Posts

Showing posts from September, 2022

IBRA CLASS AMDUNDA MMEXICO KWA KNOCKOUT

Image
BONDIA Ibrahim Mgender 'Ibrah Class' usiku wa jana amefanikiwa kumshinda mpinzani wake, Gustavo Pina Melgar  ‘Alan Pina’ wa Mexico kwa Knockout (KO) raundi ya tisa uzito wa Super Feather ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Mabondia wengine wa Tanzania walishinda kwa pointi, Juma Choki dhidi ya Jose Hernandez Rizo wa Mexico  uzito wa Super Feather , Emmanuel Mwakyembe dhidi ya Mkenya, Nicolaus Mwangi uzito wa Light na Adam Mrisho dhidi ya Sameer A. Pandya wa Kenya uzito wa Super Light . Mambo hayakuwa mazuri kwa Mwinyi Mzengela aliyedundwa kwa Knockout (KO) na Sabari J wa India.

PRISONS YAICHAPA AZAM FC 1-0 SOKOINE

Image
BAO pekee la Jeremiah Juma dakika ya 46, limeipa Tanzania Prisons ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons wanafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya nane, wakati Azam FC inabaki na pointi zake nane ikishukia nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi tano.

MECHI ZA AZAM, SIMBA NA YANGA ZAAHIRISHWA

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeahirisha mechi tatu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara ili kuzipa nafasi Azam, Simba na Yanga katika mechi zao za michuano ya Afrika.

YANGA SC YAICHAPA MBUNI YA ARUSHA 2-1 KIGAMBONI

Image
VIGOGO, Yanga jana wamecheza mechi ya kirafiki kambini kwao, Avic Town na kuichapa Mbuni ya Arusha 2-1, mabao yao yalifungwa na Fiston Kalala Mayele Mayele na Feisal Salum Abdallah.

DODOMA JIJI YAZINDUKA, YAILAZA GEITA GOLD 1-0

Image
WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamepata ushindi wa kwanza wa msimu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Geita Gold 1-0, bao pekee la Collins Opare dakika ya 29 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi tano na kusogea nafasi ya tisa, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake tatu nafasi ya 13 baada ya wote kucheza mechi tano.

IBRAH CLASS YUKO TAYARI KUMCHAKAZA MMEXICO KESHO MLIMANI

Image
BONDIA wa Tanzania Ibrahim Class anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mpinzani wake kutoka Mexico, Gustavo Pina katika pambano la kimataifa la uzito wa feather litakalofanyika kesho (Septemba 30) kwenye ukumbi wa Mlimani City. Akizungumza mara baada ya kupima uzito jana, Pina alisema kuwa kamwe hawzi kupoteza mapmbana mawili mfululizo na amekuja ili kurekebisha rekodi yake baada ya kupoteza pambano la ubingwa wa WBA dhidi ya bondia kutoka Panama, Anselmo Moreno mwezi Machi mwaka huu. Alisema kuwa anajua anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Class, lakini amejiandaa vilivyo kwai hawezi kurejea makosa yake tena. Kwa mujibu wa rekodi, Class ameshinda mapambano 27 ambapo kati ya hayo, 12 kwa njia ya KO na kupoteza mapambano sita ambapo mawili kwa njia ya KO. Pina ameshinda mapambano 10, matano kwa KO na kupoteza mawili yote kwa KO. “Nimesafiri umbali mrefu kuja hapa Tanzania si kwa kushindwa, lengo kuu ni kushinda, hivyo Class ajiandae kwani siwezi kupoteza kamwe,” alisema C

MOGELLA AKIMTAMBULISHA MOGELLA KWA MALECELA SIMBA SC 1991

Image
NAHODHA wa Simba mwaka 1991, Zamoyoni Mogella akimtambulisha mchezaji mwenzake, Method Mogella (sasa marehemu) kwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, John Samuel Malecela kabla ya moja ya mechi zao.

MAREHEMU KIZOTA NA ISSA WAKIWA WILLY MARTIN YANGA 1993

Image
WACHEZAJI wa Yanga SC mwaka 1993, kutoka kushoto, Said Nassor Mwamba 'Kizota' (marehemu), Willy Martin Mwakagonda 'Gari Kubwa' na Issa Athumani Mgaya (marehemu pia) kabla ya safari kwenda kwenye moja ya mechi zao msimu huo.   

