Posts

YANGA PRINCESS YAITOA SIMBA QUEENS KWA MATUTA NGAO YA JAMII

Image
TIMU ya Yanga Princess imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Ngao ya Jamii kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya ushindi wa penalti 4-3 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 na watani, Simba Queens Uwanja wa jioni ya leo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Yanga Princess walitangulia kwa bao la dakika ya kwanza tu la mshambuliaji wake chipukizi mzawa, Agness Palangyo, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya, Jentrix Shikangwa Milimu kuisawazishia Simba Queens dakika ya 88. Katika mikwaju ya penalty, kipa wa Mnigeria wa Yanga Princess, Rita Akarekor aliibuka shujaa baada ya kuokoa kuokoa penalty tatu, ikiwemo ya mwisho iliyopigwa na mchezaji mkongwe, mlinzi Fatma Issa Suleiman ‘Densa’. UPSOUND: Sasa Yanga Princess watakutana na JKT Queens Jumamanosi katika Fainali hapo hapo Uwanja wa KMC, huku Simba Queens wakicheza na CEASIAA Queens kuwania nafasi ya tatu. Kwa upande wao JKT Queens walitangulia Fainali...

TANZANIA PRISONS YAICHAPA FOUNTAIN GATE 3-2 SOKOINE

Image
TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Nurdin Chona kwa penalti dakika ya 25, Ezekia Mwashilindi dakika ya 48 na Vedastus Mwihambi dakika ya 50, wakati ya Fountain Gate yamefungwa na Suleiman Mwalimu dakika ya 12 na Kassim Suleiman dakika ya 37. Kwa ushindi huo wa kwanza wa msimu, Tanzania Prisons inafikisha pointi saba katika mchezo wa sita, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 13 za mechi saba sasa.

SAMATTA AREJESHWA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI DRC KUFUZU AFCON

Image
KAIMU Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco amefanikiwa kumrejesha kikosini Nahodha Mbwana Ally Samatta ambaye alidhamiriwa kustaafu. Morocco amemjumuisha kwenye kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco. Taifa Stars watakuwa wageni wa DRC Alhamisi ya Oktoba 10 Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa, kabla ya timu hizo kurudiana siku tano baadaye, Oktoba 15 Uwanja Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mara ya mwisho Samatta aliichezea Taifa Stars Januari 24, mwaka huu kwenye mechi ya Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 dhidi ya DRC Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo timu hizo zikitoka suluhu, 0-0 ambayo Samatta alimpisha Kokola Charles William M'Mombwa dakika ya 86. Makipa; Ally Salim (Simba), Zuberi Foba (Azam FC), Yona Amos (Pamba), Mohamed Hussein (Pamba FC). Mabeki; Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Pascla Msindo (Azam FC), Mohamed Hussein (Simb...

RASMI ELLIE MPANZU KIBISAWALA NI MCHEZAJI WA SIMBA

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha winga wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Elie Mpanzu Kibisawala (22) kuwa mchezaji wake mpya kwa mkataba wa miaka miwili akitokea AS Vita ya kwao, Kinshasa.

DODOMA JIJI 0-1 SIMBA SC (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YAICHAPA DODOMA JIJI 1-0 JAMHURI

Image
TIMU ya Simba SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Bao pekee la Simba SC leo limefungwa na kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua kwa mkwaju wa penalti dakika ya 63 akimchambua kipa Mkongo, Ngeleka Alain Katembua kufuatia beki na Nahodha wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kuangushwa kwenye boksi. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 12 katika mchezo wa nne, wakati Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao sita kufuatia kucheza michezo sita msimu huu.

MASHUJAA NA AZAM NGOMA DROO, 0-0 LAKE TANGANYIKA

Image
WENYEJI, Mashujaa FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Ulikuwa mchezo mkali wa kusisimua na kosakosa zikiwemo za kugongesha nguzo pande mbili huku makipa wote, Msudan Mohamed Mustafa wa Azam na Patrick Munthary wa Mashujaa wakiokoa michomo mingi. Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi tisa, Mashujaa katika mchezo wa tano na Azam FC katika mchezo wa sita.