Posts

Showing posts from May, 2024

BETPAWA YAPIGA ‘AMSHA AMSHA’ MWANZA KUELEKEA FAINALI LİGİ YA MABINGWA ULAYA

Image
Wacheza shoo wakiburudisha wakati wa hamshahamsha ya kuelekea fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid na Borrusia Dortmund kupitia “Soka Live na betPawa” mjini Mwanza.  KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya betPawa imezawadia vifaa vya michezo timu mbalimbali za mkoa wa Mwanza ikiwa sehemu ya kuchangia maendeleo ya soka na hamsha hamsha ya mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA kati ya Borussia Dortmund na Real Madrid itakayofanyika Jumamosi,  Juni 1, 2024. Tukio hilo lililopewa jina la Soka Live na betPawa litafanyika eneo la Kona ya Bwiru jijini Mwanza na lilipambwa na hamsha hamsha mbalimbali  zikiwemo za mashindano madogo ya kandanda atakayoshirikisha klabu nne za eneo hilo. Kabla ya mchuano huo, betPawa itatoa msaada wa vifaa vya mpira wa miguu kama jezi na mipira kwa timu ambazo ni Channel Africans FC, Bwiru FC, Majengo FC na Tiger FC. "Tunaposubiri fainali ya kusisimua ya shindano la kifahari zaidi la Uropa, tunataka pia kurudisha kwa jamii zetu za mpira w

YANGA SC WAWASILI ZANZİBAR KUTETEA KOMBE LA TFF

Image
KIKOSI cha Yanga SC kimewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama CRDB Bank Federation Cup dhidi ya Azam FC Jumapili kuanzia Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

AZAM FC YASAJILI MSHAMBULIAJI MWINGINE MCOLOMBIA

Image
KLABU ya Azam FC imemtambulisha mshambuliaji Jhonier Blanco, kutoka klabu ya Aguilas Doradas ya Rionegro, kwao Colombia. Blanco aliyezaliwa Oktoba 18, 2000, amesaini mkataba wa miaka minne baada ya kufaulu vipimo vya afya, kufuatuatia makubaliano baina ya klabu yake inayoshiriki Ligi Kuu ya Colombia na Azam FC. Kisoka aliibukia akademi ya Club Deportivo Estudiantil kabla ya kujiunga na timu ya ligi kuu ya Aguilas Doradas, baadaye akatolewa kwa mkopo klabu ya daraja la kwanza, Fortaleza.  Manbo yalimuendea vizuri Fortaleza akaibuka kuwa mfungaji bora akiisaidia kupanda daraja na alipomaliza uhamisho wake wa mkopo akarejea Aguilas Doradas na sasa anahamia Tanzania. Blanco anaungana na Wacolombia wenzake watatu, kiungo Ever Meza aliyesaini wiki iliyopita, beki Yeison Fuentes wote kutoka Leones FC ya kwao na mshambuliaji Franklin Navarro kutoka Cortulua ya nchini humo pia FC Colombia ambao walisajiliwa Januari mwaka huu. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

SIMBA SC 2-0 JKT TANZANIA (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

YANGA SC 3-0 TABORA UNITED (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC 1-0 KMC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

TAIFA STRAS YAENDA INDONESIA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA WENYEJI

Image
KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka leo kwenda Indonesia kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na wenyeji, Juni 2 kuanzia Saa 6:00 usiku Uwanja wa Madya Gelora Bung Karno Jijini Jakarta. Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji, Zambia Juni 11 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola. Wapinzani wengine wa Taifa Stars Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 ni Morocco, Zambia, Niger, Kongo na Eritrea ambayo imejitoa katika mbio za kuwania tiketi ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani. Taifa Stars ilianza vyema kampeni zake za Kombe la Dunia 2026 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Niger Novemba 18 mwaka jana Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao pekee la mshambuliaji mzaliwa wa DRC, Kokola Charles William M'Mombwa wa Macarthur FC ya Australia.

