Posts

Showing posts from October, 2022

DUBE TENA, AZAM FC YASHINDA 1-0 TENA LIGI KUU DAR

Image
BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 55 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 17 katika mchezo wa tisa na kusogea nafasi ya tatu, wakati Ihefu SC inabaki na pointi zake tano za mechi tisa nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka.

MBEYA CITY YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 UHURU

Image
WENYEJI, Ruvu Shooting wamechapwa 1-0 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la Mbeya City limefungwa na Hassan Nassor Maulid dakika ya 17 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 12 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya 10, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 10 za mechi 10 sasa nafasi ya 11.

SIMBA SC 5-0 MTIBWA SUGAR (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA QUEENS YACHAPWA 1-0 NA WAARABU MOROCCO

Image
TIMU ya  Simba Queens imeanza vibaya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji FAR Rabat katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Prince Moulay Hassan Jijini Rabat nchini Morocco. Simba Queens watateremka tena dimbani Novemba 2 kumenyana na Determine Girls ya Liberia kabla ya kukamilisha mechi zao za Kundi hilo kwa kumenyana na Green Buffaloes ya Zambia Novemba 5.

SIMBA SC YAIFUMUA MTIBWA SUGAR PUNGUFU 5-0 DAR

Image
WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo, Mzawa Muzamil Yassin dakika ya 38, Msenegal Pape Ousmane Sakho mawili dakika ya 48 na 90 na ushei na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri mawili pia, dakika ya 63 na 73. Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi nane, wakati Mtibwa Sugar inayobaki na pointi zake 15 za mechi 10 wanashukia nafasi ya nne. Dalili mbaya kwa Mtibwa Sugar zilianza mapema tu dakika ya 37 baada ya kipa wake wa kwanza, Farouk Shikaro kuumia na kushindwa na kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Hamadi Kadedi. Hali ikawa mbaya zaidi baada ya walinzi wake wawili wa kati kutolewa kwa kadi nyekundu wote mmoja kila kipindi, Mkongo Paschal Kitenge dakika ya 41 na Cassin Ponera d

NGORONGORO YAANZA VIBAYA KUWANIA TIKETI YA AFCON U20

Image
TIMU Taifa ya Tanzania chini ya Umri wa Miaka 20, Ngorongoro Heroes jana ilianza vibaya michuano ya kuwania kufuzu AFCON U20 baada ya kuchapwa 2-0 na Uganda katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Al Hilal nchini Sudan. Ngorongoro Heroes itateremka tena dimbani Novemba 2 kumenyana na Ethiopia kukamilisha mechi zake za Kundi B ikihitaji lazima ushindi mzuri ili iende Nusu Fainali. Ikumbukwe Kundi A linaundwa na Djibouti, Burundi, Sudan Kusini na Sudan.

BRIGHTON YAIFUMUA CHELSEA 4-1 AMEX

Image
WENYEJI, Brighton & Hove Albion jana waliiadhibu Chelsea kwa kuitandika mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Amex, Mabao ya Brighton yamefungwa na Leandro Trossard dakika ya tano, kabla ya wachezaji wawili wa Chelsea kujifunga Ruben Loftus-Cheek dakika ya 14 na Trevoh Chalobah dakika ya 42, huku bao la nne la wenyeji likifungwa Pascal Gross dakika ya 90 na ushei, wakati la kufutia machozi la The Blues lilifungwa na Kai Havertz dakika ya 48. Kwa matokeo hayom, Brighton inafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya nane, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 21 katika nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 12. 

LIVERPOOL YAPIGWA 2-1 NA LEEDS UNITED PALE PALE ANFIELD

Image
TIMU ya Leeds United jana imewachapa wenyeji Liverpool mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Anfield, Mabao ya Leeds jana yalifungwa na Rodrigo dakika ya nne na Crysencio Summerville dakika ya 89, wakati la Liverpool limefungwa na Mohamed Salah dakika ya 14. Kwa ushindi huo, Leeds wanafikisha pointi 12 katka mchezo wa 12 na kujivuta nafasi ya 15, wakati Liverpool baada ya kichapo hicho cha kwanza nyumbani tangu mwaka 2017, wanabaki na pointi zao 16 za mechi 12 pia nafasi ya tisa.

GEITA GOLD 1-1 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

YANGA SC YAICHAPA GEITA GOLD 1-0 KIRUMBA NA KUWEKA POZI KILELENI

Image
BAO la penalti la winga Mghana, Bernard Morrison dakika ya 45 na ushei limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Yanga inafikisha pointi 20 katika mchezo wa nane na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya Namungo FC na Mtibwa Sugar ambazo pia zimecheza mechi tisa kila timu.

AZAM FC YALETA KOCHA MPYA WA MAZOEZI YA VIUNGO

Image
MTUNISIA. Dk. Moadh Hiraoui amewasili kuwa Kocha mpya wa mazoezi ya viungo katika klabu ya Azam FC. Dk. Moadh Hiraoui. mwenye wasifu mkubwa, amewahi kufanya kazi na vigogo wa Afrika, Esperance ya Tunisia na Al Hilal ya Sudan. Hiraoui mwenye PhD ya Sayansi ya Michezo na Afya, pia amewahi kufanya kazi Falme za Kiarabu (UEA) katika timu ya Dibba Al-Hisn na Hajer FC ya Saudi Arabia. Tayari mtaalamu huyo ameshaanza kazi, akiwa amesaini mkataba wa mwaka mmoja, wenye kipengele cha kuongeza. Moadh, anachukua nafasi ya Mikel Guillen, ambaye kwa sasa hayupo tena na klabu.

SIMBA SC YAPATA MKATABA WA BIMA MILIONI 250 KWA MWAKA

Image
KLABU ya Simba SC imeigia mkataba wa miaka miwili wa bima ya afya kwa wachezaji, benchi la ufundi na menejimenti ya Simba na kampuni ya bima ya Moassurance kwa kipindi miaka miwili wenye thamani ya Sh. Milioni 250. 

PARIMATCH YAFANYA MABORESHO, YAJA KIBABE NA MFUMO MPYA

Image
KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha Parimatch imefanya maboresho makubwa katika tovuti yao ya kubashiri, ambayo kwa sasa itawawezesha wateja wao kusuka mikeka yao na ku-share kwa marafiki zao huku wakiwa wanatumia intaneti kidogo wakati wa kuperuzi na kasi kubwa. Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa Parimatch Tanzania,  Ismael Mohamed  wakati alipokuwa akizundua rasmi jukwaa hilo la kubashiri mtandaoni kupitia  PARIMATCH  na kusema kwamba imekuwa ni desturi yao kusikiliza maoni ya wateja wao kila mara na kuamua kuyafanyia uamuzi ili kusudi waweze kuwapatia kitu kilichokuwa bora wateja wao ambao hutumia muda wao ziada kujiburudisha akili zao na Parimatch.   “Tumefanya mabadiliko mazuri, tumerekebisha mambo mengi. Katika kipindi hiki ambacho tunaelekea katika michuano mikubwa ya Kombe la Dunia sisi kama Parimatch, tumeona wateja wetu wanastahili kupata kitu kizuri chenye speed ya uhakika ili wanapokuwa wanapata burudani basi na beti zao ziendane na kasi ya mchezo”, amesema Ismael.   “Li

AZAM FC 1-0 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

RONALDO AREJEA NA KUFUNGA MAN U YASHINDA 3-0 ULAYA

Image
TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Hatua ya Mtoano ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Sheriff Tiraspol katika mchezo wa Kundi E usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Manchester United yamefungwa na beki Diogo Dalot dakika ya 44 na washambuliaji, Marcus Rashford dakika ya 65 na Cristiano Ronaldo dakika ya 81 na kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 12, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tatu na vinara, Real Sociedad. Mashetani hao Wekundu watahitaji kushinda mabao mawili bila kuruhusu bao dhidi ya timu ya LaLiga, Real Sociedad katika mchezo wa mwisho ili kumaliza kileleni mwa Kundi lao, E.

AZAM FC YAIPIGA SIMBA 1-0 BAO PEKEE LA PRINCE DUBE

Image
BAO la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 36 limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 14 katika mchezo wa nana na kusogea nafasi ya nne,  ikizidiwa wastani wa mabao tu na Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi. Mabingwa watetezi, Yanga wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 17 za mechi saba, wakifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 za mechi tisa.

YANGA 1-0 KMC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

YANGA YAICHAPA KMC 1-0 BAO PEKEE LA FEI TOTO

Image
BAO la kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah dakika ya 80 limetosha kuipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 17 katika mchezo wa saba na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 za mechi tisa na Simba pointi 14 za mechi sita. KMC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 13 za mechi tisa nafasi ya sita.

MWENYEKITI DRFA ATOA FEDHA ZA MAENDELEO YA SOKA ILALA

Image
MWENYEKITI wa Chama  cha Soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya ametoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya mpira wa miguu mkoa wa Ilala. Alitoa fedha hizo wakati alipokuwa anafunga kozi ya makocha CAF diploma D iliyokuwa ikiendeshwa makao makuu ya Chama cha soka mkoa wa Ilala (IDFA). Aliwataka makocha hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kupitia kozi hiyo ambayo ilishirikisha makocha 30 ambalo kati yao Wanaume ni 26 na Wanawake 4. "Ninawapongeza washiriki wote ambao mmehitimu kozi hii naamini mtakwenda kufanya kazi kwa bidii Mkufunzi aliyewafundisha sina wasi wasi naye,alisema Nyambaya. Kwa upande wa Mkufunzi wa kozi hiyo Mohamed Tajdeen  alisema kuwa kozi hiyo itawasaidia washiriki hao kufundisha timu za kuwanna Ligi Daraja la 3 na Ligi Daraja la 4. "Kozi hii inawajengea uwezo wa kufundisha mpira  na kwa wale watakaofaulu watakuwa na uwezo wa kujiunga na mafunzo ya CAF diploma C,alisema Tajdeen. Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku

GEITA GOLD YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 UHURU

Image
TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Geita Gold leo yote yamefungwa na viungo wa zamani wa Yanga SC, Juma Mahadhi dakika ya nane na Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 68, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Abalkassim Suleiman dakika ya 20. Kwa matokeo hayo, Geita Gold imefikisha pointi 13 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 10 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi tisa.

POLISI TANZANIA YAACHANA NA KOCHA WAKE MFARANSA

Image
KLABU ya Polisi Tanzania imeachana na kocha wake Mrundi, Joslin Sharrif Bipfubusa baada ya miezi mitatu tu tangu ajiunge na timu hiyo Julai 26. Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Polisi Tanzania kuchapwa 2-0 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kwa ujumla mwenendo wa Polisi haukuwa mzuri chini ya Bipfubusa, kwani katika mechi tisa ilizocheza hadi sasa imeambulia pointi tano tu kufuatia kushinda moja na sare mbili, huku nyingine zote sita ikipoteza.

NEEMA SIMBA QUEENS, YAPATA UDHAMINI MNONO WA M-BET

Image
TIMU ya Simba Queens leo imeingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiriki ya M-Bet wenye thamani ya Tsh. bilioni moja. Simba Queens itaanza kutumia jezi zenye nembo ya M-Bet kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.

