Posts

Showing posts from March, 2019

AJIBU KUSAINI MIAKA MIWILI SIMBA

Image
Wakati Ibrahim Ajibu akiwa amebakiza miezi michache Yanga tayari kumaliza mkataba wake, inaelezwa vigogo wa Simba wanaendelea kumalizana naye kimyakimya. Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema wamejidhatiti kuhakikisha anarejea ndani ya uzi mwekundu na mweupe kuhakikisha anacheza msimu ujao akiwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara. Imeelezwa kuwa vigogo hao wako kwenye mipango ya kumrejesha Ajibu huku ikisemekana anaweza akapewa mkataba wa miaka miwili. Kuna uwezekano mkubwa Ajibu akarudi Simba kutokana na hali ya mpito ambayo Yanga wanapitia hivi sasa. Tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa hana shida na mchezaji yoyote Yanga anayetaka kuondoka aondoke kwani msimu ujao wamejipanga kufanya usajili wa maana.

VIDEO: SHANGWE LA KUFA MTU KWA MASHABIKI SIMBA JAMHURI, HAKIKA ITABAKI KUWA JUU

Image

VIDEO: KOCHA SIMBA AWATIA PRESHA MAZEMBE

Image

VIDEO: PENATI ZA SIMBA ZALALAMIKIWA JAMHURI STADIUM

Image

BILIONEA MAZEMBE AMPOTEZA VIBAYA MO DEWJI

Image
APRILI 6, mwaka huu Simba itakuwa kibaruani katika Ligi ya Mabingwa kwa kucheza na TP Mazembe. Mechi hiyo ni ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Robo Fainali. Mechi hiyo inatajwa kuwa kali kutokana na upinzani wa klabu hizo mbili ambapo hii mara ya kwanza kukutana kwao tangu mwaka 2011. Nje ya mechi hii itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar, kuna vita kubwa ya mabilionea wawili, Mohammed Dewji ‘Mo’ wa Simba na Moise Katumbi wa Mazembe. Mabilionea hawa kila mmoja amefanya mambo katika kikosi chake kwa ajili ya kukijenga. Cheki mambo ambayo wameyafanya. MATAJI  Akiwa ndani ya Simba tangu mwaka 1999, Mo amefanikiwa kuifanya timu hiyo itwae mataji ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Hedex na Tusker sambamba na ubingwa wa Shirikisho (FA). Bilionea huyo pia ana rekodi ya kipekee kwa kuchangia Simba itinge hatua ya makundi ya Mabingwa Afrika kwa kumng’oa Zamalek ugenini, mwaka 2003. Mo alijiweka pembeni kabla ya kurudi hivi karibuni kuidhamini timu hiyo. Katumbi tangu mwaka 1995 ndiye mdham

MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMATATU

Image
MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMATATU

TUUFYEKELEE MBALI UYANGA NA USIMBA TUWE NA NGUVU MOJA, VIPORO NA MAANDALIZI TFF MLITAZAME KWA UKARIBU

Image
REKODI zimewekwa ili zivunjwe hivyo kwa sasa kuna suala jipya ambalo limeandikwa tena kwenye vitabu vya rekodi. Miaka 39 ni mingi na inatoa picha kwamba kulikuwa kuna kitu ambacho awali hakikuwa sawa na sasa kimemalizika moja kwa moja. Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania mnapaswa kupokea pongezi kwa kuonyesha Ushujaa mbele ya timu ngumu ambayo ilikuwa haifungiki. Wakati mnaingia vitani nina amini milIkuwa mnatambua nini mnahitaji na mkaamua kuungana kwa pamoja kupambana kwa ajili ya Taifa hicho ndicho kinatakiwa. Kwa hatua ambayo mmefikia mnapaswa mtambue kwamba ni mwanzo wa hatua nyingine ngumu zaidi ya mliyotoka hakuna muda wa kupumzika. Kama mtaendelea kufurahia ushindi mpaka kesho itakuwa ni rahisi kuanguka kutokana na namna ushindani ulivyo. Kwa sasa baada ya kufuzu Afcon akili zenu na mawazo yenu nayo yanatakiwa kubadilika haraka ili kwenda sawa na upepo namna unavyokwenda kimataifa. Kikubwa kinachohitajika kwenye mpira ni maandalizi mazuri na sahihi hali itakayosaidi

