Posts
Showing posts from November, 2019
REAL MADRID WAREJEA KILELENI LA LIGA BAADA YA KUICHAPA ALAVES 2-1
- Get link
- X
- Other Apps
Real Madrid leo wamerejea kileleni mwa La Liga baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Deportivo Alaves Uwanja wa Mendizorroza mjini Vitoria-Gasteiz, mabao yake yakifungwa na Sergio Ramos dakika ya 52 na Dani Carvajal dakika ya 69. Bao pekee la Alaves limefungwa na Lucas Perez kwa penalti dakika ya 65 na sasa Real inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 14, ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Barcelona ambao kesho watamenyana na Atletico Madrid PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MANCHESTER CITY YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA NEWCASTLE UNITED
- Get link
- X
- Other Apps
Jonjo Shelvey akipiga shuti kuifungia bao la kusawazisha Newcastle United dakika ya 88 katika sare ya 2-2 na Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. James' Park. Bao la kwanza la Newcastle limefungwa na Jetro Willems dakika ya 25, wakati ya Manchester City yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 22 na Kevin De Bruyne dakika ya 82 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
CHELSEA YACHAPWA 1-0 NA WEST HAM UNITED PALE PALE DARAJANI
- Get link
- X
- Other Apps
DELE ALLI APIGA MBILI TOTTENHAM YAILAZA 3-2 BOURNEMOUTH
- Get link
- X
- Other Apps
Dele Alli akipongezwa na Heung-Min Son baada ya kuifungia Tottenham Hotspur mabao mawili dakika za 21 na 50 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya AFC Bournemouth kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur mjini London. Bao lingine la Spurs iliyo chini ya kocha Mreno, Jose Mournho limefungwa na Moussa Sissoko dakika ya 69, wakati ya Bournemouth yamefungwa na Harry Wilson dakika ya 73 na 90 na ushei baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Ryan Fraser dakika ya 63 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
VAN DIJK APIGA MBILI LIVERPOOL PUNGUFU YAICHAPA BRIGHTON 2-1
- Get link
- X
- Other Apps
Beki Virgil van Dijk akishangilia baada ya kuifungia Liverpool mabao mawili dakika za 18 na 24 mara zote akiimalizia kazi nzuri za Trent Alexander-Arnold katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion leo Uwanja wa Anfield kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England. Bao la Brighton limefungwa na Lewis Dunk dakika ya 79 katika mchezo ambao kipa wa Liverpool, Alisson alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 76 kwa kudakia mpira nje ya eneo lake PICHA ZAIDI GONGA HAPA
SIMBA SC YAACHANA NA AUSSEMS, KITAMBI APEWA TIMU HADI ATAKAPOPATIKANA KOCHA MPYA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM KLABU ya Simba SC imetangaza rasmi kuachana na kocha wake, Patrick Winand J. Aussems baada ya beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Ubelgiji kushindwa kufikia malengo ya mwajiri wake na kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Dennis Kitambi hadi hapo atakapopatikana kocha mpya. Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari leo, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mbatha Mazingisa raia wa Afrika Kusini amesema kwamba wameachana na Aussems kwa sababu ameshindwa kutekeleza majukumu yake kwa viwango na malengo aliyokubaliana na klabu kwenye mkataba wake wa ajira ikiwemo kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. “Pamoja na jitihada za dhati za Bodi kumpa ushirikiano ndugu Patrick Winand J. Aussems hata baada ya kutolewa kwenye mashindano ya klabu binga Afrika, bado ameendelea kuisimamia bila kujali malengo ya Simba kujenga timu yenye ari na mafanikio, nidhamu na ushindani kwenye mashindano ya ndani nan je ya nchi,”imesema taarifa ya Mazingisa.
