Posts

Showing posts from October, 2023

BALOZI DAVID CONCAR AWATEMBELEA NA SIMBA SC MAZOEZINI

Image
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salum Abdallah Muhene ‘Try Again’ (kushoto) akimkabidhi Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar jezi ya klabu hiyo iliyoandikwa jina leo Jijini Dar es Salaam. Baadaye Balozi huyo alitembelea mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC Jumapili Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. PICHA: BALOZI WA DAVID CONCAR MAZOEZINI SIMBA SC

BALOZI WA UINGEREZA AHUDHURIA MAZOEZI YANGA SC

Image
RAIS wa Yanga SC, Hersi Said akimkabidhi zawadi ya Jezi ya Mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar iliyosainiwa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi leo Jijini Dar es Salaam. Baadaye Balozi huyo alitembelea mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC Jumapili Uwanj wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. PICHA: BALOZI WA UINGEREZA MAZOEZINI LEO YANGA SC

IBRAHIM MAO AIUA MTIBWA UHURU, KMC YANG’ARA LIGI KUU

Image
BAO pekee la Ibrahim Mao dakika ya 15 limetosha kuipa KMC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 15 katika mchezo wa nane na kupanda nafasi ya tatu, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake tano ikiendelea kushika mkia katika Ligi y timu 16 baada ya wote kucheza mechi nane.

NI MESSI TENA MSHINDI WA BALLON D'OR 2023, HAALAND NA MBAPPE...

Image
GWIJI wa Argentina, Lionel Andrés Messi wa Inter Miami usiku wa jana amefanikiwa kushinda tuzo yake ya nane ya Ballon d'Or akiwaangusha Erling Haaland wa Manchester City na Kylian Mbappe wa Paris Saint-Germain. Katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Theatre du Chatelet Jijini Paris – Messi, ambaye ni mshindi pia wa Ballon d’Or za mwaka 2009, 2010, 2011, 2012, 2015, 2019 na 2021 – jana alikabidhiwa tuzo hiyo na mmiliki mwenza wa klabu yake, Inter Miami, David Beckham.    Messi alifunga mabao mawili katika sare yab 3-3 na Ufaransa kabla ya Argentina kutwaa Kombe la Dunia kwa ushindi wa penalty 4-2 nchini Qatar mwaka 2022, likiwa taji la kwanza kwa nchi hiyo tangu 1986. Kwa upande wake, kiungo wa Kimataifa Hispania, Aitana Bonmatí Conca anayechezea klabu ya Barcelona amefanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or upande wa wanawake, akiwashinda Sam Kerr wa Australia na klabu ya Chelsea na Mspaniola mwenzake, Salma Paralluelo wanayecheza naye Barcelona. Tuzo ya Kopa Trophy imekwenda k

DODOMA JIJI YAICHAPA KMC 1-0 AZAM COMPLEX

Image
BAO pekee la Paul Peter dakika ya 71 limeipa Dodoma Jiji FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.  Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC wanafikisha pointi 12 na kupanda nafasi ya nne, wakati KMC inayobaki na pointi zake 12 pia inashukia nafasi ya tano ikizidiwa wastani wa mabao na Walima Zabibu  baada ya wote kucheza mechi nane.

TANZANIA PRISONS YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA GEITA GOLD SOKOINE

Image
WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya 0-0 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.  Kwa matokeo hayo, Tanzania Prisons  wanafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya 12, wakati Geita Gold inafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi nane.

AZAM FC YAMUONGEZA MKATABA YAHYA ZAYD HADI 2026

Image
KLABU ya Azam FC imemsainisha mkataba mpya wa miaka miwili na kiungo wake mshambuliaji, Yahya Zaid, ambao utamfanya aendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026.

JOB, MAX AZIZ KI KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA YANGA

Image
BEKI mzawa, Dickson Nickso Job atachuana na viungo wageni, Mburkinabe Stephane Aziz Ki na Mkongo Max Mpia Nzengeli kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora klabu hiyo mwezi Oktoba. TAZAMA VIDEO ALLY KAMWE AKIZUNGUMZIA TUZO ZA YANGA Watatu hao wanaweka historia ya kuwa wachezaji wa kwanza kuwania tuzo hiyo baada ya klabu hiyo kuingia mkataba na Shirika la Bima Taifa (NIC) kudhaminizi Tuzo hizo ambazo zinaanza mwezi huu. Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance, Karim Meshack amesema mshindi wa Tuzo hiyo atazawadiwa Kiasi cha Fedha Taslimu Shilingi Milioni 4. TAZAMA VIDEO BOSI WA NIC AKITAJA ZAWADI YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI YANGA SC

KEN GOLD YAREJEA KILELEMI LIGI YA CHAMPIONSHIP

Image
TIMU ya Ken Gold ya Mbeya jana imefanikiwa kupanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship baada ya ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.  Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship, wenyeji Pan Africans waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate Talents Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, wakati Cocpo ya Mwanza iliwalaza wenyeji, Ruvu Shooting 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Ushindi wa jana unafanya Ken Gold ifikishe pointi 19 na kupanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship, ikiwazidi pointi mbili ndugu zao, Mbeya Kwanza baada ya wote kucheza mechi nane. Copco imesogea nafasi ya saba baada ya kufikisha pointi 11, Pan Africans imesogea ya 13 baada ya kufikisha pointi saba, wakati Biashara United sasa ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi tisa, Ruvu Shooting yenye pointi moja inashika mkia na Fountan Gate Talents inashukia nafasi ya 12 kwa pointi zake nane baada ya wote kucheza mechi nane.

SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 2-1 NA KUIKAMATA YANGA KWA POINTI

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na washambuliaji wake wa kigeni, Mkongo Jean Othos Baleke dakika ya 13 na Mzambia, Moses Phiri dakika ya 65, wakati la Ihefu SC limefungwa na Ismail Mgunda dakika ya 25. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa sita, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi. Ihefu SC kwa upande wao baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao saba za mechi saba nafasi ya 11.

EDDIE NKETIAH APIGA HAT TRICK ARSENAL YASHINDA 5-0

Image
WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London. Nyota wa mchezo wa leo ni mshambuliaji Muingereza Edward ‘Eddie’ Keddar Nketiah mwenye asili ya Ghana ambaye amefunga mabao matatu dakika za 28, 50 na 58, wakati mabao mengine ya Arsenal yamefungwa na Fabio Vieira dakika ya 88 kwa penalti na Takehiro Tomiyasu dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili tu na vinara, Tottenham Hotspur, wakati Sheffield United inabaki na pointi yake moja mkiani baada ya wote kucheza mechi 10.

PAMBA FC YATOA SARE NA MBEYA KWANZA 1-1 MTWARA

Image
WENYEJI, Mbeya Kwanza jana wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Pamba FC ya Mwanza katika mchezo wa Ligi ya NBC Championship Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Kwa matokeo hayo, Mbeya Kwanza inafikisha pointi 17 baad aya kucheza mechi nane na kuendelea kuongoza Ligi ya NBC Championship ikifuatiwa na Ken Gold ya Mbeya pia yenye pointi 16 za mechi saba na Pamba FC pointi 15 mechi nane pia.

NAMUNGO FC YAICHAPA AZAM 3-1 PALE PALE CHAMAZI

Image
WENYEJI, Azam FC jana wamechapwa mabao 3-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Namungo FC jana yamefungwa na Pius Buswita dakika ya 10, Hashim Manyanya dakika ya 19na Reliant Lusajo dakika ya 50, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 70. Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 13 nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi saba.   

YANGA SC YAWACHAPA SINGIDA BIG STARS 2-0 ZOTE KAPIGA MAX

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli aliyefunga mabao yote mawili, dakika ya 30 na 39. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa saba na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tatu zaidi ya Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi. Kwa upande wao, Singida Big Stars wanabaki na pointi zao nane na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wao pia kucheza mechi saba.

KMC YAAMBULIA SARE 1-1 NA TANZANIA PRISONS UHURU

Image
WENYEJI, KMC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Kipa Wilbol Maseke alianza kujifunga dakika ya 53 kuipatia Tanzania Prions bao la kuongoza, kabla ya mshambuliaji Waziri Junior kuisawazishia KMC dakika ya 82. Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 12, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Tanzania Prisons inatimiza pointi sita na kusogea nafasi ya 13 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi saba.

