Posts

Showing posts from March, 2024

MAN CITY NA ARSENAL HAKUNA MBABE, 0-0 ETIHAD

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wametoa ya bila mabao na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Matokeo hayo yanaifanya Manchester City ifikishe pointi 64, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Arsenal na wote wakiwa nyuma ya Liverpool yenye pointi 67 kufuatia timu zote kucheza mechi 29.

LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUICHAPA BRIGHTON 2-1 ANFIELD

Image
WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool. Brighton & Hove Albion walitangulia kwa bao la mshambuliaji Muingereza mwenye asili ya Ghana, Danny Welbeck dakika ya pili, kabla ya Liverpool kutoka nyuma kwa mabao ya washambuliaji wake hodari, Mcolombia Luis Díaz dakika ya 27 na   Mmisri Mohamed Salah dakika ya 65. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 67 katika mchezo wa 29 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tatu zaidi ya Arsenal inayofuatia ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Brighton & Hove Albion inabaki na pointi zake 42 za mechi 29 nafasi ya tisa.

MANCHESTER UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 KWA BRENTFORD

Image
TIMU ya Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brentford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Gtech Community mjini Brentford, Middlesex. Manchester United walitangulia kwa bao la Mason Mount dakika ya  90'+6, kabla ya Kristoffer Ajer kuisawazishia Brentford dakika ya  90'+9. Kwa matokeo hayo, Manchester United inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 29, ingawa inabaki nafasi ya sita, wakati Brentford inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 30 na kusogea nafasi ya 15.

CHELSEA YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA BURNLEY PUNGUFU STAMFORD BRIDGE

Image
WENYEJI, Chelsea FC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Burnley FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Mabao ya Chelsea leo yote yamefungwa na kiungo mshambuliaji. Cole Palmer kwa penalti dakika ya 44 na dakika ya 78 akimalizia pasi ya nyota mwenzake wa England, mshahara Raheem Sterling. Kwa upande wao Burnley FC mabao yao yamefungwa na Joshua Cullen dakika ya 47 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake, Joshua Brownhill na beki Dara O'Shea dakika ya 81 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao lao la kwanza. Burnley FC ilimaliza pungufu baada ya beki wake Mfaransa, Lorenz Assignon kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 40 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano. Ikawa siku mbaya zaidi kwao baada ya Kocha wake pia, Vincent Kompany kutolewa pia kwa kadi nyekundu baada ya kutofautiana kauli na waamuzi. Matokeo hayo yanaifanya Chelsea ifikishe pointi 40 katika mchezo wa 28 na kusogea nafasi ya 11, wakati  Burnley inafikisha pointi 18

DIARRA, AZIZ KI, AUCHO NA PACOME WAMEFANYA MAZOEZI LEO JIONI KIGAMBONI

Image
KIPA Mmali, Djigui Diarra na viungo, Mburkinabe Stephane Aziz Ki, Mganda Khalid Aucho na Muivory Coast Peadoh Pacome Zouazoua wote wamefanya mazoezi jioni ya leo Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kuekelea mchezo wa dhidi ya Mamelodi Sundowns. Leo mchana Kocha Muargentina wa Yanga SC, Miguel Ángel Gamondi akielezea hofu yake juu ya wachezaji hao akisema hajui kama atawatumia kwa sababu hadi leo asubuhi walikuwa hawajarejea kutoka kwenye majukumu yao ya timu za taifa. Pamoja na wawili hao, Gamondi pia alithibitisha atawakosa nyota wake wanne, mabeki Kibwana Shomari, Kouassi Attohoula Yao (Ivory Coast)na viungo Peadoh Pacome Zouazoua (Ivory Coast) na Khalid Aucho (Uganda) ambao wote ni majeruhi. Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kesho kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria. Mar

YANGA KUIVAA MAMELODI BILA DIARRA, YAO, AUCHO WALA PACOME

Image
KOCHA Muargentina wa Yanga SC, Miguel Ángel Gamondi amethibitisha katika mchezo wa kesho dhidi ya Mamelodi Sundowns atawakosa nyota wake watatu, mabeki Kibwana Shomari, Kouassi Attohoula Yao (Ivory Coast)na viungo Peadoh Pacome Zouazoua (Ivory Coast) na Khalid Aucho (Uganda) ambao wote ni majeruhi. Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Miguel Ángel Gamondi pia hana uhakika wa kuwatumia kipa Djigui Diarra (Mali) na kiungo Stephane Aziz Ki (Burkina Faso) katika mchezo huo kwa sababu hadi mchana wa leo walikuwa hawajarejea nchini kutoka kwenye majukumu ya timu zao za taifa. “Natarajia kuwakosa baadhi ya wachezaji wangu nyota. Siwezi kuhatarisha afya za wachezaji ambao bado hawana utimamu wa kimwili. Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuwakosa wachezaji watatu hadi wanne,”amesema Gamondi. Pamoja na hayo, Muargentina huyo pamoja na kuwakosa nyota hao, lakini ana imani na wachezaji wengine walio fiti baada ya manadalizi mazuri kambini Avic Town, Kigam

