Posts

Showing posts from November, 2023

COASTAL UNION YAIKANDA GEITA GOLD 3-1 MKWAKWANI

Image
WENYEJI, Coastal UniĆ³n wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Geita Gold ilitangulia kwa bao la Valentino Mashaka dakika ya 12, kabla ya Coastal UniĆ³n kutoka nyuma kwa mabao ya kiungo Mbenin, Roland Junior Beakou dakika ya 30, Maabad Maulid dakika ya 53 na Charles Semfuko dakika ya 59. Kwa ushindi huo, Coastal UniĆ³n inafikisha pointi 13 na kusogea nafasi ya tisa, sawa na Geita Gold inayoshukia nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 12.

TWIGA STARS YATANGULIZA MGUU MMOJA WAFCON 2024

Image
TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Togo katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili na ya mwisho ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) 2024 leo Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Mabao ya Twiga Stars yamefungwa na mshambuliaji wa Besiktas ya Uturuki, Opa Clement mawili, dakika ya 45 na ushei kwa penalti na dakika ya 81, huku lingine Yawa Konou wa Togo akijifunga dakika ya 57. Timu hizo zitarudiana Desemba 5 Uwanja wa KĆ©guĆ© Jijini LomĆ© na mshindi wa jumla atakuwa amejikatia tiketi ya WAFCON ya Morocco mwakani.

HERSI MWENYEKITI WA KWANZA CHAMA CHA KLABU ZA SOKA AFRIKA

Image
RAIS wa Yanga, Hersi Ally Said ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Klabu za Soka Afrika katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Marriot Mena House, Cairo. Chama cha Klabu za Afrika kinalenga kuwaleta pamoja wadau kutoka nyanja mbalimbali za soka barani Afrika, kukuza ushirikiano, uvumbuzi na ubora ndani ya eneo la soka la klabu za bara hili, hili likiwa wazo la Rais wa CAF mwenyewe, Dk Motsepe alipokutana na Wenyekiti wa klabu za Afrika Oktoba5, 2023 na kuwaarifu kuhusu kuundwa kwa Chama hichokwa malengo yafuatayo: 1. kulinda na kukuza maslahi ya Vilabu vya Soka vya Afrika. 2. kuhakikisha kuwa Vilabu vya Soka vya Afrika vina uwezo wa kibiashara, ushindani wa kimataifa na kuleta faida 3. kuhakikisha kuwa Waamuzi, Kamishna wa Mechi na waendeshaji VAR wanaheshimiwa, wanaaminika, wanajitegemea na wa kiwango cha kimataifa. 4. kujenga ubia na wafadhili, sekta binafsi na Serikali kujenga viwanja vinavyoendana na viwango vya CAF na FIFA na miundombinu na vifaa vingine vya mp

BENCHIKA AKUTANA NA WACHEZAJI TAYARI KUANZA KAZI SIMBA SC

Image
BAADA ya kutambulishwa rasmi jana, Kocha mpya Mkuu wa Simba SC, Mualgeria Abdelhak Benchikha leo amekutana na wachezaji na kuzungumza nao kwmbini Mbweni Jijini Dar es Salaam. Benchika anatarajiwa kuanza kukinoa kikosi cha Simba kuelekea mchezo wake wa pili Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, wa Jwaneng Galaxy Jumamosi Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana. Ikumbukwe mechi ya kwanza ya Kundi B Ligi ya Mabingwa, Simba ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Na kama utakumbuka jana wakati Benchika anatambulishwa aliahidi kurejesha furaha kwa mashabiki wa Simba iliyopotea baada ya timu kwenda mechi tatu mfululizo bila ushindi tangu ifungwe 5-1 na Yanga Novemba 5, ikadroo 1-1 mfululizo, na Namungo FC na ASEC. PICHA: BENCHIKA AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI SIMBA SC KAMBINI  

YANGA KUANZA NA HAULING FC, SIMBA NA TEMBO AZAM NA ALLIANCE ASFC

Image
MABINGWA watetezi, Yanga watamenyana na Hauling FC ya Njombe katika Hatua ya 64 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation C up (ASFC). Vigogo, Simba SC watamenyana na Tembo FC ya Tabora katika vita ya wanyama tishio nyikani, wakati Azam FC watacheza na Alliance FC ya Mwanza, mechi zote zikichezwa  kati ya Desemba 14 hadi 17.  RATIBA KAMILI 64 BORA ASFC: Singida Fountain Gate v Arusha City Dodoma Jiji v Magereza Dar Ihefu SC v Rospa FC (Mtwara) JKT Tanzania v Kurugenzi (Simiyu) Namungo FC v Hollywood (Songwe) Coastal Union v Greenland (Kagera) Mashujaa FC v Mbuga FC (Mtwara) Azam FC v Alliance FC (Mwanza) Yanga SC v Hauling FC (Njombe) Simba SC v Tembo FC (Tabora) Geita Gold v Singida Cluster Mtibwa Sugar v Nyakagwe FC (Nyang’wale, Geita)   KMC v ACA Eagles Kagera Sugar v Dar City Tabora United v Monduli Coffee (Arusha) Tanzania Prisons v TRA (Kilimanjaro) Mbuni (Arusha) v Bus Stand Biashara United v THB (Rukwa) Ken Go

MAN CITY YATOKA NYUMA NA KUICHAPA RB LEIPZIG 3-2 ULAYA

Image
WENYEJI, Manchester City jana wametoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda 3-2 dhidi ya Rasen Ballsport Leipzig katika mchezo wa Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. RB Leipzig walitangulia kwa mabao ya mshambuliaji wake Mbelgiji, Ikoma-Lois Openda dakika ya 13 na 33, kabla ya Manchester City kutoka nyuma kwa mabao ya nyota, Mnorway Erling Haaland dakika ya 54, Muingereza Phil Foden dakika ya 70 na Muargentina JuliĆ”n Ɓlvarez dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 15 na kuendelea kuongoza Kundi G kwa pointi sita zaidi ya RB Leipzig wanaofuatia baada ya wote kucheza mechi tano kuelekea mechi za mwisho za makundi.

IBRAHIM BACCA AJITIA KITANZI JANGWANI HADI 2027

Image
BEKI wa kati, Ibrahim Abdallah Hamad 'Bacca' ameongeza mkataba wa kuendelea na kazi katika klabu ya Yanga hadi mwaka 2027. Bacca (26) aliyejiunga na Yanga Januari 14, mwaka jana akitokea KMKM ya Zanzibar anapewa mkataba mpya baada ya kazi nzuri aliyofanya mwaka mmoja akiwa timu ya Wananchi. Sambamba na kumuongeza mkataba, Yanga imempa heshima Bacca kwa kuifanya mechi yake ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam iwe siku maalum ya mlinzi huyo hodari, yaani 'Bacca Day'. Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kila moja zimdhamini Bacca Day kwa dau la Sh. Milioni 20, maana yake Yanga imetengeneza Sh. Milioni 40 tukio maalum la mchezaji huyo.  Ikumbukwe Yanga ilianza mechi zake za Kundi D kwa kuchapwa 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria, huku Al Ahly wakiichapa Medeama ya Ghana 3

TWIGA STARS INAVYOJIFUA KUIVAA TOGO ALHAMISI CHAMAZI KUFUZU WAFCON

Image
MSHAMBULAJI Opah Clement anayechezea klabu ya Besiktas ya Uturuki akiwa mazoezi ya timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania leo Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kigamboni, Dar es Salaam. Twiga Stars inajijiandaa na mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili na ya mwisho ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) mwakani nchini Morocco dhidi ya Togo Alhamisi Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.  Timu hizo zitarudiana Desemba 5 Uwanja wa KĆ©guĆ© Jijini LomĆ© na mshindi wa jumla atakuwa amejikatia tiketi ya WAFCON ya Morocco mwakani. PICHA: MAZOEZI YA TWIGA STARS LEO KIGAMBONI

KAGERE AFUNGA, SINGIDA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 LITI

Image
WENYEJI, Singida Fountain Gate wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal UniĆ³n katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Mabao ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ yamefungwa na mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya 30 na beki Mkongo Felly Mulumba aliyejifunga dakika ya 52, wakati bao pekee la Coastal UniĆ³n limefungwa na mshambuliaji Maabad Maulid dakika ya 72. Kwa ushindi huo, Singida Fountain Gate inafikisha pointi 18 na kusogea nafasi ya nne, wakati Coastal UniĆ³n inabaki na pointi zake 10 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 11.

