WAOGELEAJI 63 WA TANZANIA KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA

WAOGELEAJ 63 wa timu ya taifa ya Tanzania (Tanzanites na Diamond)  kesho  (Alhamis Novemba 17) wanaanza kampeni ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kanda ya tatu Afrika kwenye bwawa la klabu ya Dar es Salaam Gymkhana jijini.
Mashindano hayo yataanza saa 2.00 asubuhi na kushirikisha waogeleaji wengine 200 kutoka nchi nyingine 10 za bara la Afrika.
Nchi hizo ni Uganda ambayo itawakilishwa na waogeleaji 45, Burundi (10), Rwanda (14), Eritrea (5), Ethiopia (7), Zambia (23), Afrika Kusini(18), Sudan (14) na Djibouti ambayo itawakilishwa na waogeleaji  16. Pia kutakuwa na waogeleaji 48 kukamilisha jumla ya waogeleaji 263.
Waogeleaji hao watashindana katika staili tano tofauti za muogeleaji mmoja mmoja na pia kutakuwa na mashindano ya relei (relay). Jumla kutakuwa na matukio 140.
Waogeleaji wa timu ya Tanzanites  ambao  wamepewa jukumu la kuiletea sifa Tanzania katika mashindano hayo kwa upande wa wanawake ni  Bridget Heep, Maryam Ipilinga, Crissa Dillip na Lorita Borega.
Wengine ni Amylia Chali, Filbertha Demello, Aminaz Kachra, Aliyana Kachra, Lina Goyayi, Sophia Latiff, Ria Save, Natalia Ladha, Sarah Tibazarwa, Muskan Gokan na Sarah Shariff.
 Waogeleaji wanaume ni  Julius Missokia, Max Missokia, Kabeer Lakhani, George Nangale, Austin Okore, Aryan BhattBhatt, Nabeel Gahhu na Mark Tibazarwa.
Wengine ni, Peter Itatiro, Delbert Ipilinga, Ethan Alimanya, Romeo Mwaipasi, Hilal Hilal, Collins Saliboko, Mohameduwais Abdulllatif, Michael Joseph na Aaron Akwenda.
Waogeleaji wa timu ya Diamond ambao watashiriki katika mashindano hayo ni  Zainab Moosajee, Aamina Takim, Myra Makwaia, Abigail Mutungwa, Mahek Desai, Amaris Nanyaro, Catherine Maokola, Aaliya Takim, Mischa Ngoshani, Naisae Teggisa, Rahma Semizigi na Kalya Temba.
Kwa upande wa wanaume ni Kaysan Kachra, Hape Coleman, Alberto Itatiro, Luke Okore, Zac Okumu, Isaac Mukani, Enrico Barretto na Sahal Harunani.  Wengine ni  Christian Fernandes, Salman Yasser, Delhem Rashid, William Chengula, Elia Kimimba, Santo Bash,George Coleman, Nathan Kagoro, Sayi Goyayi, Elia Hangi na Revocatus Joseph.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Hadija Shebe alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kuwaomba wadau wa mchezo huo kujumuika kuipa sapoti timu ya Tanzania.

Waogeleaji wa timu ya Taifa ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA