Posts

Showing posts from November, 2022

CHAMBO AIFUNGIA DODOMA JIJI YAICHAPA COASTAL 1-0

Image
TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Bao pekee la Dodoma Jiji FC limefungwa na mchezaji wa zamani wa Coastal Union hiyo hiyo, Rashid Chambo dakika ya 90. Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya 13, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 12 pia za mechi 13 nafasi ya 12.

KAGERA SUGAR YAREJEA KUCHEZA UWANJA WA KAITABA

Image
HATIMAYE klabu ya Kagera Sugar itarejea kucheza mechi zake Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kufuatia kufunguliwa kwa Uwanja wao huo.

YANGA KUMENYANA NA KURUGENZI YA SIMIYU ASFC, SIMBA NA EAGLE

DROO ya Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kamaAzam Sports Federation Cup (ASFC) imefanyika leo Jijini Dar es Salaam na mabingwa watetezi, Young Africans watamenyana na Kurugenzi ya Simiyu.    Katika droo hiyo iliyofanyika ofisi za wadhamini wa michuano hiyo, Azam TV, washindi wa pili wa msimu uliopita Coastal Union watacheza na Tanga Middle, huku vigogo wengine, Simba watamenyana na Eagle FC na Azam FC dhidi ya Malimao.  

IHEFU SC 2-1 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

IHEFU YAZIMA REKODI YA YANGA KUTOFUNGWA MECHI YA 50

Image
WENYEJI, Ihefu SC wamezima wimbi la Yanga kutopoteza mechi katika mchezo wa 50 baada ya ushindi wa 2-1 leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali mkoani Mbeya. Haukuwa ushindi mwepesi, kwani ilibidi Ihefu watoke nyuma baada ya Yanga kutangulia na bao la Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, kiungo Mkongo Yanick Bangala Litombo dakika ya tisa. Kiungo Mzimbabwe, Never Tigere aliifungia Ihefu SC bao la kusawazisha dakika ya 39, kabla ya Lenny Kissu kufunga la ushindi dakika ya 62. Kwa ushindi huo wa pili tu wa msimu kwa Ihefu iliyorejea Ligi Kuu baada ya msimu mmoja tangu ishuke, inafikisha pointi 11 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16. Yanga pamoja na kupoteza mchezo huo inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 32 za mechi 13 sasa, ikiizidi wastani wa mabao tu Azam FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.

KMC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA PRISONS UHURU

Image
  WENYEJI, KMC wamelazimishwa sare ya 0-0 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jana Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Kwa sare hiyo kila timu inafikisha pointi 15 katika mchezo wa 14, KMC ikibaki nafasi ya 10 na Prisons nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka.

KAGERA SUGAR YAICHAPA MTIBWA 1-0 KIRUMBA

Image
BAO pekee la Meshack Abraham dakika ya 68 limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inayofundishwa na kocha na Nahodha wa zamani wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya tisa. Kwa upande wao, Mtibwa Sugar wanabaki na pointi zao 21 za mechi 14 sasa nafasi ya sita.

WAOGELEAJI WA TANZANIA WANG’ARA MICHUANO YA AFRIKA

Image
WAOGELEAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania ya wanaume na wanawake (Tanzanite) wameipeperusha vyema bendera ya nchi baada ya kushinda mashindano ya Kanda ya tatu Afrika yaliyofanyika hivi kariibuni kwenye bwawa la klabu ya Dar es Salaam Gymkhana. Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya nchi 10, waogeleaji wa Tanzania walikusanya jumla ya pointi 3,061 na kuzishinda nchi tisa katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa na kusisimua. Tanzania ambayo iliwakilishwa na waogeleaji 63 pia ilikuwa nchi pekee iliyoshinda medali nyingi kushinda nchi zote zilizoshiriki katika mashindano hayo. Tanzania ilishinda jumla ya medali 110. Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na chama cha mchezo huo cha kanda ya tatu Afrika, nafasi ya pili ilikwenda kwa Kenya ambayo ilijikusanyia pointi 2,768 na kufuatiwa na Uganda iliyojikusanyia pointi 2,521.50 na Zambia katika nafasi ya nne kwa kukusanya pointi 1,878. Afrika Kusini ilishinda nafasi ya tano kwa kupata pointi 1,385. 50 ambapo Burundi

POLISI TANZANIA 1-3 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 3-2 CHAMAZI

Image
WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo mtamu wa ‘funga nikufunge’, mabao ya Azam FC yamefungwa na James Akaminko dakika ya 56, Yahya Zayd dakika ya 70 na Iddi Nado dakika ya 90 na ushei, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Maabad Maulid dakika ya 14 na Hamad Majimengi dakika ya. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 14 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi mbili mkononi. Coastal Union baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 12 za mechi 12 nafasi ya 12.