KIKAO CHA BODI NA WACHEZAJI SIMBA SC CHAAMUA; "SHUGHULI INAANZA"

Image
BODI ya Wakurugenzi ya Simba jana ilikutana na wachezaji kambini Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kujadiliana baada ya timu kwenda mechi tatu bila ya ushindi na baada yah apo wakatoka na kauli moja kwamba; “Sasa shughuli ndiyo inaanza”. VIDEO: BEKI MOHAMED HUSSEIN 'TSHABALALA' AKIZUNGUMZA VIDEO: KIUNGO CLATOUS CHAMA AKIZUNGUMZA VIDEO: MSHAMBULIAJI KIBU DENNIS AKIZUNGUMZA Baada ya kufungwa 5-1 na Yanga Novemba 5, Simba ilidroo 1-1 mara mbili mfululizo – na Namungo hizo zote zikiwa mechi za Ligi Kuu na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mechi ya Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo zote zilichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mchezo ujao Simba itakuwa mgeni wa Jwaneng Galaxy Jumamosi Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana mechi ya Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika.   PICHA: KIKAO CHA BODI NA WACHEZAJI WA SIMBA SC

YANGA YAZINDUA BACCA DAY MECHI DHIDI YA AL AHLY JUMAMOSI

Image
KLABU ya Yanga imesema mechi yao ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya mabingwa watetezi, Al Ahly Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam itakuwa siku maalum ya beki wake, Ibrahim Hamad ‘Bacca’ na itaitwa Bacca Day. Yanga imezindua ‘Bacca Day’ leo visiwani Zanzibar sambamba na kutangaza rasmi mwanzo wa hamasa za kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Ahly.  Na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) na na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kila moja imejitolea kudhamini shughuli hiyo kiwa dau la Sh. Milioni 20, maana yake kwa wiki hii moja Yanga imetengeneza Sh. Milioni 40 kwenye Bacca Day. Ikumbukwe Yanga ilianza mechi zake za Kundi D kwa kuchapwa 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria, huku Al Ahly wakiichapa Medeama ya Ghana 3-0 Uwanja wa Al Salam Jijini Cairo. PICHA: YANGA KUSAINI MKATABA NA ZIPA NA ZRA LEO

TANZANIA YAICHAPA UGANDA 1-0 MICHUANO YA CECAFA U18 KENYA

Image
TANZANIA jana imeanza vyema michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 18 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U18) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda bao pekee la Sharif Wilson Uwanja wa Kakamega nchini Kenya.

GARNACHO APIGA BONGE LA BAO MAN UNITED YASHINDA 3-0 LIVERPOOL

Image
TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool. Mabao ya Manchester United leo yamefungwa na washambuliaji Mspaniola Alejandro Garnacho dakika ya tatu, Muingereza Marcus Rashford kwa penalti dakika ya 56 na Mfaransa, Anthony Martial dakika ya 75. Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya sita, wakati Everton inabaki na pointi zake nne nafasi ya 19 baada ya wote kucheza mechi 13.

GEITA GOLD YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 NYANKUMBU

Image
BAO pekee la mshambuliaji Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 79 limeipa Geita Gold ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya Nyankumbu mjini Geita. Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 13 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 11 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 11.

ARSENAL YAICHAPA BRENTFORD 1-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND

Image
BAO la kiungo wa Kimataifa wa Ujerumani, Kai Lukas Havertz dakika ya 89 limetosha kuirejesha Arsenal kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Gtech Community mjiji Brentford, Middlesex.  Kai Havertz aliyejiunga na Arsenal msimu huu akitokea Chelsea iliyomsajili mwaka 2020 kutoka Bayer Leverkusen ya kwao, alifunga bao hilo kwa ustadi mkubwa akimalizia kazi nzuri ya winga Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 30 na kupanda juu ya msimamo wa Ligi Kuu ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 13. Kwa upande wao, Brentford wanabaki na pointi 16 nafasi ya 11 baada ya wao pia kucheza mechi 11.

NEWCASTLE UNITED YAITANDIKA CHELSEA 4-1

Image
WENYEJI, Newcastle United leo wameitandika Chelsea FC mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. James' Park mjini Newcastle upon Tyne. Mabao ya Newcastle United yamefungwa Alexander Isak dakika ya 13, Nahodha Jamaal Lascelles dakika ya 60, Joelinton dakika ya 61 na Anthony Gordon dakika ya 83, wakati bao pekee la Chelsea limefungwa na Raheem Sterling dakika ya 23. Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Reece James kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 73. Kwa ushindi huo, Newcastle United wanafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 16 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 13. 

