AZAM FC YASHINDA 3-0 MECHI YA KIRAFIKI MOROCCO
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Union Yacoub El Mansour ya Ligi Daraja la Tatu Uwanja wa Ziaida Complex mjini Zaida jimbo la Midelt, Drâa-Tafilalet nchini Morocco.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Msenegal, Cheikh Tidiane Sidibé, winga Mgambia Gibril Sillah na mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonco Blanco Yus.
Azam FC iliyoweka kambi Morocco kujiandaa na msimu mpya, I tashuka tena dimbani Julai 27 kumenyana na Union de Touarga, kabla ya kumenyana na Wydad Athletic Julai 29.
Kikosi kitarejea mapema Agosti tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union Agosti 8 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Comments
Post a Comment