Posts

Showing posts from September, 2020

STERLING APIGA MBILI MAN CTY YAUA 3-0 NA KWENDA ROBO FAINALI CARABAO

Image
Raheem Sterling akipongzwa na wachezaji baada ya kufunga mabao mawili dakika ya 35 na 49 katika ushindi wa 3-0 wa Manchester City dhidi ya Burnley kwenye mchezo wa 16 Bora Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao cup, wakati bao lingine llilifungwa na Ferran Torres dakika ya  65, na kwa ushindi huo wanakwenda Roboa Fainali  PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

MAN UNITED YAITWANGA BRIGHTON 3-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI CARABAO

Image
Wachezaji wa Manchester United wakimpongeza mwenzao, Paul Pogba (wa pili kulia) baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 80 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion usiku wa jana Uwanja wa Amex, kwenye mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup. Mabao mengine ya Manchester United yalifungwa na Scott McTominay dakika ya 44 na Juan Mata dakika ya na 73 na kwa ushindi huo Mashetani Wekundu wanatinga Robo Fainali   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

YANGA SC 2-0 KMKM (MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI)

Image
 

YANGA SC IMEIPIGA KMKM 2-0 CHAMAZI LEO MABAO YOTE AMEFUNGA KIUNGO MKONGO TONOMBE MUKOKO

Image
Wachezaji wa Yanga SC wakimpongeza kiungo Mkongo, Tonombe Mukoko baada ya kufunga mabao yote mawili dakika za 11 na 31 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kdogo ya Jiji la Dar es Salaam Kiungo Muangola, Carlos Carlinhos akiambaa na mpira kwenye mchezo dhidi ya KMKM leo Chamazi

THOMAS ULIMWENGU ANAVYOFURAHIA MAISHA NA WACHEZAJI WENZAKE TP MAZEMBE LUBUMBASHI

Image
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulmwengu (kulia) akifuraha na wachezaji wenzake baada ya mazoezi leo Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya KOngo (DRC)

BOSI WA WAAMUZI AKIWPA DARASA MAREFA WA LIGI DARAJA LA PILI TANZANIA BARA LEO DAR

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shrksho la Soka Tanzana (TFF), Soud Abdi akiwaelekeza waamuzi wa Ligi Daraja la Pili wakati wa kufunga semina ya siku tano leo Jijini Dar es Salaam

AZAM FC WAKIJIFUA KWA BIDII KUJIANDAA NA MCHEZO DHIDI YA KAGERA SUGAR JUMAPILI CHAMAZI

Image
Kiungo Awesu Awesu akimtoka beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa katika mazoezi ya timu hiyo leo kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Jumapili Uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Kipa David Kissu akiokoa hatari langoni wakati wa mazoezi ya Azam FC kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Jumapili     Wachezaji wa Azam FC wakijifua leo kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar Jumapili Uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam

SIMBA SC ILIVYOGAWA KADI KWA MASHABIKI WAKE LEO JIJINI DODOMA KUELEKEA MECHI NA JKT JUMAPILI

Image
KLABU bingwa ya Tanzania, Simba leo imeendesha zoezi la kutoa kadi za mashabiki kwa wakazi wa Jiji la Dodoma kwenye vitongoji vya Saba Saba na Majengo . Simba SC imeendesha zoezi hilo kuelekea mchezo wake wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania Jumapili Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma 

SPURS YATINGA ROBO FAINALI CARABAO CUP BAADA YA KUITOA CHELSEA KWA MATUTA

Image
TIMU ya Tottenham Hotspur imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 usiku wa jana Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London. Timo Werner alianza kuifungia Chelsea dakika ya 19, kabla ya Erik Lamela kuisawazishia Tottenham dakika ya 83 na Mason Mount akakosa penalti muhimu na kuipeleka Spurs Robo Fainali ya Carabao Cup   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

BEKI MKALI WA MABAO, LAMINE MORO AONGEZA MKATABA WA KUITUMIKIA YANGA SC HADI MWAKA 2023

Image
Beki wa Yanga SC, Mghana Lamine Moro akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Hersi Said baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuchezea Yanga SC hadi mwaka 2023 kufuatia mwanzo mzuri katika msimu huu akifunga mabao mawili katika mechi tano