HATIMAYE UWANJA WA JAMHURI WA DODOMA WAFUNGULIWA

Image
HATIMAYE timu ya Dodoma Jiji itaanza tena kuchezea nyumbani mechi zake za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia Bodi ya Ligi kuufungulia Uwanja wa Jamhuri uliopo Dodoma. Tangu mwanzo mwa msimu, Dodoma Jiji wamekuwa wakichezea mkoa wa jirani, Singida mechi zao za Ligi Kuu, ambayo imeemelezwa kama sababu Kuu ya timu hiyo kufanya vibaya.

PHIRI APIGA MBILI SIMBA YAWAADHIBU POLISI MOSHI

Image
TIMU ya Simba SC imewaadhibu wenyeji, Polisi Tanzania kwa kuwachapa mabao 3-1 leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Mabao ya Simba SC yamefungwa na washambuliaji, Nahodha John Bocco dakika ya 32 na Mzambia, Moses Phiri mawili, dakika ya 43 na 53, wakati la Polisi limefungwa Zuberi Mbogo dakika ya 90. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 14 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja tu na mabingwa watetezi, Yanga ambao wana mechi mbili mkononi. Kwa upande wao, Polisi Tanzania baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao tisa za mechi 14 sasa nafasi ya 14.

YANGA SC 2-0 MBEYA CITY (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

UCHAGUZI MKUU SIMBA SC KUFANYIKA MWAKANI

Image
MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi Simba, Boniface Lyamwike amesema uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utafanyika Januari 29, mwaka 2023. Katika taarifa yake ya leo, Lyamwike amesema; "Mwaka huu kanuni ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa Simba ni kanuni za Simba Sports Club. Huko nyumba tulikuwa tunatumia kanuni za TFF, katiba ya Simba ilikuwa inaruhusu." "Kanuni ya sita (kanuni za uchaguzi Simba), kigezo cha kwanza mgombea lazima awe mwadilifu na awe na kiwango cha juu cha uaminifu. La pili lazima awe mwanachama hai wa klabu." "Mtu yeyote ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ni lazima awe na angalau shahada ya chuo kikuu, na lazima awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha klabu ndani na nje ya nchi." "Anayegombea nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi lazima awe amefika kidato cha nne na cheti za kuhitimu, kigezo kingine awe mzoefu uliothibitishwa wa angalau miaka mitatu ya uongozi wa mpira wa miguu." "Kingine asiwe amepatikana kamwe ya hat

NAMUNGO FC YAIPIGA DODOMA JIJI 1-0 SINGIDA

Image
BAO la Abdulmalik Hamza dakika ya 82 limetosha kuipa Namungo FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI, Singida. Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 13, ingawa nafasi ya nane, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake tisa za mechi 12 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16.

GEITA GOLD YAICHAPA IHEFU 1-0 NA KUPANDA NNE BORA LIGI KUU

Image
TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Juma Luizio dakika ya 41 akimalizia pasi ya kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza. Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya nne, wakati Ihefu inabaki na pointi zake nane za mechi 13 sasa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi ya timu 16.

MBEYA CITY 1-1 MBEYA CITY (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

MBEYA CITY YATOA SARE NA SIMBA 1-1 SOKOINE

Image
WENYEJI, Mbeya City wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Ni Simba SC waliotangulia na bao la kiungo Muzamil Yassin dakika ya 15, kabla ya Tariq Seif kuisawazishia Mbeya City dakika ya 79. Kwa matokeo hayo, Simba inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 13, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja moja na zote, Yanga iliyocheza mechi 11 na Azam FC mechi 13 pia.

SINGIDA STARS YAICHAPA KMC 1-0 LITI BAO LA KAGERE

Image
BAO pekee la mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya 40 limetosha kuipa Singida Big Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Kwa ushindi huo, Singida Big Stars inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya nne, wakati KMC inabaki na pointi zake 14 za mechi 13 katika nafasi ya 10.