MAN CITY NA LIVERPOOL NGOMA DROO 1-1 ETIHAD

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City leo wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mshambuliaji wa Kimataifa wa Norway, Erling Haaland alianza kuifungia Manchester City dakika ya 27 akimalizia kazi nzuri ya beki Mholanzi, Nathan Benjamin AkƩ, kabla ya beki Muingereza, Trent John Alexander-Arnold kuisawazishia Liverpool dakika ya 80 akimalizia pigo la mshambuliaji Mmisri, Mohamed Salah. Kwa matokeo hayo, Manchester City wanafikisha pointi 29 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi moja zaidi ya Liverpool inayofuatia nafasi ya pili baada ya wote kucheza mechi 13.

SIMBA SC YAANZA NA SARE YA NYUMBANI, 1-1 NA ASEC DAR

Image
WENYEJI, Simba SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Benjamƭn Mkapa Jijini Dar es Salaam. Ni Simba SC waliotangulia na bao la penalti la kiungo wa Kimataifa wa Burundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 44, kabla ya mshambuliaji Muivory Coast, Serge N'guessan Archange Pokou kuisawazishia ASEC Mimosas dakika ya 77 akimtungua kipa Mmorocco, Ayoub Lakred. Mechi nyingine ya Kundi B itafuatia baadaye Saa 4:00 usiku baina ya wenyeji, Wydad Athletic Club na Jwaneng Galaxy ya Botswana Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco. Simba SC itateremka tena dimbani Desemba 2 Uwanja wa Francistown Jijini Francistown nchini Botswana kumenyana na wenyeji, Jwaneng Galaxy wakati ASEC Mimosas watakuwa nyumbani siku hiyo kuwakaribisha Wydad Casablanca Uwanja wa FƩlix Houphouƫt-Boigny Jijini Abidjan.

SINGIDA BIG STARS YAWACHAPA MAJIRANI DODOMA 2-1 JAMHURI

Image
TIMU ya Singida Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mabao ya Singida Fountain Gate ‘The Big Stars’ yamefungwa na kiungo Morice Chukwu dakika ya na saba na beki Augustino Samson aliyejifunga dakika ya 13, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefungwa na Paul Peter Dalila ya 64. Kwa ushindi huo, Singida Fountain Gate wanafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya tano, wakati Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 15 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 10.

AZAM FC YAITANDIKA MTIBWA SUGAR 5-0 KIPRE APIGA HAT TRICK

Image
WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo mshambuliaji Muivory Coast, Kipre Junior matatu dakika za 29,43 na 63 na beki Lusajo Mwaikenda dakika ya 61 na kiungo Feisal Salum dakika ya 86. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 10 ingawa inabaki nafasi ya pili kwa kuzidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi. Kwa upande wao Mtibwa Sugar baada ya kichapo cha leo wanaendelea kushika mkia katika Ligi ya timu 16 wakibaki na pointi zao tano baada ya kucheza pia mechi 10.

NAMUNGO FC YAICHAPA IHEFU 2-0 RUANGWA MABAO YA BUSWITA NA MAJIMENGI

Image
WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Namungo FC leo yamefungwa na kiungo Pius Buswita dakika ya 36 na mshambuliaji Hamad Majimengi dakika ya 76. Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Ihefu SC inabaki na pointi zake nane nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 10.

FIFA YAIFUNGIA SIMBA SC KUSAJILI KISA PAPE SAKHO

Image
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifungia klabu ya Simba kufanya usajili hadi itakapoilipa klabu ya Teungueth ya Senegal sehemu ya mauzo ya mchezaji Pape Ousmane Sakho kwenda QRM ya Ufaransa. Baada ya taarifa hiyo ya FIFA iliyotolewa na TFF - Simba nayo ikatolea ufafanuzi sakata hilo na kuahidi kuilipa Teungueth haraka iwezekanavyo.

TANZANIA PRISONS YATAMBULISHA KOCHA MBADALA WA MINZIRO

Image
KLABU ya Tanzania Prisons imemtambulisha Hamad Hamisi Ally kuwa kocha wake mpya Mkuu, ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kufundisha timu hiyo katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. “Tumefanikiwa kuingia mkataba wa miaka miwili (2) na Kocha Hamad Hamisi Ally. Kocha Hamad anakuja kuwa kocha mkuu wa timu yetu kuanzia hii leo na uongozi unaimani kubwa juu yake,” imesema taarifa ya Tanzania Prisons leo. Uongozi wa Tanzania Prisons chini ya Mtendaji Mkuu, Ajabu Adam Kifukwe umemtakia kila la kheri kocha Hamad katika majukumu yake yake mapya. Hamad anachukua nafasi ya Freddy Felix Minziro aliyeondolewa mapema wiki hii kutokana na mwenendo mbaya wa timu katika Ligi Kuu ikiambulia pointi saba katika mechi tisa za awali, hivyo kujikuta nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki.

