Posts

Showing posts from March, 2020

MJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA KLABU YA SIMBA, IDDI MBITA AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI DAR

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba, Idd Hashimu Mbitta amefariki dunia Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam. “Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi, Iddi Mbita kilichotokea leo Alfajiri ya Machi 31, 2020 Jijini Dar es Salaam,” imesema taarifa ya SImba SC leo. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Simba SC, Mohamed ‘Mo’ Dewji amesema kwamba ameumizwa mno na kifo cha Mbitta kwa sababu wamesoma pamoja shule ya Arusha, wamekuwa marafiki wa muda mrefu. “Pumzika kwa amani mpendwa wetu Iddi. Tumesoma pamoja Arusha School, urafiki wetu tukaurithisha hadi kwa watoto wetu kuwa marafiki na sisi kuendelea kufurahia mechi za Simba pamoja. Pumzika kwa amani rafiki yangu, nasi tuko njiani. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un,”amesema Mo Dewji. Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Brig

HUU NDIYO 'MSOSI' ANAOGONGA KIUNGO MSHAMBULIAJI HATARI WA YANGA SC, BERNARD MORRISON, MBOGA...

Image
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Bernard Morrison akiwa ameshika ugali wa dona kabla ya kjuanza kula katika picha hii ambayo ameiposti na kuiandikia ujumbe; Unakaribishwa kwa nyumba yangu katika msimu huu wa karantini.😂".  

KAKOLANYA HANA KINYONGO NA AISHI MANULA KUDAKA MECHI NYINGI ZAIDI YAKE SIMBA SC

KIUNGO WA SIMBA SC, FRANCS KAHATA NYAMBURA AGAWA LITA 10,000 ZA MAJI SAFI KWAO MATHARE KUSAIDIA JAMII DHIDI YA CORONA

Image
KIUNGO wa Simba SC, Francis Kahata Nyambura leo ametoa msaada wa maji safi lita 10, 000 katika eneo la Mathare nyumbani kwao, Jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya wakazi wa eneo hilo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19. Kahata aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC ya Dar es Salaam bada ya kuwasili kutoka Gor Mahia ya kwao, Kenya ametoa msaada huo baada ya mashabiki wake wa eneo hilo kumuomba.

NYOTA WA TP MAZEMBE, MTANZANIA THOMAS EMMANUEL ULIMWENGU AKIFANYA MAZOEZI YA VIUNGO NYUMBANI LUBUMBASHI

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emanuel Ulimwengu akifanya mazoezi ya viungo nyumbani kwake mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) anakochezea klabu ya TP Mazembe, kipindi hiki michezo dunia nzima imesitishwa baada ya mlipuko wa homa ya virusi ya corona inayosababisha ugonjwa wa COVID 19 

NYOTAI WA MAN UNITED, ANTHONY MARTIAL NA MWONEKANO MPYA

Image
Mshambuliaji Mfaransa wa klabu ya Manchester United, Anthony Jordan Martial akionyesha mwonekano mpya kichwani kwake baada ya kunyoa nywele kama alivyoposti mwenyewe picha hii leo akiambatanisha na ujumbe; BAKI nyumbani 

MSHAMBULIAJI WA MTIBWA SUGAR YA MOROGORO, STAHMIL MBONDE NAYE 'ACHUKUA JIKO' LEO MAPEMAA

Image
Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, Stahmil Mbonde akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa leo Jijini Dar es Salaam Mshambuliaji wa timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, Stahmil Mbonde akiwa na mkewe baada ya kufunga ndoa leo Jijini Dar es Salaam

RONALDO ANUNUA BUGATTI CENTODIECI SPORTS YA KISASA ZAIDI PAUNI MILIONI 8.5

Image
Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo ameripotiwa kutoa Pauni Milioni 8.5 kununua Bugatti Centodieci, toleo maalum sports ambayo ni moja kati ya 10 zilizotolewa dunia nzima   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

NYOTA WA KLABU YA AZAM FC NA TAiFA STARS SHAABAN IDDI CHILUNDA AUAGA UKAPERA BAADA YA KUFUNGA NDOA DAR

Image
Mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Iddi Chilunda (kushoto) akimvisha pete mkewe baada ya kufunga ndoa jana Jijini Dar es Salaam Mshambuliaji wa klabu ya Azam FC na timu ya taifa, Taifa Stars, Shaaban Iddi Chilunda (kushoto) akivishwa pete na mkewe baada ya wawili hao kufunga ndoa jana Jijini Dar es Salaam 

MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI MTANZANIA ASAINI MKATABA WA KUJIUNGA NA NYASA BIG BULLETS YA MALAWI

Image
Mshambuliaji chipukizi Mtanzania, Meshack Suleiman mwenye umri wa miaka 22 akisaini mkataba wa kujiunga na klabu ya Nyasa Big Bullets, zamani Bata Bullets Jijini Blantyre baada ya kuachana na Karonga United, zote za Ligi Kuu ya Malawi 

DK MSOLLA AWASIMAMISHA ‘WABISHI’ WAWILI KATIKA ORODHA YA WAPINGA UDHAMINI WA GSM

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM UONGOZI wa Yanga SC umewasimamisha wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji, Salim Rupia na Frank Kamugisha kuanzia leo Machi 27, 2020 hadi hapo mkutano mkuu utakapofanya maamuzi kwa mujibu wa katiba. Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa klabu, Dkt. Mbette Mshindo Msolla leo, imesema kwamba uamuzi huo umefikiwa leo baada ya kikao cha siku mbili mfululizo kilichofanyika Dar es Salaam kuanzia Mach 26 hadi 27. Na hatua hiyo imefuatia kutokea sintofahamu iliyosababisha mdhamini wa klabu, Kampuni ya GSM kusitisha kutoa misaada iliyo nje ya mkataba wake. Aidha, Kamati ya Utendaji ya Yanga imepokea na kukubali maombi ya wajumbe wengine watatu, Rodgers Gumbo, Shijja Richard na Said Kambi kujiuzulu nafasi zao na kwamba nafasi ya mjumbe wa kuchaguliwa itajazwa mara moja kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) wa Katiba ya Yanga. Wakati huo huo Kamati ya Utendaji wa Yanga imewasilisha barua GSM kujibu barua yao yenye kumbu kumbu namba GSMGROUP/YANGA/LETTER/2/2020 ya tarehe

MAGWIJI AFRIKA WAUNGANA KATIKA DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Image
MAGWIJI wa soka Afrika wameungana kutoa video fupi ya kampeni dhidi ya maambukizi virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 iitwayo #MikonoSalama na #MsishikaneMikono. Video hiyo ya sekunde 98 imehusisha wachezaji wakiwa katika maeneo wanayoishi ikisistiza kunawa mikono na kuepuka kushikana mikono, ambayo husababisha kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19, unaotikisa dunia nzima kwa sasa. Wawakilishi wa vizazi tofauti wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Anthony Baffoe wameshiriki video hiyo. https://ift.tt/2xpUrFF Hao ni pamoja na Roger Milla, Joseph Antoine Bell wa Cameroon, Herita Ilunga, Tresor Lomana Lualua wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), El Hadji Diouf, Alassane N’Dour, Khalilou Fadiga na Diomansy Kamara wa Senegal. Wengine ni Mustafa El Haddaoui wa Morocco, Jean Ssenide wa Uganda, Wael Gomaa wa Misri, Fatau Dauda wa Ghana na Vincent Enyeama wa Nigeria. Akina Diouf na Lualua wamezungumza kwa lugha na lafudhi za kwao, Wolof ya

MJUMBE YANGA SC AWA WA KWANZA KUJIUZUKU TUHUMA ZA KUUTILIA SHAKA UDHAMINI WA GSM

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Shijja Richard amejiuzulu wadhifa huo leo, kufuatia tuhuma za kuhusishwa katika orodha ya wajumbe wanne wa klabu wanaodaiwa kuutilia shaka udhamini wa kampuni ya GSM. Shijja, Mwandishi wa habari za michezo wa zamani, amesema kwamba ameamua kwa hiari yake kujiuzulu nafasi zote za uongozi katika klabu yangu ya Yanga.  “Yanga ni kubwa kuliko mimi na kuliko mtu yeyote. Yamezungumzwa mengi lakini mimi sitazungumza chochote. Wakati utaongea. Ukweli hata usipousema, huwa una tabia ya  kujitokeza wenyewe japo taratibu lakini huwa unadumu milele,”amesema Shijja katika taarifa yake. Shijja aliyewahi kugombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliopita na kuangushwa na Wallace Karia ni mmoja kati ya Wajumbe wanne wanaodaiwa kumpinga mdhamini wa klabu, kampuni ya GSM. Pamoja na kuwa na mkataba wa udhamini wa vifaa vya michezo, kampuni ya GSM imekuwa ikijitolea kufanya mambo zaidi kuisaidia Yang