CHOMOKA NA NDINGA MPYAA MSIMU HUU WA KOMBE LA DUNIA

Image
ZIKIWA zimepita siku chache tokea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Qatar, K ampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch Tanzania imewapa wateja wake na wadau wote wa kubeti mchongo wa kujishindia gari mpya na ya kisasa kabisa, simu janja pamoja na bodaboda kutoka katika kampeni yao ya Chomoka na Ndinga. Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo leo na kusema kuwa Promosheni hiyo ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi hichi cha Kombe la Dunia.   “Katika kipindi cha kuanzia 22.11.2022 hadi 26.12.2022, mteja wa Parimatch akifanya bashiri  kwenye mchezo wowote basi ataingia moja kwa moja katika droo wa kuwania Gari aina ya Urban Cruiser yenye O kilometa kutoka kwenye Showroom ya Toyota Tanzania, Bodaboda aina ya Hero Hunter  125cc na smartphone aina ya Samsung Galaxy A03 Core (Simu janja)”,   alisema Is

DODOMA JIJI 0-2 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

MAYELE APIGA MBILI YANGA YASHINDA 2-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU

Image
MABAO ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 42 na 67 yameipa Yanga SC ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC Uwanja wa LITI mjini Singida. Mayele alifunga bao la kwanza akimalizia krosi ya Mkongo mwenzake, Tuisila Kisinda kutoka upande wa kulia na la pili akimalizia pasi ya winga chipukizi, Dennis Nkane. Mkongo huyo sasa anafikisha mabao manane na kupanda kileleni kwenye chati ya ufungaji kwa bao moja zaidi ya Sixtus Sabilo wa Mbeya City. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 11 na kurejea kileleni ikiizidi wastani wa mabao tu Azam FC ambayo imecheza mbili zaidi.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA PATRICK BETWELL WA SIMBA

Image
 

KAGERA SUGAR YAICHAPA PRISONS 1-0 SOKOINE

Image
BAO pekee la Meshack Abraham dakika ya 86 limeipa Kagera Sugar ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 15 katika mchezo wa 13 na kujivuta nafasi ya tisa, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 14 za mechi 13 nafasi ya 11.

AZAM FC YAIPIGA NAMUNGO 1-0 MAJALIWA NA KUREJEA KILELENI

Image
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki  Charles Edward Manyama dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya kiungo, Ayoub Reuben Lyanga. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 13 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi pointi mbili Simba SC ambayo imecheza mechi 12. Mabingwa watetezi, Yanga SC sasa wanashukia nafasi ya tatu na pointi zao 26 za mechi 10, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 15 za mechi 12 nafasi ya nane.

IHEFU SC YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 UBARUKU

Image
WENYEJI, Ihefu SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali, Ubaruku mkoani Mbeya.  Mabao ya Ihefu SC leo yamefungwa na kiungo Mzimbabwe, Never Tigers dakika ya 41 na beki Mganda dakika ya 46, wakati la Coastal Union limefungwa na kiungo mshambuliaji, Mbaraka Hamza dakika ya 38. Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi nane katika mchezo wa 12, ingawa inaendelea kushika mkia, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 12 za mechi 11 nafasi ya 11. Mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo, wenyeji Mbeya City wamelazimishwa sare ya bila mabao na Geita Gold Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Matokeo hayo yaanifanya kila timu ifikishe pointi 18, Mbeya City katika mchezo wa 12 nafasi ya sita na Geita Gold mchezo wa 13 nafasi ya saba.

MBEYA CITY YATOA SARE YA 0-0 NA GEITA GOLD SOKOINE

Image
WENYEJI, Mbeya City wamelazimishwa sare ya bila mabao na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Matokeo hayo yaanifanya kila timu ifikishe pointi 18, Mbeya City katika mchezo wa 12 nafasi ya sita na Geita Gold mchezo wa 13 nafasi ya saba.

SIMBA SC 4-0 RUVU SHOOTING (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

BOCCO APIGA HAT TRICK SIMBA YASHINDA 4-0

Image
MABINGWA wa zamani, Simba SC wamepangwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba leo yamefungwa na Nahodha John Raphael Bocco matatu dakika za nne, 18 na 69 na beki mkongwe, Shomari Kapombe dakika ya 36. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 12 na kurejea kileleni ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi. Kwa upande wao, Ruvu Shooting wanabaki na pointi zao 11 za mechi 13 nafasi ya 13.