OKRAH APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA KIPANGA 3-0

Image
KLABU ya Simba imekamilisha ziara yake ya mechi za kirafiki visiwani Zanzibar kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Kipanga usiku wa Jumatano Uwanja wa Amani. Mabao ya Simba yamefungwa na viungo washambuliaji Mghana, Augustine Okrah mawili, dakika ya 36 na 59 na Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kibu Dennis dakika ya 65. Huo ni ushindi wa pili kwenye ziara yao hiyo ya wiki moja kipindi hiki cha mapumziko mafupi ya Ligi Kuu ya Bara, baada ya awali kuichapa Malindi 1-0.

TANZANIA YAPATA USHINDI WA KWANZA SOKA LA UFUKWENI COSAFA

Image
TANZANIA imekaza msuli na kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya Soka la Ufukweni ya COSAFA baada ya ushindi wa 5-2 dhidi ya Mauritius leo ufukwe wa South Beach nchini Afrika Kusini. Ikumbukwe mechi zote mbili za awali Tanzania ilifungwa 4-3 na Misri na 4-2 na Uganda.

IBRAH CLASS ATAMBA KUMCHAPA BONDIA WA MEXICO

Image
BONDIA nyota   wa  Tanzania Ibrahim Class  ametamba   kumchapa   mpinzani  wake Gustavo Pina  Melgar kutoka  Mexico  katika   pambano  la  kimataifa   lililopangwa kufanyika   Ijumaa  ( Septemba  30)   kwenye   ukumbi   wa   Mlimani  City. P ambano   hilo   limeandaliwa   na   kampuni   ya  MO Boxing,  ikiwa ni   mara   ya  kwanza  kwa   kampuni   hiyo   chini   ya   mfanyabiashara maarufu , Mohammed  Dewji . Class  alisema   kuwa   baada   ya   kukaa   nje   ya   ulingo   kwa   muda mrefu ,  ameamua   kurejea   kwa   kasi   kwa   lengo  la  kutwaa   mikanda mbalimbali   ya   ngumi   za   kulipwa   nchini .’ Alisema   kuwaamejiandaa   vyema   kwa   ajili   ya   pambano   hilo   na hatamdharau   mpinzani  wake  kwani   anaamini   naye   amekuja   kwa ajili   ya   ushindi .    “ Najua   Melgar   ni   bondia   mzuri   lakini   si   kwa kufikia   kwangu ,  nimejiandaa   vyema   na   nimuonyesha   jinsi   gani Tanzania  ina   mabondia   wazuri   na   wenye   vipaji   vikubwa ,”  alisema

MSHAMBULIAJI MSERBIA, DEJAN ATANGAZA KUONDOKA SIMBA SC

Image
MSHAMBULIAJI Mserbia, Dejan Georgejevic ametangaza kuondoka Simba baada ya kuvunjiwa mkataba na klabu hiyo. “ Ninathibitisha kwamba Mkataba wangu wa Ajira umesitishwa kwa sababu za haki kutokana na ukiukwaji wa kimsingi wa Mkataba na Klabu,” ameandika Dejan katika ukurasa wake wa Instagram na kuongeza; “Asanteni mashabiki kwa support na upendo mlionipa,”.

TAIFA STARS YACHAPWA 2-1 NA LIBYA JIJINI BENGHAZI

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imechapwa mabao 2-1 na wenyeji, Libya katika mchezo wa kirafiki usiku wa Jumanne Uwanja wa Modern Jijini Benghazi. Bao pekee la Taifa Stars kwenye mchezo huo limefungwa na kiungo Said Hamisi Ndemla huo ukiwa mchezo wa pili wa kirafiki nchini humo ndani ya wiki moja baada ya awali kushinda 1-0 dhidi ya Uganda.

HUYU NDIYE MRITHI WA SENZO MAZINGISA YANGA SC

Image
YANGA leo imemtambulisha Mzambia, Adre Mtine kuwa Afisa Mtendaji wake Mkuu mpya, akichukua nafasi iliyoachwa na Senzo Masingiza, raia wa Afrika Kusini aliyejiuzulu miezi miwili iliyopita. Mtine amesaini mkataba wa miaka miwili.

