SINGIDA YATOA SARE NYINGINE NYUMBANI 0-0 NA TABORA UNITED


TIMU ya Singida Fountain Gate imelazimishwa sare ya bila kufungana na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
Ni sare ya pili mfululizo Singida ‘ The Big Stars’ wanatoa, tena za bila mabao katika mechi mbili za mwanzo za msimu nyumbani baada ya kutoka suluhu pia na Tanzania Prisons kwenye mechi ya kwanza.
Kwa upande wao Tabora United, zamani Kitayosce leo wameokota pointi ya kwanza ya Ligi kufuatia kufungwa mabao 4-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. 


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YAAFIKI KUCHEZA ZANZIBAR MARUDIANO NA BERKANE

KYLLIAN MBAPPE NDIYE MFALME MPYA WA MABAO HISPANIA

PEDRO AIPOKONYA TONGE MDOMONI INTER MILAN, 2-2 NA LAZIO