SIMBA SC YAACHANA NA PA OMAR JOBE PIA


KLABU ya Simba SC imetangaza kuachana na mshambuliaji wa Kimataifa wa Gambia, Pa Omar Jobe baada ya miezi sita tu tangu awasili Januari mwaka huu kutoka 
Zhenis ya Kazakhstan.
Huyo anakuwa mchezaji wa tisa kuachwa Simba baada ya mabeki, Mkongo Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Msenegal, Babacar Sarr, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji, Sadio Kanoute wa Mali na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda. 
Aidha, Simba SC imesajili wachezaji wapya 13, ambao ni mabeki, Kelvin Sospeter Kijiri (24) kutoka Singida Big Stars, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya (DRC), wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
Wengine ni viungo, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma, Yusuph Ally Kagoma (28) kutoka Singida Big Stars, Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia.
Kuna washambuliaji pia, Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.
Fadlu Davids amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.
Kikosi cha Simba SC kwa sasa kipo mjini Ismailia nchini Misri ambako kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya.


Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA