TUKIWAPA THAMANI WACHEZAJI WETU, WATAFANYA MAKUBWA
Na Ibrah Mkemia, DAR ES SALAAM NIANZE kwa kuliombea na kulitakia afya njema Taifa langu la Tanzania, Taifa ambalo lina watu wakarimu na wenye busara, amani, na upendo. Tukiwa bado tunaendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa hatari wa corona, yapo mambo mengi ambayo kama wanamichezo wapenda burudani ya mpira wa miguu tunapaswa kujadili kwa kina ili kuweza kupata mawazo chanya kama sio muarubaini kabisa. Kipindi hiki ambapo kuna mengi magumu tunayapiti lakni kwa uwezo wa Mungu naimani yatapita na Taifa litaendelea kubaki kama Taifa lenye malengo, matumaini ya kufika katika uchumi wa kati wa viwanda. Kama kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais kwamba Tanzania iwe nchi ya viwanda. Na kiwanda kimoja wapo kipo kwenye michezo nacho ni mpira wa miguu (kandanda). Maswali mengi ya watanzania, wapenda michezo yamekuwa yakiuliza ni kwanini tumekuwa na hatua za mtoto mdogo katika kuyatafuta mafanikio na sio hatua za mtu mzima hususani katika swala la michezo. Hili limekuwa gonjwa sugu ambal