CHELSEA YATOKA NYUMA BADO DAKIKA SITA YASHINDA 2-1 CARDIFF

Image
Cesar Azpilicueta (kushoto) na Ruben Loftus-Cheek (kulia) wakishangilia baada ya kuifungia Chelsea mabao ya dakika za lala salama ikitoak nyuma kwa 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Cardiff City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Cardiff City. Víctor Camarasa alianza kuifungia Cardiff City dakika ya 46, kabla ya Azpilicueta kuisawazishia Chelsea dakika ya 84 na Loftus-Cheek kufunga la pili dakika ya 90 na ushei. Chelsea inafikisha pointi 60 baada ya kucheza mechi 31, ingawa wanabaki nafasi ya sita wakizidiwa wastani wa mabao na Arsenal iliyo nafasi ya tano   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

BOCCO APIGA MBILI, KAGERE MOJA SIMBA SC YAIPIGA MBAO FC 3-0 LIGI KUU MOROGORO

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SIMBA SC imeendeleza furaha kwa mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya Nahodha John Raphael Bocco na Mnyarwanda Meddie Kagere unaifanya Simba SC ifikishe pointi 57 baada ya kucheza mechi 22, lakini inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 59 na Yanga SC pointi 67 baada ya wote kucheza mechi 28. Bocco, mmoja wa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichokata tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa uya Afrika mwaka huu nchini Misri wiki iliyopita, alifunga bao la kwanza kwa kichwa  dakika ya 25 akimalizia krosi ya beki wa kushoto Mohammed Hussein ‘Tshabalala’. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko na kipindi cha pili Bocco akafunga bao la pili kwa penalti dakika ya 59 baada ya beki Peter Mwangosi kuanguka na kuunawa mpira uliopigwa na kiungo Muzamil Yassin. Kagere, mwenye asili

SIMBA WAENDELEZA MOTO WAO WA LIGI LEO MBELE YA MBAO, BOCCO NA KAGERE WACHEKA NA NYAVU

Image
KIKOSI cha Simba kimeendelea na moto wake wa kumaliza viporo vya ligi kwa ushindi baada ya kusepa na ushindi wa mabao 3-0 na pointi tatu dhidi ya Mbao FC mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Nahodha wa Simba, John Bocco alianza kuitanguliza Simba dakika ya 24 kwa kichwa akimalizia pasi ya Mohamed Hussein aliyepiga mpira wa adhabu na Bocco kuuzamisha nyavuni kwa kichwa. Kipindi cha pili kasi ya Mbao ilikuwa kubwa wakitafuta bao la kusawazisha ila mambo yalikuwa magumu kwao kwani dakika ya 59 Simba walipata penalti baada ya Peter Mwangosi wa Mbao kuunawa mpira eneo la hatari mwamuzi akamua ipigwe penalti iliyozamishwa wavuni na Bocco. Dakika ya 80 beki wa Mbao alimchezea rafu Meddie Kagere eneo la hatari na kusababisha mwamuzi kuamua iwe penalti iliyopigwa na Kagere mwenyewe na kuiandika Simba bao la tatu la ushindi. Kwenye mchezo wa leo kila mfungaji kajiongezea idadi yake ya bao ambapo Bocco leo amefikisha bao la 11 na Kagere akifikisha bao la 14 kama jezi yake ya mgong

TPL: SIMBA 1-0 MBAO FC, UWANJA WA JAMHURI, MOROGORO

Image
MCHEZO wa Ligi Kuu kati ya Simba na Mbao unaendelea kwa sasa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo kwa sasa ni kipindi cha kwanza John Bocco anafunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Simba leo wameanzisha jeshi lao kamili huku mlinda mlango namba moja Aishi Manula akiwa ameanza benchi akimtazama Deogratius Munish. Mashambulizi kwa timu zote ni ya kushtukiza huku kasi ya mpira ikiwa ni ya kukimbizana. Mashabiki waliojitokeza ni wengi kuona namna timu zao zitakavyoonyesha umwamba leo huku Mbao wakiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