TRA YAITUNUKU CHETI CHA ULIPAJI BORA WA KODI AZAM FC

Image
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imepatia cheti cha pongezi Azam FC kwa kufuata taratibu zote za kikodi kama taasisi kwa mwaka wa kifedha wa 2021/22. TRA huwa na utaratibu wa kuwatambua na kuwapongeza walipa kodi bora, kupitia siku maalumu ya mlipa kodi kila mwaka.

SHABIKI WA SIMBA NA LIVERPOOL ASHINDA SH MILIONI 11 ZA 10BET

Image
 Mshindi wa jackpot ya katikati ya wiki wa 10bet apatikana Na Mwandisho wetu SHABIKI  wa Simba SC na Liverpool ya England, Richard Mkumbo ameshinda Sh11 milioni kupitia jackpot ya katikati ya wiki ya kampuni ya 10bet Tanzania. Mkumbo ambaye ni mkazi wa Singida ameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 10 za ligi mbalimbali duniani kwa sh500 tu.  ameshametia kibindoni Sh11 milioni kati ya jackpot ya 10bet Tanzania katikati ya wiki, na kumfanya kuwa mshindi wa kwanza kuwahi kutokea Tanzania. Mkumbo alitia kibindoni kiasi hicho baada ya kutabiri kwa usahihi mechi 10 za ligi mbalimbali duniani akiwa na Sh500 pekee. Ushindi huo unamfanya Mkumbo kuwa mshindi wa kwanza wa jackpot hiyo hapa nchini na kukakabidhiwa zawadi yake na Meneja Masoko wa kampuni hiyo, George Abdulrahman katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika jana. Mkumbo alisema aliamua kubashiri na 10bet kwa sababu kuwa na ‘odds’ iliyowekwa na kampuni hiyo katika mechi mbalimbali.  “Mimi ni m

YANGA SC 4-1 SINGIDA BIG STARS (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

BODI YAUFUNGIA UWANJA WA IHEFU SABABU YA PITCH MBOVU

Image
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungia Uwanja wa Highland Estate unaotumiwa na klabu ya Ihefu SC kwa sababu ya kutokuwa na eneo zuri la kuchezea mpira.

MAYELE APIGA HAT TRICK YANGA YAICHAPA SINGIDA 4-1

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji wake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fiston Kalala Mayele matatu, dakika za 16, 27 na 56 na beki wa pembeni, Kibwana Shomari dakika ya 48, wakati la SBS limefungwa na mkongwe, Meddie Kagere dakika ya 66. Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 10 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi tu wastani wa mabao Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi, wakati Simba SC yenye pointi 24 za mechi 11 inashukia nafasi ya tatu.

MBEYA CITY YATOA SARE 2-2 NA KAGERA SUGAR

Image
WENYEJI, Mbeya City wamelazimishwa sare ya 2-2 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Kagera Sugar walitangulia kwa mabao ya Anuary Jabir dakika ya 18 na Mbaraka Yussuf dakika ya 48, kabla ya Mbeya City kuchomoa kwa mabao ya Tariq Seif dakika ya 61 na Hassan Mahmoud dakika ya 81. Kwa sare hiyo, Mbeya, inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya sita, wakati Kagera Sugar imefikisha pointi 12 katika mchezo wa 12 nafasi ya 12.

POLISI TANZANIA YAICHAPA IHEFU 2-1 MBARALI

Image
TIMU ya Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya. Mabao ya Polisi Tanzania yamefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 51 na Samuel Onditi aliyejifunga dakika ya 79 baada ya Andrew Simchimba kuanza kuwafungia Ihefu SC kwa penalti dakika ya 19. Kwa ushindi huo, Polisi Tanzania inafikisha pointi tisa katika mchezo wa 12, ingawa inabaki nafasi ya 15, wakati Ihefu SC inaendelea kushika mkia kwa pointi zake tano za mechi 11 sasa.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA SHEKHAN RASHID

Image
 

MTIBWA SUGAR YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MANUNGU

Image
WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro. Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Adam Adam dakika ya pili na Juma Nyangi dakika ya 32, wakati la Coastal Union limefungwa na Mubarak Hamza dakika ya 23. Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 12 za mechi 10 nafasi ya 11.