KAGERA SUGAR YAAMBULIA SARE TU KWA KMC 1-1 KAITABA

Image
WENYEJI, Kagera Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Kagera Sugar walitangulia na bao la beki wake Mganda, Deus Bukenya dakika ya 49, kabla ya mshambuliaji Waziri Junior Shentembo kuisawazishia KMC dakika ya 74. Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 16 na kupanda nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar sasa ina jumla ya pointi 13 na inasogea nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 10.

GEITA GOLD YAIKANYAGA JKT TANZANIA 1-0 NYANKUMBU

Image
BAO pekee la Edmund John dakika ya 42 limetosha kuipa Geita Gold ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita. Ushindi huo unaifanya Geita Gold ifikishe pointi 10 na kusogea nafasi ya 10, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 14 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 10.

HIZI NDIZO JEZI ZA YANGA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

Image
KLABU ya Yanga imemtambulisha jezi zake maalum kwa ajili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuelekea mchezo wake wa Kundi D dhidi ya wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Julai 5 1962 Jijini Algiers. VƍDEO: UTAMBULISHO WA JEZI ZA YANGA LIGI YA MABINGWA AFRIKA 

SIMBA SC YATAMBULISHA JEZI ZA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

Image
KLABU ya Simba imetambulisha jezi zake maalum itakazotumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Kundi B dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Jumamosi Uwanja wa BenjamĆ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ni kipa Aishi Manula na mshambuliaji Kibu Dennis ambao wameungana na wenzao mazoezini Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam. Aidha, kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza aliyekuwa kwenye kikosi cha Burundi ambacho kinachezea mechi zake hapa Dar es Salaam pia leo ameingia kambini – na sasa wanasubiriwa beki Henock Inonga Baka ‘Varane’ aliyekuwa DRC na kiungo Clatous Chotta Chama wa Zambia warejee kesho. PICHA: JEZI ZA SIMBA LIGI YA MABINGWA 

TAIFA STARS YACHAPWA 2-0 NA MOROCCO DAR, ZIYECH AKOSA PENALTI

Image
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imechapwa mabao 2-0 na Morocco katika mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 uliofanyoka Uwanja wa BenjamĆ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam leo. Katika mchezo huo wa kuwania tiketi ya Fainali zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada, Mexico na Marekani, mabao ya Morocco yamefungwa na kiungo wa Galatasaray ya Uturuki, Hakim Ziyech dakika ya 28 na beki wa Azam FC, Lusajo Maaikenda aliyejifunga dakika ya 53. Morocco ingeweza kuondoka na ushindi mtamu zaidi kama beki wake, Achraf Hakimi anayechezea PSG asingepiga juu mkwaju wa penalti dakika ya tatu. Taifa Stars ilimaliza pungufu baada ya kiungo wake, Novatus Dismas Miroshi anayechezea Shakhtar Donetsk ya Ukraine kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 65. Wakati Taifa Stars ilianza kwa ushindi wa ugenini 1-0 dhidi ya NĆ­ger Jumamosi bao pekee la kiungo mshambuliaji Charles William M'Mombwa, Morocco imeanza kibarua leo kwa sababu waliopaswa

PRISONS YAACHANA NA KOCHA MINZIRO, TIMU APEWA MTUPA

Image
KLABU ya Tanzania Prisons imeachana na Kocha wake, Freddy Felix Minziro kutokana na mwenendo mbaya wa timu katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Taarifa ya Tanzania Prisons leo imesema kwamba baada ya kuachana na Minziro aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja Julai 14 mwaka huu sasa timu itakuwa chini aliyekuwa Msaidizi wake, Shaaban Mtupa. Baada ya mechi tisa za awali, Tanzania Prisons imevuna pointi saba tu ikiwa inashika nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kwenye mchujo wa kuwania kubaki.

YANGA SC YAIFUATA CR BELOUIZDAD UFUNGUZI MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

Image
KIKOSI cha Yanga kimeondoka Alfajiri ya leo kwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, CR Belouizdad Ijumaa kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Julai 5 1962 Jijini Algiers. Yanga wanarejea kwenye Uwanja ambao Juni 3, mwaka huu walikaribia kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika wakiwachapa wenyeji, USM Alger 1-0, lakini wakaangushwa na kanuni ya mabao ya ugenini kufuatia kufungwa 2-1 Dar es Salaam Mei 28. Safarini Yanga inawakosa wachezaji wake 11 waliopo kwenye timu zao mbalimbali za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia – Afrika, makipa Abdutwalib Mshery, Metacha Mnata, Djigui Diarra (Mali). Wengine ni walinzi Nickson Kibabage, Dickson Job, Bakari Mwanyeto, Ibrahim Ahmed ‘Bacca’, viungo Mudathir Yahya, Khalid Aucho (Uganda), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso) na mshambuliaji Clement Mzize – ambao wataungana na timu Algeria. VIDEO: YANGA WALIVYOIFUATA CR BELOUIZDAD LEO

MAMELODI SUNDOWNS MALKIA WA LIGI YA MABINGWA WANAWAKE

Image
TIMU ya Mamelodi Sundowns imefanikiwa kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake baada ya kuifunga SC Casablanca ya Morocco mabao 3-0 katika mchezo wa Fainali jana Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo nchini Ivory Ivory Coast. Mabao ya mabinti hao wa Afrika Kusini yamefungwa na Tholakele Refilwe mawili, dakika ya 21 kwa penalti na 78 akimalizia pasi ya Melinda Kgadiete na lingine, Boitumelo Rabale dakika ya 24. Huo ulikuwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo baada ya Mamelodi Sundowns kuichapa SC Casablanca 1-0 katika mechi ya Kundi A. Kwa kutwaa taji hili kwa mara ya pili kihistoria kwao, Mamelodi wamezawadiwa dola za Kimarekani 400,000, huku washindi wa pili SC Casablanca wakiondoka na dola  250,000 kwa kumaliza nafasi ya pili. Waliokuwa mabingwa watetezi, AS FAR ambao walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuifunga Ampem Darkoa ya Ghana mabao 2-0 kwa pamoja wamezawadiwa dola 200,000. Timu za AS Mande ya Mali na JKT Queens ya Tanzania kila moja imepata dola 15

TANZANITE YATUPWA NJE KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U20

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Colombia baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji, Nigeria leo katika mchezo wa marudiano Raundi ya Tatu kufuzu Uwanja wa Taifa wa Moshood Abiola Jijini Abuja. Kwa matokeo hayo, Tanzanite inaaga kwa kichapo cha jumla cha 3-2 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

KWA KIASI KIKUBWA MAFANIKIO YA YANGA YAMETOKANA NA GSM - HERSI

Image
RAIS wa Yanga, Hersi Ally Said amesema kwamba mafanikio ya klabu hiyo kwa Asilimia 80 yametokana na msaada wa mfadhili na mdhamini mwenza wa klabu hiyo, Ghalib Said Mohamed ‘GSM’. Hersi ameyasema hayo leo wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Ghalib ambayo ameifanyia katika hospitali ya Ocean Road na kutoa msaada wenye thamani ya Shilingi Milioni 137.  “Mafanikio ya klabu ya Yanga SC kwa zaidi ya asilimia 80 yamechangiwa na uwepo na Ghalib Said Mohamed. Tunamshukuru sana GSM yeye pamoja na familia yake. Ametutoa mbali sana na tunaendelea kumsihi aendelee kuinga mkono klabu hii. Nasi tutamuombea katika kila hatua kwenye maisha yake,” amesema Hersi na kuongeza; “Leo ni siku maalumu ya kuzaliwa kwa GSM. Siku hii angeweza kusheherekea kwa namna tofauti, lakini kwa mapenzi aliyo nayo kwa jamii ameona thamani ya kusheherekea na wenyewe uhitaji,”. Katika hafla hiyo GSM ametoa msaada wenye thamani ya Shilingi Milioni 137, wazo ambalo limetolewa mke wake Salha. VIDEO: HAFLA YA GSM

SIMBA SC YAITANDIKA DAR CITY 4-0 WACAMEROON WOTE WAFUNGA

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dar City ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Mo Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC katika mchezo huo wa kujiandaa na hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika yamefungwa na Wacameroon, beki Che Malone Fondoh na kiungo mshambuliaji Leandre Willy Essomba Onana, beki mzawa Israel Patrick Mwenda na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri. Simba itateremka Uwanja wa BenjamĆ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam Jumamosi kumenyana na ASEC Mimosas ya Ivory Coast katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika. Wakati huo huo, mchezaji wa timu hiyo, Mohamed Mussa amefiwa na baba yake mzazi, Mussa Mzee Saleh aliyefariki Dunia mapema leo visiwani ZanzĆ­bar na anatarajiwa kuzikwa baada ya sala ya Alaasir huko Malindi.

NYOTA MPYA AING’ARISHA TAIFA STARS UFUNGUZI KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Image
TANZANIA imeanza vyema harakati za kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, NĆ­ger katika mchezo wa Kundi E leo Uwanja wa Marrakech mjini Marrakech nchini Morocco. Akiichezea kwa mara ya kwanza Taifa Stars, kiungo mshambuliaji Charles William M'Mombwa mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndiye aliyeifungia timu hiyo bao hilo pekee. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anayecheza ya Macarthur FC ya Ligi Kuu ya Australia alifunga bao hilo dakika ya 56 Nahodha na mshambuliaji wa PAOK Thessaloniki FC ya Ugiriki, Mbwana Ally Samatta. Mara tu baada ya mchezo huo, Taifa Stars inafunga safari kurejea nyumbani kwa ajili ya mechi ya pili ya Kundi E dhidi ya Morocco Jumanne Uwanja wa BenjamĆ­n Mkapa Jijini Dar es Salaam kuwania tiketi ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada, Mexico na Marekani. Pamoja na Taifa Stars, Niger na Morocco timu nyingine zilizopo Kundi E ni Kongo  na Zambia, wakati Eritrea imeji

MAPRO WATANO WAITWA KUIPIGANIA TWIGA STARS TIKETI YA WAFCON 2024

Image
KOCHA Bakari Shime ameita wachezaji watano wanaocheza timu mbalimbali Ulaya, Amerika na Asƭa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya wanawake kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya pili na ya mwisho kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake Jumatano ijayo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Hao ni beki Julieath Singano anayecheza Juarez ya Morocco, viungo Enekia Kasonga wa Eastern Flames ya Saudi Arabia na Diana Lucas wa Ameds FK ya Uturuki na washambuliaji, Opa Clement wa Besiktas ya Uturuki pia na Aisha Masaka wa BK Hancken ya Sweden. Kwa kiasi kikubwa kikosi cha Twiga Stars kinaundwa na nyota wa klabu bingwa ya Tanzania na Afrika Mashariki na Katƭ, JKT Queens pamoja na wawili wa Simba Queens na mmoja wa Yanga Princess. Timu hizo zitarudiana mapema Desemba Uwanja wa KƩguƩ Jijini LomƩ na mshindi wa jumla atafuzu Fainali za WAFCON mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.

MECHI YA GOR MAHIA NA AZAM YAPEPERUKA, SASA NI JKU

Image
MCHEZO wa kirafiki baina ya wenyeji, Gor Mahia na Azam FC uliopangwa kufanyika Jumapili Uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya umefutwa. Taarifa ya Azam FC imesema kwamba kutokana mchezo huo kufutwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao - sasa watacheza na JKU ya Zanzibar Jumapili Uwanja wa Azam Complex kuamzia Saa 1:00 usiku.

YANGA YAINGIA FAINALI TUZO YA KLABU BORA AFRIKA

Image
KLABU ya Yanga imeingia kwenye orodha ya mwisho ya timu tano kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika katika dola ya Wanaume ikichuana na USM Alger ya Algeria, Al Ahly ya Misri, Wydad Athletic ya Morocco na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. Aidha, mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele aliyesaidia Yanga kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ameingia kwenye 10 Bora ya kuwania Tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika. Yanga ilitoa sare ya jumla ya 2-2 na USM Alger waliotwaa ubingwa kwa Sheria ya mabao ya ugenini kufutia kushinda 2-1 Dar es Salaam na kufungwa 1-0 Algiers. Kipa wa Kimataifa wa Mali na Yanga aliyeingia kwenye vipengele viwili vya awali, Kipa Bora na Mchezaji Bora Anayecheza Afrika hakuvuka hatua ya mwisho.

AUCHO AFUNGIWA MECHI TATU, REFA COASTAL NA YANGA NJE NUSU MWAKA

Image
KIUNGO wa Kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho amefungiwa mechi tatu na kutozwa Faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumpiga kiwiko kiungo wa Coastal UniĆ³n, Ibrahim Ajibu katika mchezo baina ya timu hizo mwezi huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Aidha, refa wa mchezo huo, Emmanuel Mwandembwa wa Arusha amefungiwa miezi sita kwa kosa kutotafsiri Sheria 17 za kandanda kwa ufasaha.

KIBU, INONGA NA DIARRA WATOZWA FAINI PAMOJA NA SIMBA NA YANGA

Image
WACHEZAJI wa Simba SC, beki Mkongo Henock Inonga Baka ‘Varane’ na mshambuliaji Kibu Dennis Prosper pamoja na kipa wa Yanga, Djigui Diarra raia wa Mali wametozwa Faini kwa makosa yanayofanana kwenye mchezo baina ya timu zao Novemba 5 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao Yanga ilishinda 5-1, pia kocha wake Msaidizi, Msenegal Moussa N’Daw ametozwa faini pamoja na klabu yenyewe na watani wao, Simba SC kwa makosa tofauti. PICHA: TAARIFA YA KAMATI YA BODI YA LIGI ADHABU ZA SIMBA NA YANGA

ZANZIBAR MABINGWA CECAFA U15, BARA WASHINDI WA TATU

Image
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya ZanzĆ­bar leo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U15) baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji, Uganda kufuatia sare ya 1-1 mjini Kampala. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Njeru mjini Kampala nchini Uganda, mabao yote yalipatikana kipindi cha kwanza wenyeji wakitangulia kabla ya Karume Boys kusawazisha. Kwa upande wao, Tanzania Bara wamefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini katika mchezo uliotangulia hapo hapo Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha FUFA. PICHA: ZANZIBAR WALIVYOKABIDHIWA UBINGWA CECAFA U15

KINDA WA AZAM FC KACHWELE AJIUNGA NA VANCOUVER WHITECAPS

Image
CHIPUKIZI wa Azam FC, Cyprian Kachwele amejiunga na klabu ya Vancouver Whitecaps ya CaƱada inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS). Azam FC imetoa taarifa rasmi ya kumuaga na kumtakia kila la heri katika maisha mapya Vancouver Whitecaps inayofundishwa na Kocha Mtaliano, Vanni Sartini. “Tunamtakia kila la kheri mshambuliaji wetu chipukizi, Cyprian Kachwele, aliyejiunga na timu yake mpya ya Vancouver Whitecaps inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani (MLS),” imesema Taarifa ya Azam FC. Kachwele aliibukia akademi ya Azam FC, kabla ya kupandishwa timu kubwa mwishoni mwa msimu uliopita na kucheza baadhi ya mechi, akifunga mabao matatu katika mechi za mashindano. Anakuwa Mtanzania wa pili Kihistoria kucheza Vancouver Whitecaps baada ya kiungo Nizar Khalfan aliyecheza kuanzia mwaka 2009 hadi 2011 kabla ya kurejea nyumbani kumalizia soka yake ya Yanga na sasa ni Kocha Msaidizi wa Singida Fountain Gate.

TAIFA STARS WAENDA MOROCCO KUANZA MAWINDO YA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA 2026

Image
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeondoka leo kwenda Morocco kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada, Mexico na Marekani. Taifa Stars watakuwa wageni wa Niger Jumamosi Uwanja Marrakech nchini Morocco, kabla ya kuwakaribisha Morocco katika mchezo wa pili wa Kundi hilo Novemba 21, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Pamoja na Taifa Stars, Niger na Morocco timu nyingine zilizopo Kundi E ni Kongo  na Zambia, wakati Eritrea imejitoa. Timu tisa zitakazoongoza makundi zitafuzu moja kwa moja kuiwakilisha kwenye Fainali za Kombe la Dunia, wakati washindi wa pili bora wanne wa makundi watamenyana katika Nusu Fainali na Fainali na mshindi atakwenda kushiriki mchujo wa Mabara kuwania nafasi ya kwenda Kombe la Dunia pia. Mchujo wa Mabara, unaojulikana kama Inter-Confederation Play-Offs ni michuano mingine midogo inayoshirikisha timu sita za Mabara manne duniani, kasoro UE

TANZANITE WALIVYOONDOKA LEO KUIFUATA NIGERIA MECHI JUMAMOSI ABUJA

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imeondoka leo Jijini Dar es Salaam kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wenyeji Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Colombia Jumapili Uwanja wa Taifa wa Moshood Abiola Jijini Abuja. Tanzanite inahitaji ushindi wa ugenini au sare ya kuanzia mabao 2-2 kufuatia kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo mkali na wa kusisimua uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Nigeria ilitangulia kwa bao la Chioma Oliseh dakika ya 57, kabla ya Asnath Ubamba kuisawazishia Tanzanite dakika ya 70. PICHA: TANZANITE WALIVYOONDOKA DAR KUIFUATA NIGERIA