MAMELODI SUNDOWNS WAWASILI DAR KUIKABILI YANGA SC KESHO

Image
KIKOSI cha Mamelodi Sundowns kimewasili usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Yanga SC. Kundi liliotua jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ni la pili ambalo ndilo kubwa, baada ya kikundi cha wachezaji sita waliokuwa na timu ya taifa, Bafana Bafana kutangulia kuwasili juzi. Mamelodi Sundowns watakuwa wageni wa Yanga kesho kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria. Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Mshindi wa jumla baina ya Yanga na Mamelodi Sundwons atakutana na mshindi wa jumla katí ya Esperance ya Tunisia na ASEC Mimosas ya Ivory Coast. TAZAMA VÍDEO MAME

MWAMBA HUYU HAPA! AUCHO TAYARI KWA SHUGHULI NA MAMELODI JUMAMOSI

Image
KIUNGO Mganda wa Yanga, Khalid Aucho leo amefanya mazoezi kikamilifu kuelekea mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns Jumamosi Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Aucho aliumia kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly Machi 1 mwaka huu Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri. Katika mchezo huo, Aucho alishindwa kuendelea dakika ya 73, nafasi yake ikichukuliwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Yanga ikichapwa 1-0 bao pekee la Hussein El Shahat dakika ya 46. Wachezaji wengine waliokuwa wanasumbuliwa na maumivu, beki Kibwana Shomari, kiungo Zawadi Mauya wote wamefanya mazoezi vizuri leo - na shaka bado ipo kwa nyota wa Ivory Coast, beki Kouassi Attohoula Yao na kiungo Peodoh Pacôme Zouzoua. Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus

BENCHIKA: TUNA KAZI NGUMU MBELE YA AHLY KESHO

Image
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Mualgeria Abdelhak Benchika amesema wana kazi ngumu kesho mbele ya Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Becnhika amesema kwamba Al Ahly ni timu nzuri na yenye uzoefu mkubwa wa michuano hiyo wao wakiwa wanashikilia taji hilo.  "Tuna kazi kubwa ya kwenda kufanya ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo wa nyumbani na wachezaji wote wanalifahamu hilo," amesema Abdelhak Benchika. Kwa upande wake beki wa timu hiyo, Shomari kapombe akizungumza kwa niaba ya wachezaji amewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu ipate matokeo mazuri. "Tunaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuja kutupa nguvu muda wote wa mchezo, kwani kutokana na maandalizi tuliyoyafanya, naamini tunakwenda kupambana na kufanya vizuri kwa kupata ushindi," amesema Shomari Kapombe. Simba SC watakuwa wenyeji wa mabingwa

AL AHLY TAYARI WAPO DAR KUIKABILI SIMBA IJUMAA

Image
  KIKOSI cha Al Ahly ya Misri kimewasili mchana huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Simba SC. Mabingwa hao watetezi, Al Ahly  watakuwa wageni wa Simba Ijumaa kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 6 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo. Mshindi wa jumla katí ya Simba SC na Al Ahly atakutana na mshindi wa jumla katí ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali. Ikumbukwe timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini. GONGA KUTAZAMA VÍDEO AHLY WAKIWASILI DAR

SIMBA SC YAREJEA DAR TAYARI KUMVUA TAJI AHLY IJUMAA

Image
KIKOSI cha Simba SC kimerejea leo Jijini Dar es Salaam kutoka visiwani Zanzíbar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly. Simba iliweka kambi ya wiki moja visiwani Zanzíbar kujiandaa na mechi hiyo itakayofanyika Ijumaa kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana Ijumaa ya wiki ijayo, Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya TP Mazembe na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali. Ikumbukwe timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

BEKI WA ZAMANI SIMBA NA YANGA, RAMAZANI WASSO AFARIKI DUNIA

Image
BEKI wa zamani wa Kimataifa wa Burundi, Ramazani Wasso amefariki dunia leo kwa Bujumbura nchini Burundi baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda. Wasso alijiunga na Simba SC mwaka 2001 na alikuwemo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichoitoa kwa penalti Zamalek ya Misri baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2003. Wasso alihamia kwa watani, Yanga mwaka 2004 baada ya kuwahadaa Simba anakwenda Ubelgiji kucheza soka ya kulipwa, ingawa mwaka 2007 alirejea Msimbazi na kucheza hadi 2009 akahamia Coastal Unión ya Tanga kumalizia soka yake. Mungu ampumzishe kwa amani Ramazani Wasso. GONGA KUTAZAMA MAHOJIANO YA WASSO NA BIN ZUBEIRY ENZI ZA UHAI WAKE 