CHELSEA YASONGA MBELE LIGI YA MABINGWA

Image
TIMU ya Chelsea imefanikiwa kufuzu Hatua ya Mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Red Bull Salzburg katika mchezo wa Kundi E usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena mjini Wals-Siezenheim nchini  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Mateo Kovacic dakika ya 23 na Kai Havertz dakika ya 64, wakati la Red Bull Salzburg limefungwa na Junior Adamu dakika ya 49. Kwa matokeo hayo, Chelsea inafikisha pointi 10 na kuendelea kuongoza Kundi kwa pointi tatu zaidi ya AC Milan wanaofuatia mbele ya Red Bull Salzburg yenye pointi sita baada ya wote kucheza mechi tano.

MICHAEL HAJI DAHAKI

Image
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya  Bodi ya Ligi Luu Tanzania juzi ilikutana katika kikao kawaida Oktoba da Kuchukua Hatua kadhaa.

NAMUNGO FC YAIKANDAMIZA KAGERA SUGAR 2-1 MAJALIWA

Image
WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Lucas Kikoti dakika ya nane na Jacob Massawe dakika ya 67, wakati la Kagera Sugar limefungwa na Mbaraka Yussuf dakika ya 45 na ushei. Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 14 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake nane za mechi tisa sasa nafasi ya 13.

MTIBWA SUGAR YAICHAPA DODOMA JIJI 1-0 LITI

Image
BAO pekee la Charles Ilamfya dakika ya 60 limetosha kuipa Mtibwa Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC Uwanja wa LITI mjini Singida. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 15 katika mchezo wa tisa na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ikizizidi pointi moja moja Simba na Yanga ambazo hata hivyo zimecheza mechi sita kila moja. Kwa upande wao, Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao tano za mechi nane wakiendelea kushika mkia.

PRISONS YAIKANDAMIZA POLISI 2-0 SOKOINE

Image
WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Jeremiah Juma kwa penalti dakika ya tano na Samson Mbangula dakika ya 45 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 12 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya sita. Kwa upande wao Polisi Tanzania wanabaki na pointi zao tano baada ya kucheza mechi tisa sasa ikihamia mkiani mwa Ligi Kuu.

SINGIDA STARS YAIZIMA IHEFU 1-0 LITI

Image
BAO pekee la Shafiq Batambuze dakika ya 17 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Kwa ushindi huo, Big Stars inafikisha pointi 14 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya tatu, ikizidiwa tu wastani wa mabao na Simba na Yanga, ambazo hata hivyo zimecheza mechi sita kila timu. Kwa upande wao, Ihefu SC wanabaki na pointi zao tano za mechi nane pia katika nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16.

DABODABO YA 888 BET YAENDELEA KUZALISHA WASHINDI

Image
KWA  wiki  ya  pili  sasa   kampuni   ya   michezo   ya kubahatisha  888 bet  imeendelea   kuonesha   kuwa   ina   nia ya   kuendelea   kuwapa   fursa   watanzania   kupitia   michezo ya   kubashiri   kwa   kuwazawadia   washindi   wengine   wa wiki  ya  pili  ya   droo   ya   Dabodabo   pikipiki ,  runinga pamoja   na   simu   tatu . Droo   hiyo   ya   dabodabo   inategemea   kuendelea kutunuku   washindi   zawadi   hizo   za   kila  wiki  kwa  wiki  sita ,  ambapo   kwa  wiki  ya   saba   mshindi   mmoja atajinyakulia   zawadi   kubwa   ya   kitita  cha  milioni   mia moja . “ Hii   ni   kampuni   pekee   ambayo   inakupa   ushindi   kwa kuweka   mkeka   wako   tu ,  haijalishi   kama   umetiki  au  haujatiki ,  hakutakua   na   nafasi   kama   hii   tena .”,  Alisema  Oka Martin,  mmoja   wa   wachekeshaji   wa kundi  la  Wanyabi   ambao   ni   mabalozi   wa   kampuni   hiyo wakiwa   wanatangaza   washindi   wa  wiki  ya  pili  ya Dabodabo .  “ Niwasisitize   wadau   wote   wa