RAIS WA TFF, KARIA AWAONYESHA ENEO LA KIGAMBONI WALIOSHINDA TENDA YA UJENZI WA VITUO VYA SOKA

Image
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia akiwaonyesha eneo la Kigamboni Maofisa wa Kampuni ya Group Six International ambayo imeshinda tenda ya ujenzi wa Vituo vya Tanga na Kigamboni unaotarajia kuanza Oktoba 1, 2020 

LIVERPOOL YATOKA NYUMA NA KUICHAPA ARSENAL 3-1 ANFIELD

Image
Mshambuliaji Sadio Mane akishangila baada ya kuifungia Liverpool bao la kwanza dakika ya 28 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Anfield. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Andy Robertson dakika ya 34 na Diogo Jota dakika ya 88, baada ya Arsenal kutangulia kwa bao la Alexandre Lacazette dakika ya 25   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

ALGERIA KUMENYANA NA NIGERIA KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI AUSTRIA

Image
MABINGWA wa Afrika, Algeria watamenyana na Nigeria katika mchezo wa kirafiki Oktoba 9 Uwanja wa Jacques Lemans Arena mjini Sankt Veit an der Glan, Austria.  Mechi hiyo itakuwa marudio ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 nchini Misri, ambayo Algeria ilishinda 2-1 Jijini Cairo. Mchezo huo wa kirafiki utatumika kama sehemu ya maandalizi ya mechi za Novemba za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Cameroon mwaka 2021. Kikosi cha Djamel Belmadi kitakuwa na mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Mexico siku nne baadaye nchini Uholanzi.  Algeria kama wapinzani wao kutoka Afrika Magharibi, Nigeria walioshika nafasi ya tatu kwenye AFCON ya Misri 2019, watarejea kusaka tiketi ya fainali za Afrika mwakani zilizosimama kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19. Algeria itamenyana na Zimbabwe mwezi Novemba nyumbani na ugenini, wakati Nigeria itamenyana na Sierra Leone kama hivyo. Les Fennecs ina

KOCHA MRENO PACHECO AREJEA KUINOA TENA ZAMALEK YA MISRI

Image
KOCHA Mreno, Jaime Pacheco amewasili Jijini Cairo, Misri juzi kwa ajili ya kuanza kuifundisha klabu bingwa mara tano Afrika, Zamalek. Pacheco, ambaye awali aliiongoza Zamalek kati ya Oktoba na Desemba mwaka 2014, amechukua nafasi ya Mfaransa Patrice Carteron, ambaye alijiuzulu ghafla mwezi uliopita na kuhamia Al Taawun ya Saudi Arabia. “Nimerejea Misri kwa sababu naipenda Zamalek. Lengo langu ni kushinda taji la Ligi ya Mabingwa ya CAF,” amesema Mreno huyo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuwasili. Kocha Jaime Pacheco amerejea Cairo kuifundisha tena klabu ya Zamalek   Pacheco mwenye umri wa miaka 62 alianzia kufundisha kwao, zaidi klabu ya Boavista aliyoiwezesha kutwaa taj la Ligi Kuu ya Ureno msimu wa 2000-2001.  Pia alizifundisha klabu za Mallorca ya Hispania, Al Shabab ya Saudi Arabia, Beijing Guoan na Tianjin Teda ya China. Zamalek kwa sasa inashika nafasi ya pli katika Ligi Kuu ya Misri  msimu huu, ambao tayari mahasimu wao, Al Ahly wameshajihakiki

TAIFA STARS KUCHEZA NA BURUNDI MECHI YA KIRAFIKI OKTOBA 11 UWANJA WA BENJAMIN MKAPA

Image
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi katika kalenda ya FIFA Oktoba 11 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Maana yake mechi za Raundi ya Sita za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zilizopangwa kuchezwa kati ya Oktoba 9 na 12 zinaweza kuahirishwa kupisha mchezo huo. 

