Posts

Showing posts from July, 2019

HEVRE RENARD AWATEMA MOROCCO, KOCHA MPYA WA SAUDI ARABIA,

Image
BINGWA mara mbili wa Kombe la Mataifa Afrika, kocha Herve Renard, ametangazwa rasmi na Shirikisho la soka Saudi Arabia kuwa kocha mkuu kuelekea FIFA World Cup Qatar™ 2022. Akiwa na kibarua cha kwanza kuitafutia nafasi ya mara ya sita kuirejesha Saudia arabia kwenye fainali hizo ambapo waliweza kushiriki mwaka 2018 huko Urusi. Saudia Arabia au maarufu kwenye soka mwewe wa kijana, wapo kundi D dhidi ya Uzbekistan, Palestine, Yemen na Singapore.  Ambapo kinara wa kundi ataenda hatua  ya tatu kuungana na timu kumi na mbili. Herve Renard amezipa ubingwa wa mataifa ya Afrika zambia na Ivory Coast, mwaka 2018 akiiongoza morocco kushiriki kombe la dunia baada ya miaka ishirini taifa hilo kukosa kushiriki kombe la dunia.

BOATENG ASAINI MIAKA MIWILI KUJIUNGA NA FIORENTINA

Image
Na Mohamed Mshangama, TANGA  KLABU ya fiorentina imemsaini mchezaji Kevin-Prince Boateng kutoka Sassuolo kwa ada ya euro million moja kwa mkataba wa miaka miwili. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 mzaliwa wa ujerumani mwenye asili ya ghana aliweza hapo nyuma kukipiga Tottenham Hotspur, Borussia Dortmund, Schalke, portsmouth ,Eintracht Frankfurt , AC Milan na Barcelona.

MSHAMBULIAJI MKONGO AWASILI DAR ES SALAAM KUKAMILISHA USAJILI WAKE YANGA SC

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI David Molinga (pichani kushoto) amewasili Alfajiri ya leo mjini Dar es Salaam kutoka kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Yanga.   Mchezaji huyo anakuja nchini baada ya kumaliza mkataba na FC Lupopo ya kwao aliyojiunga nayo akitokea Renaissance zote za Ligi Kuu ya RDC, Linafoot. Na ujio wa mchezaji huyo unafanya Mkongo mwenzake, kipa Klaus Kindoki aruhusiwe kuondoka klabu hiyo ili Yanga ibaki na wachezaji 10 wa kigeni kwa mujibu wa kanuni. Wachezaji wengine wa kigeni Yanga SC ni Nahodha Papy Kabamba Tshishimbi pia kutoka DRC, kipa Mkenya Farouk, Sadney Urikhob kutoka Namibia, Lamine Moro kutoka Ghana, Juma Balinya kutoka Uganda, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana wote wa Rwanda, Mustapha Seleman kutoka Burundi na Maybin Kalengo kutoka Zambia. Kwa ujumla Yanga SC imeimarisha kikosi chake msimu huu kwa kusajili nyota wengine sita wapya, kipa Metacha Mnata kutoka Mbao FC alikokuwa anacheza kwa m

HAZARD AKIWA KAZINI KWA MWAJIRI MPYA, REAL KOMBE LA AUDI

Image
Mchezaji mpya wa Real Madrid, Eden Hazard akipambana na kiungo wa Tottenham Hotspur, Harry Winks katika mchezo wa Komnbe la Audi mjini Munich, Ujerumani. Spurs ilishinda 1-0, bao pekee la Harry Kane   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SPURS YAIFUNGA MADRID, MAN UNITED YAICHAPA TIMU YA SOLSKJAER

