Posts

Showing posts from January, 2023

AL HILAL YAICHAPA AZAM FC 1-0 CHAMAZI

Image
BAO pekee la Mohamed Abdelrahman dakika ya 45 limeipa Al Hilal ya Sudan ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Azam FC katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Ulikuwa mchezo wa wa pili wa kirafiki kwa Al Hilal ambayo imekuja nchini kuweka kambi ya kujiandaa na mechi yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini Februari 11 baada ya sare ya 1-1 na Namungo FC. Timu hiyo ya kocha Mkongo, Florent Ibenge itashuka tena dimbani Jumapili kumenyana na wenyeji wao, Simba SC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

SIMBA SC YAONGOZA KWA HAT-TRICK LIGI KUU

Image
KUELEKEA Raundi tisa za mwisho za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba ndio inaongoza kwa kutoa waliofunga mabao matatu kila mmoja kwenye mechi moja, yaani hat-trick. Hadi sasa ndani ya Raundi 21 zilizochezwa, wachezaji wawili wa Simba, Nahodha John Bocco na kiungo Mrundi, Said Ntibanzokiza wamefunga hat-trick ikiwa klabu pekee ya Ligi Kuu kutoa wachezaji wawili waliofanya hivyo. Bocco amepiga hat-trick mbili hadi sasa na Ntibanzokiza moja, huku wengine waliofanya hivyo ni mshambuliaji Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele wa Yanga na mshambuliaji Mzanzibari wa Namungo FC, Ibrahim Abdallah Mkoko.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA ATHANAS MICHAEL

Image
 

YANGA YAPATA MDHAMINI MPYA WA BILIONI 1.5

Image
KLABU ya Yanga imeingia mkataba na kampuni ya Haier wenye thamani ya Sh. Bilioni 1.5 kama mdhamini mkuu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

YANGA SC 7-0 RHINO RANGERS (KOMBE LA TFF)

Image
 

MANGUNGU ASHINDA TENA UENYEKITI SIMBA SC

Image
HATIMAYE matokeo ya Uchaguzi wa Simba SC yametangwzwa na Murtaza Ally Mangungu ameshinda tena nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu kwa kupata kura 1,311. Walioshinda nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ni; 1. Dr Seif Ramadhan Muba - kura 1636 2. Asha Baraka - kura 1564 3. CPA Issa Masoud Iddi - kura 1285 4. Rodney Chiduo - kura 1267 5. Seleman Harubu - kura 1250

LIVERPOOL YATUPWA NJE KOMBE LA FA ENGLAND

Image
WENYEJI, Brighton & Hove Albion wamesonga Raundi ya Tano ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool leo Uwanja wa The Amex, Falmer, East Sussex. Mabao ya Brighton & Hove Albion yamefungwa na Lewis Dunk dakika ya 39 na Kaoru Mitoma dakika ya 90 na ushei, wakati la Liverpool limefungwa na Harvey Elliott dakika ya 30.

SIMBA SC 1-0 COASTAL UNION (KOMBE LA TFF)

Image
 

SIMBA SC YAITOA COASTAL UNION KWA KUICHAPA 1-0 DAR

Image
BAO pekee la kiungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute dakika ya 56 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.  Kwa matokeo hayo, Simba SC watakutana na wapinzani wengine kutoka Tanga, African Sports ambayo leo imewatoa wenyeji, New Dundee kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

KMC YAICHAPA COPCO 1-0 NA KUSONGA MBELE ASFC

Image
BAO pekee la mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi, Steve Nzigamasabo dakika ya 84 limeipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya Copco FC ya Mwanza katika mchezo wa Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mechi nyingine za 32 Bora leo, African Sports ya Tanga imesonga mbele kwa ushindi wa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 na New Dundee Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na Mbeya City imeitupa nje Mbeya Kwanza kwa kuichapa 1-0 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea. Singida Big Stars imeitupa nje Ruvu Shooting kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa LITI mjini Singida na wenyeji wengine, Geita Gold imeitoa Nzega United kwa kuichapa 1-0 Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. 

