Posts

Showing posts from August, 2023

AZAM TV SASA KUONYESHA LIGI YA KENYA MIAKA SABA BILIONI 23

Image
KAMPUNI ya Azam Media Limited jana imeingia mkataba na Shirikisho la Soka Kenya (FKF) wa haki ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya Kenya wenye thamani ya Shilingi za Tanzania Bilioni 23 kwa muda wa miaka saba.  Mkataba huo umesainiwa jana Jijini Nairobi nchini, Kenya ukishuhudiwa pamoja na Maafisa hao Azam Media na FKF lakini pia walikuwepo viongozi wa klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Kenya.

SINGIDA YATOA SARE NYINGINE NYUMBANI 0-0 NA TABORA UNITED

Image
TIMU ya Singida Fountain Gate imelazimishwa sare ya bila kufungana na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Ni sare ya pili mfululizo Singida ‘ The Big Stars’ wanatoa, tena za bila mabao katika mechi mbili za mwanzo za msimu nyumbani baada ya kutoka suluhu pia na Tanzania Prisons kwenye mechi ya kwanza. Kwa upande wao Tabora United, zamani Kitayosce leo wameokota pointi ya kwanza ya Ligi kufuatia kufungwa mabao 4-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. 

CHELSEA WATINGA RAUNDI YA TATU KOMBE LA LIGI ENGLAND

Image
TIMU ya Chelsea imefanikiwa kwenda ya Tatu ya Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AFC Wimbledon ya Daraja la Pili katika mchezo uliofanyika Uwanja wa  Stamford Bridge Jijini London  usiku wa jana. Haukuwa ushindi mwepesi kwa Vijana wa Kocha Muargentina, Mauricio Pochettino, kwani walilazimika kutoka nyuma kwa mabao ya Noni Madueke kwa penalti dakika ya 45 na ushei na Enzo Fernandez dakika ya 72 kufuatia AFC Wimbledon kutangulia na bao la James Tilley dakika ya 19 kwa penalti pia. Kwa ushindi huo, The Blues watakutana na wapinzani wa Ligi Kuu ya England katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, Brighton & Hove Albion Septemba 26 hapo hapo Stamford Bridge.

JKT QUEENS MABINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI WANAWAKE

Image
WACHEZAJI wa JKT Queens wakifurahia na Kombe lao la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya CBE y Ethiopia leo Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha FUFA, Njeru mjini Kampala nchini Uganda leo katika mchezo wa Fainali. PICHA: JKT QUEENS WAKIFURAHIA UBINGWA WA CECAFA WANAWAKE 

SABA YANGA WAITWA TAIFA STARS, SIMBA WANNE, AZAM…

Image
WACHEZAJI saba wa klabu bingwa ya Tanzania, Yanga SC wameitwa katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast dhidi ya Algeria Septemba 7 Jijini Algiers. Watani wao, Simba wametoa wachezaji wanne, huku Azam FC ikitoa wachezaji mmoja tu. Taifa Stars itamenyana na Algeria Septemba 7 Uwanja wa Mei Venue Stade du 19, 1956 Annaba ikihitaji ushindi ili kufuzu AFCON. Kwa sasa Algeria ambayo imekwishafuzu inaongoza Kundi F kwa pointi 15, ikifuatiwa a Tanzania yenye pointi saba, wakati ina pointi nne mbele ya Níger wanaoshika mkia kwa pointi zao mbili. Uganda itamaliza na Níger siku hiyo hiyo, Septemba 7 Uwanja wa Marrakech nchini Morocco. Tanzania imefuzu AFCON mara mbili tu kihistoria, mwaka 1980 nchini Nigeria na mwaka 2009 nchini Misri.

YANGA SC 5-0 JKT TANZANIA (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

MAX NZENGELI APIGA MBILI YANGA YAUA 5-0 TENA

Image
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC baada ya kuitandika JKT Tanzania mabao 5-0 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na nyota wake wa kigeni, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 45 na ushei, Mzambia Kennedy Musonda dakika ya 54, Muivory Coast Kouassi Attohoula Yao dakika ya 64 na Mkongo Max Mpia Nzengeli mawili, dakika ya 79 na 88. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi sita na kupanda kileleni ikizizidi wastani wa mabao Azam FC na Simba SC baada ya wote kucheza mechi mbili, wana Jangwani wakijiwekea rekodi ya kipekee kuvuna mabao 10 kwenye mechi mbili. 