YANGA NA MAMELODI SUNDOWNS MACHI 30 NI ‘MUDA DAY’ MTAMBO WA MABAO JANGWANI

Image
KLABU ya Yanga imeamua mchezo wake wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns Machi 30 Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam utapewa heshima ya kiungo wao mzawa, Mudathir Yahya Abbas ‘Muda Day’. Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Shaaban Kamwe amesema kwamba tayari Mudathir Yahya na wachezaji wengine wawili, beki Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na mshambuliaji, Clement Francis Mzize waliokuwa na timu ya taifa nchini Azebairjani wamerejea na kujiunga na timu. Kuhusu wachezaji wanaosumbuliwa na maumivu, Kamwe amesema beki Kibwana Shomari, viungo Zawadi Mauya na Mganda Khalid Aucho wanaendelea vizuri na mazoezi na mashaka bado yapo kwa nyota wa Ivory Coast, beki Kouassi Attohoula Yao na kiungo Peodoh Pacôme Zouzoua. Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya Machi 30 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria. Mara ya mwisho timu h

SIMBA SC YATOZWA FAINI KWA VITENDO VYA USHIRIKINA

Image
KLABU ya Simba SC imetozwa faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la mashabiki wake kuingia uwanjani na kwenda golini kuchimba kutoa vitu, ambayo imetafsiriwa ni imani za Kishirikina. Tukio hilo lilifanyika katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya Simba SC na Mashujaa FC ya Kigoma Machi 15 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar Salaam ambao Wekundu hao wa Msimbazi walishinda 2-0. GONGA HAPA KUSOMA TAARIFA ZAIDI

NYONI NA ULIMWENGU WAFUTIWA KADI NYEKUNDU YA KIRUMBA

Image
BEKI wa Namungo FC, Erasto Edward Nyoni na mshambuliaji wa Singida Fountain Gate, Thomas Emmanuel Ulimwengu wamefutiwa kadi nyekundu waliyoonyeshwa katika mchezo baina ya timu zao Machi 16 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Namungo FC waliibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mechi hiyo, kabla ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kupitia upya taarifa na matukio ya mchezo huo na kufuta adhabu ya Nyoni na Ulimwengu. GONGA HAPA KUSOMA TAARIFA ZAIDI

MSEMAJI WA SERIKALI MATINYI AFAFANUA KAULI YA WAZIRI NDUMBARO MECHI ZA SIMBA NA YANGA

Image
MKURUGENZI wa Idara ya Habari, MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro kwamba Shabiki atakayekwenda uwanjani kutazama mechi za Kimataifa za Simba na Yanga anapaswa kuvaa jezi za Simba au Yanga, kinyume na hapo atalazimika kuwa  na Hati ya kusafiria  ya Nchi ambayo klabu anayoishangilia inatokea au vinginevyo hatoruhusiwa kuingia uwanjani. Msemaji Mkuu katika ufafanuzi wake leo Machi 24, 2024 katika Mkutano wake na Vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam amesema Waziri alikuwa anahamasisha  uzalendo wa timu na hakumaanisha kuwa kweli watu watazuiliwa kushangilia timu hizo bila Hati ya kusafiria. “Alichozungumza Waziri (Dk. Ndumbaro) alikuwa anahamasisha uzalendo wa Timu zetu na katika lugha zetu za michezo waandishi wa michezo tunafahamu, Mimi niliwahi kuwa wakati fulani Mwandishi wa Michezo na niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) sisi tukizu

ITABA ACHAPWA KWA TKO RAUNDI YA KWANZA ENGLAND

Image
BONDIA Hussein Itaba wa Tanzania usiku wa jana amepigwa na mwenyeji, Liam Cameron kwa Technical Knockout (TKO) Raundi ya kwanza katika pambano la Raundi sita uzito wa Light Heavy ukumbi wa Sheffield Arena, Sheffield, England. Katika pambano hilo lililoandaliwa na promota maarufu, Muingereza Eddie Hearn - refa Reece Carter wa Wales alimaliza mchezo baada ya Hussein Itaba kuangushwa mara mbili katika Raundi hiyo ya kwanza. Itaba jana alipigana pambano la pili ndani ya siku nane Uingereza, baada ya Machi 16 kupoteza kwa pointi mbele ya mwenyeji mwingine, Thomas O'Toole ukumbi wa Salthill Leisureland Complex, Galway nchini Ireland pambano lililondaliwa na Kampuni ya MHD Promotions. Baada ya kupigana vizuri siku hiyo, MHD Promotions wakavutiwa na Itaba na kumuumganishia pambano la jana.

