AHOUA APIGA MBILI SIMBA SC YASHINDA 3-0 MISRI


TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El-Qanah, ambayo pia inajulikana kama Canal SC au Suez Canal katika mechi ya kwanza ya kujipima umbavu kwenye kambi yake ya mjini Ismailia nchini Misri Uwanja wa Old Suez Canal.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Muivory Coast Jean Charles Ahoua mawili, dakika ya 14 na 16 na Mnigeria,  Augustine Okejepha dakika ya 120.
Simba SC imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mjini Ismailia nchini Mısri na inatarajiwa kurejea nchini mapema Agosti kwa ajili ya tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Baada ya hapo Simba itarejea Uwanja wa Mkapa Agosti 8 kumenyana na watani, Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA