Posts

Showing posts from June, 2020

LEROY SANE ATUA BAYERN MUNICH KWA DAU LA PAUNI MILIONI 55

Image
HATMAYE Bayern Munich imefanikisha kumsajili Leroy Sane kwa dau la Pauni Milioni 55 kutoka Manchester City. Sane tayari amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ujerumani baada ya kuweka bayana nia yake ya kutaka kuondoka Etihad. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alithaminishwa kwa dau la Pauni Milioni 130 wakati klabu hizo mbili zilipokuwa zinavutana kwenye mauzo yake, kabla ya hajaumia mguu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Leroy Sane anakwenda kujiunga na Bayern Munich kwa dau la Pauni Milioni 55 kutoka Manchester City   PICHA ZAIDI GONGA HAPA Tangu hapo, Sane amecheza mechi moja tu tena kwa dakika 11 tu katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Burnley wiki iliyopita. Sane anakwenda Bavaria kujiunga na kikosi cha Hans-Dieter Flick kwa mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki, lakini hatacheza Bayern hadi msimu ujao.

RONALDO AFUNGA JUVENTUS YAICHAPA GENOA 3-1 SERIE A

Image
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Juventus dakika ya 56 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Genoa kwenye mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Comunale Luigi Ferraris. Mabao mengine ya Juventus yalifungwa na Paulo Dybala dakika ya 50 na Douglas Costa dakika ya 73 wakati la Genoa lilifungwa naAndrea Pinamonti dakika ya 76.  Kwa ushindi huo, Juventus inafikisha pointi 72 baada ya kucheza mechi 29 ikiendelea kuongoza Serie A kwa pointi nne zaidi ya Lazio inayofuatia   PICHA ZAIDI GONGA HAPA       

MESSI AFUNGA BAO LA 700 BARCELONA YALAZIMISHWA SARE NA ATLETICO, 2-2

Image
Lionel Messi akishangilia baada ya kufunga Barcelona bao la pili kwa penalti dakika ya 50 katika sare ya 2-2 na Atletico Madrid kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou, hilo likiwa bao lake la 700 tangu aanze soka na la 630 katika klabu hiyo. Bao la kwanza Diego Costa alijifunga dakika ya 11, wakati mabao ya Atletico Madrid yalifungwa na Saul kwa penalt yote dakika ya  19 na 62. Cristiano Ronaldo ni mchezaji mwingine pekee wa sasa zaidi ya Messi aliyefunga mabao 725 katika mechi 1002 akiwa na klabu za Sporting, Manchester United, Real Madrid, Juventus na timu yake ya taifa ya Ureno.   Josef Bican anaendelea kushikilia rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwenye mechi za mashindano kwa mabao yake 805 aliyofunga akiwa na Rapid Vienna, Slavia Prague zote za Austria na timu za taifa za Czechoslovak. Wanaomfuatia Bican ni Romario mabao 772, mechi 994, Pele mabao 767, mechi 831, Ferenc Puskas mabao 746, mechi 754, Gerd Muller mabao 735, mechi 793 na Mbrazil, Ronaldo ma

YANGA SC 2-1 KAGERA SUGAR (KOMBE LA TFF)

Image

MAN UNITED YAICHAPA BRIGHTON 3-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUMALIZA "TOP FOUR"

Image
Bruno Fernandes akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Manchester United dakika za 29 na 50 kufuatia Manchester United kufunga la kwanza dakika ya 16 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Brighton & Hove Albion kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa The AMEX. Ushindi huo unaifanya Manchester United ifikishe pointi 52 baada ya kucheza mechi 32 na kurejea nafasi ya tano ikiizidi wastani wa mabao tu Wolverhampton Wanderers   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

YANGA SC YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 TAIFA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM VIGOGO, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar ya Bukoba usiku huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwa wana Jangwani hao, kwani walilazimika kutoka nyuma baada ya Kagera Sugar inayofundishwa na kocha mzalendo, Mecky Mexime kutangulia kwa bao la kiungo wake Awesu Awesu. Awesu alimtungua kipa Metacha Boniphace Mnata dakika ya 20 kwa shuti la kiufundi la umbali wa mita 20 baada ya kupokea pasi ya kisigino ya kiungo mwenzake, Yusuph Mhilu, mchezaji wa zamani wa Yanga. Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga akaisawazishia Yanga SC kwa kichwa dakika ya 52 akimalizia pasi ya kichwa ya kiungo Mrisho Khalfan Ngassa, mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar. Kiungo Deus David Kaseke akaifungia Yanga bao la ushindi dakika ya 76 kwa penalti iliyotolewa na refa

MAN CITY NA ARSENAL, MAN U NA CHELSEA NUSU FAINALI FA

Image
Raheem Sterling akiifungia bao la pili Manchester City dakika ya 68 kufuatia Kevin De Bruyne kufunga la kwanza dakika ya 37 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Newcastle United 2-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la FA England usiku wa jana Uwanja wa St. James Park. Man City sasa itakutana na Arsenal iliyoitoa Sheffield United na Chelsea iliyoitoa Leicester City itakutana na Manchester United iliyoitoa Norwich City Julai 18 Uwanja wa Wembley Jijni London   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

DANI CEBALLOS AIPELEKA ARSENAL NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND

Image
Dani Ceballos akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la ushindi dakika ya 90 na ushei ikiwalaza Sheffield United 2-1 usiku wa jana Uwanja wa Bramall Lane katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la FA England. Bao lingine la Arsenal lilifungwa na Nicolas Pepe kwa penalti dakika ya 25, wakati la Sheffield United lilifungwa na David McGoldrick dakika ya 87   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

REAL MADRID YAICHAPA ESPANYOL 1-0 NA KUSHIKA KASI MBIO ZA UBINGWA LA LIGA

Image
Kiungo Mbrazil, Carlos Henrique Casemiro akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Real Madrid bao pekee dakika ya 45 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Espanyol kwenye mchezo wa La Liga Uwanja wa RCDE. Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha pointi 71 baada ya kucheza mechi 32, sasa Los Blancos wakiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Barcelona   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

ROSS BARKLEY AIPELEKA CHELSEA NUSU FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND

Image
Ross Barkley akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Chelsea dakika ya 63 ikiwalaza wenyeji, Leicester City 1-0 Uwanja wa King Power na kutinga Nusu Fainali ya Kombe la FA England  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

TANZANIA PRISONS 0-0 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

SIMBA SC YATWAA TAJI LA TATU MFULULIZO LIGI KUU BAADA YA SARE YA 0-0 NA PRISONS SOKOINE

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SIMBA SC wamefanikiwa kutwaa taji la tatu mfululizo la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Tanzania Prisons jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kwa sare hiyo, Simba SC wanafikisha pointi 79 baada ya kucheza mechi 32, wakiwaacha mbali watani wao wa jadi, Yanga SC wanaofuatia katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 60 baada ya kucheza mechi 32 pia.   Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Abubakar Mturo aliyesaidiwa na Janeth Balama na Paschal Joseph, timu hizo zilishambuliana kwa zamu na sifa ziwaendee makipa Aishi Manula wa Simba na Jeremiah Kasubi wa TZ Prsions kwa kazi nzuri ya kuokoa michomo langoni. Hilo linakuwa taji la 21 la Ligi Kuu kwa Simba SC baada ya awali kubeba taji hilo katika misimu ya 1965, 1966, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007 (Ligi Ndogo), 2010, 2012, 2018 na 2019. Vigogo, Yanga SC wanabaki kuwa mabingwa mara nyingi zaidi wa taji hilo

YANGA SC 3-2 NDANDA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

SUAREZ APIGA ZOTE MBILI LAKINI BARCA YAAMBULIA SARE 2-2 KWA CELTA VIGO

Image
Luis Suarez akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 20 kabla ya kufunga la pili dakika ya 67, Barcelona ikilazimisha sare ya 2-2 na Celta Vigo ambayo mabao yake yamefungwa na Fedor Smolov dakika ya 50 na Iago Aspas dakika ya 88 katika mchezo wa La Liga usiku huu Uwanja wa Camp Nou. Pamoja na sare hiyo, Barcelona inarejea kileleni ikifikisha pointi 69 baada ya kucheza mechi 32, sasa ikiizidi Real Madrid pointi moja tu ambayo pia ina mechi moja mkononi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA                                                           