SINGIDA BIG STARS YAACHANA NA HANS VAN DER PLUIJM

Image
KLABU ya Singida Fountain Gate imeachana na Kocha wake Mholanzi, Hans van der Pluijm kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu tangu kuanza kwa msimu licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa kikosini.

AZAM FC 3-1 TANZANIA PRISONS (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMON MSUVA AJIUNGA NA JS KABYLIE YA ALGERIA

Image
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Simón Happygod Msuva amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na klabu ya JS Kabylie ya Algeria kutoka Al Qadisiya ya Saudi Arabia.

AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA PRISONS 3-1

Image
TIMU ya Azam FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 11 na wazawa Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 47 na Nathaniel Chilambo dakika ya 82, wakati la Prisons limefungwa na Zabona Khamis dakika ya 90 na ushei. Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi sita sawa na Simba, lakini wanakaa kileleni kwa wastani mzuri wa mabao, wakati Prisons inabaki na pointi yake moja baada ya wote kucheza mechi mbili mbili.

SIMBA SC YAACHANA NA WINGA MMALAWI PETER BANDA

Image
KLABU ya Simba imeachana na winga wake Mmalawi, Peter Banda baada ya misimu miwili tangu ajiunge na Wekundu hao wa Msimbazi akitokea Big Bullets ya kwao, Malawi.

ABDALLAH SHAIBU ‘NINJA’ ATUA FC LUBUMBASHI YA KONGO

Image
BEKI Mzanzibari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amejiunga klabu ya  FC Lubumbashi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga ya Dar es Salaam.

KMKM YACHAPWA 3-1 NA KUTUPWA NJE ETHIOPIA LIGI YA MABINGWA

Image
TIMU ya KMKM ya Zanzibar imetupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-1 na wenyeji, St George katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali usiku wa Jumapili Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, Ethiopia. Mabao ya St George yamefungwa na  viungo Dawit Tefera Alemu dakika ya 49, Natnael Zeleke Tadesse dakika ya 65 na mshambuliaji Abel Yalew Tilahun dakika ya 79, baada ya KMKM kutangulia na bao la mshambuliaji wake, Salum Akida Shukuru dakika ya 24. Kwa matokeo hayo, St George wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2 kufuatia kushinda 2-1 kwenye mechi ya kwanza Jijini Dar es Salaam na sasa watamenyana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.

NUNEZ ATOKEA BENCHI DAKIKA ZA JIONI KUIBEBA LIVERPOOL

Image
TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya wenyeji, Newcastle United leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Venue St. James' Park, Newcastle upon Tyne. Newcastle United walitangulia na bao la Anthony Gordon dakika ya 25, kabla ya Liverpool kupata pigo kufutia beki wake, Virgil van Dijk kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 28. Shujaa wa Liverpool leo ni Darwin Nunez aliyetokea benchi dakika ya 77 na kufunga mabao yote dakika ya 81 na 90 na ushei huo ukiwa ushindi wa pili katika mechi tatu, nyingine wakitoa sare. Newcastle United baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao tatu za mechi tatu sasa.

JKT QUEENS YATINGA FAINALI KLABU AFRIKA MASHARIKI NA KATI WANAWAKE

Image
TIMU ya JKT Queens imefanikiwa kuingia Fainali ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake Afrika Mashariki na Katí baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Burundi leo Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha FUFA, Njeru nchini Uganda. Mabao ya JKT Queens yamefungwa na Donisia Minja, Stumai Abdallah na Winfrida Gerlad, wakati bao pekee la la Abuja Queens limefungwa na Teopostar Situma. Sasa JKT Queens itakutana na mshindi kati ya CBE F.C.  ya Ethiopia Vihiga Queens FC ya Kenya zinazomenyana hivi sasa katika Fainali ambayo itapigwa Jumatano.