AZAM FC YAWACHAPA ZIMAMOTO 1-0 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI

Image
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Zimamoto ya Zanzíbar katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na mawinga wake hatari, Muivory Coast Kipre Tiagori Emmanuel Junior Zunon dakika ya 10 na Iddi Suleiman Nado kwa penalti dakika ya 59. Kwa upande wao Zimamoto bao lao pekee la katika mchezo huo limefungwa na mshambuliaji Ibrahim Hamad Ahmada ‘Hilika’ dakika ya 28.

MENEJA AIELEZA MAHAKAMA MWANAMUZIKI LAMECK DITTO AMEKOSESHWA SH. BILIONI 1.8

Image
Mwanamuziki Lameck Ditto ambaye amekoseshwa Sh 1.8bilioni  kampuni ya MultiChoice Tanzania Limited KESI ya Madai baina ya mwanamuziki Lameck Ditto na kampuni ya MultiChoice Tanzania Limited iliendela kusikilizwa jana katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam. Meneja wa mwanamuziki huyo, Rodney Rugambo aliieleza Mahakama Kuu hiyo namna ambavyo Lameck Ditto aliathirika baada ya wimbo wake wa Nchi Yangu kutumiwa na MultiChoice Tanzania Limited kwenye matangazo yao ya biashara kipindi cha Kampeni ya Afcon 2019. Akitoa ushahidi wake, mbele ya jaji mfawidhi, Salma Maghimbi jana, Rodney ambaye ni shahidi wa nne kati ya watano  katika kesi hiyo ya madai, alisema amekuwa meneja wa Ditto tangu mwaka 2016. Alisema, mwaka 2017, Ditto aliandika wimbo huo, wakilenga kuutumia kama nembo (brand) kwenye kampeni ya Kibanda umiza. "Wimbo ulipotengenezwa, tulikuwa na mpango wa kuitumia kwenye kampeni ya Kibanda umiza," alisema. Katika ushahidi wake, alidai kwenye kampeni hiyo, katika

MZIZE AWAKOSAKOSA BULGARIA, TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 BAKU

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeanza vibaya michuano ya FIFA Series baada ya kuchapwa bao 1-0 na Bulgaria leo Uwanja wa  Liv Bona Dea Arena Jijini Baku nchini Azerbaijani. Bao pekee lililoizamisha Taifa Stars limefungwa na mshambuliaji wa PAOK ya Ugiriki, Kiril Vasilev Despodov kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 52 na kumshinda kipa Kwesi Zion Pira Kawawa anayedakia Orebro Syrianska ya  Sweden. Kawawa alitokea benchi dakika ya 31 kuchukua nafasi ya Aishi Salum Manula wa Simba SC ya nyumbani aliyeumia na kushindwa kuendelea na mchezo licha ya juhudi za Daktari Lisobin Kisongo kumtibu. Naye mshambuliaji wa Yanga, Clement Francis Mzize aliyetokea benchi dakika ya 61 kuchukua nafasi ya Kibu Dennis Prosper wa Simba alikaribia kufunga dakika ya 88 kama si shuti lake kupanguliwa na kipa Dimitar Veselinov Mitov wa St. Johnstone ya Scotland na kwenda juu kidogo ya lango. Taifa Stars itashuka tena dimbani Jumatatu kumenyana na Mongolia kuanzia Saa 10:00 jioni katika mchezo

SERIKALI YATUMIA BILIONI 2.4 KUGHARAMIA TIMU ZA TAIFA

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 Wizara kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  imetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 2.4 kugharamia Timu mbalimbali za Taifa katika mashindano ndani na nje ya nchi. Amesema hayo wakati akiwasilisha utekekezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2023/24  na Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 24/25 kwenye Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo leo Machi 22, 2024 Bungeni Jijini Dodoma. Amezitaja baadhi ya timu hizo  kuwa ni Timu ya Taifa ya ya Gofu Wanawake iliyoshiriki mashindano ya Gofu Afrika Mashariki na Kati nchini Rwanda mwezi Novemba na kuwa mshindi wa kwanza, Timu ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars) ambayo iliwezeshwa kushiriki michuano ya kufuzu  kucheza WAFCON yanayotarajiwa kufanyika  Juni, 2024 nchini Morocco, kuwezesha Timu nane ikiwemo Judo, Riadha, Mpira wa Miguu Wanawake, ngumi kriketi wanaume na Wanawake kushindana mashindano ya Mi

KARIA AKABIDHIWA JEZI ZA SIMBA NA YANGA KAMPENI YA KUZING’OA AHLY NA MAMELODI AFRIKA

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia leo amekabidhiwa jezi za Simba na Yanga kuelekea mechi za kwanza za Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo Jijini Dar es Salaam. Hii ni katika kuunga mkono agizo la Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro kwamba mashabiki wa timu hizo waungane kusapoti timu hizo za nyumbani dhidi ya wageni Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Simba SC watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali Ijumaa ya Machi 29 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Ijumaa itakayofuata Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri. Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini.