AZAM FC YAIPIKU SIMBA LİGİ YA MABINGWA, AZİZ Kİ MFUNGAJI BORA

Image
MSIMU wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara umehitimishwa leo kwa Azam FC kumaliza nafasi ya pili nyuma ya mabingwa, Yanga huku vigogo, Simba SC wakimaliza nafasi ya tatu na Coastal Union nafasi ya nne. Azam FC imemaliza nafasi ya pili baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya JKT Tanzania mabao ya Yeisson Fuentes Mandoza dakika ya 58 na Feisal Salum Abdallah dakika ya 71 Uwanja wa Sekondari ya Nyankumbu, Geita. Simba imemaliza ilipokuwa, nafasi ya tatu licha ya ushindi wa 2-0 pia dhidi ya JKT Tanzania, mabao ya Saido Ntibanzokiza dakika ya 88 kwa penaltı Ande Essomba Onana dakika ya 90’+2 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Azam imemaliza na pointi 69, ikiizidi tu wastani wa mabao Simba SC - wote wakiwa nyuma ya Yanga iliyomaliza na pointi 80 baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 11, 12 na 79, lingine likifungwa na Mzambia, Kennedy Musonda d

BIASHARA UNITED YAJISOGEZA KARIBU NA LİGİ KUU, MBEYA KWANZA KUJARIBU TENA MSIMU UJAO

Image
TIMU ya Biashara United imefuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kupanda Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuitoa Mbeya Kwanza kufuatia kuichapa 2-0 jana Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Mabao ya Biashara United jana yalifungwa na Charles Lukindo na Abeid Athumani na kwa matokeo hayo Biashara United inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-0 kufuatia kuichapa Mbeya Kwanza 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Karume mjini Musoma. Biashara sasa itasubiri timu itakayoporomoka kutoka Ligi Kuu ikutane nayo katika mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao na atakayefungwa atacheza Championship.

SHIME AMUITA CLARA LUVANGA TWIGA STARS YA KUCHEZA NA MALI NA SUDAN

Image
KOCHA Bakari Nyundo Shime amemjumuisha mshambuliaji wa Al Nasr ya Saudi Arabia katika kikosi cha wachezaji 22 cha timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Mali na Sudan wiki ijayo.

YANGA SC YAENDELEZA UMBWAMBA LIGI KUU, YAICHAPA TABORA UNITED 3-0

Image
MABINGWA mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Gnadou Guede dakika ya 19 na viungo, Mkongo Maxi Mpia Nzengeli dakka ya 49 na Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 90’+1. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 77 kileleni ikifuatiwa na Azam FC na Simba SC zenye pointi 66 kila moja, wakati Tabora United inabaki na pointi zake 27 nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu zote kucheza mechi 29.  Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu. Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.

TANZANIA BINGWA MASHINDANO YA SHULE ZA AFRIKA KWA WAVULANA

Image
TANZANIA imefanikiwa kutwaa Kombe la Ubingwa wa Soka kwa Shule za Afrika (ASFC) upande wa wavulana baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Guinea jana Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Nayo Afrika Kusini imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo upande wa wanawake kufuatia ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 na Morocco hapo hapo New Amaan Complex.   Fainali ya michuano hiyo ya siku nne iliyofanyika kuanzia Mei 21 hadi 24, ilihudhuriwa na Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe, ambaye mapema siku hiyo alitembelea Ikulu ya Zanzibar kukutana na Rais wa nchi hiyo Dk. Hussein Mwinyi. Fainali hizo zilitanguliwa na mechi za kuwania nafasi za tatu, Uganda ikiifunga Tanzania 1-0 kwa wasichana na Senegal wakiifunga Benin kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0. Baada ya mashindano kuhitimisha, Abel Samson wa Tanzania alitangazwa Mchezaji Bora wa ASFC 2024 kwa wavulana, huku Meryem Oubella wa Morocco akiwa MVP upande wa wasichana. Kipa Bora Wasichana ni Sphumelele Zibula wa Afrika Kusini