TAIFA STARS MMEFUNGUA NJIA, KAZI INAYOFUATA NI NGUMU MSIBWETEKE, MASHABIKI SAPOTI MUHIMU

Image
HISTORIA imeandikwa Uwanja wa Taifa kwa namna ambavyo kikosi cha timu ya Tanzania Taifa Stars kilivyofanikiwa kuvunja ule mwiko ambao wengi walikuwa wakifikiria itakuwa ngumu kuvunjwa. Kufuzu kwa Stars pale kwa kuitungua Uganda mabao 3-0 haikuwa rahisi na wengi wamefurahi kuona safari imeiva hasa kwa vijana wetu wa timu ya Taifa. Pongezi kwa wachezaji kwa kuonyesha uzalendo na kujituma kuandika historia hicho ni kitu muhimu na cha kujivunia kwa kila mmoja. Watanzania wamepata kile ambacho walikwa wamekikosa kwa muda mrefu hali inayofanya furaha kuzidi kuongezeka. Miaka 39 kukatika bila timu yetu kushiriki michuano ya Afcon si haba ni mingi sana hasa kwenye ulimwengu wa michezo. Ikumbukwe kwamba ni viongozi wengi wamepita wakitazama namna ambavyo soka la Tanzania linakwenda kwa kasi ya kupanda na kushuka ila sasa kuna mabadiliko yameanza kuonekana. Ilifika wakati kiongozi mkubwa wa nchi aliamua kuita Tanzania kuwa ni kichwa cha mwendawazimu kwa upande wa mpira hakukosea alikuwa

KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA MBAO HIKI HAPA

Image
Kikosi cha Simba kitachoanza dhidi ya Mbao FC, mechi ya Ligi Kuu Bara 1. Deogratius Munishi 2. Zana Coulibaly 3. Mohammed Hussein 4. Erasto Nyoni 5. Pascal Wawa 6. James Kotei 7. Haruna Hakizimana  8. Mzamiru Yassin 9. John Bocco 10. Meddie Kagere 11. Mohammed Ibrahimu Kikosi cha akiba 12. Aishi Manula 13. Said Ndemla 14. Yusuph Mlipili 15. Paul Bukaba 16. Adam Salamba 17. Hassan Dilunga 18. Rashid Juma

WAARABU KUMG'OA KAGERE SIMBA

Image
MENEJA wa Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, Patrick Gakumba anatua nchini hivi karibuni kukutana na viongozi wa Simba kuhusu dili ya nne tofauti. Kwa mujibu wa meneja huyo Raja Casablanca ya Morocco, Zamalek ya Misri, TP Mazembe na SC Vita zote za DR Congo zimefika bei kwa Kagere. “Simba ndio wanashikilia mkataba wa Kagere kwa sasa, siwezi kuweka wazi kitu chochote hadi nitakapokutana na uongozi wa klabu hiyo ili niweze kuzungumza nao na ninatarajia kuja Dar hivi karibuni ndio nitajua kama atabaki ama la. “Kuna timu nyingi ambazo zinamuhitaji Kagere ambazo ni TP Mazembe, SC Vita, Casablanca na Zamaleki zote hizo zilimfuata na kumtaka lakini hatujafikia makubaliano nazo. “Kitaaluma na kibiashara watu wanakwenda kimkataba, Kagere ni mchezaji wangu ninammeneji lakini Simba ndio wenye mamlaka naye kwa sasa na ndio wenye maamuzi ya kumtoa ama la, hadi tukutane tukae na tuzungumze niwaombe ndipo nitakapowatangazia. “Watu wakae watambue kwamba, Simba sasa hivi sio timu ya kawaida, ma

TUYISENGE ATOA TAMKO KUHUSIANA NA SIMBA

Image
UKISIKIA tu mshambuliaji Jacques Tuyisenge ameshatambulishwa Simba SC, basi jua kuwa kila timu itakayokutana na Simba itakuwa inakula si chini ya mabao 3-0. Tusiyenge alipoulizwa na Championi Jumamosi jana jijini hapa alizuga kwamba hajafanya mazungumzo rasmi na Simba lakini yuko tayari kuwapokea muda wowote. Championi Jumamosi linajua kwamba Simba wameshamcheki kwenye simu lakini anafanya siri mpaka mipango yote ikae sawa. “Niko tayari kuzungumza na timu yoyote kwa sababu mkataba wangu na Gor Mahia unamalizika Desemba, mwaka huu na hawajaniambia kama wanataka tuongeze,” alisema staa huyo jijini hapa. “Ishu ya Simba haijaja rasmi mezani kwangu nimeisikia tu, mimi napendelea sana nchi zinazoongea Kifaransa, Kiswahili na Kinyarwanda. “Dili nilizonazo sasa ni kutoka AS Vita na timu nyingine za Cyprus lakini akili yangu iko kwa Gor Mahia zaidi sasa kwa vile nina mkataba nao,” alisisitiza mchezaji huyo ambaye ni swahiba mkubwa wa Meddie Kagere wa Simba. Simba chini ya mwekezaji mkubwa