TANZANIA YAAMBULIA MEDALI TATU ZA SHABA NDONDI ALL AFRICAN GAMES

Image
MATOKEO ya kushangaza ya Majaji usiku wa jana yalimnyima Ushindi Nahodha wa Timu ya Taifa Yusuf Changalawe baada ya kupoteza kwa points katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Pita Kabeji kutoka DR Congo katika michezo ya Afrika Accra 2023 inayoendelea nchini Ghana. Ilikuwa katika uzani wa Light Heavyweight 80kg ambapo Changalawe alicheza kwa ustadi wa hali ya juu lakini cha kushangaza maamuzi ya Majaji yakampa ushindi mpinzani wake Pita Kabeji.  Matokeo hayo yamemuudhunisha sana Changalawe aliyejiwekea dhamira ya kuwa Bingwa wa Afrika katika uzani huo. Wakati huohuo bondia mwingine Musa Maregesi wa uzani wa Cruiserweight 86kg naye haikua siku nzuri kazini baada ya kupoteza pia katika hatua hio ya nusu fainali dhidi ya Kanouni O. kutoka Algeria kwa points 5-0.  Safari ya ngumi ndio imeishia hapo ambapo sasa Tanzania imejihakikishia kupata medali 3 za Shaba kutoka katika mchezo wa ngumi za Yusuf Changalawe, Musa Maregesi  na Ezra Paulo Mwanjwango. _"Hakika ni mwanzo mzuri wa

KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA AL AHLY NI SH 5,000 MACHI 29 DAR

Image
Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally akizungumza na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam. KIINGILIO cha chini katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Simba SC Ijumaa ya Machi 29 Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh. 5,000. Afisa Habari wa Simba SC Ahmed Ally ametaja viingilio vingine ni Sh. 10,000 kwa viti vya Rangi ya Chungwa, Sh. 20,000 VIP C, Sh. 30,000 VIP B, Sh. 40,000 VIP A, Sh. 200,000 Platinum na Sh. 250,000 Tanzanite. “Tunaamini viingilio hivi ni rafiki kwa kila Mwanasimba. Tunakwenda kucheza mechi dhidi ya Al Ahly, lazima tuelezane ukweli kwamba hii ni mechi ngumu kweli kweli,” amesema Ahmed. Simba SC watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali Ijumaa ya Machi 29 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Ijumaa itakayofuata Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri. Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana timu

MASHABIKI KUINGIA BURE UWANJANI YANGA NA MAMELODI MACHI 30

Image
Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe akizungumza na Waandishi wa Habari   leo Jijini Dar es Salaam . KLABU ya Yanga imesema hakutakuwa na kiingilio kwa mashabiki wa eneo la Mzunguko kwenye mchezo wa kwanza wa Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Jumamosi ya Machi 30 Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba uongozi umeamua eneo la mzunguko watu waingie bure. Aidha, Kamwe ametaja viingilio vya maeneo mengine kuwa ni Sh. 𝟏𝟎,𝟎𝟎𝟎  Kwa 𝐕𝐈𝐏 C, Sh. 𝟐𝟎,𝟎𝟎𝟎 𝐕𝐈𝐏 B na 𝟑𝟎,𝟎𝟎𝟎 kwa 𝐕𝐈𝐏 A. “Tunafahamu mechi itaisha usiku sana, kwa kuwajali mashabiki wetu na dhamira ya nchi yetu hasa kwenye sekta ya michezo Viongozi wetu wameamua jukwaa la mzunguko litakuwa bure,” amesema Kamwe. Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya Machi 30 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kur

EZRA PAUL KUREJEA NA MEDALI YA SHABA ALL AFRICAN GAMES

Image
BONDIA Ezra Paul Mwanjwango amekuwa mwanamasumbwi wa kwanza wa Tanzania kuandikwa jina lake kwenye orodha ya washindi wa Medali katika Michezo wa Afrika inayoendelea nchini Ghana. Ezra amejihakikishia Medali ya Shaba baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Andrew Chilata wa Zambia kwa points za matokeo ya kurejewa 5-2 (Bout review)  baada ya matokeo ya awali 3-2 katika uzito wa Light. Mabondia wengine wawili wa Tanzania watapanda ulingoni katika mapambano ya Nusu Fainali ambao ni Nahodha wa timu, Yusuf Changalawe atakayezipiga na Pita Kabejii wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Mussa Maregesi atakayepigana na Kanouni O. wa Algeria.