MAN UNITED YATOLA NYUMA KWA 2-0 NA KUSHINDA 3-2

Image
WENYEJI, Manchester United wametoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 3-2 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa  Old Trafford Jijini Manchester. Nottingham Forest ilitangulia kwa mabao ya Taiwo Awoniyi dakika ya pili na Willy Boly dakika ya nne, kabla ya Manchester United kuzinduka kwa mabao ya Christian Eriksen dakika ya 17, Casemiro dakika ya 52 na Bruno Fernandes dakika ya 76 kwa penalti. Hata hivyo, Nottingham Forest wanaobaki na pointi zao tatu za mechi tatu - walimaliza pungufu mchezo huo baada ya beki Joseph Adrian Worrall kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 67 na kwa ushindi huo Man United wanafikisha pointi sita katika mchezo wa tatu pia.

MAX APIGA MBILI YANGA YAWACHAPA ASAS 5-1 CHAMAZI

Image
MABINGWA wa Tanzania wamefanikiwa kwenda Raundiya mwisho ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya AS Ali Sabieh (ASAS) ya Djibouti leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na winga Mkongo, Max Mpia Nzengeli dakika ya saba na 90 na ushei, mshambuliaji Mghana Hafiz Konkoni dakika ya 45, kiungo Muivory Coast Pacome Zouazoua na mshambuliaji chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Clement Mzize dakika ya 69, wakati bao pekee la ASAS limefungwa na Tito Mayor kwa penalti dakika ya 85. Yanga inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 7-1 baada ya kuichapa AS Ali Sabieh 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita hapo hapo Azam Complex na sasa itakutana na Al-Merreikh ya Sudan mechi ya kwanza wakianzia ugenini Septemba 15 na marudiano na dar es Salaam Septemba 29.

RAHEEM STERLING APIGA MBILI CHELSEA YASHINDA 3-0

Image
TIMU ya Chelsea imepata ushindi wa kwanza chini ya kocha Muargentina, Mauricio Pochettino baada ya kuichapa Luton Town FC mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Mabao ya The Blues yalifungwa na washambuliaji Muingereza Raheem Sterling, mawili dakika ya 17 na 68 na Mgambia Nicolas Jackson dakika ya 75. Chelsea inafikisha pointi nne katika mchezo wa tatu kufuatia sare ya 1-1 na Liverpool Agosti 13 hapo hapo Stamford Bridge na kichapo 3-1 kutoka kwa West Ham United Agosti 20 Uwanja wa London. Kwa upande wao Luton Town FC wanapokea kipigo cha pili mfululizo wakitoka kufungwa 4-1 na Brighton & Hove Albion Agosti 12 Uwanja wa The Amex.

AZAM FC ILIVYOTOLEWA NA BAHIR DAR CHAMAZI

Image
 

AZAM FC YATOLEWA KWA MATUTA KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
TIMU ya Azam FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 3-3 na Bahir Dar ya Ethiopia leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Dakika 90 za leo zilimalizika kwa Azam FC kushinda 2-1 na kufanya sare ya jumla ya 3-3 baada ya Bahir Dar kushinda 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa. Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya kwanza na Prince Dube dakika ya 10, wakati la Bahir Dar limefungwa na Habtamu Tadesse dakika ya 17. Katika mikwaju ya penalti kipa Mghana wa Azam FC, Idrissou Abdulai aliokoa penalti moja ya Bahir Dar na moja ikaenda juu ya lango. Upande wa Azam FC waliofunga ni Yanick Bangala, Feisal Salum na Cheikh Sidibe, wakati Sospeter Bajana, Idris Mbombo na Djibril Sylla wote wamekosa.  VÍDEO: MIKWAJU YA PENALTI AZAM FC V BAHIR DAR

YANGA SC 5-0 KMC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

YAMGA SC YAANZA LIGI KWA KISHINDO, KMC YAFA 5-0

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameanza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuitandika KMC mabao 5-0 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na beki Dickson Job dakika ya 17, viungo Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 58, mshambuliaji Mghana Hafiz Konkoni dakika ya 69 na viungo Mzanzibari Mudathir Yahya dakika ya 76 na Muivory Coast Pacome Zouazoua dakika ya 80. Ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Yanga msimu huu, huku KMC wakicheza mechi ya pili baada ya sare ya 1-1 ugenini na Namungo FC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