SHABIKI WA SIMBA, MAN UNITED ASHINDA SH. MILIONI 49.8 ZA 10BET

Image
SHABIKI wa klabu ya Simba na timu ya Manchester United Derick Mustafa, ameshinda Sh49.8 milioni baada ya kubashiriki kwa kwa usahihi mechi 14 za ligi mbalimbali za soka duniani kupitia ‘mkeka’ wa kampuni ya 10 Bet. Mustafa ambaye ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kushinda kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kupata ugumu katika baadhi ya mechi zilizokuwa zinachezwa. Alisema mechi iliyompa wakati mgumu zaidi ni kati ya Manchester United na Sheriff Tiraspol zilizokuwa zinacheza mchezo wa ligi ya Europa na Manchester United kuibuka washindi wa mabao 2-0 kwenye uwanja wa ugenini. Kwa mujibu wa Mustafa, timu hizo hizo zilikuwa na uwiano sawa na alikuwa na wasiwasi wa timu yake kutokana na matokeo ya nyuma ambayo hayakuwa mazuri. "Nilitumia uzoefu wangu katika kutabiri mechi hiyo na baadaye kupatia ambapo Manchester United ilishinda mabao 2-0. Nilifurahi kwani mbali yaushindi nimeweza kupata fedha kwa kupitia 10Bet,” alisema,” alisema Must

TANZANIA YAENDELEA KUBORONGA SOKA LA UFUKWENI COSAFA

Image
TANZANIA imeendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya Soka la Ufukweni ya COSAFA baada ya leo kuchapwa mabao 4-3 na Misri katika ufukwe wa South Beach Arena nchini Afrika Kusini. Ikumbukwe mechi ya kwanza Tanzania ilichapwa 4-2 na Uganda juzi hapo hapo South Beach.

TANZANIA YAITOA SUDAN KUSINI KWA MABAO YA UGENINI AFCON U23

Image
TANZANIA imefanikiwa kusonga mbele katika kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 licha ya sare ya 3-3 na Sudan Kusini leo Uwanja wa Hure mjini Butare nchini Rwanda. Mabao ya Tanzania yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 10 kwa penalti, Ally Msengi dakika ya 40 na Kelvin John dakika ya 67, wakati ya Sudan Kusini yamefungwa na Dani Thon dakika ya 25, Joseph Manase dakika ya 53 na Rehan Malong dakika 66 kwa penalti. Kutokana na mechi ya kwanza kumalizia kwa sare ya 0-0 Dar es Salaam, Tanzania inasonga mbele kwa faida ya mabao ya ugenini na sasa itakutana na Nigeria.

MAYELE APIGA MBILI, YANGA YASHINDA 4-1 KIGAMBONI

Image
KLABU ya Yanga jana asubuhi imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Eagle Air Force ya Daraja la Nne katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Avic Town, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yalifungwa na Wakongo, beki Joyce Lomalisa na mshambuliaji, Fiston Kalala Mayele mawili na lingine beki Mzanzibari, Ibrahim Bacca. Bao pekee la Eagle Air Force ya Ubungo, timu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi (JWTZ) inayofundishwa na kocha Joseph Kanakamfumu, lilifungwa na Kennedy Bago.

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA FUMO FELICIAN

Image
 

SIMBA SC YAICHAPA MALINDI 1-0 MECHI YA KIRAFIKI ZANZIBAR

BAO pekee la Nassor Kapama dakika ya 13 limetosha kuipa  Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya 13 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Malindi katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

TANZANIA YACHAPWA 4-2 NA UGANDA MICHUANO YA COSAFA

Image
TANZANIA imechapwa mabao 4-2 na Uganda katika mchezo wa Soka la Ufukweni michuano ya COSAFA inayoendelea katika ufukwe es South Beach Arena Jijini nchini Afrika Kusini.

TAIFA STARS YAICHAPA UGANDA 1-0 BAO LA MSUVA

Image
BAO pekee la Simon Happygod Msuva dakika ya 28 limeipa Tanzania ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa usiku wa Ijumaa Uwanja wa Modern Jijini Benghazi, Libya. Taifa Stars itashuka tena dimbani Jumanne kumenyana na wenyeji, Libya katika mchezo wa mwisho wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), kabla ya kurejea nyumbani.