RAIS DK MWINYI AISHUKURU CAF KUIPA ZANZIBAR UENYEJI ASFC

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika(CAF) kwa kuifanya Zanzibar kuwa mmoja ya waandaaji wa Mashindano ya Ubingwa wa Soka kwa Shule za Afrika (ASFC) mwaka huu. Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipokutana na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Dk.Patrice Motsepe na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Mei 2024. Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar itaendeleza na kudumisha uhusiano wake na CAF . Rais Dk.Mwinyi amemueleza Dk.Motsepe kuwa Zanzibar inahitaji msaada wa kuendeleza vipaji vya soka kuanzia ngazi za academy kwa kushirikiana na CAF. Rais wa CAF Dk.Motsepe leo atashuhudia mchezo wa kwanza wa fainali za Mashindano ya African Schools Football Championship yanayofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

HÜKÜMÜ YA KESİ YA DITTO DHIDI YA DSTV KUTOLEWA JULAI 16

Image
HUKUMU ya kesi ya madai ya mwanamuziki Lameck Ditto dhidi ya kampuni ya Multchoice Tanzania Limited maarufu DSTV itatolewa Julai 16. Ditto ambaye jina lake halisi ni Dotto Bwakeya alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam mwaka 2020 akiiomba Mahakama hiyo iamuru kampuni Multichoice Tanzania imlipe fidia ya Sh 6bilioni kwa kutumia wimbo  wa Nchi Yangu aliodai ni wake kwenye matangazo yao ya biashara bila ridhaa yake wakati wa kampeni za  fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019. Pia ameiomba Mahakama iamuru alipwe Milioni 200 kutokana na madhara ya jumla, pia alipwe riba ya asilimia 25 tangu siku alipofungua shauri hilo akidai kampuni hiyo imemnyima fursa ya kunufaika na kazi yake. Kesi hiyo inayosikilizwa na jaji mfawidhi, Salma Maghimbi, imekamilisha ushahidi wa pande zote, Ditto akileta mashahidi watano na DSTV ikiwa na mashahidi wawili, Astrid Mapunda na Johnson Mshana. Upande wa Ditto, baadhi ya mashahidi wake walikuwa ni produzya wa wimbo huo, Emman

DODOMA JIJI FC 0-4 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

AZİZ Kİ APIGA MBILI YANGA YAIBABUA DODOMA JIJI 4-0 JAMHURI

Image
MABINGWA, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji mzawa, Clement au Walid Francis Mzize kwa jina jipya baada ya kusilimu dakika ya 10 na viungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki mawili dakika ya 45’+4 kwa penaltı na dakika ya 51 na Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 78. Kwa ushindi huo, Yanga ambao tayari ni mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo na mara 30 jumla ambayo ni rekodi - wanafikisha pointi 74 katika mchezo wa 28, wakifuatiwa na Azam FC na Simba zenye pointi 63 kila moja. Kwa upande wao Dodoma Jiji baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 28 pia na wanashuka kwa nafasi moja hadi ya 12. Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu. Timu itak

FAINALI KOMBE LA TFF AZAM NA YANGA KUPIGWA ZANZIBAR JUNI 2

Image
FAINALI ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup itafanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar Juni 2 badala ya Uwanja wa Tanzanite uliopo Babati mkoani Manyara. Mchezo huo utazikutanisha timu za Azam FC na mabingwa watetezi, Yanga SC na sababu za kuuhamishia mchezo huo Zanzibar ni Babati kutokuwa na miundombinu rafiki kuhodhi mchezo mkubwa kama huo.