SHANGHAI SHENHUA YAMPA IGHALO OFA YA MKATABA MPYA MNONO AONDOKE MAN UNITED

Image
KLABU ya Shanghai Shenhua ya China imetoa ofa ya kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake Odion Ighalo (30) ambaye anacheza kwa mkopo Manchester United. Mkataba wa sasa ulikuwa unamalizika mwaka 2022, lakini Shanghai baada ya kuridhika na kiwango chake cha hivi karibuni, wanataka kuendelea kumiliki Mnigeria huyo hadi mwaka 2024, kwa malipo ya paundi 400,000 kwa wiki. Kwa upande wake Ighalo anachusubiri ni ofa itakayotolewa na Man United baada ya mkopo wake kumalizika mwezi Juni mwaka huu kwani imekuwa ni ndoto yake ya maisha kukipiga kwa mashetani hao wekundu wa Jiji la Manchester. Shanghai Shenhua inataka Odion Ighalo arejee China kwa mshahara wa Pauni 400,000 kwa wiki   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

UMATI ULIOJITOKEZA KUMSINDIKIZA ASHA MUHAJI KATIKA SAFARI YAKE YA MWISHO LEO DAR ES SALAAM

Image
Umati wa watu uliojitokeza kwenye mazishi ya aliyewahi kuwa Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Asha Muhaji jioni ya leo kwenye makaburi ya Mwinyi Mkuu, Magomeni Jijini Dar es Salaam. Asha Muhaji aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo katika magazeti mbalimbali nchini, alifariki dunia jana mchana katika hosptali ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu

KWA BERNARD MORRISON WA YANGA SC, MAZOEZI NI POPOTE KIPINDI HIKI CHA MLIPUKO WA VIRUSI VYA CORONA

Image
Winga Mghana wa Yanga SC, Bernard Morrison akifanya mazoezi ya kuruka kamba katika maegesho ya magari kwenye nyumba anayoishi eneo la Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam kujiweka fiti kipindi hiki ambacho klabu yake imesimamisha mazoezi ya timu kwa agizo la Serikali kufuatia mlipuko wa virusi vya corona dunaini kote  

ALIYEKUWA AFISA HABARI WA SIMBA SC, ASHA MUHAJI AFARIKI DUNIA LEO HINDU MANDAL

Image
Na Mwandishi  Wetu, DAR ES SALAAM ALIYEWAHI kuwa Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Asha Muhaji amefariki dunia mapema leo katika hosptali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.  Taarifa ya klabu ya Simba leo imesema; “Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyewahi kuwa Msemaji wetu, Asha Muhaji kilichotokea leo katika hospital ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu,”. Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwamba amezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Asha Muhaji, kwani alikuwa mmoja wa wana habari wenye mchango mkubwa kwa soka ya nchi hii. Buriani Asha Muhaji, umekamilisha yako ya duniani. Tangulia na kapumzike kwa amani.  Asha aliibukia katika magazeti ya Majira na Spoti Starehe mwanzoni mwa miaka ya 1990 kabla ya kuhamia Uhuru na Mzalendo na baadaye Bingwa, Dimba, Mtanzania na Rai kabla ya kuwa Msemaji wa Simba SC wakati wa uongozi wa Alha

MBWANA SAMATTA AONYESHA YEYE NI “CHIZI MABENZI” BAADA YA KUNUNUA BENZ YA TATU ULAYA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameonyesha yeye ni mpenzi mno wa gari aina ya Mercedes Benz. Akiwa katika mwezi wa pili tu tangu ajiunge na klabu yake mpya, Aston Villa nchini England, Nahodha huyo wa Taifa Stars, Samatta tayari amenunua gari mpya aina ya Mercedes Benz ya kisasa kabisa, kwa maana ya toleo jipya. Kwake hiyo inakuwa Mercedes Benz ya tatu tangu ahamie Ulaya Januari mwaka 2016 alipojiunga na KRC Genk ya Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mbwana Samatta amenunua Mercedes Benz mpya na ya kisasa kabisa baada ya kutua England Katika miaka yake minne ya kuwa Genk, Samatta anayejulikana kama Captain Diego kwa jina la utani, amemiliki Mercedes Benz mbili, moja nyeusi iliyokuwa na namba za usajili 1- HRP - 835 na nyingine nyekundu, iliyokuwa na namba za usajili 1- HRP -853. Lakini pia akiwa Genk, Samatta aliyeuzwa kwa dau la Pauni Milioni 10 kwenda Aston Villa ya England – alimi