LIVERPOOL YAICHAPA TOULOUSE 5-1 EUROPA LEAGUE

Image
TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Toulouse ya Ufaransa katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota dakika ya tisa, Wataru Endo dakika ya 30, Darwin Núñez dakika ya 34, Ryan Gravenberch dakika ya 65 na Mohamed Salah dakika ya 90, wakati la Toulouse limefungwa na Thijs Dallinga dakika ya 16. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi tisa na kuendelea kuongoza Kundi hilo, ikifuatiwa na Union Saint-Gilloise ya Ubelgiji na Toulouse zenye pointi nne kila moja, wakati LASK ya Austria ambayo haina pointi inashika mkia. 

NYOTA WA ULAYA WAING’ARISHA TWIGA STARS KUFUZU OLIMPIKI 2024

Image
TIMU ya taifa ya wanawake ‘Twiga Starst’ imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kufuzu Olimpiki ya mwakani Paris uliofanyika leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na washambuliaji wake tegemeo, Opa Clement anayecheza Besiktas ya Uturuki kwa penalti dakika ya pili na Aisha Masaka wa BK Häcken ya Sweden dakika ya 85. Timu hizo zitarudiana Oktoba 31, Uwanja wa Taifa wa Gaborone na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu. Kuna raundi ya Nne na ya Tano pia na ya mwisho na baadaye timu mbili zitaiwakilisha Afrika huko Paris.

MTIBWA SUGAR YAZINDUKA NA KUICHAPA GEITA GOLD 3-1

Image
TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ladack Chassmbi dakika ya 20 na Seif Abdallah Karihe mawili, dakika ya 49 na 58, wakati la Geita Gold alijifunga kipa Mohamed Makaka dakika ya 83. Ushindi huo wa kwanza kwa Mtibwa Sugar na wa kwanza kwa kocha Zubery Katwila tangu arejee Manungu unaifanya Mtibwa Sugar ifikishe pointi tano na kusogea nafasi ya 13, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake tano na kushukia nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi saba.

HAALAND APIGA MBILI MAN CITY YASHINDA 3-1 LIGI YA MABINGWA

Image
MABINGWA watetezi,  Manchester City FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, BSC Young Boys katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Uwanja wa Wankdorf mjini Bern nchini Uswisi. Mabao ya Manchester City yamefungwa na Manuel Akanji dakika ya 48 na Erling Haaland mawili, moja kwa penalti dakika ya 67 na lingine akimalizia pasi ya Rodri dakika ya 86, wakati bao pekee la BSC Young Boys limefungwa na mshambuliaji Mkongo,  Meschack  Elia Lina dakika ya 52. Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi tisa kileleni, ikifuatiwa na  RB Leipzig pointi sita, wakati Young Boys ina pointi moja sawa na Red Star Belgrade ya Seriba.

COASTAL UNION YAICHAPA MASHUJAA FC 2-0 MKWAKWANI

Image
TIMU ya Coastal Unión ya Tanga imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mabao ya Coastal Unión yamefungwa na Bakari Suleiman dakika ya 19 na Lucas Kikoti dakika ya 89 kwa penalti na kwa ushindi huo wanafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya 12, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake nane nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi saba.

JKT TANZANIA YAICHAPA TABORA UNITED 1-0 CHAMAZI

Image
TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la JKT Tanzania ambayo Tabora United zote zimepanda Ligi Kuu msimu huu limefungwa na kiungo na Maka Edward Mwasomola dakika ya 17. Kwa ushindi huo, JKT Tanzania ambao ni mabingwa wa Ligi ya Championship msimu uliopita inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tano, wakati Tabora United inayobaki na pointi zake tisa inaangukia nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi saba.

AL AHLY 1-1 SIMBA SC (AFRICAN FOOTBALL LEAGUE)

Image
 

MAGUIRE AFUNGA, ONANA AOKOA PENALTI MAN U YASHINDA ULAYA

Image
WENYEJI, Manchester United jana wamepata ushindi wa kwanza katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuilaza Copenhagen 1-0 Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Bao pekee la Manchester United katika mchezo huo wa Kundi A limefungwa na beki wa Kimataifa wa England, Harry Maguire kwa kichwa dakika ya 72 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Mdenmark, Christian Eriksen. Ikawa siku nzuri pia kwa kipa Mcameroon, Andre Onana aliyeokoa mkwaju wa penalti wa Jordon Larsson dakika ya 90 baada ya Scott McTominay kumchezea rafu Mohamed Elyounoussi wa Copenhagen. Ushindi wa kwanza kundini unaifanya timu hiyo ya kocha Mholanzi, Erik ten Hag ifikishe pointi tatu katika mchezo wa tatu tatu na kusogea nafasi ya tatu ikizidwa pointi moja  na Galatasaray, wakati Bayern Munich yenye pointi tisa inaongoza.