YANGA WATANGAZA MAAMUZI MENGINE MAGUMU JUU YA AJIBU NA TSHISHIMBI

Image
MZEE wa mi-assist ndani ya Yanga na ligi kwa sasa Ibrahim Ajibu akiwa ametoa 15, pamoja Papy Tshishimbi ambao inasemekana kwamba wanaweza sepa msimu ujao uongozi wa Yanga umewapa miezi miwili tu. Ajibu amekuwa akihusishwa kurejea kwenye kikosi chake cha zamani Simba huku kiungo msumbufu kutoka Congo,  Papy Tshishimbi naye akiunganishwa katika faili hilo. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa anasikia taarifa za wachezaji wake ambao wanataka kuondoka ila hilo halimtishi kwani ni maisha ya soka. "Kuhusu kuondoka kwa mchezaji sina tatizo kwao na nimekaa kikao na viongozi wa Yanga nimewaambia wasiogope wala kutetemeka, hakuna mchezaji aliye mkubwa kuliko Yanga, kikubwa tunachoangalia ni namna ya kupambana kupata matokeo. "Kwa mchezaji ambaye ataondoka mimi nampa miezi miwili tu ligi ikishaanza mtajionea wenyewe namna itakavyokuwa kwao na ligi inayokuja Yanga itakuwa ina wachezaji wakubwa, hakuna mchezaji anayeniogopesha," amesema Zahera.

ALICHOKIANDIKA KIGWANGALLA KUHUSIANA NA PIERRE LIQUID BAADA YA KUPIGWA MKWARA NA MAKONDA

Image
Alichokiandika Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla kuhusiana na Mchekeshaji, Pierre Liquid. Andiko hili limekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kusema wanahahabari waache kumpa kiumbele Pierre sababu ya ulevi It’s ok! It’s ok! It’s ok, very ok kwa Pierre Liquid kufanya anachofanya na kufurahisha wanaoona ‘anachekesha’.  Nchi haiwezi kujengwa na watu wanaofanya mambo magumu magumu pekee. Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake. Pierre anatuchekesha na kutukumbusha kufurahia maisha tunapopata nafasi, haswa tunapotoka kufanya hayo mambo yetu magumu magumu! Jamani maisha ni magumu, yana mitihani mingi na ni mafupi sana. Katika kuleta furaha na shangwe kwenye maisha ndiyo maana ‘wachekeshaji’ wakapata ajira! Wengine tusome udaktari, uhandisi na tufanye uvumbuzi na utatuzi wa changamoto na wengine watutetemeshe, watuvuruge akili, watupe raha na furaha, watuchekeshe, siku zisogee. Maisha ndiyo haya haya! Zaidi ya yote, Pierre ni mtu huru kwenye nchi yake

SERIKALI YAZIAGIZA BMT NA TFF ZIHAKIKISHE UCHAGUZI YANGA UNAFANYIKA NDANI YA SIKU 30

Image
Na Shamimu Nyaki –WHUSM SERIKALI imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha uchaguzi wa klabu ya Yanga ya  Dar es Salaam unafanyika ndani ya siku 30 kuanzia leo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo katika mkutano na Waandishi wa Habari jana mjini Dodoma ambapo amesema kuwa migogoro iliyokuwepo huko nyuma imeshafika tamati hivyo uchaguzi ndani ya Klabu hiyo ni lazima ufanyike. “Nailekeza BMT iwaelekeze TFF kuhakikisha taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa na uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans unafayika ndani ya siku 30 kuanzia sasa,” alisema Singo. Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari jana mjini Dodoma uchaguzi wa Yanga.  Kulia ni Katibu Mtendaji wa BMT, Alex Nkenyenge. Aidha, Singo amewasihi Viongozi, wanachama na wapenzi wa Yanga kutoanzisha migogoro wala vikwazo vingine bali kutumia siku 30 hizo k