CLARA LUVANGA WA YANGA ASAINI MIAKA MITATU KLABU YA HISPANIA

Image
MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya vijana ya wanawake Tanzania, Clara Cletus Luvanga amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Dux Logrono ya Hispania kutoka Yanga Princess ya nyumbani. Dux Logroño kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake, ambayo ni ya pili kwa ukubwa Hispania inayojulikana kama Reto Iberdrolana. Timu hiyo ipo chini ya kocha Gerardo García León, ambaye ni beki wa zamani wa kulia klabu za Villarreal, Valencia na Real Socieadad pamoja na timu C na B za Real Madrid.

SINGIDA BIG STARS YAAMBULIA SULUHU KWA PRISONS LITI

Image
WENYEJI, Singida Fountain Gate ‘ The Big Stars’ wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI, Singida.

ARSENAL YAICHAPA CRYSTAL PALACE 1-0 BAO LA TUTA EMIRATES

Image
WASHINDI wa Ngao ya Jamii, Arsenal wameshinda mechi ya pili mfululizo ya Ligi Kuu ya England baada ya usiku wa jana pia kuwalaza wenyeji, Crystal Palace 1-0 Uwanja wa Selhurst Park Jijini London. Bao pekee la Washika Bunduki hao limefungwa na kiungo Mnorway, Martin Odegaard kwa penalti dakika ya 53 kufuatia kipa Sam Johnstone kumchezea faulo Eddie Nketiah kwenye boksi. Lakini Arsenal ilimaliza pungufu mchezo huo kufuatia Takehiro Tomiyasu kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 67. Ikumbukwe mechi ya kwanza Vijana wa Mikel Arteta waliichapa Nottingham Forest 2-1 Uwanja wa Emirates, wakati Crystal Palace ilianza na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Sheffield United.

MASHUJAA YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA GEITA GOLD KIGOMA

Image
TIMU ya Mashujaa FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Hiyo ni sare ya kwanza kwa timu zote baada ya kuanza na ushindi katika mechi za kwanza, Mashujaa ikiichapa Kagera Sugar 2-0 hapo hapo Lake Tanganyika na Geita Gold ikiwalaza wenyeji, Ihefu SC huko Mbarali mkoani Mbeya.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA SHAURI IDDI

Image
 

SIMBA SC 2-0 DODOMA JIJI (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

WEST HAM YAICHAPA CHELSEA 3-1 LONDON

Image
WENYEJI, West Ham United wameitandika Chelsea mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London Jijini London. Mabao ya West Ham United yamefungwa na Nayef Aguerd dakika ya saba, Michail Antonio dakika ya 53 na Lucas Paqueta dakika ya 90 kwa penalti, wakati bao pekee la Chelsea limefungwa na Carney Chukwuemeka dakika ya 28. Ni ushindi wa kwanza kwa West Ham baada ya sare ya 1-1 ugenini na AFC Bournemouth, wakati Chelsea inapoteza mechi ya kwanza baada ya sare ya 1-1 nyumbani na Liverpool.

YANGA SC YAWACHAPA ASAS 2-0 CHAMAZI

Image
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, ASAS ya Djibouti katika mchezo wake wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na wachezaji wake wa kigeni, kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 22 na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda dakika ya 53. Timu hizo zitarudiana Agosti 26 hapo hapo Chamazi Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya kati ya Otoho ya Kongo Brazzaville na El Mereikh ya Sudan kuwania tiketi ya makundi.

HISPANIA MABINGWA KOMBE LA DUNIA WANAWAKE 2023

Image
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya wanawake ya Hispania wakifurahia na Kombe la Dunia baada ya kuichapa England 1-0 pekee la Olga Carmona leo mjini Sydney, Australia.