MAN CITY YAITUPA NJE ARSENAL KOMBE LA FA ENGLAND

Image
TIMU ya Manchester City imefanikiwa kwenda Raundi ya Tano ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal usiku huu Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Bao pekee la Man City inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pep Guardiola limefungwa na beki wa Kimataifa wa Uholanzi, Nathan Benjamin Akes dakika ya 64 akimalizia pasi ya kiungo wa Kimataifa wa England, Jack Peter Grealish.

AZAM FC YAITANDIKA DODOMA JIJI 4-1 NA KUSONGA MBELE ASFC

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Edward Charles Manyama dakika ya 10, Daniel Amoah dakika ya 27, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 47 na Justin Bilal aliyejifunga dakika ya 51, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Muhsin Makame dakika ya 17.

BODI YA LIGI YAISHUSHA DARAJA NA KUIFUNGIA MISIMU MIWILI

Image
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeishusha Daraja na kuifungia kwa misimu miwili klabu ya Gwambina FC kushiriki.

KASEKE AFUNGIWA NA FAINI JUU KWA USHIRIKINA

Image
MCHEZAJI wa Singida Big Stars, Deus Kaseke amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh. 500,000 kwa tuhuma za kufanya mambo ya kishirikina kwenye mchezo dhidi ya Azam FC Januari 23, mwaka huu Uwanja wa LITI mjini Singida.

NAMUNGO FC YATOA SARE 1-1 NA AL HILAL CHAMAZI

Image
TIMU ya Namungo FC leo imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Namungo ilitangulia kwa bao la Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya 37, kabla ya Yesir Awadh kuisawazishia Al Hilal dakika ya 90 na ushei. 

KAJULA NDIYE MTENDAJI MKUU MPYA SIMBA SC

Image
KLABU ya Simba imetambulisha Imani Kajula kuwa Mtendaji wake Mkuu mpya, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Barbara Gonzalez aliyejiuzulu Desemba kwa notisi ya mwezi mmoja na kuondoka madarakani Januari mwaka huu.

MAN UNITED YATANGULIZA MGUU FAINALI CARABAO CUP

Image
  TIMU ya Manchester United imetanguliza mguu mmoja katika Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest usiku wa jana Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire. Katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya kwanza, mabao ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya sita, Wout Weghorst dakika ya 45 na Bruno Fernandes dakika ya 89. Timu hizo zitarudiana Februari 1 Uwanja wa Old Trafford na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Southampton na Newcastle United. Mechi ya kwanza Newcastle ilishinda 1-0 ugenini.

MUSONDA NA AZIZ KI WAFUNGA YANGA YASHINDA 2-0 KIGAMBONI

Image
TIMU ya Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Transit Camp katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Avic Town, Somangira, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji mpya, Mzambia, Kennedy Musonda na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki.

CAF YAMPA JUKUMU LIUNDA MECHI YA USM ALGER NA LUPOPO

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua Mkufunzi wa Waamuzi nchini, Leslie Liunda kuwa Mtathimini wa Waamuzi wa mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, U.S.M Alger na FC Saint Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Februari 12 Jijini Algiers nchini Algeria.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA NGADE CHABANGA DYAMWALE

Image
 

GEITA GOLD YAILAZA COASTAL UNION 1-0 NYANKUMBU

Image
TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Bao pekee la Geita Gold limefungwa na Edmund John dakika ya 17 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 31 katika mchezo wa 22, ingawa wanabaki nafasi ya tano wakizidiwa pointi 12 na Singida Big Stars ambao wamecheza mechi 21. Kwa upande wao Coastal Union baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 19 za mechi 22 nafasi ya 13.

AL HILAL YAJA NCHINI KUCHEZA NA AZAM, NAMUNGO NA SIMBA SC

Image
KLABU ya Al Hilal ya Sudan inatarajiwa kuwasili nchini kesho kuweka kambi ya kujiandaa na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikiwa nchini, Al Hilal itacheza mechi tatu za kirafiki ikiwemo dhidi ya wenyeji wao, Simba SC Februari 5, mwaka huu. Kabla ya hapo, Hilal itacheza na Azam FC na Namungo FC katika mechi nyingine mbili za kirafiki.