SIMBA SC YAFA KIUME CAIRO, YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI

Image
TIMU ya Simba SC imetupwa nje ya michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) licha ya sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa Robo Fainali leo Uwanja wa Cairo International, Misri. Kiungo wa Kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute alianza kuifungia Simba dakika ya 68 akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama kabla ya mshambuliaji Mmisri, Mahmoud Abdulmonem Abdelhamid Soliman ‘Kahraba’ kuisawazishia Al Ahly dakika ya 76 akimalizia pasi ya beki Mtunisia, Ali Maâloul. Simba inayofundishwa na Kocha Mbrazil, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ inatolewa kwa Sheria ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 3-3 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Sasa Al Ahly inasubiri kukutana na mshindi wa jumla katí ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Petro de Luanda ya Angola zinazorudiana baadaye leo Jijini Pretoria. Mechi ya kwanza Mamelodi Sundowns walishinda 2-0 mjin Luanda.

YANGA SC 3-2 AZAM FC (LIGI KUU YA TZ BARA)

Image
 

KAZE AAMUA KUACHIA NGAZI NAMUNGO FC

Image
MRUNDI Cedric Kaze amejiuzulu Ukocha Mkuu wa Namungo FC baada ya mechi sita tu za msimu kutokana na mwendendo usioridhisha katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Kaze anajiuzulu Namungo FC siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa na Singida Big Stars mabao 3-2 jana Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Anaondoka akiiacha timu ina pointi tatu tatu baada ya mechi sita ikiwa inashika nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16. Kaze alikuwa na msimu mzuri uliopita akiwa na vigogo, Yanga kama Kocha Msaidizi wa Mtunisia, Nasredeen Nabi wakishinda mataji ya Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.

MAN UNITED YAWAKANDA VIBONDE SHEFFIELD UNITED 2-1 BRAMALL

Image
TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Bramall Lane, Sheffield. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Scott McTominay dakika ya 28 na Diogo Dalot dakika ya  77, wakati la Sheffield United limefungwa na Oliver Robert McBurnie kwa penalti dakika ya 34 kwa penalti. Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya nane, wakati  Sheffield United inabaki na pointi yake moja nafasi ya mwisho kwenye ligi ya timu 20 baada ya wote kucheza mechi tisa.  

MAKOCHA AZAM ACADEMY WAZUIA KUFANYA KAZI LIGI YA VIJANA U20

Image
MAKOCHA wa timu ya vijana ya Azam FC, Mohamed Badru Juma na Msaidizi wake, Mwalu Hashim Ilunga wamezuiwa kufundisha timu hiyo katika Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 iliyoanza leo Jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), makocha hao wote wana leseni za Diploma C za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wakati makocha wanaotakiwa kufundisha kwenye ligi hiyo ni wenye leseni za Diploma B na A za CAF. Aidha makocha wenye Diploma A ma B lakini wamesoma muda mrefu na hawakushiriki kozi za Maboresho hivi karibuni nao pia wamezuiwa kufundisha kwenye ligi hiyo.

GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA DODOMA JIJI NYANKUMBU

Image
WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya Nyanmkumbu mjini Geita. Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Tariq Seif dakika ya 10 na Hassan Mahmoud dakika ya 86, wakati ya Dodoma Jiji yote yamefungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 62 na 64. Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi tano nafasi ya 12 na Dodoma Jiji pointi sita na inasogea nafasi ya 10 kutoka ya 12 baada ya wote kucheza mechi sita.