BETPAWA YATOA MABILIONI YA FEDHA KUDHAMINI TIMU ZA TAIFA ZA KIKAPU UGANDA

Image
Maafisa wa kamati ya timu za Taifa wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Uganda (FUBA), watendaji wa betPawa na wawakilishi wa timu mbili za kitaifa za mpira wa kikapu  za wanaume na wanawake wakiwa katika picha ya pamoja  baada ya sherehe ya kusaini mkataba wa udhamini. TIMU za taifa za mpira wa kikapu za  wanaume (Silverbacks) na wanawake (Gazelles) zimepata udhamini mnono kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri ya betPawa wenye thamani ya sh2.6 bilioni za Uganda, sawa n ash Bilioni 1.8 za Kitanzania. Mkataba wa udhamini huo wa miaka mitatu ulisainiwa jana kati ya maofisa wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Uganda (FUBA) na viongozi wa ngazi za juu wa betPawa. Mbali ya kugharimia timu hiyo katika michezo mbalimbali ya kimataifa, betPawa pia itagharimia kambi ya timu, usafiri, malazi, gharama za kushiriki katika mashindano mbalimbali, bifa ya afya na mambo mengine muhimu za timu hizo. Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Afisa Mkuu wa Chapa wa betPawa, Spencer Okach alis

HUSSEIN ITABA KUPIGANA PAMBANO LA EDDIE HEARN JUMAMOSI UINGEREZA

Image
Bondia Hussein Itaba atapanda tena ulingoni Jumamosi ya Machi 23 kuzipiga na Muingereza mwingine, Liam Cameron ukumbi wa Sheffield Arena, Sheffield, Yorkshire pambano linalondaliwa na promota Eddie Hearn KAMPUNI ya MHD Promotions ya Uingereza imeamua kumchukua bondia Hussein Itaba wa Tanzania baada ya kuvutiwa na uwezo wake akipigana na mwenyeji, Thomas O'Toole Jumamosi ya Machi 16 ukumbi wa Salthill Leisureland Complex, Galway nchini Ireland. Itaba alipoteza kwa pointi pambano hilo la uzito wa Light Heavy, ingawa macho ya wengi yaliona Mtanzania huyo ndiye kashinda - na baada ya mchezo huo Promota Mark Dunlop amemuambia Itaba abaki kwa ajili ya pambano lingine. Watanzania wengine wawili walipanda ulingoni siku hiyo, Tampela Maharusi akipoteza pia kwa pointi mbele ya Colm Murphy uzito wa Feather na Godfrey Paulo Kamata akapigwa kwa Technical Knockout (TKO) Raundi ya sita na Luke Keeler uzito wa Light Heavy. Wakati Maharusi na Kamata wanarejea nyumbani, Itaba amebaki Ireland

SERIKALI YASISITIZA UZALENDO SIMBA NA YANGA DHIDI YA AHLY NA MAMELODI ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amewaomba Watanzania  waziunge mkono Simba na Yanga kwenye michezo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika ili zishinde na kuiletea heshima kwa nchi.  Aidha, amewaonya baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa na tabia ya kuzipokea na kuzishangilia timu ngeni zinapokuja kucheza na timu za Tanzania waache tabia hiyo kwa kuwa inarudisha nyuma juhudi kubwa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye katika uongozi wa miaka mitatu amefanya mambo makubwa kuendeleza michezo nchini. Dk. Ndumbaro ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao mpya wa Simba SC uliopewa jina la "Simba Executive Network" ambao una lengo kukusanya fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya Klabu hiyo. "Natamani kuziona timu zote  nusu fainali, inaleta heshima kwa nchi, inaleta heshima kwa mpira wetu na vilabu vyetu,” amesis

YANGA YAANZA KUJIFUA KIGAMBONI KUIKUSANYIA NGUVU MAMELODI

Image
KIKOSI cha Yanga SC leo kimeingia kambini, Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo miwili ya nyumbani na ugenini Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Yanga watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns Jumamosi ya Machi 30 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana  Ijumaa ya Aprili 5 Uwanja wa Loftus Jijini Pretoria. Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2001 na Mamelodi Sundowns wakaitoa Yanga kwa jumla ya mabao 6-5, wakishinda 3-2 Pretoria na kutoa sare ya 3-3 Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

SIMBA SC YAINGIA KAMBINI ZANZÍBAR KUJIANDAA NA AL AHLY

Image
KLABU ya Simba leo imeingia kambini visiwani Zanzíbar kujiandaa na mechi mbili za nyumbani na ugenini Robó Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly. Simba SC watakuwa wenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa Robó Fainali Ijumaa ya Machi 29 kuanzia Saa 3:00 usiku Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya timu hizo kurudiana Ijumaa itakayofuata Aprili 5 Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo, Misri. Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana timu hizo zilikutana katika Robó Fainali ya michuano mipya, African Football League na kutoa sare ya jumla ya 3-3, wakifungana 2-2 Oktoba 20 Dar es Salaam na 1-1 Oktoba 24 Cairo, hivyo Al Ahly kwenda Nusu Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