KOCHA ROBERTINHO AREJEA KWAO BRAZIL KWA WIKI

Image
KOCHA mpya Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameondoka usiku wa kuamkia leo kwenda nchini kwao Brazil kwa shughuli binafsi za kifamilia. Taarifa ya Simba SC imesema kocha huyo aliyejiunga na timu mapema mwezi huuna atarejea nchini mwishoni mwa mwezi huu, yaani baada ya wiki moja. Robertinho anaondoka baada ya kuiongoza Simba kushinda mechi mbili za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, 3-2 nyumbani dhidi ya Mbeya City na 1-0 ugenini dhidi ya Dodoma Jiji FC.

YANGA SC 1-0 RUVU SHOOTING (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

YANGA SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 BAO LA KUJIFUNGA

Image
BAO la kujifunga la Nahodha wa Ruvu Shooting, Mpoki Mwakinyuke limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 56 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mahasimu, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 21. Kwa upande wao Ruvu Shooting hali inazidi kuwa mbaya wakiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 wakibaki na pointi zao 14 za mechi 21 pia.

SINGIDA BIG STARS YAICHAPA AZAM FC 1-0 LITI

Image
BAO pekee la kiungo Mbrazil, Bruno Gomez dakika ya 45 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI, Singida. Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 43, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 21.

ARSENAL YAICHAPA MANCHESTER UNITED 3-2 EMIRATES

Image
WENYEJI, Arsenal FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London. Mabao ya Arsenal yamefungwa na Eddie Nketiah mawili, dakika ya 24 na 90 na Bukayo Saka dakika ya 53, wakati ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 17 na Lisandro Martínez dakika ya 59. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 19 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City waliocheza mechi 20, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 39 za mechi 20 nafasi ya nne.

BALEKE AING’ARISHA SIMBA SC DODOMA, YASHINDA 1-0

Image
BAO pekee la mshambuliaji mpya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean Toria Baleke Othos limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Baleke aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya kwao, Lubumbashi baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo pia Nejmeh SC ya Lebanon alifunga bao hilo dakika ya 45 na ushei akitumia makosa ya kipa wa Dodoma Jiji na walinzi wake. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi. Kwa upande wao Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 21 za mechi 21 sasa nafasi ya 12.

SHIRAZ SHARRIF, MFADHILI WA ZAMANI YANGA AFARIKI DUNIA

Image
ALIYEKUWA Mfadhili wa Yanga tangu miaka ya 1960, Shiraz Sharrif amefariki dunia leo katika hospitali ya Seif Jijini Dar es Salaam. Taarifa za awali zinasema Sharrif ambaye ndiye mwasisi wa klabu ya Pan Africans atazikwa kesho Saa 6:45 mchana katika makaburi ya Jamathkhana, Upanga Jijini Dar es Salaam.

UCHAGUZI MKUU SIMBA SC KUFANYIKA JULIUS NYERERE CENTRE

Image
UCHAGUZI Mkuu wa klabu ya Simba utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Januari 29, mwaka huu.

HUYU MAMADOU DOUMBIA TAYARI KUANZA KAZI JANGWANI

Image
BEKI mpya wa Yanga, Mamadou Doumbia aliyesajiliwa kutoka Stade Malien ya kwao, Mali akiwa na Rais wa klabu hiyo, Mhandisi Hersi Said baada ya kuwasili nchini tayari kuanza kazi kwa mwajiri wake huyo mpya.

LIVERPOOL YALAZIMISHWA SULUHU NA CHELSEA ANFIELD

Image
WENYEJI, Liverpool FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool. Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 28, Liverpool waliocheza mechi 18 wakiwa juu ya Chelsea yenye mechi moja zaidi kutokana na wastani wa mabao.

MECHI YA WATANI SIMBA NA YANGA YASOGEZWA MBELE LIGI KUU

Image
MCHEZO wa marudiano wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani, Simba na Yanga uliopangwa kufanyika Aprili 9, mwaka huu umesogezwa mbele hadi Aprili 16 Saa 11:00 jioni, ingawa siku inabaki kuwa Jumapili.