VIDEO: WAZIRI KIGWANGALA, HAJI MANARA ‘WATETEMA’ HADHARANI

Image

YANGA YATUA DAR, ZAHERA ATOA MAAGIZO KWA WACHEZAJI WAKE

Image
Kikosi cha Yanga kimewasili jijini Dar es Salaam kikitokea Mwaza ambako kilicheza mchezo wa robo fainali wa kombe la Azam Sports Federation Cup na kushinda kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya mabao 1-1. Baada ya kurejea Kocha mkuu Mwinyi Zahera amewapa mapumziko wachezaji wake kwa leo na kesho asubuhi wataendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi kurasini. Mazoezi hayi yataanza  kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC April 04 katika dimba la Nagwanda Sijaona Mtwara. Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho jana na sasa itacheza dhidi ya Lipuli Fc kwenye mchezo ujao utakaopigwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.

MUUAJI WA SIMBA APANIA KUWAVURUGA TENA LEO JAMHURI, MORO

Image
SAID Junior, mshambuliaji wa Mbao FC ambaye alifanikiwa kuipa ushindi timu yake walipocheza na Simba mzunguko wa kwanza amepania kufanya makubwa leo Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Junior amesema wamejipanga kiasi cha kutosha na wapo  tayari kuonyesha ushindani kutokana na umuhimu wa mchezo na hesabu zao ni kuona wanashinda. "Tupo vizuri na tumejipanga sawasawa hatuna hofu yoyote, nakumbuka mzunguko wa kwanza nilipata bahati ya kuifungia timu yangu, hivyo itakuwa vema pia nikipata nafasi leo na kuitumia kwa ajili ya ushindi wa timu yangu. "Mchezo utakuwa mgumu ila kikubwa ni dakika 90 ndio zitaamua, mashabiki wajitokeze kwa wingi tunatambua ni timu ya aina gani ambayo tunakutana nayo sisi tupo tayari," amesema Junior. Junior amepachika mabao 7 mpaka sasa TPL na ni kinara kwa upande wa Mbao FC kwa sasa.

VIDEO: MANARA AMPA SHARTI JOKATE KISA JEZI YA SIMBA, AITAJA MILIONI 10

Image

SIMBA: HAWA MBAO WETU KABISA LEO TUNAWAMUDU

Image
MOHAMMED Hussein 'Tshabalala' nahodha msaidizi wa Simba, amewatazama wachezaji wa Simba namna walivyojiandaa, akamaliza kutazama na rekodi za mechi zao zilizopita akacheka kwa furaha na kusema 'hawa wetu kabisa'. Leo Simba watakuwa Uwanja wa Jamhuri kumenyana na Mbao mchezo wa ligi wa mzunguko wa pili huku Simba wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Kirumba. Tshabalala amesema kuwa wanatambua utakuwa ni mchezo mgumu ila watapambana kupata matokeo kwenye mchezo wa leo. "Tulipoteza mchezo wetu wa kwanza hayo yameshapita kwa sasa tunazungumzia wakati uliopo ni muda wetu wa kupata matokeo chanya kwani tumejipanga na morali ya wachezaji ni kubwa. "Mbinu ambazo tumepewa na kocha wetu zinatufanya tujiamini zaidi na kupambana kupata matokeo hilo linawezekana mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema Tshabalala.

KINDOKI ATUMA UJUMBE SIMBA

Image
KLAUS Kindoki jana alivua jezi yake huku akipiga kifua chake mara kadhaa akiwaambia mashabiki wa Simba; “Leteni fyokofyoko tena” Kipa huyo raia wa DR Congo ambaye mashabiki wa Simba na Alliance jana walikuwa wakimkejeli kwa madai kuwa hana uwezo, ndiye aliyeibuka shujaa wa mchezo kwa kupangua penalti muhimu zilizoipeleka Yanga nusu fainali ya Kombe la Shirikisho. Baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90, kanuni ziliamuru kwenda kwenye penalti ambako ndiko Kindoki alipoibuka shujaa na kuibuka shangwe ndani ya CCM Kirumba. Mashabiki wa Yanga jana kwenye mitandao ya kijamii walimuomba radhi pia Kindoki kwa kumkejeli na kutomuamini kipindi cha nyuma. Katika kipindi cha kwanza mchezo huo ulionekana kuchangamka kutokana na mashambulizi ya hapa na pale huku ikiwatumia Yanga dakika 38 kupata bao lililofungwa nje ya kumi na nane na Heritier Makambo akipokea pasi ya Pius Buswita. Alliance wakatulia na kuanza kupiga mipira mirefu ambayo kipindi cha pili dakika ya 62, Joseph James a