AMOKACHI, ADEBAYOR NA BABBI WATOA NASAHA MASHINDANO YA SHULE AFRIKA

Image
MAGWIJI wa Afrika, Emmanuel Adebayor (Togo), Daniel Amokachi (Nigeria) na Abdi Kassim Sadalla 'Babbi' (Tanzania) walitembelea hoteli ya timu ya wavulana ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika ya CAF ya Shule za Afrika Jumatatu, 20 Mei kabla ya kuanza kwa michuano hiyo visiwani Zanzibar. Vigogo watatu wa Afrika ambao ni sehemu ya Magwiji waalikwa wa CAF walitoa maneno ya hekima na kutia moyo wakati timu hizo zikijiandaa kuchuana katika mashindano ya siku nne yanayotarajiwa kuanza kati ya tarehe 21 - 24 Mei katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Sambamba na kuwapa vijana wanaoshiriki uzoefu usioweza kusahaulika kwenye Fainali, CAF iliwaalika wababe hao kwenye chakula maalum cha jioni kwa timu hizo ambapo waliwahimiza vijana wa U-15 kukubali ari ya mchezo wa haki na kutumia jukwaa la kusisimua walilopewa. na CAF. "Inatia moyo sana kushuhudia wanasoka chipukizi wa Kiafrika kama nyinyi wakipewa fursa ya kushiriki katika mashindano kama haya. Hii ni zaidi ya soka. Ni kuhusu kukup

SIMBA SC 4-1 GEITA GOLD (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YAICHAPA GEITA GOLD 4-1 CHAMAZI

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza mawili dakika ya 45’+3 kwa penaltı na dakika ya 72 na mzawa, Ladack Chasambi dakika ya 86 na 90 +3 baada ya Geita Gold kutangulia na bao la Geoffrey Julius dakika ya 11. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 63, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 28, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 25 za mechi 28 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16. Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu. Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.

COASTAL UNION YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1 PALE PALE KAITABA

Image
TIMU ya Coastal Union imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Shadrack Mulungwe dakika ya 16 na Denis Modzaka dakika ya 69, wakati bao pekee la Kagera Sugar limefungwa na Mbaraka Yussuf Abeid dakika ya 73.  Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 41, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Kagera Sugar inabaki na pointi zake 31 nafasi ya tisa.

MASHUJAA YAICHAPA PRISONS 2-1 PALE PALE SOKOINE

Image
TIMU ya Mashujaa FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Mashujaa FC yamefungwa na David Ulomi dakika ya 14 na Mgandila Shaaban kwa penaltı dakika ya 20, wakati bao pekee la Tanzania Prisons limefungwa na Omar Kindamba aliyejifunga dakika ya 63. Kwa ushindi huo, Mashujaa FC inafikisha pointi 29, ingawa inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 33 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 28. Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.

MTIBWA SUGAR BADO KIDOGO TU KUIAGA RASMI LİGİ KUU

Image
WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya bila mabao na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 21, ingawa inabaki nafasi ya mwisho katika ligi ya timu 16, wakati Namungo FC inafikisha pointi 32 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba baada ya wote kucheza mechi 28. Ikumbukwe, mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja moja kwa moja na nyingine mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kurudi Ligi Kuu.

IHEFU SC 0-1 YANGA SC (KOMBE LA TFF)

Image
 

ZAMALEK MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Image
WENYEJI, Zamalek SC wamefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Renaissance Sportive de Berkane (RSB) usiku wa jana Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo nchini Misri. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, nyota mwenye umri wa miaka 26, Ahmed Hamdi Hussein Hafez dakika ya 23 akimalizia kazi nzuri ya kiungo mwenzake, Ahmed Mostafa Mohamed Sayed ‘Zizo’ wote Wamisri. Zamalek wanakuwa mabingwa kwa faida ya mabao ya bao ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia kufungwa 2-1 wiki iliyopita kwenye mchezo ya kwanza Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Morocco. Huu unakuwa msimu wa pili mfululizo, bingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika anapatikana kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya msimu uliopita USM Alger ya Algeria kutoa sare ya jumla ya 2-2 na Yanga ya Tanzania.