KWA RONALDO HAKUNA MAPUMZIKO, PAMOJA NA CORONA YEYE NA MAZOEZI TU

Image
Pamoja na wanamichezo wengi kujipa mapumziko kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona, mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameposti picha akiwa gym anafanya mazoezi na ndugu na jamaa zake. Wengine kutoka kushoto ni Rodrigo Pereira, mpwa wake Alicia, dada yake Katia, Eleanor Caires na dada yake mwingine, Elma   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MTANZANIA ANAYECHEZA SOKA YA KULIPWA MOROCCO, SIMON MSUVA AAMUA KUPAMBANA NA VIRUSI VYA CORONA KWA KUOGELEA

Image
Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva akcheza kwenye bwawa la kuogelea nchini Morocco ambako anachezea klabu ya Difaa Hassan El-Jadidi pamoja na Mtanzania mwenzake, beki Nickson Kibabage. Kwa sasa Ligi karibu zote duniani zimesimamishwa kufuatia mlipuko wa virusi vya corona na wachezaji wote wamepumzika nyumbani kwao  

TIMU YA TAIFA YA KARATE TANZANIA YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA DUNIA JAPAN OKTOBA

Image
Na Mwandishi Wetum DAR ES SALAAM TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Karate imepata Nafasi ya kwenda  kushiriki katika mashindano ya Dunia ya Karate yatakayofaanyika nchini Japan Oktoba mwaka huu. Mashindano hayo ya Karate ya Dunia huwa yanafanyika kila baada ya miaka mitatu na kwa mwaka huu Tanzania pia imepata nafasi ya kipekee kwa kutoa Jaji wa michuano hiyo ambaye ni Sensei Jerome Mhagama. BBC Imezungumza Jerome Muhagama ambaye Pia ni  Mkufunzi mkuu wa Karate Tanzania Juu ya nafasi hiyo iliyopata nchi ya Tanzania. Sensei Jerome Mhagama (kushoto) atakuwa Jaji katika mashindano ya Dunia ya Karate Japan Oktoba mwaka huu  Haya ni mashindano ya 15 ya Dunia Tangu kuanzishwa kwake,na Tanzania imewahi kushirikiki mara Mbili katika mashindano hayo. Kwa mara ya kwanza mwaka 2011 mashindano hayo yaliyofanyika Nchini Tailand,Tanzania Ilipeleka mchezaji mmoja ambaye alifika katika hatua ya 16 Bora. Mwaka 2014 Katika mashindano yaliyofanyika Japan Tanzania Ilishiriki katika mashindano

KASEJA AJIFUA KWA BIDII BAADA YA KUPONA GOTI ILI AREJESHWE TAIFA STARS AKACHEZE CHAN

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KIPA mkongwe nchini, Juma Kaseja amesema kwamba atapambana kurejesha kiwango chake baada ya kupona maumivu ya goti ili awe fiti na kurejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajil ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN). “Nitapambana, nitarejesha kiwango, na ninaamini nitakuwemo kwenye timu,” amesema Kaseja ambaye kwa sasa anadakia klabu ya KMC, baada ya kudakia, Moro United, Simba, Yanga, Mbeya City na Kagera Sugar. Juma Kaseja amesema anaamini kikosi kipya cha Taifa Stars kitakachoitwa kwa ajili ya michuano ya CHAN na yeye atakuwemo kwa kuwa ameshapona jeraha lake na sasa anarejea kwenye mapambano ya kuwania namba, asema KMC haijaanguka. Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kwa ugonjwa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona. Mechi zilizofutwa ni za tatu za na za nne kufuzu Fainali za AFCON 2021 ambazo zil