AZAM FC YACHAPWA 2-1 NA BAHIR DAR LEO ETHIOPIA

Image
TIMU ya Azam FC imefungwa Mabao 2-1na wenyeji, Bahir Dar katika mchezo wake wa kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mabao yote ya Bahir Dar yamefungwa na Fitsum Gebremariam dakika ya 20 na 60, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji wa wake Mkongo, Idris Ilunga Mbombo dakika ya 72. Timu hizo zitarudiana Agosti 25 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na Club Africain ya Tunisia kuwania kuingia hatua ya makundi.

MTIBWA SUGAR YATOA SARE 1-1 NA COASTAL UNION MANUNGU

Image
WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Unión ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Coastal Union walitangulia kwa bao la Ibrahim Ajibu dakika ya 70, kabla ya Kassim Haruna ‘Tiote’ kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 84, kila timu ikiokota pointi ya kwanza ndani ya mechi mbili baada ya wote kupoteza mechi za kwanza. Wakati Mtibwa Sugar ilifungwa 4-2 na Simba SC hapo hapo Manungu, kwa upande wao Coastal Unión walichapwa 2-1 na wenyeji, Dodoma Jiji Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

MAN CITY YAWACHAPA NEWCASTLE UNITED 1-0 ETIHAD

Image
BAO pekee la Julian Alvarez dakika ya 31 jana lilitosha kuipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Ni ushindi wa pili mfululizo kwa mabingwa hao watetezi, baada ya ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Burnley, wakati Newcastle inapoteza mchezo wa kwanza kufuatia kuanza na ushindi wa 5-1 dhidi ya Aston Villa.

NAMUNGO FC YAAMBULIA SARE YA 1-1 KWA KMC RUANGWA

Image
TIMU ya Namungo imecheza mechi ya pili nyumbani ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara bila ushindi baada ya leo kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. KMC walitangulia na bao la Rashid Chambo dakika ya 69, kabla ya mshambuliaji Mkongo, Fabrice Ngoye kuisawazishia Namungo FC kwa penalti dakika ya 80. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza katika msimu mpya kwa KMC, wakati Namungo mechi yao ya kwanza walifungwa 1-0 na JKT Tanzania hapo hapo Majaliwa.

LIVERPOOL YAICHAPA BOURNEMOUTH 3-2 ANFIELD

Image
WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool. Mabao ya Liverpool inayofundishwa na Kocha Mjerumani, Jurgen Klopp yamefungwa na Luis Diaz dakika ya 27, Mohamed Salah dakika ya 36 na Diogo Jota dakika ya 62 katika mchezo ambao kiungo wake Muargentina, Alexis Mac Allister alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 58 Bao pekee la Bournemouth lilifungwa na mshambuliaji Mghana, Antoine Semenyo dakika ya tatu hicho kikiwa kipigo cha kwanza kwao msimu huu baada ya sare ya 1-1 nyumbani na West Ham United, huku Liverpool ikifikisha pointi nne baada ya sare ya 1-1 ugenini na Chelsea.

KOCHA WA ZAMANI WA YANGA SC, SAM TIMBE AFARIKI DUNIA

Image
ALIYEWAHI kuwa kocha wa Yanga, Mganda San Timbe (69) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Nakasero Jijini Kampala, alipokuwa amelazwa wadi ya wagonjwa taabani (ICU). Sam Timbe amefariki akiwa kocha wa klabu ya URA FC ambayo imethibitisha msiba huo unaokuja siku moja kabla ya timu hiyo kumenyana na KCCA katika Nusu Fainali ya michuano ya Nane Bora ya Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) Super Eight Uwanja wa Lugogo. Timbe alikuwa kocha wa Yanga msimu wa 2010 - 2011 akiipa timu hiyo mataji ya ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Kagame kabla ya kufukuzwa na nafasi yake kuchukua Mserbia, Kostadin Papic. Timbe aliyezaliwa Januari 1, mwaka 1954 kwa baba Stanley Wabuteya na Dorothy Wabuteya, alipata elimu yake katika shule ya Msingi Bupoto, kabla ya kwenda sekondari ya Nabumali na baadaye Chuo cha & Tororo. Katika soka alianza kama kipa wa klabu ya Coffee FC ya kwao na alipostaafu akafundisha klabu mbalimbali na kwa mafanikio zikiwemo Coffee, Polisi, Lyantonde, Mbale Heroes, Simba FC, S