KOCHA JUMA MWAMBUSI ABWAGA MANYANGA MBEYA CITY, MOHAMED KIJUSO APEWA MIKOBA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KOCHA wa Mbeya City Juma Mwambusi (pichani) amejiuzulu kuifundisha timu hiyo kutokana na mwenendo usioridhisha kwenye ligi kuu msimu huu. Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya James Kasusura imeeleza kuwa Kocha Mwambusi aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu mnamo tarehe 26/11/2019 kwa maslahi mapana ya timu hiyo. Amesema kwa sasa bodi ya timu hiyo imekabidhi timu kwa kocha msaidizi Mohamed Kijuso wakati mchakato wa kumtafuta kocha mwingine ukiendelea. Hadi sasa timu hiyo ikiwa imecheza michezo 12 kwenye ligi kuu msimu huu, imeshinda mchezo mmoja, imetoka sare michezo mitano, imepoteza michezo sita, imefunga magoli manane, imefungwa mabao 19, ina pointi 8 na inakamata nafasi ya 19 juu ya Singida United ambao wanaburuza mkia wakiwa na pointi 7. “Bodi inamshukuru mwalimu Juma Mwambusi kwa mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya timu na bado inahitaji ushauri na uzoefu wake katika tasnia ya michezo”, amesema Kasusura.
HASSAN MWAKINYO AMSHINDA KWA POINTI MFILIPINO, KIDUKU AMMALIZA ‘MSAUZI’ KWA TKO
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM BONDIA Mtanzania, Hassan Mwakinyo amefanikiwa kutetea taji lake la UBO International uzito wa Super Welter baada ya kumshinda Mfilipino, Arnel Tinampay kwa pointi katika pambano la raundi 10 usiku wa jana Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Jaji wa kwanza alitoa pointi 97-93, wa pili akatoa 98-92 wote wakimpa mshindi bondia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 24 na wa tatu akatoa 96-96 kwa maana ya sare. Hilo linakuwa pambano la 16 kwa Mwakinyo kushinda kati ya 18, mengi mawili akipoteza tangu aanze ngumi za kulipwa miaka minne iliyopita pambano lake la kwanza akimshinda Alibaba Ramadhani kwa pointi ukumbi wa Tangamano, Tanga Novemba 29, mwaka 2015. Katika mapambano ya utangulizi, Twaha Kassim Rubaha ‘Twaha Kiduku’ alipeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya kufanikiwa kumshinda France Ramabolu wa Afrika Kusini kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya tatu uzito wa Super Welter pia. Na katika pambano baina ya wapinzani wa kitongoji kimoja, Ma
YANGA SC YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI LIGI KUU, YAICHAPA ALLIANCE 2-1 CCM KIRUMBA
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, MWANZA KIKOSI cha Yanga kimeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Alliance FC 2-1 jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Kwa ushindi huo, Yanga SC mabingwa mara nyingi zaidi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa saba na kupanda hadi nafasi ya 12 kutoka ya 15. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Emmanuel Mwandemwa aliyesaidiwa na Abdulaziz Ally wote wa Arusha na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumzuko Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wake mpya kutoka Rwanda, Patrick Sibomana dakika ya 25 akimalizia mpira uliorudi baada ya kuokolewa kwa pigo la kichwa na Nahodha Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi aliyeunganisha krosi ya beki wa kushoto, Jaffar Mohamed. Lakini dakika 10 tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Alliance FC ikasawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wake, Juma Nyangi akimalizia pasi ya David Richard. Na ndipo msham
MANULA ATEULIWA KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS PAMOJA NA KASEJA KWA AJILI YA CHALLENGE
- Get link
- X
- Other Apps
