MÉXICO

Image
BEKI wa kati wa Simba Queens, Julietha Singano ameijiunga na klabu ya FC Juárez ya Mexico kwa kujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF).

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA GORDIAN MAPANGO

Image
 

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA AHMAD AMASHA

Image
 

AZAM ACADEMY WATWAA UBINGWA WA LIGI Y U17

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Pan African kwenye mchezo wa mwisho leo Jijini Dar es Salaam. Azam Academy imemaliza na pointi 34 baada ya kushinda mechi 11 na kutoa droo moja, mbele ya Simba waliomaliza nafasi ya pili kwa pointi zao 21 sawa na JMK Park wa tatu, wakati Yanga iliyomaliza na pointi 19 ni ya nne.

MAMBO YA KIPRE JUNIOR MAZOEZINI AZAM FC KAMBI YA MISRI

Image
NYOTA mpya wa Azam FC, Kipre Junior kutoka Ivory Coast akimiliki mpira kwenye mazoezi ya timu hiyo katika kambi ya kujiandaa na msimu huko Gunna nchini Misri.

SAKHO APIGA MBILI, SIMBA YASHINDA 6-0 MISRI

Image
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa 6-0 dhidi ya wenyeji, Abo Hamad ya Misri katika mchezo wa kirafiki mjini Ismailia nchini Ismailia usiku wa Jumamosi. Mabao ya Simba yamefungwa na mshambuliaji mpya, Mzambia Moses Phiri, kiungo Jonas Mkude, mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere, winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho mawili na kiungo mkongwe Erasto Edward Nyoni. Huo ulikuwa mchezo wa pili wa Simba chini ya kocha mpya, Mserbia Zoran Manojilovic ‘Maki’ katika kambi yake ya Misri kujiandaa na msimu mpya, baada ya awali kutoka sare ya 1-1 na Ismailia.

AZIZ KI MAZOEZINI YANGA IKIJIANDAA NA MECHI YA NGAO AGOSTI 13

Image
KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki (kulia) akiwa na winga chipukizi Mtanzania, Dennis Nkane kwenye mazoezi ya Yanga jana Uwanja wa Avic Town, Somangira, Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani, Simba Agosti 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

SAKHO ALIVYOPOKEWA NA TUZO YAKE KAMBINI SIMBA

Image
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Pape Ousmane Sakho alivyopokewa kambini  jijini Ismailia, Misri akitokea nchini Morocco ambako ameshinda Tuzo ya Bao Bora la Mwaka Afrika.

TANZANIA YACHAPWA 3-2 MALAWI SOKA LA UFUKWENI AFRIKA

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania yansoka la Ufukweni imechapwa mabao 3-2 na wenyeji Malawi leo mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika zitakazofanyika baadaye mwaka huu nchini Msumbiji.  Mechi ya marudiano itachezwa Dar es Salaam kati ya Agosti 5 na 7 na mshindi wa jumla atasonga mbele.

TAIFA STARS YAICHAPA SOMALIA 1-0 KUFUZU CHAN

Image
BAO pekee la kiungo mshambuliaji mpya wa Azam FC, Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ limeipa Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Somalia katika mchezo wa kwanza wa kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Sopu aliyeng'ara akiwa na Coastal Union ya Tanga misimu mitatu iliyopita baada ya awali kuchezea Ndanda FC ya Mtwara na Simba ya Dar es Salaam, alifunga bao hilo dakika ya 46 akimalizia krosi ya beki wa Yanga, Kibwana Shomari kutoka kulia. Timu hizo zitarudiana Jumamosi ijayo Uwanja wa Mkapa, Tanzania wakiwa wenyeji kwenye mbio hizo za CHAN ya mwakani Algeria.

SIMBA YAMTAMBULISHA BEKI WA KATI MUIVORY COAST

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha rasmi beki Muivory Coast, Mohamed Outtara kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao. Ouattara, mwenye umri wa miaka 23, anajiunga na Simba akitokea klabu ya Al-Hilal Omdurman ya Sudan aliyojiunga nayo mwaka  2020.

YANGA SC YAMKINGIA KIFUA HAJI MANARA ADHABU YA TFF

Image
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema Msemaji wake, Haji Sunday Manara hajatendewa haki na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF$ kwa kufungiwa miaka miwili sambamba na kutozwa faini ya Sh. Milioni 20.