TAIFA STARS YATOA SARE NA SUDAN 1-1 SAUDI ARABIA

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa King Fahd Sport City mjini Ta'if, Saudi Arabia. Bao la Taifa Stars inayoundwa na kikosi cha chipukizi wapya kabisa limefungwa na Oscar Adam Paul anayechezea Kakamega FC ya Kenya. Taifa Stars inakamilisha ziara yake ya mechi mbili za kujipima nguvu na Sudan kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mechi ya kwanza Mei 15 hapo hapo King Fahd Sport City.

NI MAN CITY MABINGWA ENGLAND MARA YA NNE MFULULIZO

Image
TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutetea tena ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa West Ham United mabao 3-1 leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Mabao ya Manchester City yamefungwa na viungo Muingereza mwenye umri wa miaka 23, Philip Walter Foden mawili, dakika ya pili na 18 na Mspaniola Rodrigo Hernández Cascante (27) dakika ya 59, wakati bao pekee la West Ham United limefungwa na kiungo pia, Mghana Mohammed Kudus (23) dakika ya 42. Kwa ushindi huo Manchester City inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pep Guardiola inamaliza na pointi 91, mbili zaidi ya Arsenal iliyomaliza nafasi ya pili na kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa mara nne mfululizo katika historia ya Ligi Kuu ya England. Arsenal imemaliza nafasi ya pili baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton Uwanja wa Emirates Jijini London, mabao yake yakifungwa na beki Mjapan Takehiro Tomiyasu dakika ya 43 na kiungo Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 89. Bao pekee la Everton lilifungwa na kiungo Msenegal, Idrissa G

AZİZ Kİ AIPELEKA YANGA FAINALI KOMBE LA TFF, IHEFU ‘YAFA KIUME’

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ‘CRDB Bank Federation Cup’ baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso dakika ya 101 akimalizia krosi ya mchezaji mwenzake wa zamani wa ASEC Mimosas, Peodoh Pacome Zouzoua kutoka upande wa kulia. Yanga sasa itakutana na Azam FC katika Fainali hayo yakiwa marudio ya Fainali ya msimu uliopita ambayo Wananchi walishinda 2-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Azam FC ilitangulia Fainali jana kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union mabao ya Abdul Hamisi Suleiman ‘Sopu’ mawili na Feisal Salum Abdallah moja Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

USYK ASHINDA KWA POINTI ZA MAJAJI KUPISHANA, FURY ASEMA 'AMEBEBWA' KISA VITA

Image
BONDIA Oleksandr Usyk wa Ukraine usiku wa jana amesmshinda Muingereza Tyson Fury kwa pointi za majaji kupishana, 2-1 ukumbi wa Kingdom Arena Jijini Riyadh, Saudi Arabia na kuwa bingwa wa kwanza asiyepingika wa uzito wa juu wa mataji manne. Jaji mmoja tu alimpa ushindi Fury wa pointi 114-113, wakati wengine wawili walimpa Usyk ushindi wa pointi T115-112 na 114-113, hivyo kuwa bingwa mpya asiyepingika duniani uzito wa juu akihodhi mataji ya WBC, WBA, IBF na WBO.  Lilikuwa pambano la aina yake, Fury akianza kutawaka raundi za mwanzo, kabla ya Usyk kuzinduka baadaye na kufanikiwa hadi kumpeleka chini Gypsy King raundi ya tisa. Hata Hivyo, baada ya pambano hilo Fury alidai watu wanaegemea upande wa Usyk kwa sababu vita inayoendelea nchini kwao, Ukraine.  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI NA VIDEO

AZAM YATINGA FAINALI KIBABE KOMBE LA TFF, YAITWANGA COASTAL 3-0

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inatambulishwa kama CRDB Bank Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na viungo washambuliaji, Abdul Hamisi Suleiman 'Sopu' (23) mawili dakika ya 42 kwa penalti na 79 na lingine Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' (26) dakika ya 68. Sasa Azam FC itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili ya CRDB Bank Federation Cup baina ya mabingwa watetezi, Yanga na Ihefu SC zitakazomenyana kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. 