GEITA GOLD YATOKA SARE 1-1 NA POLISI TANZANIA 1-1 NYANKUMBU

Image
  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Geita walitangulia kwa bao la mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 25, kabla ya Salum Ally kuisawazishia Polisi Tanzania dakika ya 90. Kwa matokeo hayo, Geita Gold imefikisha pointi 28, katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi 12 na Singida Big Stars ambayo pia ina mechi moja mkononi. Kwa upande wao Polisi Tanzania wanafikisha pointi 15 katika mechi ya 21 na kusogea nafasi ya 15.

GEITA GOLD YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0 NYANKUMBU

Image
BAO pekee la mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 25 limeipa Geita Gold ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi 10 na Singida Big Stars ambayo pia ina mechi moja mkononi. Kwa upande wao Polisi Tanzania hali bado ni mbaya, kwani baada ya kupoteza mchezo wa leo wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 wakibaki na pointi zao 14 za mechi 21.

MAN CITY YAIBAMIZA TOTTENHAM HOTSPUR 4-2 ETIHAD

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur usiku wa jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Alvarez dakika ya 51, Erling Haaland dakika ya 53 na Riyad Mahrez mawili dakika za 63 na 90, wakati ya Spurs yamefungwa na Dejan Kulusevski dakika ya 44 na Emerson Royal dakika ya 45. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na vinara, Arsenal ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati Spurs inabaki na pointi zake 33 za mechi 20 nafasi ya tano.

CHAMA AKABIDHIWA TUZO YAKE YA MCHEZAJI BORA WA SIMBA DESEMBA

Image
KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Clatous Chotta Chama akiwa ameshika Tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Simba SC baada ya kukabidhiwa na wadhamini, Emirate Aluminium Profile sambamba mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 2 leo Jijini Dar es Salaam.

SIMBA SC YASHUSHA KOCHA MSAIDIZI KUTOKA TUNISIA

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha Ouanane Sellami kuwa Kocha Msaidizi, hilo likiwa pendekezo la kocha mpya, Mbrazil Robert Oliviera ‘Robertinho’. Taarifa ya Simba SC jioni ya leo imesema kwamba Sellami ataungana na makocha waliopo kikosini - pamoja na Robertinho wengine ni wazawa Juma Mgunda na Suleiman Matola, kocha wa makipa, Mmorocco, Physio Faried Cassiem na Kocha wa Fiziki Kelvin Mandla Ndlomo wote kutoka Afrika Kusini.  Wengine katika benchi la Ufundi ni wazawa, Meneja Patrick Rweyemamu, Daktari Edwin Kagabo na Mtunza Vifaa, Hamisi Mtambo.

MCHEZAJI WA SINGIDA BIG STARS AFARIKI MAZOEZINI

Image
KLABU ya Singida Big Stars ile thibitisha kutokea kwa kifo cha aliyekuwa mchezaji na Nahodha wa timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Mohammed Banda, kilichotokea leo asubuhi Januari 19, 2023.  Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Magereza, Singida.  “Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito,” imesema taarifa ya Singida Big Stars.

MAN UNITED YATOA SARE 1-1 NA CRYSTAL PALACE

Image
TIMU ya Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumatano Uwanja wa Selhurst Park Jijini London. Kiungo Mreno, Bruno Fernandes alianza kuifungia Manchester United ya kocha Mholanzi, Erik ten Hag dakika ya 43, kabla ya Michael Olise kuisawazishia Crystal Palace dakika ya 90 na ushei. Man United inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 19 baada ya sare hiyo na inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na majirani, Manchester City yenye mechi moja mkononi. Kwa upande wao, Crystal Palace wanafikisha pointi 23 na wao wanabaki nafasi ya 12 wakizidiwa pointi mbili na Aston Villa baada ya wote kucheza mechi 19.

