TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA SUDAN MECHI YA KUFUZU CHAN MAURITANIA


TIMU ya soka ya taifa ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku wa jana imefungwa bao 1-0 na Sudan kwenye Uwanja wa Cheikha Ould Boïdiya Jijini Nouakchott katika mchezo wa kwanza wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
Bao pekee la Sudan lilifungwa na mshambuliaji wa Al Hilal, Mohamed Abdelrahman Yousif Yagoub Al Gharbal dakika ya 23 na timu hizo zitarudiana Jumapili ya Novemba 3 Uwanja Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Ethiopia na Eritrea mwezi Desemba katika hatua ya mwisho ya mchujo wa tiketi ya CHAN, ingawa Tanzania na Kenya zimekwishafuzu kwa tiketi ya uenyeji.


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA SC YAAFIKI KUCHEZA ZANZIBAR MARUDIANO NA BERKANE

KYLLIAN MBAPPE NDIYE MFALME MPYA WA MABAO HISPANIA

PEDRO AIPOKONYA TONGE MDOMONI INTER MILAN, 2-2 NA LAZIO