DODOMA JIJI 0-1 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI FC 1-0 JAMHURI

Image
VIGOGO, Simba SC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Muivory Coast Freddy Michael Koublan dakika ya saba akimalizia kazi nzuri ya winga Edwin Barua. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 60, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC baada ya wote kucheza mechi 27. Kwa upande wao Dodoma Jiji FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 30 za mechi 27 nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16, ambazo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja.

YANGA SC WALIVYOWASILI ARUSHA KUIVAA IHEFU JUMAPILI

Image
KIKOSI cha Yanga kimewasili salama Jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Ihefu SC keshokutwa kuanzia Saa 9:30 Alasiri Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini humo. Mshindi wa mechi za michuano hiyo ambayo sasa inatambulishwa kama CRDB Bank Federation Cup atakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kati ya Azam FC na Coastal Union zinazomenyana kesho Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. GONGA KUTAZAMA PICHA YANGA ILIVYOWASILI ARUSHA 

MAHODHA WA ZAMANI TAIFA STARS JELLAH MTAGWA AFARIKI DUNIA

Image
BEKİ na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Jellah Mtagwa (70) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Muhimbili Mloganzila alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Mtagwa aliyekuwa beki hodari wa kati enzi zake - amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kiharusi tangu mwaka 2004 kufuatia kuanguka akiwa anatembea katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Mtagwa alikuwa Nahodha wa Taifa Stars kwa miaka 10 mfululizo kuanzia mwaka 1973 akimrithi beki wa kati pia, Omar Zimbwe hadi 1983 alipomuachia Charles Boniface Mkwasa mlinzi pia na kiungo. Aliiongoza Taifa Stars kufuzu Fainali za Kwanza za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria na mwaka 1982 sura yake iliwekwa kwenye stempu kutokakana na umaarufu wakati huo. Ilikuwa wakati wa mechi za Kufuzu Kombe la Dunia mwaka 1982 nchini Hispania ambazo Taifa Stars ilitolewa na Nigeria katika Raundi ya Pili baada ya kuitoa, Kenya katika Raundi ya kwanza ya mchujo huo. Jellah alizaliwa mwaka 1953 Morogoro mjini akapata elimu

AZİZ Kİ ATANGAZA JEZI YA UBINGWA WA 30 YANGA

Image
KIUNGO was Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki ametumika kwenye kampeni maalum ya klabu yake, Yanga SC kutangaza jezi za ubingwa wa 30 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. GONGA KUTAZAMA VIDEO AZİZ KI AKITANGAZA JEZI YA UBINGWA WA 30

SIMBA SC WAWASILI MAKAO MAKUU YA NCHI KUIVAA DODOMA JIJI

Image
KIKOSI cha Simba SC kimewasili salama Jijini Dodoma mapema leo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, kesho Uwanja wa Jamhuri. Simba SC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 57 za mechi 26 nyuma ya Azam FC yenye pointi 60 za mechi 27, wakati Dodoma Jiji ina pointi 30 za mechi 26 nafasi ya 11. Na wote wapo nyuma ya mabingwa tayari, kwa mara ya tatu mfululizo, Yanga SC yenye pointi 71 za mechi 27. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

MAN UNITED YAICHAPA NEWCASTLE 3-2 OLD TRAFFORD

Image
WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Mancheater United yamefungwa na washambuliaji, chipukizi wa umri wa miaka 19, Muingereza mwenye asılı ya Ghana, Kobbie Boateng Mainoo dakika ya 31, Muivory Coast Amad Diallo Traoré mwenye umri wa miaka 21 dakika ya 57 na Mdenmark Rasmus Winther Højlund dakika ya 84. Kwa upande wao Newcastle United mabao yao yamefungwa na washambuliaji Muingereza Anthony Michael Gordon (23) dakika ya 49 na bwana mdogo wa umri wa miaka 19, Lewis Kieran Hall dakika ya 90. Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 57, ingawa inabaki nafasi nane ilizidiwa tu wastani wa mabao na Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 37.

TAIFA STARS YACHAPWA 2-1 NA SUDAN KIRAFIKI SAUDI ARABIA

Image
TIMU ya taifa ya Tanzania imefungwa bao 1-0 na Sudan katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa King Fahd Sport City mjini Ta'if, Saudi Arabia. Katika mchezo huo, kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemtumia kinda wa umri wa miaka 17, Jabir Seif Mpanda (pichani) wa akademi ya Getafe ya Hispania, huo ukiwa mchezo wake wa kwanza Taifa Stars na alikuwa mchezaji mdogo zaidi zaidi ya wote uwanjani leo.

CHILAMBO ASAINI MKATABA MPYA AZAM FC HADI 2026

Image
BEKI wa kulia, Nathaniel Raphael Chilambo (24) amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Azam FC hadi mwaka 2026.

MTIBWA SUGAR 1-3 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

DURAN APIGA MBILI ASTON VILLA YATOA SARE 3-3 NA LIVERPOOL

Image
WENYEJI, Aston Villa usiku wa jana wametoa sare ya kufungana mabao 3-3 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham. Mabao ya Aston Villa yalifungwa na kiungo Mbelgiji, Youri Marion Tielemans dakika ya 12 na mshambuliaji Mcolombia, Jhon Jader Duran mawili dakika ya 85 na 88. Mabao ya Liverpool yalifungwa na kipa Muargentina, Emiliano Martínez aliyejifunga dakika ya pili, winga Mholanzi Cody Mathes Gakpo dakika ya 23 na beki Muingerea mwenye asili ya Ghana, Jarell Amorin Quansah dakika ya 48. Kwa matokeo hayo, Liverpool inafikisha pointi 79, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati Aston Villa inafikisha pointi 78 nayo inabaki nafasi ya nne baada ya wote kucheza mechi 37.

YANGA SC MABINGWA TENA LIGI KUU YA NBC TZ BARA

Image
RASMI, Yanga ni mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo na mara ya 30 jumla baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mtibwa Sugar walitangulia kwa bao la Charles Ilamfya dakika ya 32, kabla ya Yanga kutoka nyuma kwa mabao ya Mzambia Kennedy Musonda dakka ya 62, Nasry Kyombo aliyejifunga dakika ya 66 na Clement Mzize dakika ya 81. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 71 katika mchezo wa 27 ambazo hakuna timu nyingine katika Ligi Kuu inayoweza kuzifikisha, hivyo kujihakikishia taji la ubingwa msimu huu, 2023-2024. Hali inazidi kuwa mbaya kwa Mtibwa Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo ikibaki na pointi zake 20 za mechi 27 mkiani kabisa mwa Ligi Kuu. Sehemu pekee ya Mtibwa Sugar kujinusuru kutoshuka Daraja ni kwenye mchujo, Play-Offs kama itashinda mechi zake zote tatu zilizobaki dhidi ya Namungo nyumbani na Ihefu na Mashujaa ugenini na kumaliza nafasi ya 14 au ya 13. Na hiy

TABORA UNITED YAICHAPA MASHUJAA 1-0 UWANJA WA MWINYI

Image
BAO pekee la Eric Okutu dakika ya 70 jana liliipa Tabora United ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Kwa ushindi huo, Tabora United inafikisha pointi 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14, wakizidiwa wastani wa mabao na Mashujaa FC baada ya wote kucheza mechi 27. Wapo mbele ya Geita Gold yenye pointi 24 nafasi ya 15 na Mtibwa Sugar pointi 20 nafasi ya mwisho, ya 16 baada ya wote kucheza mechi 26. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu zitashuka daraja na mbili nyingine, ya 13 na 14 zitamenyana baina yao nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kusalia Ligi Kuu.

NICOLAS JACKSON AIPIGIA LA USHINDI CHELSEA YAICHAPA NOTTINGHAM 3-2

Image
  TIMU ya Chelsea imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire. Mabao ya Chelsea yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Ukraine, Mykhailo Mudryk (23) dakika ya nane, washambuliaji Muingereza mwenye asili ya Jamaica, Raheem Shaquille Sterling (29) dakika ya 80 na Msenegal mzaliwa wa Gambia, Nicolas Jackson dakika ya 82. Kwa upande wao  Nottingham Forest mabao yao yamefungwa na beki Muivory Coast, mzaliwa wa Ufaransa, Willy-Arnaud Zobo Boly (33) dakika ya 16 na winga mwenye asili ya Ghana, Callum James Hudson-Odoi (23) dakika ya 74. Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 57 katika mchezo wa 36, ingawa inabaki nafasi ya saba, wakati Nottingham Forest inabaki na pointi zake 29 za mechi 37 nafasi ya 17 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.

MAN CITY YAITANDIKA FULHAM 4-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND

Image
MABINGWA watetezu, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London. Mabao ya Man City yamefungwa na beki Mcroatia, Josko Gvardiol (22) mawili dakika ya 13 na 71, huku mengine yakifungwa na kiungo Muingereza, Philip Walter Foden (23) dakika ya 71 na mshambuliaji Muargentina, Julian Alvarez (24) kwa penalti dakika ya 90'+6. Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 85 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England ikiizidi pointi mbili Arsenal baada ya wote kucheza mechi 36, wakati Fulham inabaki na pointi zake 44 za mechi 37 nafasi ya 14.

COASTAL UNION YAICHAPA SINGIDA FG 2-0 MKWAKWANI

Image
WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Mabao ya Coastal Union yamefungwa na mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagama (25) dakika ya 26 na kiungo Greyson Gerard Gwalala (30) dakika ya 46. Kwa ushindi huo, Coastal Union inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi zake 29 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 26.

MASAWE APIGA ZOTE MBILI NAMUNGO FC YAILAZA GEITA GOLD 2-0 RUANGWA

Image
WENYEJI, Namungo FC wameibukana ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Namungo FC yamefungwa na kiungo mkwenye anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, Jacob Raymond Masawe (31) dakika ya 43 na 45'+4. Kwa ushindi huo, Namungo FC wanafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya saba, wakizizidi tu wastani wa mabao JKT Tanzania na Kagera Sugar baada ya wote kucheza mechi 26. Hali ni mbaya kwa Geita Gold baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao24 za mechi 26 nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili za mwisho zitashuka Daraja. Nyingine mbili, ya 13 na 14 mwisho wa msimu zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu. 

TASWA KUWAFUNDA WAANDISHI CHIPUKIZI NCHINI

Image
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatarajiwa kuendesha mafunzo kwa waandishi wa Habari wanaochipukia katika nchi mbalimbali nchini.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA TWENZETU DUBAİ NA PARIMATCH WAPATIKANA

Image
Mkurugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya Parimatch, Eric Gelard (kushoto) akikabidhi ticket kwa mmoja wa washindi wa promosheni ya Twenzetu Dubai, Daniel Kasanga.  WASHINDI promosheni ya Twenzetu Dubai na Parimatch wapatikana, kupaa Jumatatu kwenda Dubai Dar es Salaam. Washindi wawili wa promosheni ya Twenzetu Dubai na Parimatch inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch wamepatikana na watasafiri Dubai Jumatatu ijayo. Washindi hao ni Daniel Kasanga, mkazi wa Ruvuma na Mohamed Salim mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Parimatch, Ismail Mohamed. Ismail alisema kuwa Kasanga ni mshindi wa droo ya wiki ya kwanza na Salim ameshinda droo ya wiki ya pili kupitia mchezo Aviator ndani ya Casino. Alisema kuwa safari hiyo itagharimiwa na kampuni yao ikiwa pamoja na usafiri, visa, malazi kwenye hoteli ya kifahari na gharama za kutembelea maeneo mbalimbali ya kitalii na kihistoria wakiwa Dubai. “Kasanga na Salim wameshinda tiketi ya