KAGERA SUGAR YAANZA KUIPIGIA HESABU AZAM FC

Image
UONGOZI wa Kagera Sugar, umesema kuwa umeanza kujipanga kwa ajili ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Azam utakaopigwa Aprili 3 Uwanja wa Nyamagana. Kagera Sugar walipoteza mchezo wao wa hatua ya robo fainali kwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC uwanja wa Kaitaba. Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kupoteza mchezo wa kwanza haina maana utapoteza michezo yote kwani mpira una matokeo ya ajabu. "Kwenye ligi hatupo kwenye nafasi nzuri hivyo nimewaambia vijana wanakazi ya kupambana kupata matokeo chanya, makosa kwenye michezo iliyopita nimeyaona hivyo tumeyafanyia kazi," amesema Maxime. Kagera Sugar ipo nafasi ya 12 kwenye ligi baada ya kucheza michezo 29 imejikusanyia pointi 36 kibindoni.

EXCLUSIVE VIDEO: DOGO JANJA AJIBU KUMPIGA UWOYA ‘KULALA NA MFANYAKAZI’

Image
Mwanamuziki Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, amekanusha tetesi zilizowahi kuvuma mitandaoni kuwa aliwahi kumpiga aliyekuwa mkewe Muigizaji Irene Uwoya.

SIMBA WATOA KITISHO KWA MBAO

Image
Simba leo Jumapili itakuwa ikisaka rekodi ili kuweza kupoteza machungu na kuaibishwa na Mbao FC mwanzoni mwa msimu baada ya kipigo wakiwa ugenini. Kocha wa Simba, Patrick Aussem amewatoa hofu mashabiki. Simba na Mbao FC zitapambana katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya ule wa awali ambao walicheza CCM Kirumba, Simba kupigwa bao 1-0. Katika mchezo huo, Simba atakuwa mwenyeji lakini atatumia Uwanja wa Jamhuri baada ya ule wa Taifa kufungwa ili kupisha marekebisho ambao unatarajiwa kutumika kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana U-17. Timu hizo zimekutana mara tano huku Simba ikiibuka na ushindi mara tatu na ushindi huo ugenini mara moja na kwenye uwanja wa nyumbani mara mbili huku ikipoteza mara moja tena ugenini msimu huu. Simba na Mbao ni timu ambazo hazijawahi kukutana mwezi wa tatu lakini katika ushindi wa nyuma, wachezaji wa Simba ambao wameifunga mara nyingi zaidi ni Mzamiru Yassin (2), Emmanuel Okwi(2), na Shiz

SAMATTA ATOA PASI YA BAO LA KWANZA KRC GENK YAITANDIKA MABAO 3-0 ANDERLECHT

Image
Na Mwandishi Wetu, GENK MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ametoa pasi ya bao la kwanza na kuonyeshwa kadi ya njano, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 3-0 katika mchezo wa ufunguzi wa Championship Round ya Ligi Daraja la Kwanza A Ubeligji dhidi ya Anderlecht Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk. Samatta alitoa pasi hiyo dakika ya 32 kwa beki Mdenmark, Joakim Maehle aliyefunga bao la kwanza dakika ya 32, kabla ya Nahodha huyo wa Tanzania kuonyeshwa kadi ya njano dakika ya 75. Mabao mengine ya Genk yalifungwa na washambuliaj Mjapan, Junya Ito dakika ya 55 na Mghana, Joseph Paintsil dakika ya 79. Championship Round inashirikisha timu sita ambazo pamoja na Genk, nyingine ni Club Brugge, Standard Liège, Anderlecht, Antwerp na Gent baada ya hatua ya awali, ijulikanayo kama Regular Season ambyo Genk imeongeza.  Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana amecheza mechi ya 147 kwenye mashindano yote na akiwa amefunga mabao 59 tangu amejiunga na KRC Genk Janua

VIDEO: KOCHA SIMBA AWATAJA WACHEZAJI WOTE WANAIKOSA MBAO LEO, YUMO CHAMA

Image
Kocha wa klabu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amewataka wachezaji wote ambao watakosekana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Mbao FC.

