Posts

PETRO DE LUANDA YA KWANZA KUTINGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

Image
MABINGWA wa Angola, Petro de Luanda wamekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuitoa timu ya Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA). Petro de Luanda wamefuzu kwa faida ya mabao ya ugeninibaada ya sare ya 1-1 na KCCA leo Uwanja wa Lugogo mjin Kampala. Na hiyo ni baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza mjini Luanda wiki mbili zilizopita. Katika mchezo wa leo, Petro de Luanda walitangulia kwa bao la Ricardo Estevao dakika ya 34 kwa penalti iliyotolewa baada ya kipa wa KCCA, Charles Lukwago kumchezea rafu, Isaac Mensah ndani ya boksi. Pamoja na hayo, KCCA ikapambana na kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Mustafa Kizza aliyemalizia kazi nzuri ya Sadat Anaku dakika ya 57.  Sasa KCCA watamenyana na moja ya timu zilizovuka Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

KAGERA SUGAR 0-3 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

TANZANIA BARA KUIVAA UGANDA ROBO FAINALI CHALLENGE U20 BAADA YA KUIPIGA ZENJI 5-0 LEO

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Tanzania Bara itakutana na wenyeji, Uganda katika Robo Fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge U20) Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni mjini Gulu nchini humo. Hiyo ni baada ya leo kuwachapa 5-0 ndugu zao, Zanzibar katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa Jinja nchini Uganda, chipukizi Kelvin Pius Jonh ‘Mbappe’ akifunga mabao matatu dakika za 51,87 na 90, mengine Lusajo Mwaikenda dakika ya tano na Novatus Dominic dakika ya 67. Tanzania Bara imepwwa uongozi wa Kundi B kwa sheria ya mchezo wa kiungwana kutokana na kuwa na kadi chache kuliko Kenya waliofungana nao kwa kila kitu. Robo Fainali nyingine ni kati ya Sudan na Sudan Kusini itakayochezwa Gulu pia kuanzia Saa 7:00 mchana, Burundi na Kenya Saa 7:00 mchana na Eritrea na Zanzibar Saa 10:00 jioni ambazo zote zitachezwa Njeru. Hatua ya Nusu Fainali itafuatia Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itap...

SIMBA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0 KAITABA

Image
Na Mwandishi Wetu, BUKOBA SIMBA SC imeanza mapema utawala katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jioni ya leo. Kwa ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya mshambuliaji wake wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere na beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Simba SC sasa inafikisha pointi tisa kufuatia kushinda mechi zake zote tatu za mwanzo. Maana yake, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick J Aussems ndiyo inaongoza Ligi Kuu kufuatia Lipuli FC kupunguzwa kasi leo baada ya sare ya 2-2 na Mbeya City mjini Iringa leo. Katika mchezo wa leo, Kagere alifunga bao la kwanza dakika ya 14 akimalizia kwa kichwa krosi ya winga wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Deo Kanda anayecheza kwa mkopo Msimbazi kutoka TP Mazembe ya kwao. Nahodha Msaidizi wa klabu na beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ akaifunga timu yake ya zamani dakika ya 35 akimalizia pa...

VINICIUS JR AANGUA KILIO BAADA YA KUFUNGA BAO LA KWANZA REAL TANGU FEBRUARI

Image
Vinicius Junior akibubujikwa machozi kwa furaha baada ya kuifungia bao la kwanza Real Madrid dakika ya 36, hilo bao la kwanza kwa ujumla katika timu hiyo tangu Februari katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Osasuna usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid. Bao la pili la Real Madrid lilifungwa na Rodrygo Goes dakika ya 72   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

CHELSEA V MAN UNITED, LIVERPOOL V ARSENAL RAUNDI YA NNE CARABAO

MAN UNITED YASONGA MBELE KWA USHINDI WA MATUTA CARABAO CUP

Image
Wachezaji wa Manchester United wakipongezana baada ya ushindi wa penalti 5-3 kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Rochdale kwenye mchezo wa Raundi ya Tatu Kombe la Ligi England usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford. Manchester United ilitangulia kwa bao la Mason Greenwood dakika ya 68, kabla ya Luke Matheson kuisawazishia Rochdale dakika ya 76. Waliofunga penalti na Man United ni Juan Mata, Andreas Pereira, Fred, Greenwood na Daniel James wakati za Rochdale zilifungwa na Calvin Andrew, Aaron Morley na Aaron Wilbraham huku Jimmy Keohane pekee akikosa   PICHA ZAIDI GONGA HAPA