SINGIDA STARS YAITANDIKA JKU 4-1 KOMBE LA SHIRIKISHO CHAMAZI

Image
TIMU ya Singida Fountain Gate ‘Big Stars’ imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusogea mbele kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKU ya Zanzibar usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Singida Fountain Gate leo yamefungwa na viungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya nne na 39 yote kwa penalti, Mnigeria Maurice Chukwu dakika ya 44 na Duke Abuya dakika ya 47, wakati la JKU limefungwa na Saleh Abdullah kwa penalti pia dakika ya 63. Timu hizo zitarudiana Agosti 27 hapo hapo Azam Complex na mshindi wa jumla atamenyana na Future ya Misri.

KMKM YAANZA VIBAYA AFRIKA, YACHAPWA 2-1 NA ST GEORGE CHAMAZI

Image
TIMU ya KMKM imejiweka njia panda katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-1 na St George ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana Agosti 27 Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, Ethiopia na mshindi wa jumla atakutana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri.

MTIBWA SUGAR 2-4 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 4-2 PALE PALE MANUNGU

Image
TIMU ya Simba imeanza vyema Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Jean Othos Baleke dakika ya tano na viungo, Mcameroon Willy Essomba Onana dakika ya tisa, Mkongo Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 45 na Mzambia Clatous Chotta Chama dakika ya 81. Kwa upande wa wenyeji, Mtibwa Sugar mabao yote yamefungwa na mshambuliaji wao mpya, mzawa Matheo Anthony Simon dakika ya 20 na 22.

NI MANCHESTER CITY WASHINDI WA UEFA SUPER CUP

Image
TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutwaa taji la UEFA Super Cup kwa mara ya kwanza katika histora yao baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Sevilla kufuatia sare ya 1-1 usiku wa jana Uwanja wa Georgios Karaiskáki mjini Athens nchini Ugiriki. Sevilla, mabingwa wa UEFA Europa League walitangulia kwa bao la Youssef En-Nesryi dakika ya 25, kabla ya Cole Palmer kuwasawazishia Manchester City, mabingwa wa UEFA Champions League dakika ya 63. Na katika mikwaju ya penalti, waliofunga za Man City ni Mnorway Erling Haaland, Muargentina Julián Álvarez, Mcroaria, Mateo Kovačić na Waingereza Jack Grealish na Kyle Walker, wakati za Sevilla zilifungwa na Muargentina, Lucas Ocampos, Mspaniola, Rafa Mir, Mcroatia Ivan Rakitić na Muargentina Gonzalo Montiel, huku  Nemanja Gudelj pekee akikosa.

FEISAL APIGA HAT TRICK AZAM YAICHAPA KITAYOSCE 4-0

Image
WENYEJI, Azam FC wameanza vyema Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kitayosce ya Tabora usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 18 tu, mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Feisal Salum Abdallah matatu dakika za tatu, tisa na 13 huku lingine likifungwa na Prince Dube Mpumelelo dakika ya tano. Sababu za mechi hiyo kuishia dakika ya 18 ni Kitayosce kubaki na wachezaji watano uwanjani baada ya wawili kati ya saba walioanza kuumia, hivyo kwa mujibu wa kanuni refa akamaliza mchezo. Kitayosce ililazimika kuanza na wachezaji saba tu baada ya wengine wote kutokuwa na leseni za kuwaruhusu kucheza. VIDEO: HAT TRICK YA FEISAL DHIDI YA KITAYOSCE VIDEO: BAO LA PRINCE DUBE V KITAYOSCE VIDEO: UFAFANUZI WA BODI YA LIGI MECHI KUVUNJWA

MASHUJAA YAWAKANDA KAGERA SUGAR 2-0 LAKE TANGANYIKA

Image
WENYEJI, Mashujaa FC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Mabao ya Mashujaa FC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu yamefungwa na Adam Adam dakika ya 15 na Othman Dunia dakika ya 73 wakifuata nyayo za JKT Tanzania iliyopanda pia msimu na kuanza na ushindi wa 1-0 jana ya wenyeji, Namungo FC.