HARRY MAGUIRE AIPELEKA MANCHESTR UNITED NUSU FAINALI KOMBE LA FA

Image
Harry Maguire akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la ushindi dakika ya 118 ikiwalaza wenyeji, Norwich 2-1 katika Nusu Fainali ya Kombe la FA England usiku huu Uwanja wa Carrow Road. Odion Ighalo alianza kuifungia Man United dakika ya 51, kabla ya Todd Cantwell kuwasawazishia wenyeji dakika ya 75 na dakika ya 89 wakampoteza Timm Klose aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Odion Ighalo. Man United wanakwenda Nusu Fainali ya Kombe la FA   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SAMATTA ACHEZA MECHI YOTE ASTON VILLA YACHAPWA 1-0 NA WOLVERHAMPTON WANDERERS NYUMBANI

Image
Na Mwandishi Wetu, Birmingham MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta leo amecheza kwa dakika zote timu yake, Aston Villa ikichapwa 1-0 na Wolverhampton Wanderers FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham. Aston Villa ambao leo wamecheza mechi ya nne ndani ya siku 11, sasa wamefikisha mechi nane za ligi bila kushinda na mbaya zaidi wanaonekana wana tatizo kubwa katika safu yao ya ushambuliaji. Kipigo hicho kinazidi kuwachimbia kaburi Aston Villa, wakibaki nafasi ya 19 na pointi zao 27 baada ya kucheza mechi 32.  Aston Villa wapo juu ya Norwich City inayoshika mkia kwa pointi zake 21 za mechi 31 na nyuma West Ham United na AFC Bournemouth zenye pointi 27 pia za mechi 31 ambao kwa pamoja wanaifuatia Watford yenye pointi 28 za mechi 31. Tayari Lverpool wamejihakikishia taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya waliokuwa wapinzani wao kwenye mbio hizo, Manchester City kuchapwa 2-1 na Chelsea juzi. Liverpool imetwaa ubingw

SERIKALI YARUHUSU MASHABIKI KUINGIA KWENYE MECHI YA PRISONS NA SIMBA SC KESHO SOKOINE

Image
Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu mashabiki kuingia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Kati ya Tanzania Prisons na Simba SC kesho Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.  Taarifa ya Wizara kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) imesema kwamba hatua hiyo inafuatia ombi la Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya kutaka mechi za Prisons Uwanja wa Sokoine mashabiki waruhusiwe kuingia.   Ombi hilo lilifuatia Serikali kuzuia mashabiki kuingia viwanjani katika mechi zote zinazohusu Simba na Yanga nje ya Dar es Salaam baada ya klabu ya kukiuka mwongozo wa wizara ya Afya juu ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona katika mchezo wake dhidi ya Simba SC. Simba SC inahitaji sare tu katika mchezo wa kesho ili kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa imebekiza mechi sita. Kwa sasa Simba SC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 78 baada ya kucheza mechi 31, ikifuatwa kwa mbali na watani wao wa

YANGA SC YATOKA NYUMA YAWACHAPA NDANDA 3-2 TAIFA NA KUREJEA NAFASI YA PILI LIGI KUU

Image
Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM VIGOGO Yanga SC wametokea nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Ndanda SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Ushindi huo unairejesha Yanga SC nafasi ya pili, ikifikisha pointi 60 katika mchezo wa 32, sasa inazidiwa pointi 18 na mabingwa watetezi, SImba SC ambao wana mechi moja mkononi.   Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na refa Raphael Ikambi wa Morogoro aliyesaidiwa na Sunday Komba wa Kilimanjaro na Credo Mbuya wa Mbeya, Yanga walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wake, Deus David Kaseke dakika ya tano tu akimalizia pasi ya mshambuliaji Ditram Adrian Nchimbi. Lakini Ndanda SC wakatoka nyuma kwa mabao mawili ya Abdul Hamisi dakika ya 10 na 15 mara zote akimalizia kazi nzuri ya mchezaji mwenzake Omary Mponda na kuongoza kwa 2-1. Mchezaji wa zamani wa Mbeya City, Deus Kaseke akaisawazishia Yanga dakika ya 45 akimalizia kazi nzuri ya beki wa kulia, Juma Abdul Mnyamani. Mkongwe Mrisho K