KAZE MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TIMU ZA VIJANA YANGA

Image
UONGOZI wa klabu ya Yanga umemteua Mrundi, Cedric Kaze kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa timu za vijana chini ya umri wa miaka 17 na 20 pamoja na timu ya Wanawake, Yanga Princess.

WAOGELEAJI 63 WA TANZANIA KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA

Image
WAOGELEAJ 63 wa timu ya taifa ya Tanzania (Tanzanites na Diamond)  kesho  (Alhamis Novemba 17) wanaanza kampeni ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kanda ya tatu Afrika kwenye bwawa la klabu ya Dar es Salaam Gymkhana jijini. Mashindano hayo yataanza saa 2.00 asubuhi na kushirikisha waogeleaji wengine 200 kutoka nchi nyingine 10 za bara la Afrika. Nchi hizo ni Uganda ambayo itawakilishwa na waogeleaji 45, Burundi (10), Rwanda (14), Eritrea (5), Ethiopia (7), Zambia (23), Afrika Kusini(18), Sudan (14) na Djibouti ambayo itawakilishwa na waogeleaji  16. Pia kutakuwa na waogeleaji 48 kukamilisha jumla ya waogeleaji 263. Waogeleaji hao watashindana katika staili tano tofauti za muogeleaji mmoja mmoja na pia kutakuwa na mashindano ya relei (relay). Jumla kutakuwa na matukio 140. Waogeleaji wa timu ya Tanzanites  ambao  wamepewa jukumu la kuiletea sifa Tanzania katika mashindano hayo kwa upande wa wanawake ni  Bridget Heep, Maryam Ipilinga, Crissa Dillip na Lorita Borega. Wengine ni Amylia

AZAMFC YAREJEA KILELENI BAADA YA KUIPIGA RUVU 1-0 CHAMAZI

Image
BAO la penalti la mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 73 limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 12 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Yanga ambao wamecheza mechi tisa. Kwa upande wao, Ruvu Shooting wanabaki na pointi zao 11 za mechi 12 nafasi ya 13 kwenye ligi y timu 16.

DODOMA JIJI YAICHAPA KMC 2-1 UHURU

Image
TIMU ya Dodoma Jiji imeibuka na ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja we Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Seif Abdallah Karihe dakika ya nane na 18, wakati la KMC alijifunga beki Anderson Solomon dakika ya 48. Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi tisa katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya 14, wakati KMC inabaki na pointi zake 14 za mechi 12 sasa katika nafasi ya tisa.

SIMBA YAAJIRI KOCHA WA MAKIPA MMOROCCO

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha Mmorocco, Zakaria Chlouha kuwa kocha mpya wa makipa akichukua nafasi ya Muharami Mohamed ‘Shilton’.

KOCHA WA MAKIPA SIMBA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Image
MMILIKI wa kituo cha soka cha Cambianso Academy kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam na Kocha wa Makipa wa Simba SC wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya Dawa za Kulevya.

MAN UNITED YAICHAPA FULHAM 2-1 PALE PALE LONDON

Image
TIMU ya Manchester United jana iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Fulham FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Craven Cottage Jijini London. Mabao ya Manchester United yalifungwa na C. Eriksen dakika ya 14 na A. Garnacho dakika ya 90 na ushei, wakati la Fulham lilifungwa na D. James dakika ya 61. Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 26 katika mchezo wa 14, ingawa wanabaki nafasi ya tano wakizidiwa pointi tatu na Tottenham Hotspur ambayo pia imecheza mechi moja zaidi. Kwa upande wao, Fulham baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 19 za mechi 15 nafasi ya tisa.

KAGERA SUGAR 0-1 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

KINDA CLEMENT AING’ARISHA YANGA KIRUMBA

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, chipukizi Clement Mzize aliyepandishwa kutoka timu ya vijana dakika ya 19 akitumbukiza mpira nyavuni kwa kichwa cha mkizi kumalizia krosi ya kiungo Feisal Salum kutoka kulia. Shujaa mwingine wa pointi tatu za leo Yanga ni kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra aliyepangua mkwaju wa penalti wa Erick Mwijage baada ya yeye mwenyewe kumuangusha mshambuliaji mkongwe, Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ kwenye boksi. Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi 23 katika mchezo wa tisa na kurejea kileleni ikiizidi tu wastani wa mabao Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi. Baada ya kichapo cha leo, Kagera Sugar inabaki na pointi zake 11 za mechi 11 nafasi ya 13.