YANGA SC KUSHIRIKIANA NA KITUO CHA MORO KIDS

Image
KLABU ya Yanga imeingia makubaliano na kituo cha kukuza vipaji cha Moro Kids kilichopo Morogoro juu ya kujenga uwezo kitaaluma, vifaa vya michezo, uwezeshaji wa kiuchumi, kubadilishana uzoefu na utafutaji wa masoko kwa wachezaji wanaozalishwa katika kituo.

KITAYOSCE YAFUTIWA ADHABU, KUIVAA AZAM FC NA KIKOSI KAMILI

Image
KLABU ya Kitayosce imefutiwa adhabu ya kutofanya usajili katika dirisha hili - hivyo iko huru kuwatumia wachezaji wake wote katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhido ya wenyeji, Azam FC.

MWENYEKITI WA SIMBA SC AHUDHURIA KOZI YA FIFA AUSTRALIA

Image
MWENYEKITI wa Bodi ya Simba SC, Salim Abdallah Muhene 'Try Again' amehudhuria kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika jijini Sydney, Australia. Akiwa huko, Try Again amepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino kuhusu Africa Super League na ushiriki wa Simba kwenye michuano hiyo pamoja na kuzungumzia mambo mengi yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na hasa Tanzania. Rais Infantino amepongeza hatua kubwa ya maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na zaidi Tanzania.  Ameipongeza pia Tanzania kwa kazi kubwa ambayo inafanyika katika kukuza mpira akifurahishwa zaidi Simba na vilabu vingine chini ya usimamizi mzuri wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

KITAYOSCE YAFUNGIWA KUSAJILI LEO INACHEZA NA AZAM FC CHAMAZI

Image
WAKATI leo inashuka dimbani kumenyana na Azam FC katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, klabu ya Kitayosce imefungiwa kusajili katika dirisha hili la usajili kwa kosa la kutowalipa wachezaji wake wa kigeni waliopandisha timu.

DODOMA JIJI WANG’ARA MECHI YA KWANZA YA LIGI KUU NYUMBANI

Image
WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Unión katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwa Dodoma Jiji, kwani walilazimika kutoka nyuma baada ya Coastal Unión kutangulia na bao la dakika ya 46 Hijja Ugando, kabla ya wenyeji hao kuzinduka kwa mabao ya kipa Justin Ndikumana aliyejifunga dakika y 54 na Meshack Abraham dakika ya 60. Dodoma Jiji wanakuwa wenyeji pekee leo kupata ushindi katika mechi za kwanza za msimu baada ya Ihefu kufungwa 1-0 Geita Gold Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya na Namungo FC kuchapwa 1-0 pia na JKT Tanzania Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

MAZOEZI YA AZAM FC KUJIANDAA NA MECHI YA KWANZA YA LIGI KUU

Image
MSHAMBULIAJI Msenegal wa Azam FC, Alassane Diao akiwa mazoezini leo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kesho dhidi ya Kitayosce, Tabora United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. PICHA: AZAM FC MAZOEZINI LEO

KIPA MPYA MMOROCCO MAZOEZINI SIMBA SC LEO MOROGORO

Image
KIPA mpya wa Simba SC, Mmorocco Ayoub Lakred akiwa mazoezini leo Morogoro kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Alhamisi mjini humo. VIDEO: AYOUB LAKRED ALIVYOKARIBISHWA MAZOEZINI SIMBA SC LEO MOROGORO

NAMUNGO FC YAANZA NA KICHAPO CHA JKT 1-0 RUANGWA

Image
BAO la Martin Kigi dakika ya 43 limeipa mwanzo mbaya Namungo FC nyumbani baada ya kuchapwa 1-0 na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

GEITA GOLD YAANZA VYEMA LIGI KUU, YAICHAPA IHEFU 1-0

Image
BAO pekee la Elias Maguri dakika ya tano limetosha kuipa Geita Gold ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ihefu SC katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.