Image
Na Mohamed Mshangama, TANGA Klabu ya Tottenham Hotspur imeingia fainali kwenye kikombe cha Audi baada ya kuifunga klabu ya Real madrid goli moja kwa bila. Goli pekee lilofungwa na mshambuliaji wa uingereza na mfungaji bora wa kombe la dunia 2018, Harry kane kwenye dimba la Allianz arena, liliweza kuipa tiketi ya kwenda kucheza mchezo wa fainali. Huku kwenye mchezo mwengine wa kombe hilo Bayern Munich waliweza kuibuka na ushindi mnono wa bao 6-1. Magoli yaliofungwa na Sanches (22'), 2-0 Goretzka (28'), 3-0 Müller (31'), 4-0 Coman (40'), 5-0 Müller (pen. 44'), 6-0 Müller (58') yaliweza kuipeleka bayern fainali. Hivyo baryern watacheza mchezo wa fainali na Tottenham. Manchester united wakiwa ziarani huko Norway, walipata mchezo wakujipima ubavu na Kristiansund mchezo ulio chezwa kwenye dimba la Ullevaal Stadion.  Goli pekee lilofungwa na kiungo wa hispania Juan Mata dakika ya 91 ndio liloleta ushindi kwenye mechi hiyo. Huo ni mchezo wa tano kwa manchester

IKIMKOSA MAGUIRE MANCHESTER UNITED INAMLETA UMTITI

Image
Na Mohamed Mshangama, TANGA KLABU ya Manchester United imeonesha nia ya kutaka kumsajili bingwa wa michuano ya kombe la dunia 2018 Samuel Umtiti  kwa ada ya paundi za kiingereza millioni 46. Inaripotiwa barca wanaona thamani ya beki huyu wa katikati anathamani ya paundi za uingereza million 55. Manchester united wanawania saini ya mchezaji huyo baada ya dili la harry maguire kuwa na ugumu kwa upande wa Leicester kutaka paundi 80 million kwa mchezaji harry maguire. Klabu ya Manchester City nayo imeonesha nia ya kumtaka umtiti amabae alijiunga na barcelona akitokea Lyon kwa ada ya uamisho wa paundi million 25 na mpaka sasa kacheza barcelona michezo 97.

HIMID MAO AJIUNGA NA ENPPI BAADA YA PETROJETI KUSHUKA DARAJA LIGI KUU MISRI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Himid Mao Mkami ‘Ninja’ amesaini mkataba wa kujiunga na klabu ya klabu ya ENPPI ya Ligi Kuu ya Misri. Mkami anajiunga na ENPPI baada ya klabu yake, Petrojet kushuka Daraja kwenye Ligi Kuu ya Misri baada ya msimu uliopita.  “Nina furaha kujiunga na klabu yangu mpya, ENPPI na ninaelekeza nguvu zangu katika msimu mpya kwa ajili ya mafanikio zaidi,”amesema Mao akizungumza baada ya kutambulishwa katika klabu hiyo. Himid Mao ‘Ninja’ amejiunga na ENPPI baada ya Petrojet kushuka daraja Misri  Mao alijiunga na Petrojet Juni mwaka jana akitokea Azam FC, klabu iliyomuinua kisoka nchini Tanzania akianza kuichezea ngazi ya timu za vijana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyerithi kipaji cha baba, Mao Mkami ‘Ball Dancer’, kiungo wa zamani wa Pamba, Mtibwa Sugar na Moro United aliibukia akademi ya Elite mwaka 2005 kabla ya 2007 kujiunga na Azam. Mao ni mchezaji aliyeanza kuchezea timu za vijana za taifa Tanzania kuanzia

CHAMA AFUNGA SIMBA SC YALAZIMISHA SARE YA 1-1 NA ORLANDO PIRATES LEO JO’BURG

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Simba SC imekamilisha mechi zake za kujipima nguvu kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Orlando Pirates katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Orlando mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Mabao ya yote ya leo yamefungwa na wachezaji wa kimataifa wa Zambia, akianza Clatous Chota Chama kuifungia Simba SC dakika ya 33, kabla ya mshambuliaji, Augustine Kabaso Mulenga kuisawazishia Orlando Pirates dakika ya 40. Huo ulikuwa mchezo wa nne wa kujipima nguvu kwa Simba SC katika kambi yake ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya, baada ya awali kushinda mechi mbili mfululizo na kutoa sare moja.  Clatous Chama alianza kuifungia Simba SC kabla ya Mzambia mwenzake, Augustine Mulenga kuisawazishia Orlando Pirates  Mabingwa hao wa Tanzania Bara walianza kwa kuifunga 4-0 timu ya Chuo Kikuu cha Orbit Tvet, kabla ya kuwachapa wenyeji, Platinums Stars FC 4-1 na kutoa sare ya 1-1 na Township Rollers mechi zote zikipigwa

IDRISSA GUEYE RASMI NI MCHEZAJI MPYA WA PSG

Image
KLABU ya Everton “Toffees”na wamefika makubaliano mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain “PSG” juu ya kiungo huyo raia wa Senegal. Akitokea Aston villa na kujiunga na everton, Gueye ameichezea takriban michezo 108. Kiungo huyo mwenye miaka 28 amesaini miaka 4 kwenye mkataba wake kukipiga PSG huku kiwango cha uhamisho kikiwa hakijawekwa wazi. Hii ikiwa ni mara ya pili akirudi kuchezea ligi ya ufaransa ,Idrissa Gueye  kabla ya hapo kujiunga astonvilla na everton alianzia maisha ya mpira ulaya akiwa na klabu  ya Lille inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa.

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA SHAABAN KATWILA

Image

YANGA SC YAENDELEZA UBABE MECHI ZA KUJIPIMA NGUVU MORO, YAICHAPA 2-0 FRIENDS RANGERS

Image
Na Mwandishi Wetu, MOROGORO YANGA SC leo imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu kwenye kambi yake Morogoro kujiandaa na msimu mpya baada kuichapa Friends Rangers ya daraja la Kwanza mabao 2-0 Uwanja wa Chuo cha Biblia, Bigwa. Mabao ya Yanga SC katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji wake mpya kutoka Namibia, Sadney Urikhob dakika ya 38 na Nahodha mpya, kiungo Papy Kabamba Tshishimbi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 64. Yanga SC itateremka tena dimbani Jumapili wiki hii kumenyana na Kariobangi Sharks ya Kenya Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika kilele cha Wiki ya Mwananchi. Mechi nne zilizotangulia Yanga imeshinda 10-1 dhidi ya dhidi ya Tanzanite, 7-0 dhidi ya ATN, 2-0 dhidi ya Moro Kids na 1-0 dhidi ya Mawenzi Market. Na yote hayo ni maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga SC wakianza na Township Rollers ya Botswana kati ya Agosti 9 na 11 mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana nao mjini

AJIBU AUMIA GOTI, HATARINI KUKOSEKANA MECHI YA MARUDIANO TAIFA STARS NA HARAMBEE

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIUNGO mshambuliaji wa Tanzania, Ibrahim Ajibu Migomba yuko hatarini kuukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Kenya Jumapili mjini Nairobi kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuumia kwenye mechi ya kwanza. Ajibu aliyerejea klabu yake, Simba SC baada ya misimu miwili ya kucheza Yanga, Jumapili aliingia akitokea benchi dakika ya 54 kwenda kuchukua nafasi ya Ayoub Lyanga wa Coastal Union Taifa Stars ikilazimishwa sare ya 0-0 na Harambee Stars. Lakini mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki alimaliza mechi hiyo ya kwanza ya kuwania tiketi ya CHAN ya 2020 akiwa anachechemea baada ya kuumia, kabla ya jana kupelekwa hospitali kwa matibabu. Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini Dar es Salaam, Meneja wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kwamba Ajibu yuko shakani kushiriki mchezo wa marudiano kutokana na maumivu ya goti. “Tunaendelea vizuri na mazoezi, lakini bahati mbaya Ajibu naye ameingia

GARETH BALE ACHOMOLEWA KIKOSINI REAL MADRID

Image
Na Mohamed Mshangama, TANGA MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Wales, Gareth Bale, ameondolewa kikosini kinachoenda kwenye mashindano ya Kombe la Audi. Taarifa zilizotoka kwenye kikosi cha Real Madrid kinachoelekea ujerumani, mshambuliaji huyo Gareth Bale amewekwa pembeni kuwa hayupo fiti kiakili baada ya uhamisho wake kwenda klabu ya Jiangsu Suning ya China kuzuiwa.

JUVENTUS YASEMA TIMU NYINGI ZINAMTAKA DYBALA

Image
Na Mohamed Mshangama, TANGA MAKAMU wa raisi wa Juventus, pavel Nedved ameweka wazi kuwa kuna maombi na mapendekezo kwa klabu za manchester united, psg na Intermilan kutaka kufanya usajili wa mchezaji Paul Dybala. Kwenye hafla ya kupangwa ratiba ya ligi ya Italia Serie A 2019 - 20, paul nedved aliweka bayana klabu muhitaji mshambuliaji huyo wa juve  na kwa njia zipi zimeweka ofa juu ya paul dybala. Klabu ya Manchester United wakitaka bei, huku Tottenham wameweka paundi Million 80 PSG wakiweka  euro million 50 na Intermilan wakitaka kubadilishana na Mshambuliaji Maurio Icard. Habari zinasema kuwa Juventus imemueleza tayari Dybala yupo sokoni na wao wanataka ofa itakoeleweka.

MAGUIRE HAJAONEKANA MAZOEZINI LEICESTER, MANCHESTER UNITED WAHUSISHWA.

Image
Na Mohamed Mshangama, TANGA BEKI wa timu ya taifa ya England, Harry Maguire, hakuonekana kwenye mazoezi ya timu yake ya Leicester City huku ikisemekana anamalizana na manchester united. Muingereza huyo alimpigia simu daktari wa timu na kusisitiza anaumwa na kiweza kupata ruhusa ya kupumzika kwa siku nzima na kutofika mazoezini. Leicester city wamepiga chini ofa mbili sasa zilizo letwa na Manchester United kwa kile kilichoelezwa kuwa wanataka million 80 pound za kiingereza huku manchester united ofa yao ya mwisho ilikua million 70 pounds. Ikumbukwe maguire alikosekana kwenye mechi za kujipima ubavu za kujiandaa na ligi.

CAF YATEUA NAREFA WANNE WA TANZANIA KUCHEZESHA MICHUANO YA KLABU AFRIKA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua Waamuzi Wanne (4) na Makamishna Wawili(2) kutoka Tanzania kusimamia mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho. Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema kwamba refa Elly Sasii atasimama katikati kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Aigle Noir ya Burundi na Gor Mahia ya Kenya utakaochezwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore, Burundi Agosti 11, 2019. Ndimbo amesema Sasii atasaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Frank Komba,Mwamuzi msaidizi namba 2 Ferdinand Chacha,Mwamuzi wa Akiba Emmanuel Mwandembwa na Kamishna wa mchezo anatokea Rwanda, Gaspard Kayijuka. Aidha Mtanzania Ahmed Mgoyi atakua Kamishna wa mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Gor Mahia dhidi ya Aigle Noir utakaochezwa kati ya Agosti 23,24 na 25 nchini Kenya. Naye Mtanzania Khalid Abdallah ameteuliwa kuwa Kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Proline FC ya Uganda na Master Sec

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA MIKE CHUMA

Image

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA ALLY MALILO 'LOKETO'

Image

YANGA SC YAENDELEZA UBABE MECHI ZA KUJIPIMA NGUVU MORO, YAICHAPA 1-0 MAWENZI

Image
Na Mwandishi Wetu, MOROGORO YANGA SC jana imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kujipima nguvu kwenye kambi yake Morogoro kujiandaa na msimu mpya baada ya jana kuichapa Mawenzi Marketi 1-0 Uwanja wa Jamhuri. Bao pekee la Yanga SC katika mchezo wa jana lilifungwa na mshambuliaji mpya kutoka Rwanda, Issa Bigirimana, wakati kiungo mshambuliaji, mkongwe Mrisho Khalfan Ngassa alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi.  Yanga SC itateremka tena dimbanki Jumapilki wiki hii kumenyana na Kariobangi Sharks ya Kenya Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika kilele cha Wiki ya Mwananchi. Mkongwe Mrisho Ngassa akiwaongoza wenzake kuingia uwanjani jana Kikosi cha Yanga kilichoanza jana dhidi ya Mawenzi Market na kushinda 1-0   Mrisho Ngassa akikabidhiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi jana Uwanja wa Jamhuri Mechi tatu zilizotangulia Yanga ilishinda kuichapa ATN 7-0, mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana akifunga mabao matatu peke yake, huku mengine mawili yakifu

UWEKEZAJI KATIKA KLABU TANZANIA UMEGUBIKWA NA SINTOFAHAMU

Image
Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM WASWAHILI wanamisemo sana na nimepata bahati ya kusikia misemo mingi mno baada ya kuingia na kuishi ukanda huu wa Pwani kule kwetu shinyanga hakuna sana misemo hii zaidi ya kukigonga kisukuma kwenda mbele. Moja ya misemo ambayo nimekutana nayo hapa mjini ingawa sikuja na gari la mkaa ni ule msemo wa SHAMBA LA BIBI ni msemo ambao sikuelewa lakini nilipo wauliza waungwana walio kulia pwani waliniambia kuwa huu msemo una maana kuwa shamba la bibi linakuwa huru kwa maneno mengine ni ruksa kuvuna chochote kwa kadri uwezavyo na hakuna mwenye uchungu nalo na ukiwa mjanja kuliko wengine ndio mahali unapoweza kupigia na kutoka kimaisha kwa misemo ya kimjini.Duuuh kumbe ndio hivi! Tuachane na hilo la shamba la bibi turudi kwenye mada yetu kuhusu uwekezaji katika soka letu na bila ubishi huwezi zungumzia soka la Tanzania bila kuhusisha vilabu viwili vikongwe hapa nchini YANGA SC na SIMBA SC ni kongwe kwani ndiyo timu za mwanzo kabisa kuanzishwa moja ikianza m

TAIFA STARS YAJIWEKA PAGUMU KUFUZU CHAN 2020 BAADA YA SARE YA 0-0 NYUMBANI NA KENYA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa Tanzania, Ettiene Ndayiragije amesema ataenda kufanyia kazi mapungufu yaliyojitojeza na kwenda kusaka ushindi katika michezo wa marudiano nchini Kenya. Tanzania imeshindwa kupata matokeo katika mchezo wa leo dhidi ya Kenya kwa kutoa sare ya bila kufungana katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya CHAN kati ya Taifa umekamilika uwanja wa Taifa kwa sare ya bila kufungana. Alisema ameona mapungufu ya kikosi chake na kufanyia kazi kwa lengo la vijana wake kupambana katika mchezo wa marudiano  Kipindi cha kwanza kwa timu zote mbili hakuna hata timu moja iliyopiga shuti lililolenga lango kwa mpinzani. Dakika ya tatu beki wa Tanzania, Gardiel Michael alipiga krosi na mpira kutoka nje. Dakika ya 34 Nahodha John Raphael Bocco alipiga shuti mpira ukatoka pembeni ya lango baada ya kupokea pasi kwa Ayubu lyanga  Kelvin John aliyeingia dakika 67 kuchukua nafasi ya Hassan Dilunga alifanya kazi nzuri na Idd Seleman nusura aipatie Tanzania bao

COSTA AFUNGA MABAO MANNE ATLETICO YAICHAPA REAL MADRID 7-3 MAREKANI

Image
Mshambuliaji Diego Costa akishangilia baada ya kuifungia Atletico Madrid mabao manne dakika ya kwanza, 28, 45 kwa penalti na 51 katika ushindi wa 7-3 dhidi ya mahasimu wao, Real Madrid kwenye mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa MetLife mjini East Rutherford, New Jersey, New York, Marekani. Mabao mengine ya Atletico Madrid yalifungwa na Joao Felix dakika ya nane, Ángel Martin Correa dakika ya 19 na Vitolo dakika ya 70, wakati ya Real Madrid yamefungwa na Nacho dakika ya 59, Karim Benzema kwa penalti dakika ya 85 na Javi Hernandez dakika ya 89. Lakini Costa hakumaliza mchezo baada ya kutolewa dakika ya 65 kwa pamoja na Carvajal baada ya wawili hao kugombana   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

