Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MABINGWA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba SC wamekabidhiwa Kombe lao baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems imemaliza Ligi Kuu na pointi 93, zikiwa ni saba zaidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC waliomaliza na pointi 86 katika nafasi ya pili, wakati Azam FC imeshika nafasi ya tatu kwa pointi zake 75. Hilo linkuwa taji la pili mfululizo la ubingwa wa Ligi Kuu kwa Simba SC na la 20 jumla kihistoria baada ya awali kulibeba katika miaka ya 1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007, 2010, 2012 na 2018. Watani wao, Yanga SC ndio mabingwa mara nyingi zaidi wa Ligi Kuu, mara 27 wakiwa wamebeba taji hilo miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011, 2013, 20