Na Asha Said, DAR ES SALAAM KIPA namba moja wa timu ya Simba, Aishi Manula amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, baada ya jana kutajwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kitachoshiriki michuano ya CECAFA Senior Challenge nchini Uganda . Chini ya kocha wa sasa Etienne Ndayirajige, Manula aliitwa mara moja pekee katika mechi za awali kufuzu CHAN, lakini kuumia kukamuweka pembeni, hakujumuishwa tena Katika mtanange mingine ikiwamo kufuzu Makundi ya awali Kombe la Dunia pamoja na Afcon mechi za awali. Katika kikosi hicho kipya cha Tanzania Bara wameitwa wachezaji wapya kutoka timu mbalimbali za ligi kuu ambao ni Juma Abdul (Yanga),Nickson Kibabage (Difaa El Jadid) ,Mwaita Gereza (Kagera Sugar), Abdulimajid Mangalo(Biashara United), Fred Tangalu (Lipuli) na Kikoti Lucas (Namungo). Wengine ni Yussuf Mhilu (Kagera Sugar), Eliud Ambokile (TP Mazembe), Paul Nonga (Lipuli), Mkandala Cleophace (Tz Prisons) na Zawadi Mauya (Kagera Sugar) . Wachezaji walioku
MAN UNITED NAO WALICHEZEA 2-1 KWA ASTANA EUROPA LEAGUE
- Get link
- X
- Other Apps
Wachezaji wa Astana wakishangilia ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester United usiku wa jana kwenye mchezo wa Kundi L UEFA Europa League Uwanja wa Astana Arena, mabao yao yakifungwa na Dmitri Shomko dakika ya 55 na Di'Shon Bernard aliyejifunga dakika ya 62 baada ya wageni kutangulia kwa bao la Jesse Lingard dakika ya 10 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KAMADA AWAPIGA MBILI ARSENAL PALE PALE EMIRATES, WALALA 2-1 KWA FRANKFURT
- Get link
- X
- Other Apps
KIUNGO Mjapan, Daich Kamada (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Eintracht Frankfurt mabao mawili dakika za 55 na 64 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Arsenal kwenye mchezo wa Kundi F UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Emirates mjini London, bao la wenyeji likifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 45 na ushei PICHA ZAIDI GONGA HAPA
LUKAKU AFUNGA INTER MILAN YASHINDA 3-1 LIGI YA MABINGWA
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji Romelu Lukaku akishangilia baada ya kuifungia Inter Milan bao la pili dakika ya 81 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Slavia Praha kwenye mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Sinobo mjini Praha. Mabao mengine ya Napoli yote yalifungwa na Lautaro Martinez dakika ya 19 na 88, wakati bao pekee la Slavia Praha lilifungwa na Tomas Soucek kwa penalti dakika ya 37 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
DEJAN LOVREN AINUSURU LIVERPOOL KUPIGWA ANFIELD NA NAPOLI, 1-1
- Get link
- X
- Other Apps
Dejan Lovren akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao la kusawazisha Liverpool dakika ya 65 ikitoa sare ya 1-1 na Napoli iliyotangulia kwa bao la Dries Mertens dakika ya 21 usiku wa jana Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa matokeo hayo, Liverpool inaendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Napoli pointi tisa, Salzburg saba na Genk yenye pointi moja inashika mkia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
CHELSEA YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA VALENCIA MESTALLA
- Get link
- X
- Other Apps
Wachezaji wa Chelsea wakimpongeza mwenzao Christian Pulisic baada ya kufunga bao la pili dakika ya 50 kufuatia Mateo Kovacic kufunga kufunga la kwanza dakika ya 41 katika sare ya 2-2 na wenyeji, Valencia kwenye mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Mestalla. Mabao ya Valencia yalifungwa na Carlos Soler dakika ya 40 na Daniel Wass dakika ya 82 na matokeo hayo yanazifanya timu hizo zifungane kwa pointi, nane kila moja baada ya kucheza mechi tano zikiwa nyuma ya Ajax inayoongoza kwa pointi zake 10, wakati Lille inaendelea kushika mkia na pointi yake moja PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MESSI, SUAREZ NA GRIEZMANN WOTE WAFUNGA BARCELONA YAICHAPA DORTMUND 3-1
- Get link
- X
- Other Apps
Lionel Messi (kushoto) akishangilia na wenzake, Antoine Griezmann na Luis Suarez baada ya wote kufunga katika ushindi wa 3-1 wa Barcelona dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Suarez alifunga la kwanza dakika ya 29, Messi la pili dakika ya 33 na Griezmann la tatu dakika ya 67, wakati bao pekee la Dortmund lilifungwa na Jadon Sancho dakika ya 77 na kwa ushindi huo Barcelona inatinga hatua ya 16 Bora kufuatia kufikisha pointi 11, nne zaidi ya Inter Milan wanaofuatia nafasi ya pili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