KAGERE AFUNGA SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA TOWNSHIP ROLLERS LEO RUSTERNBURG

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Township Rollers katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo asubuhi mjini Rusternburg, Afrika Kusini. Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere alianza kuifungia Simba SC dakika ya 58 kabla ya kiungo wa kimataifa wa Botswana, Phenyo Nicolas Serameng kuisawazishia Township Rolleres dakika ya 70. Huo ulikuwa mchezo wa tatu wa kujipima nguvu kwa Simba SC katika kambi yake ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya, baada ya awali kushinda mechi mbili mfululizo.   Mabingwa hao wa Tanzania Bara walianza kwa kuifunga 4-0 timu ya Chuo Kikuu cha Orbit Tvet, kabla ya kuwachapa wenyeji, Platinums Stars FC 4-1, mechi zote zikipigwa mjini Rusternburg. Kwenye mechi na Orbit Tvet, mabao ya Simba SC yalifungwa na Nahodha na mshambuliaji tegemeo, John Raphael Bocco dakika ya tisa na 28, kiungo Hassan Dilunga dakika ya 23 na mshambuliaji mpya, Wilker Henrique da Silva kutoka Bragantino ya Daraja la

SAMATTA AISAIDIA GENK KUANZA VYEMA KUTETEA TAJI LA LIGI YA UBELGIJI, YASHINDA 2-1

Image
Na Mwandishi Wetu, GENK MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Ijumaa ameisaidia timu yake, KRC Genk kuanza vyema msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya KV Kortrijk. Samatta alicheza kwa dakika zote 90 mechi hiyo ya Uwanja wa nyumbani, Luminus Arena mjini Genk, ingawa tu alikuwa chini ya ulinzi mkali wa mabeki wa KV Kortrijk na haikuwa ajabu alipomaliza bila kufunga. Wageni walitangulia kwa bao la kiungo Julien De Sart dakika ya 14, kabla ya mshambuliaji Msweden Benjamin Nygren kuwasawazishia mabingwa watetezi, Genk dakika ya 50 na kiungo Mturuki, Ianis Hagi kufunga la ushindi dakika ya 76. Mbwana Samatta ameisaidia KRC Genk kuanza vyema msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji  Mbwana Samatta akiwania mpira wa juu dhidi ya kipa wa  KV Kortrijk, Sebastien Bruzzese   Samatta mwenye umri wa miaka 26, ameichezea Genk jumla ya mechi 157 za mashindano yote na kuifungia mabao 62 tangu amejiunga nayo Januari

KIINGILIO CHA CHINI TAIFA STARS NA HARAMBEE JUMAPILI NI SH 3,000 TU TAIFA

Image
Na Asha Said, DAR ES SALAAM    VIINGILIO vya mchezo wa kuwania fainali ya Kombe la Maitafa ya Afrika kwa wachezaji wa Ndani CHAN kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na timu ya Taifa ya Kenya ni 3000 kwa jukwaa la mzunguko na VIP B na C itakuwa sh.5000.                                               Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo, amesema katika mchezo huo utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, tiketi zitaanza kuuzwa kesho.     Amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, huku wapinzani wanatarajia kuwasili nchini leo jioni.Katika kuelekea mchezo huo baadhi ya waandishi wa habari walipata nafasi ya kuzungumza na waandishi ambapo kwa niaba yao Fatma Likwata, amewataka mashabiki wa soka wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu hiyo. Amesema kujitokeza kwa wingi kutasiadia kuwapa molari wachezaji wa Stars waweze kufanya vizuri katika mchezo huo muhimu.       'Naomba tujitokeze kwa wingi katika Uwanja wa Taifa tuweze kuwapa