UJENZI UWANJA MPYA WA KISASA WA KABUMBU ARUSHA MAMBO YAIVA

Image
KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa (kushoto) akisaini Mkataba na Mkandarasi China Southwest Architectural Design and Research Institute Corp. Ltd kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja mpya wa kisasa Soka Jijini Arusha katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshuhudiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dk. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela na viongozi wengine wa Wizara hiyo.  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

TANZANIA YAJIHAKIKISHIA MEDALI MBILI NDONDI ALL AFRICAN GAMES

Image
BONDIA Ezra Paul Mwanjwango wa Tanzania amefanikiwa kutinga Nusu Fainali katika Michezo ya Afrika (All African Games) inayoendelea nchini Ghana baada ya kumshinda Mujinga Frazier wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa pointi 5-0 katika uzito wa Light ukumbi wa Bukom Arena Jijini Accra. Kwa ushindi huo, Ezra Paul Mwanjwango amejihakikishia Medali ambayo inakuwa ya pili kwa timu ya taifa ya Tanzania  ya Ndondi za Ridhaa ‘Faru Weusi wa Ngorongoro’ baada ya Mussa Maregesi wa uzito wa Cruiser. Katika Nusu Fainali, Ezra Paul Mwanjwango atakutana na Andrew Chilata wa Zambia na hata kama atapoteza tayari ana uhakika wa kupata Medali ya Shaba, ambayo hutolewa kwa wana Nusu Fainali wote.

AZAM FC 2-1 YANGA SC (LIGI KUU YA NBC TZ BARA )

Image
 

FEI TOTO AFUNGA LA USHINDI AZAM YAILAZA YANGA 2-1

Image
TIMU ya Azam FC imetoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize alianza kuifungia Yanga dakika ya 10, kabla ya Azam FC kutokea nyuma kwa mabao ya winga Mgambia, Gibrill Sillah dakika ya 19 na kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah dakika ya 51. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi. Vigogo wengine katika mbio za ubingwa, Simba SC wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45 za mechi 19.

MAN UNITED YAINYUKA LIVERPOOL 4-3 NA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA

Image
WENYEJI, Manchester United wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Liverpool leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Ilikuwa mechi ya funga nikufunge ndani ya dakika 120, ambayo mwishowe shujaa ameibuka mshambuliaji kijana mdogo wa miaka 21, Muivory Coast, Amad Diallo Traoré aliyefunga bao la ushindi dakika ya 120. Katika dakika 90 timu hizo zilifungana mabao 2-2, kiungo Mscotland Scott Francis McTominay akianza que kuifungia Manchester United dakika ya 10, kabla ya kutoka nyuma kwa mabao ya kiungo Muargentina, Alexis Mac Allister dakika ya 44 na Mohamed Salah dakika ya 45'+2. Mshambuliaji Mbrazil, Antony Matheus dos Santos akaisawazishia Manchester United dakika ya 87 baada ya 71 kuchukua nafasi ya Mdenmark, Rasmus Winther Højlund. Mchezo ukaenda kwenye dakika 30 za nyongeza na Liverpool wakatangulia kwa bao la kiungo chipukizi wa Kimataifa wa England, Harvey Elliott dakika ya 105 na mshambuliaji Kimataifa wa Engl

CHELSEA YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND

Image
WENYEJI, Chelsea wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Leicester City leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Mabao ya Chelsea yamefungwa na Marc Cucurella dakika ya 13, Cole Palmer dakika ya 45'+1, Carney  Chukwuemeka dakika ya 90'+2 na  Noni Madueke dakika ya 90'+8 ,  wakati ya Leicester City yamefungwa na Axel Disasi aliyejifunga dakika ya 51 na Stephy Mavididi dakika ya 62. Haikuwa siku nzuri kwa Raheem Sterling wa Chelsea aliyekosa penalti dakika ya 27, kabla ya Callum Doyle wa Leicester City kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 73 kwa kumchezea rafu Nicolas Jackson.

