RAIS MWINYI AWAZAWADIA SH MILIONI 50 WACHEZAJI ZANZIBAR HEROES


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ameizawadia Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Shilingi Milioni 50 baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi 2025.
Akizungumza  katika Hafla Maalum ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya Wachezaji wa Timu hiyo katika Viwanja Vya Ikulu, Rais Dk, Mwinyi  ameeeleza kuwa  timu hiyo imeiletea Heshima kubwa Zanzibar na Kudhihirisha Kuwa kuna Vipaji vingi vya Soka hapa nchini vinavopaswa Kuendelezwa katika Maeneo mbalimbali..
Dk,,Mwinyi  Amefahamisha kuwa  kwa Mafanikio ya  Zanzibar Heroes kuna  kila sababu  kwa Serikali  Kuendelea na UjenzI wa Academy za Soka Kila Mkoa  kwa Lengo la.Kuviibua Vipaji vya Vijana.
Rais Dk, Mwinyi ametangaza Dhamira  ya Kuunda Kamati Maalum ya Kitaifa hivi  karibuni itakayokuwa na Jukumu la  Kumshauri Namna Bora ya  kuuendeleza Mpira wa Miguu hapa nchini.
Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Hatua za Timu za Zanzibar Kulibakisha Kombe la Mapinduzi kwa  Mwaka wa Tatu Mfululizo  kunaashiria Uwezo Mkubwa wa Soka na Vipaji  viliopo .
"Wengi tulishtuka tuliposikia Timu za Afrika Magharibi zinakuja Kushiriki Michuano  ya Mapinduzi,Lakini Mumefanya kazi Nzuri Ahsanteni sana " alisema Dk,Mwinyi
Rais Dk, Mwinyi amefahamisha kuwa Tayari  Wataalamu wa Soka (SCOUT) wa Nchini Uturuki wameonesha nia ya kuja Zanzibar baada ya Kuushuhudia  Mchezo wa Fainali baina ya  Zanzibar na Burkinafaso na kukiri Kuwepo Vipaji Vingi.
Dk. Mwinyi amesisitiza kuwa Lengo ni kuwa na Timu Imara za Mpira wa Miguu  katika ngazi zote zitakazoiletea heshima Zanzibar.
Rais wa Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFF) Suleiman Mahmoud Jabir alitumia Fursa hiyo Kumkabidhi  Rais Mwinyi Kombe la Mapinduzi 2025.




Comments

Popular posts from this blog

NYOTA WA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOFIKA FAINALI KOMBE LA CAF 1993, DAMIAN KIMTI AFARIKI DUNIA