VIDEO: KOCHA MBAO - NAPELEKA KILIO SIMBA

Image

VIDEO: SIKILIZA MICHAMBO HATARI YA BIBI MWENYE SIMBA YAKE KISA MBAO

Image

VIDEO: WALICHOKIFANYA ZANA, WAWA MAZOEZINI HIKI HAPA

Image

MANARA AWAPIGA DONGO YANGA

Image
Baada ya Yanga kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameandika hiki kupitia ukurasa wake wa Instagram.

MATOLA AMTISHA MWINYI ZAHERA

Image
Kocha Msaidizi wa Lipuli FC, Suleiman Matola, amesema kuwa mchezo ujao wa nusu fainali dhidi ya Yanga utakuwa wa aina yake. Matola ameeleza kuwa mechi hiyo itakuwa na changamoto kubwa ambapo hata wao wanahitaji ushindi ili kutinga hatua ya fainali. Yanga imeingia nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuifunga Alliance Schools kwa mabao 4-3 yaliyopatika kwa njia ya penati baada ya dakika 90 kwenda 1-1. Baada ya Yanga kuungana na Lipuli, Matola amesema hata Yanga wakija na Kocha wao Mwinyi Zahera haitakuwa sababu ya wao kushindwa kupata matokeo. "Tunajua Zahera hakuwepo wakati Yanga tunaifunga bao 1-0 kwenye mechi ya ligi kuu. "Sasa hata kama akija hakuna sababu ya kutomfunga, ni jambo la kawaida. "Tunaendelea na maandalizi ili kuja kuhakikisha tunatinga fainali." amesema Matola.

MESSI APIGA ZOTE MBILI BARCELONA YAICHAPA ESPANYOL 2-0 LA LIGA

Image
Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia mabao yote Barcelona dakika ya 71 na 89 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Espanyol kwenye mchezo wa La Liga usiku wa Jumamosi Uwanja wa Camp Nou.  Kwa ushini huo, Barcelona inafikisha pointi 69 baada ya kucheza mech 29 na kuendelea kuongoza La Liga, ikifuatiwa na Atletico Madrid pointi 56 na Real Madrid pointi 54   

MAN UNTED WAICHAPA WATFORD 2-1 OLD TRAFFORD

Image
Marcus Rashford akiteleza kushangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la kwanza dakika ya 28, kabla ya Anthony Martial kufunga la pili dakika ya 72 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Watford ambayo bao lake limefungwa na Abdoulaye Doucoure dakika ya 90 usiku wa leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford. Kwa ushindi huo wa kwanza baada ya kocha Ole Gunnar Solskjaer kusaini mkataba wa miaka mitatu kuwa kocha wa kudumu, Man United inafikisha pointi 61 baada ya kucheza mechi 31 na kurejea nafasi ya nne ikiizidi pointi moja Arsenal   PICHA ZAIDI GONGA HAPA     

MUONEKANO WA GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMAPILI

Image
Muonekano wa gazeti la Spoti Xtra katika ukurasa wa mbele leo Jumapili

MAN CITY YAREJEA KILELENI ENGLAND BAADA YA KUIPIGA FULHAM 2-0

Image
Sergio Aguero na Bernardo Silva wakishangilia pamoja baada ya wote kufunga katika ushindi wa 2-0 wa Manchester City dhidi ya Fulham kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Craven Cottage mjini London. Silva alifunga dakika ya tano na Aguero dakika ya 27 na kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 77 baada ya kucheza mechi 31, ikirejea kileleni mwa Ligi Kuu England, sasa ikiizidi pointi moja Liverpool ambayo kesho itamenyana na Tottenham Hotspur Uwanja wa Anfield   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

VIDEO: SHABIKI SIMBA AMWAHIDI GUNIA LA MCHELE RAIS MAGUFULI

Image