NTIBANZOKIZA APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA MBEYA CITY 3-2

Image
WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza mawili dakika ya 11 akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama na la pili kwa penalti dakika ya 49, wakati la tatu limefungwa na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 56. Mabao ya Mbeya City iliyomaliza pungufu baada ya mchezaji wake Samson Maderaka kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65 yamefungwa na Richardson Ng’ondya dakika ya 13 na Juma Shemvuni dakika ya 78. Kocha mpya wa Simba, Robert Oliveira ‘Robertinho’ aliwaduwaza mashabiki wa timu hiyo baada ya kuwatoa Chama na Nahodha John Bocco dakika ya 33 na kuwaingiza Sakho na Kibu Dennis. Kwa ushindi wa leo Simba inafikisha pointi 47, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 20. Kwa upande wao, Mbeya City nao baada ya k

LIVERPOOL YATINGA RAUNDI YA NNE KOMBE LA FA ENGLAND

Image
MABINGWA watetezi, Liverpool wametinga Raundi ya Nne ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers usiku wa Jumanne Uwanja wa Molineux . Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Harvey Elliott dakika ya 13 tu ya mchezo na sasa Liverpool watakutana na Brighton & Hove Albion katika Raundi ya Nne.

SINGIDA BIG STARS YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 LITI

Image
BAO pekee la kiungo Mbrazil, Bruno Gomes dakika ya 14 limeipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi a Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 40 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi tatu na Azam FC ambayo imecheza mechi 19. Kwa upande wao Kagera Sugar baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 24 za mechi 20 nafasi ya nane.

AZAM FC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 3-0 CHAMAZI

Image
WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Jumatatu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Yona Amos aliyejifunga dakika ya tano, Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Kipre Junior dakika ya 70. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi. Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kichapo hicho inabaki na pointi zake 21 za mechi 20 sasa nafasi ya 11.

YANGA SC YAICHAPA IHEFU 1-0 BAO LA MAYELE

Image
BAO pekee la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 64 limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 20 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tisa zaidi ya mahasimu, Simba SC waliocheza mechi 19. Ihefu SC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 20 za mechi 20 sasa nafasi ya 13.

HAWA NDIO WALIOPITISHWA KUWANIA UBOSI SIMBA SC MWISHO WA MWEZI

Image
KAMATI ya Uchaguzi ya klabu ya Simba imetoa orodha ya mwisho ya wagombea waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa Januari 29, mwaka huu Jijini Dar es Salaam.

YANGA YAMREJESHA KIKOSINI KIPA METACHA MNATA

Image
KLABU ya Yanga imemrejesha kipa Metacha Boniphace Mnata baada ya msimu mmoja na nusu tangu iachane naye. Baada ya kutemwa Yanga kwa utovu wa nidhamu mwaka juzi, Mnata alicheza Polisi Tanzania msimu mmoja, kabla ya mwanzoni mwa msimu kujiunga na Singida Big Stars.

SIMBA YASAJILI MSHAMBULIAJI MKONGO JEAN BELEKE KUTOKA LEBANON

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji Mkongo, Jean Toria Baleke Othos (21) kutoka Nejmeh SC ya Lebanon kuwa mchezaji wake mwingine mpya katika dirisha hili dogo. Beleke anayesajiliwa katika siku ya mwisho ya kufunga pazia, anakuwa mchezaji mpya wa tatu dirisha hili dogo baada ya kiungo wa ulinzi Mburkinabe, Hemed Ismael Sawadogo kutoka Difaa El Jadida ya Morocco na kiungo mshambuliaji Mrundi, Saido Ntibanzokiza kutoka Geita Gold. Kabla ya kwenda Lebanon Agosti mwaka jana tu, Beleke alicheza TP Mazembe kuanzia Januari mwaka 2021 baada ya kuibukia klabu ya JS Kinshasa zote za kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

ARSENAL YA MOTO, YAICHAPA SPURS 2-0 LONDON

Image
VINARA, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London. Mabao ya Arsenal inayofundishwa na kocha Mikel Arteta yamefungwa na Hugo Lloris aliyejifunga dakika ya 14 na Martin Odegaard dakika ya 36 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 47 na kutanua uongozi wao kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 18. Kwa upande wao, Tottenham Hotspur baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 33 za mechi 19 nafasi ya tano.