SERENGETI BOYS YAICHAPA SUDAN KUSINI 1-0 KARATU

Image
TIMU ya taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu.

AZAM FC YATOA SARE 1-1 NA TP MAZEMBE NDOLA

Image
TIMU ya Azam FC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Levy Mwanawaswa Jijini Ndola nchini Zambia. Bao la Azam FC limefungwa na kiungo mshambuliaji Muivory Coast, Kipre Junior dakika ya 36, kabla ya Zemanga kuisawazishia TP Mazembe dakika ya 57.

KARIA, NYAMLANI NA BARBARA WAULA CAF

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewateua Watanzania wanne katika Kamati zake tofauti, akiwemo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba.

MORRISON AFUNGIWA MECHI TATU, ARAJIGA KIKAANGONI

Image
WINGA Mghana wa Yanga, Bernard Morrison amefungiwa mechi tatu kwa kumchezea rafu mchezaji wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda katika mechi baina ya timu hizo, wakati refa wa mechi hiyo Ahmed Arajiga amepelekwa Kamati ya Waamuzi.

SIMBA SC WAENDA ZANZIBAR KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI

Image
KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka kesho kwenda Zanzibar kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki kipindi huku cha mapumziko ya Ligi Kuu kupisha kalenda ya FIFA ya mechi za kirafiki za Kimataifa.

MAKOCHA WOTE WA CHAMPIONSHIP WATAKIWA KUWA NA DIPLOMA C YA CAF

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kimeagiza makocha wote wa timu za Championship wawe na Daraja la Elimu ya Diploma C ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) au zaidi.

GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE NA SINGIDA STARS 1-1 KIRUMBA

Image
TIMU ya Geita Gold imelazimishwa sare ya 1-1 na Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Geita Gold ilitangulia na bao la mfungaji bora wa msimu uliopita, George Mpole dakika ya tisa tu, kabla ya Mbrazil Rodrigo Figueiredo kuisawazishia Singida Big Stars dakika ya 42: Kwa matokeo hayo, Singida Big Stars inafikisha pointi nane na kusogea nafasi ya tano, wakati Geita Gold sasa wana pointi tatu katika nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi nne.

BODI YAFANYA TENA MABADILIKO YA RATIBA LIGI KUU

Image
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya marekebisho madogo ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuipa nafasi timu ya taifa katika mechi zake za kirafiki za Kimataifa.

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA JUMA AMIR MAFTAH

Image
 

KMC YAICHAPA IHEFU SC 2-1 UWANJA WA UHURU

Image
WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mabao ya KMC yamefungwa na Matheo Anthony dakika ya tatu na Nzigamasabo Steve dakika ya 77, wakati la Ihefu SC limefungwa na Raphael Daudi dakika y 34. KMC inafikisha pointi tano baada ya ushindi huo ikisogea nafasi ya nane, wakati Ihefu inaendelea kuwa timu pekee ambayo haijavuna pointi hadi sasa kufuatia wote kucheza mechi nne.

SSEMWOGERERE KOCHA MPYA PAMBA FC

Image
NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda, George Ssemwogerere ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Pamba ya Mwanza akichukua nafasi ya Mkenya, Yussuf Chipo aliyehamia Coastal Union ya Tanga. Pamba, mabingwa wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanapambana kurejea Ligi Kuu kutoka Championship iliyoanza mwishoni mwa wiki wakipata ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Ken Gold ya Mbeya. Mechi hiyo ya kwanza timu ilikuwa chini ya kocha mwingine mzoefu nchini, Steven Matata aliyekuwa Msaidizi wa Chipo wakati wa maandalizi ya msimu na mechi ijayo Jumamosi dhidi ya Mbeya Kwanza ndiyo Ssemwogerere ataanza kazi.

ALLY MAYAY TEMBELE MKURUGENZI MPYA WA MICHEZO

Image
ALIYEWAHI kuwa Nahodha wa timu ya taifa na klabu ya Yanga, Ally Mayayi Tembele ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo akichukua nafasi ya Yusuph Singo.