AZAM FC YASAJILI KIUNGO MSHAMBULIAJI KUTOKA MALİ
KLABU ya Azam FC imemsajili kiungo mshambuliaji, Cheickna Diakite (19) kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Real Bamako ya kwao, Mali.
Huyo anakuwa mchezaji mpya wa saba kusajiliwa Azam FC kuelekea msimu ujao, wengine ni beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien.
Wengine ni Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia.
Kuna wazawa pia wawili, kiungo Nassor Saadun Hamoud kutoka Geita Gold na mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma.
Aidha, Azam FC pia imemnunua moja kwa moja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili kipa wa Kimataifa was Sudan, Mohamed Mustafa kutoka El Merreikh ya Sudan.
Hatua hiyo inafuatia kazi nzuri ya kipa huyo kufuatia kusajiliwa kwa mkopo mwezi Januari akiisaidia Azam FC kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la CRDB la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
Comments
Post a Comment