ARSENE WENGER AJUMUIKA NA WACHEZAJI WA SIMBA SC

Image
MKUU wa Idara ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Mfaransa Arsene Wenger akiwa na kiungo Sadio Kanoute kutoka Mali, mfungaji wa bao la pili la Simba SC jana katika sare ya 2-2 na Al Ahly ya Misri Uwanja wa Benjamin kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Afrika (AFL). Wenge, kocha wa zamani wa Arsenal alikuwa nchini kwa ajili ya kushuhudia ufunguzi wa michuano ya Ligi ya Afrika (AFL) inayofanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa FIFA na CAF.  VIDEO: ARSENE WENGER NA WACHEZAJI WA SIMBA SC

SIMBA SC YAIKOSAKOSA AL AHLY, WATOA SARE 2-2 DAR

Image
WENYEJI, Simba SC wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) uliofanyika Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Al Ahly yamefungwa na Reda Slim dakika ya 45 na ushei na Mahmoud ‘Kahraba’ Soliman dakika ya 63, wakati ya Simba SC yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 53 na Sadio Kanoute dakika ya 59. Timu hizo zitarudiana Jumanne Uwanja wa Cairo International, Misri na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Petro de Luanda ya Angola na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

RAIS WA CAF MOTSEPE AMTEMBELEA RAIS DK SAMIA IKULU DODOMA

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea kumbukumbu ya zawadi ya uenyeji wa ufunguzi wa michuano ya kwanza ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe ambaye amemtembelea leo Ikulu, Chamwino Jijini Dodoma. Motsepe ambaye aliongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alipeleka shukrani hizo kwa Rais Samia kutokana na Tanzania kuwa mwenyeji wa ufunguzi wa michuano ya AFL inayoanza leo kwa Simba kumenyana na Al Ahly ya Misri Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. PICHA: RAIS MOTSEPE WA CAF ALIPOMTEMBELEA RAIS SAMIA IKULU CHAMWINO DODOMA

WAZIRI WA MICHEZO DK. NDUMBARO ATETA NA UONGOZI WA FIFA NA CAF

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA ) katika Ukanda wa CECAFA, Andrea Silva na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Veron Mosengo - Omba kwa mazungumzo Jijini Dar es Salaam. Wawili hao wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya mechi ya Ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFC) kati ya Timu ya Simba ya Tanzania na Al Alhy ya nchini Misri, utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Oktoba 20,2023. Katika kikao hicho viongozi hao pamoja na mambo mengine wamejadili maendeleo ya Michezo nchini ambapo kwa sasa Tanzania inafanya vizuri katika michezo hususani mchezo wa soka, kwa Timu za Taifa za wanaume na Wanawake pamoja na Ligi mbalimbali na mashindano ya Kimataifa. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Neema Msitha, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzani

MWONEKANO MPYA UWANJA WA MKAPA KUELEKEA UFUNGUZI AFL KESHO

Image
MWONEKANO wa benchi la wachezaji wa akiba baada ya ukarabati uliofanywa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuelekea ufunguzi wa michuano ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) kesho kwa mchezo baina ya wenyeji, Simba SC na Al Ahly ya Misri, VIDEO: MWONEKANO WA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA BAADA YA UKARABATI

TWIGA STARS WAKIJIFUA KUJIANDAA KUIKABILI BOTSWANA WIKI IJAYO

Image
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya wanawake, 'Twiga Starst’ wakiwa mazoezini Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha TFF, Kigamboni, Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili kufuzu Olimpiki ya mwakani Paris dhidi ya Botswana Oktoba 26 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana Oktoba 31, Uwanja wa Taifa wa Gaborone na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Afrika Kusini katika Raundi ya Nne. Kuna raundi ya Tano pia nay a mwisho na baada ya timu mbil zitaiwakilisha Afrika huko Paris. PICHA: MAZOEZI YA TWIGA STARS KIGAMBONI JANA

AISHI ANAVYOANDALIWA KUZUIA MICHOMO YA AL AHLY KESHO DAR

Image
KIPA namba wa Simba SC, Aishi Manula akidaka mpira mbele ya wasaidizi wake wakati wa mazoezi ya jana Uwanja wa Mo Simba Afrena Jijini Dar es Salaam kuelekea mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Soka Afrika (AFL) dhidi ya Al Ahly ya Misri kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Simba SC ina jumla ya makipa wanne, mbali na Aishi wengine ni Mmorocco Ayoub Lakreb, Ally Salum, Hussein Abel na Ally Ferouz. Timu hizo zitarudiana Jumanne ijayo, Oktoba 24 Uwanja wa Cairo International na mshindi wa jumla atakwenda Nusu Fainali ambako atakutana na mshindi wa jumla kati ya Petro de Luanda na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. PICHA: MAZOEZI YA SIMBA SC JANA JIJINI DAR ES SALAAM

HABIB KONDO ATUPIWA VIRAGO MTIBWA SUGAR, KATWILA AREJEA MANUNGU

Image
KLABU ya Mtibwa Sugar imefikia makubaliano ya pande zote mbili kuachana na Kocha wake, Habib Kondo baada ya mechi tano tu za mwanzo za msimu. Hatua hiyo inakuja siku moja kabla ya Mtibwa Sugar kumenyana na wapinzani wao wa kutengeneza Sukari, Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar ya Bukoba kesho Saa 10:00 jioni Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro na waliokuwa makocha wasaidizi, Awadh Juma na Patrick Mwangata ndio wataiongoza timu kesho. Lakini taarifa za ndani zinasema kwamba aliyekuwa kocha wa Ihefu SC, Zubery Katwila yupo kwenye mazungumzo yanayoendelea vizuri na uongozi wa Mtibwa Sugar ili arejee kwneye timu hiyo aliyoichezea na kuifundisha awali.

KAKOLANYA MCHEZAJI BORA WA MWEZI SINGIDA BIG STARS

Image
KIPA Beno David Kakolanya ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba wa klabu ya Singida Big Stars na kuzawadiwa kitita cha Sh. Milioni 1 kutoka kwa wadhamini, kampuni ya JET & Sons.

WASHINDI SANYA SANYA NA M-BET KUZAWADIWA TV, SIMU, FEDHA TASLIMU

Image
KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania imezindua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la Sanya Sanya na M-Bet ambayo ina mwezesha mshindi kushinda fedha taslimu, simu ya mkononi na televisheni ya kisasa (“Smart TV). Akiuzungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana, Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema lengo la kuanzisha  kampeni ya Sanya Sanya na M-Bet ni kuwazawdia wateja wao kuelekea kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka. Mushi alisema kuwa wameanza kampeni mapema zaidi kwa lengo la kuwazawadia wateja wao wengi na kuweza kubadili maisha yao. Alisema kuwa kwa wateja wa M-Bet Tanzania wenye simu za kawaida maarufu kama ‘kitochi’, unatakiwa kutumia USSD menyu yao  kwa kupiga *149*19# na kuanza kubashiri matokea ya mechi kuanzia mbili za ligi mbalimbali duniani.   Mushi alisema kuwa mbali ya kutumia USSD menyu hiyo, pia unaweza kubashiri kwa kutumia app ambayo lazima uipakue kwa watumiaji wa simu janja (smartphone). Alisema kuwa wateja wao wa

NYOTA TAIFA STARS WAENDA KUFANYA IBADA YA UMRAH MAKKA

Image
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, mshambuliaji na Nahodha Mbwana Samatta (kulia) akiwa na beki Abdi Banda (kushoto) wakiwa na Kocha Mualgeria, Adel Amrouche katika msikiti mtukufu wa Makkah, Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya Umrah. Wachezaji kadhaa wa Taifa Stars ambao ni waumini wa dini ya Kiislam walikwenda Makka baada ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Sudan nchini humo jana uliomalizika kwa timu hizo kutoa sare ya 1-1. PICHA: WACHEZAJI WA TAIFA STARS KATIKA MSIKITI WA MAKKA

TAIFA STARS YATOA SARE 1-1 NA SUDAN LEO SAUDIA ARABIA

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoa sare ya 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa leo Uwanja wa King Fahd Sports City mjini Ta'if, Saudi Arabia. Sudan ilitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Al Hilal, Musab Ahmed Alsharif Eisa dakika ya saba, kabla ya kiungo wa Azam FC, Sospeter Israel Bajana kuisawazishia Tanzania dakika ya 40.

KOCHA ALIYEZIPELEKA NUSU FAINALI MERREIKH NA HILAL AFRIKA ATUA SINGIDA

Image
KLABU ya Singida Big Stars imemtambulisha Mbrazil, Heron Ricardo Ferreira kuwa Kocha wake mpya Mkuu akichukua nafasi ya Mjerumani, aliyedumu ofisini kwa wiki mbili tu. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka kuanzia nyumbani kwao mwaka 1992, Olaria ikiwa ni klabu yake ya kwanza kabla ya kufanya kazi Asía na Afrika. Miongoni mwa klabu alizofundisha Afrika ni pamoja na Ismailia ya Misri, Al-Ahly Shendi, Al Ahly na Al Merreikh zote za Sudan. Mafanikio yake makubwa barani ni kuifikisha Al Hilal Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2006-2007 na Al Al-Merreikh Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2012. 

PAMBA FC NA POLISI TANZANIA ZASHINDA, BIASHARA YATOA SARE CHAMPIONSHIP

Image
LIGI ya NBC Championship iliendelea jana kwa michezo minne kupigwa viwanja tofauti, Pamba ya Mwanza ikiibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Green Warriors ya Dar es Salaam bao pekee la Frank Mwenga kwa penalty kipindi cha kwanza Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza. Mechi nyingine za NBC Championship jana Ken Gold iliichapa Pan Africans 4-0 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Faountain Gate Talents ikalazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na TMA ikaichapa Mbeya Kwanza 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Ikumbukwe juzi Mbeya City ililazimishwa sare ya 1-1 na Cosmopolitan ya Dar es Salaam Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na Polisi Tanzania ikailaza Stand United 2-1 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Ligi ya NBC Championship inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili zaidi, Cocpo na Transit Camp Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Mbuni FC dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Msimamo wa NBC Champio

IHEFU SC YAACHANA NA KOCHA ZUBERI KATWILA

Image
KLABU ya Ihefu imeachana na Kocha wake, Zuberi Katwila baada ya takriban miaka minne ya kuwa timu hiyo tangu awasili kutoka Mtibwa Sugar. Taarifa ya Ihefu SC leo imesema; “Uongozi wa timu yetu umefikia makubaliano ya pande mbili ya kuvunja Mkataba na aliyekua Kocha wetu Mkuu Zuber Katwila,”. “Hata hivyo uongozi wa timu unamshukuru Kocha katwila kwa wakati wote aliokua nasi ndani ya timu kama Kocha Mkuu tangu alipojiunga nasi mwaka 2020,” “Ihefu Sc inamtakia kila la kheri Kocha Katwila katika maisha yake mapya ya soka na atabaki kuwa Mwanafamilia wa MbogoMaji,”. Lakini taarifa hiyo haijasema kwa wakati huu timu itakuwa chini ya nani kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

DIARRA NA AUCHO BAADA YA MALI KUICHAPA UGANDA 1-0 JANA BAMAKO

Image
KIPA wa Mali, Djigui Diarra (kushoto) na kiungo wa Uganda, Khalid Aucho ambao wote ni wachezaji wa klabu ya Yanga baada ya mechi ya kirafiki baina ya timu zao za taifa jana Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako nchini Mali ambayo wenyeji walishinda 1-0.

SIMBA SC YAWATUMIA SALAM AL AHLY, YASHINDA 5-1 MECHI YA KIRAFIKI

Image
TIMU ya Simba SC leo imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Dar City katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Shaaban Iddi Chilunda mawili na viungo  Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana, Luis Jose Miquissone kutoka Msumbiji na Mrundi, Saido Ntibanzokiza kila mmoja moja. Simba SC inajiandaa na michuano ya CAF African Football League ikianza na mechi mbili dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri Oktoba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa na Oktoba 24 Uwanja wa Cairo International.

JONÁS MKUDE MAZOEZINI LEO YANGA IKIJIANDAA KUIVAA AZAM FC

Image
KIUNGO Jonás Mkude akiwa mazoezini leo Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam Yanga ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC Oktoba 25, mwaka huu. PICHA: WACHEZAJI WA YANGA SC MAZOEZINI LEO KIGAMBONI 

TAIFA STARS YAPANGWA NA MOROCCO, DRC NA ZAMBIA AFCON YA MWAKANI IVORY COAST

Image
TANZANIA imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast. Katika droo iliyopangwa usiku huu Jijini Abidjan, Kundi A lina wenyeji Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea na Guinea-Buissau. Kundi B linaundwa na Misri, Ghana, Cape Verde na Msumbiji, wakati Kundi C lina Senegal, Cameroon, Guinea na The Gambia. Kundi G linazikutanisha Algeria, Burkina Faso, Mauritania na Angola wakati E kuna Tunisia, Mali, Afrika Kusini na Namibia. Fainali hizo zinatarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11, 2024, hii ikiwa mara ya tatu kwa Tanzania kushiriki Kihistoria baada ya 1980 Nigeria na 2019 Misri.