MANCHESTER CITY YAICHAPA NEWCASTLE UNITED 2-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI FA

Image
TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la FA England kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United mabao ya Bernardo Silva dakika ya 13 na 31 jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mapema katika mchezo uliotangulia jana nayo Coventry City ilitinga Nusu Fainali pia kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands. Robo Fainali za mwisho za Kombe la FA England zinapigwa leo; Chelsea na Leicester City Saa 9:45 Alasiri Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London na Manchester United dhidi ya Liverpool Saa 12:30 jioni Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

SINGIDA FOUNTAIN GATE YAZINDUKA CHINI YA JULIO, YAICHAPA NAMUNGO 1-0

Image
TIMU ya Singida Fountain Gate imezinduka kwa kuichapa Namungo FC 1-0, bao pekee la beki Mghana, Nicholas Gyan dakika y 15 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Kwa ushindi huo wa kwanza ndani ya mechi 10 Singida Fountain Gate inafikisha pointi 24 na kupanda nafasi ya saba, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 23 na inashukia nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 21. Mechi tisa zilizopita, Singida Fountain Gate imepoteza sita, 0-1 Geita Gold, 0-1 Kagera Sugar, 1-3 Tanzania Prisons, 0-1 Azam FC, 0-2 Mtibwa Sugar na 1-3 Simba SC na kutoa sare tatu, 2-2 JKT Tanzania, 0-0 KMC na 1-1 Tabita United. Baada ya mechi nane za bila kushinda Singida walimfukuza Kocha Thabo Senong raia wa Afrika Kusini na mzawa, Ngawina Ramadhani akaiongoza timu kufungwa 3-1 na Simba, kabla ya kocha maarufu mzawa, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kupewa madaraka na leo wamezinduka.

UONGOZI YANGA WAKUTANA SERENA KABLA YA KUIVAA AZAM KESHO

Image
RAIS wa Yanga SC, Hersi Ally Said leo ameongoza kikao maalum cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini. Taarifa ya Yanga imesema kikao kilijadili zaidi ajenda mbili, Hatua ya mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa Klabu na Ujenzi wa Uwanja wa klabu makao makuu, Jangwani Jijini Dar es Salaam. GONGA HAPA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

BONDIA WA KWANZA WA TANZANIA ATOLEWA ALL AFRICAN GAMES

Image
AJALI ya kuvunjika mkono katika round ya mwisho ya mchezo imemuondoa katika mashindano bondia Abdallah Abdallah "Katoto" aliyekuwa akipambana na Wibshet Bekele kutoka Ethiopia. Ilikua katika bout no. 3 ya hatua ya 16 bora ya mashindano hayo katika uzani wa Fly weight 51kg ambapo Katoto alipata ajali hiyo akijiandaa kufanya shambulizi dhidi ya mpinzani wake katika round ya 3 na ya mwisho ambapo alipata ajali hio na kumlazimu mwamuzi wa mchezo kusimamisha pambano na Katoto kupelekwa moja kwa moja hospital kwa ajili ya matibabu. "Katoto tulimwahisha kwenda University of Ghana Medical Center kwa ajili ya matibabu na baada ya kuchukuliwa vipimo alionekana amevunjika sehemu ya katikati ya mkono, ila tunashukuru Mungu hali yake binafsi inaendelea vizuri ingawa hatoweza kucheza kwa kipindi cha karibuni" alisema Muhsini Mng'ola, mwalimu msaidizi wa timu ya Taifa ya ngumi. Abdallah Katoto (kulia) akiwa na Kocha Mkuu, Samuel Kapungu kwenye matibabu Kituo cha Tiba ch

CHAMA APIGA ZOTE SIMBA SC YAICHAPA MAAHUJAA 2-0

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao yote ya Simba SC leo yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama dakika ya 57 na 53 na kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 45 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi saba na mabingwa watetezi,  Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 19. Wakati Mashujaa ibaki na pointi zake 21 za mechi 21 nafasi ya 12.

NI MAN CITY NA REAL MADRID, ARSENAL NA BAYERN MUNICH ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City ya England watamenyana na mabingwa wa kihistoria, Real Madrid ya Hispania katika Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika droo ya michuano hiyo iliyopangwa leo Jijini Nyon, Uswisi, vinara wa Ligi Kuu England, Arsenal watamenyana na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich, wakati  Atletico Madrid ya Hispania itacheza na Borussia Dortmund ya Ujerumani na bingwa wa Ufaransa, PSG  ataumana na Barcelona ya Hispania pia. Nusu Fainali zitakutanisha mshindi kati ya Atletico Madrid na Borussia Dortmund na mshindi kati ya PSG na Barcelona na mshindi kati ya Arsenal na Bayern Munich dhidi ya mshindi kati ya Real Madrid na Manchester City. Mechi za kwanza za Robó Fainali zitachezwa Aprili 9 na 10 na marudiano yatafuatia April 16 na 17, wakati Nusu Fainali za kwanza ni Aprili 30 na Mei 1 na marudiano ni May 7 na 8, wakati Fainali ni Juni 1 Uwanja wa Wembley Jijini London. RATIBA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA: Arsenal vs Bayern Munich Atletico Ma