TAYLOR AMMALIZA KHONGSONG KWA KO NDANI YA SEKUNDE 161

Image
Josh Taylor akiwa ameshika mikanda ya WBA na IBF baada ya kummaliza Apinun Khongsong kwa Knockout (KO) ndani ya sekunde 161 katika pambano la uzito wa welter jana ukumbi wa York Hall, York Hall, Bethnal Green nchini Scotland   na kutetea mataji yake hayo   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

NI MIAMI HEAT NA LOS ANGELES LAKERS FAINALI NBA 2020

Image
KATIKA Ligi ya mpira wa Kikapu Marekani, Miami Heat wametawazwa kuwa mabingwa wa Eastern Conference baada ya kuifunga Boston Celtics 125-113. Pongezi kwa Bam Adebayo aliyefunga pointi 32 na rebounds 14 na Jimmy Butler pointi 22 kuiwezesha Miami Heat kushinda kwa series 4-2 na kutwaa taji hilo kwa mara ya sita – na sasa watakutana na Los Angeles Lakers ya akina LeBron James, mabingwa wa West kuwania taji la NBA 2020. Los Angeles Lakers jana iliichapa Denver Nuggets 117-107 na kutwaa ubngwa wa Western Conference. Miami Heat wametawazwa kuwa mabingwa wa Eastern Conference baada ya kuifunga Boston Celtics 125-113   PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

RONALDO AFUNGA MAWILI JUVENTUS YALAZIMISHA SARE NA ROMA 2-2

Image
Mshambuliaji Mreno, Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifunga mabao yote Juventus ikilazimisha sare ya 2-2 na wenyeji, AS Roma katika mchezo wa Serie A usiku wa jana Uwanja wa Olimpico, Roma. Ronaldo alifunga dakika ya 44 kwa penalti na 69 wakati ya Roma yalifungwa na Jordan Veretout kwa penalti pia dakika ya 31 na 45   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SAMATTA AINGIA KIPINDI CHA PILI FENERBAHCE YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA GALATASARAY

Image
Na Mwandishi Wetu, ISTANBUL  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa Jumapili ametokea benchi kipindi cha pili, timu yake mpya, Fenerbahce ikilazimishwa sare ya 0-0 na Galatasaray katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki Uwanja wa Telekom Jijini İstanbul. Samatta aliyeejiunga na Fenerbahce juzi kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Aston Villa ya England – aliingia uwanjani dakika ya  66 kuchukua nafasi ya Mame Baba Thiam. Samatta, mwenye umri wa miaka 27 atacheza Uturuki kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu atakapouzwa moja kwa moja kwa ada ya Pauni Milioni 5.5 kumalizia mkataba wake wa Villa. Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania alijiunga na Aston Villa Januari mwaka huu kwa dau la Pauni Milioni 10 kutoka klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akisaini mkataba wa miaka minne na nusu. Amecheza mech 14 tu hadi sasa na kufunga mabao mawili – Aston Villa ikichapwa 2-1 na wenyeji, AFC Bournemouth mechi ya Ligi Kuu alifunga kwa kichwa dakika ya 70 Uwanja wa Vitality. Sik

MTIBWA SUGAR 0-1 YANGA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image
 

BAYERN MUNCH YAFUMULIWA 4-1 NA HOFFENHEIM BUNDESLIGA

Image
Wachezaji wa Hoffenheim wakipongezana kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya mabingwa watetezi, Bayern Munich kwenye mchezo wa Bundesliga usiku wa Jumapili Uwanja wa Rhein-Neckar-Arena. Mabao ya Hoffenheim yamefungwa na Ermin Bicakcic dakika ya 16, Mu'nas Dabbur dakika ya 16 Andrej Kramaric dakika ya 16 77 na 90,wakati la Bayern Munich limefungwa na Joshua Kimmich  dakika ya  36   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

ANSU FATI APIGA MBILI, MESSI MOJA BARCELONA YASHINDA 4-0 LA LIGA

Image
Mshambuliaji kinda, Ansu Fati akishangilia baada ya kuifungia Barcelona mabao mawili dakika ya 15 akimalizia pasi ya Jordi Alba na dakika ya 19 akimalizia pasi ya Philippe Coutinho katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Villarreal kwenye mchezo wa La Liga usku wa Jumapili Uwanja wa Camp Nou. Mabao mengine ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi kwa penalti dakika ya 35 na Pau Torres aliyejifunga dakika ya 45   PICHA ZAIDI GONGA HAPA