YANGA SC 2-2 NAMUNGO FC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

RONALDO, DYBALA, HIGUAIN WAFUNGA JUVENTUS YASHINDA 4-0 SERIE A

Image
Cristiano Ronaldo na Paulo Dybala wakishangilia baada ya Juventus kupata bao la kwanza katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Lecce kwenye mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Allianz Jijini Torino. Mabao ya Juve yalifungwa na Paulo Dybala dakika ya 53, Cristiano Ronaldo dakika ya 62, Gonzalo Higuain dakika ya 83 na Matthijs de Ligt dakika ya 85 na kwa ushindi huo dhidi ya Lecce iliyocheza pungufu tangu dakika ya 32 kufuatia Fabio Lucioni kutolewa kwa kad nyekundu ya moja kwa moja kwa kucheza rafu mbaya, kikosi cha Maurizio Sarri kinafikisha pointi 69 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kuongoza Serie A kwa pointi saba zaidi ya Lazio ambayo ina mechi moja mkononi   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

LAMINE MORO AFUNGIWA MECHI TATU NA FAINI SH 500,000 KWA KUMPIGA TEKE MWINYI KAZIMOTO

Image
Na Mwandshi Wetu, DAR E SAALAM BEKI wa Yanga SC, Lamine Moro amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto ambaye naye amefungiwa mechi mbili kwa kosa la kusababisha vurugu kwenye mchezo wao uliopigwa Juni 17, 2020 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi jana, imesema kwamba, Kamati ya Saa 72 pia imepokea malalamiko ya Azam FC kuhusu uamuzi uliofanywa katika mchezo wao dhidi ya Yangasc  na kuyapeleka kwenye Kamati ya Waamuzi.

SERIKALI YAZUIA MASHABIKI KUINGIA MECHI ZA SIMBA NA YANGA MIKOANI, MBEYA CITY YAKIONA CHA MOTO

Image
Na Mwandshi Wetu, DAR E SAALAM SERIKALI imeizuia Mbeya City kucheza na mashabiki katika uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine Jijini Mbeya, ikidaiwa kukiuka mwongozo wa wizara ya Afya juu ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona katika mchezo wake dhidi ya Simba SC juzi. Taarifa iliyotolewa leo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema serikali imezuia pia mashabiki kuingia viwanjani katika mechi zote zinazohusu Simba na Yanga nje ya Dar es Salaam.

MASHABIKI LIVERPOOL WAMWAGIKA MITAANI KUSHEREHEKEA UBINGWA

Image
Mashabiki wa Liverpool wakishangilia nje ya Uwanja wa Anfield baada ya taarifa za kutwaa taji la kwanza la ubingwa wa Ligi Kuu ya England ndani ya miaka 30 kufuatia Manchester City kufungwa 2-1 na Chelsea usiku wa jana Uwanja wa Stamford Bridge London   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

ARSENAL YAICHAPA SOUTHAMTON 2-0 NA KUPANDA NAFASI YA TISA

Image
Mshambuliaji Eddie Nketiah akishangilia baada ya kuifungia Arsenal dakika ya 20 kabla ya Joe Willock kufunga la pili dakika ya 86 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton usiku wa jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. Mary's. Ushindi huo unaifanya Arsenal ifikishe pointi 43 baada ya kucheza mechi 31 na kupanda hadi nafasi ya tisa kutoka ya 11, wakati Southampton inabaki nafasi ya 14 na pointi zake 37 za mechi 31   PICHA ZAIDI GONGA HAPA