SAMATTA AFUNGA BAO LA TATU LIGI YA MABINGWA ULAYA GENK IKICHAPWA 4-1 NYUMBANI SALZBURG
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, GENK MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amefunga bao lake la tatu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa timu yake, KRC Genk ilichapwa 4-1 na Salzburg ya Ausrtia katika mchezo wa Kundi E Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk. Samatta alifunga bao lake dakika ya 85 hilo la pili kuwafunga Salzburg, kwani hata kwenye mchezo wa kwanza pia Genk ikichapwa 6-2 Septemba 17 Uwanja wa Red Bull Arena, yeye ndiye aliyefunga bao la pili la timu yake. Bao lingine Samatta amefunga dhidi ya Liverpool Novemba 5 Uwanja wa Anfield kwenye mchezo uliopita na Napoli ambayo itamenyana na Genk katika mchezo wa mwisho Desemba 10 Uwanja wa San Paolo mjini Napoli inabaki kuwa timu pekee ambayo haijafungwa na Mtanzania huyo kwenye kundi lao. Mabao ya Salzburg jana yalifungwa na Mzambia Patson Daka dakika ya 43, Mjapan Takumi Minamino dakika ya 45, Mkorea Hwang Hee-Chan dakika ya 69 na Mnorway, Erling Haland dakika ya 87. Bao hilo la tatu katika Ligi ya
ZLATAN AJIUNGA NA TIMU YA KWAO SWEDEN BAADA YA KUTEMWA LA GALAXY
- Get link
- X
- Other Apps
DYBALA APIGA BAO PEKEE JUVENTUS YAICHAPA ATLETICO MADRID 1-0
- Get link
- X
- Other Apps
Paulo Dybala akishangilia baada ya kuifungia Juventus bao pekee la ushindi dakika ya 45 na ushei ikiilaza 1-0 Atletico Madrid katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Allianz mjini Torino. Juve sasa wanaizidi pointi sita Atletico Madrid, ambayo italazimika kuminyana na Bayer Leverkusen kuwania kuingia hatua ya mtoano PICHA ZAIDI GONGA HAPA
BENZEMA APIGA MBILI PSG WACHOMOA ZOTE SARE 2-2 REAL NA PSG
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji Karim Benzema akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Real Madrid striker dakika za 17 na 79 katika sare ya 2-2 na Paris Saint Germain kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid kabla ya PSG kusawazisha mwishoni kwa mabao ya Kylian Mbappe dakika ya 81na Pablo Sarabia dakika ya 83 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MAN CITY YAFUZU HATUA YA MTOANO LICHA YA KUTOA SARE 1-1 ETIHAD
- Get link
- X
- Other Apps
Kiungo lkay Gundogan akiifungia bao la kuongoza Manchester City dakika ya 56 katika sare ya 1-1 na Shakhtar Donetsk kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Etihad usiku wa jana. Bao la Shakhtar Donetsk lilifungwa na Manor Solomon dakika ya 69, lakini Man City imefanikiwa kutinga hatua ya mtoano baada ya kufikisha ponti 11 katika mchezo wa tano, ikiwazidi pointi tano Shakhtar Donetsk wanaofuatia nafasi ya pili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
TOTTENHAM YATOKA NYUMA NA KUICHAPA OLYMPIAKOS 4-2
- Get link
- X
- Other Apps
Jose Mourinho akipiga ngumi hewani kushangilia ushindi wa 4-2 wa Tottenham Hotspur dhidi ya Olympiacos ya Ugiriki katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur mjini London. Mabao ya Spurs yalifungwa na Dele Alli dakika ya 45, Harry Kane mawili dakika ya 50 na 77 na Serge Aurier dakika ya 73, baada ya Olympiacos kutangulia kwa mabao ya Youssef El-Arabi dakika ya sita na Ruben Semedo dakika ya 19 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
LEWANDOWSKI APIGA NNE BAYERN MUNICH YASHINDA 6-0 UGENINI LIGI YA MABINGWA
- Get link
- X
- Other Apps
Mshambuliaji Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuifungia Bayern Munich mabao manne dakika za 53 kwa penalti, 60, 64, 67 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya wenyeji, Red Star Belgrade kwenye mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Rajko Mitic mjini Belgrade, mabao mengine yakifungwa na Leon Goretzka dakika ya 14 na Corentin Tolisso dakika ya 89 PICHA ZAIDI GONGA HAPA