YAHYA ZAYD ACHEZA SAA NZIMA LAKINI ISMAILIA YAPIGWA 1-0 NA HARAS EL HODOOD
Na Mwandishi Wetu, CAIRO MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Yahya Zayd usiku wa jana amecheza kwa karibu saa nzima timu yake, Ismailia ikichapwa 1-0 na Haras El Hodood katika mchezo wa Ligi Kuu ya Misri Uwanja wa Gehaz El Reyada mjini Cairo. Pamoja na kuwa wenyeji, Ismailia hawakufurukuta wakiadhibiwa na Haras El Hodood na wapinzani wenzao wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam kwa bao pekee la mshambuliaji kinda wa miaka 21 kutoka Nigeria, Edu Moses dakika ya 28. Zayd aliyejiunga na Ismailia msimu huu kutoka Azam FC ya nyumbani, Tanzania alitolewa dakika ya 58, nafasi yake ikichukuliwa na Karim Bambo. Yahya Zayd usiku wa jana amecheza kwa karibu saa nzima Ismailia ikichapwa 1-0 na Haras El Hodood katika Ligi Kuu ya Misri Hata hivyo, mabadiliko hayo hayakuweza kuinusuru Ismailia kupoteza 10 katika msimu huu, hivyo kubaki na pointi zake 37 baada ya kucheza mechi 29 na sasa ipo nafasi ya saba. Baada ya ushindi wa jana, Haras El Hodood sasa wanasogea nafasi ya 15 kat