MBEYA CITY YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA COASTAL UNION SOKOINE

Image
WENYEJI, Mbeya City wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Sixtus Sabilo yote dakika ya 39 na lingine kwa penalti dakika ya 80, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Greyson Gwalala dakika ya 24 na Hamad Majimengi dakika ya 68. Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Union nayo sasa ina pointi 12 za mechi tisa nafasi ya 11.

NABI AWA KOCHA BORA LIGI KUU OKTOBA, SABILO MCHEZAJI BORA

Image
MTUNISIA wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Oktoba, huku mshambuliaji wa Mbeya City, Sixtus Sabilo akichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi huo.

SMBA SC 1-0 HEFU SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 1-0 NA KUISHUSHIA YANGA NAFASI YA TATU

Image
BAO pekee la winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 63 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Simba was SC inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na vinara, Azam FC ambao pia wamecheza mechi moja zaidi. Mabingwa watetezi, Yanga wanashukia nafasi ya tatu sasa na pointi zao 20 za mechi nane, ingawa kesho unaweza kurejea kileleni kama itashinda dhidi ya Kagera Sugar Jijini Mwanza. Ihefu yenyewe baada ya kichapo cha leo hali inazidi kuwa mbaya, ikiendelea kushika mkia kwa pointi zake tano za mechi 10 sasa.

AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA 4-3 MTIBWA

Image
TIMU ya Azam FC imepanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa ugenini wa mabao 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani Morogoro. Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo mawili dakika ya 18 na 30 na mabeki Abdallah Kheri dakika ya 41 na Daniel Amoah dakika ya 64, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na mshambuliaji Adam Adam mawili dakika ya 61 na 75 na kiungo Nassor Kiziwa dakika ya 76. Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 11 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi pointi tatu Yanga ambayo ina mechi tatu mkononi. Kwa upande wao Mtibwa Sugar wanabaki na pointi zao 15 za mechi 11 nafasi ya saba.

GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 KMC NYANKUMBU

Image
WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. Ni Geita Gold waliotangulia na bao la kiungo wake mshambuliaji Mrundi, Said Ntibanzokiza dakika ya 36, kabla ya KMC kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake, Waziri Junior dakika ya 41. Kwa matokeo hayo, kila timu inafikisha pointi 14 katika mchezo wa 11, KMC nafasi ya nane Geita Gold nafasi ya 10, zote zikilingana pointi na Tanzania Prisons iliyocheza mechi 11 oí nafasi ya tisa.

COASTAL UNION YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-0 PALE PALE SOKOINE

Image
WENYEJI, Tanzania Prisons wamepewa kichapo cha mabao 2-0 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Maabad Maulid dakika ya tano na Hamadi Majimengi dakika ya 60 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 11 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi 11. Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kichapo hicho inabaki na pointi zake pointi 14 za mechi 11 nafasi ya nane.

DADA SHAMA AJINYAKULIA TV YA DABODABO 888 BET

Image
WIKI ya nne ya droo ya Dabodabo kutoka 888 bet Tanzania imekuja kipekee Zaidi baada ya Bi Shama Kihampa kutoka Mikocheni kuondoka na Tv ya inchi 65. Bi Shama amekua kati ya washindi wa wiki ya nne ambapo wenzake wamejishindia simu janja na pikipiki. Akikabidhi zawadi hiyo, balozi wa 888 bet Maulid Kitenge, ameonesha kufurahishwa na ushindi wa Bi Shama ambaye anakua mwanamke wa kwanza kujishindia zawadi toka droo hiyo ya Dabodabo ianze. “Ushindi wa Bi Shama unaonesha kuwa sasa michezo ya kubashiri inazidi kushika kasi na inazidi kukubalika katika jamii, hii ni motisha kwa wanawake na mabinti wote ambao walidhani michezo hii ni kwaajili ya wanaume tu.” Alisema Bwana Maulid kwa furaha. “888 bet wametoa fursa hii kwa watanzania wote, haijalishi jinsia, kama una umri wa miaka 18 na kuendelea jukwaa ni lako kujaribu bahati yako leo. Tembelea www.888bet.tz na uweke mkeka wako, zimebaki wiki mbili lakini zawadi ni nyingi sana na hapo bado kuna zawadi kubwa ya milioni 100!” Kwa wiki nne s

CLUB AFRICAIN 0-1 YANGA SC (KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA)

Image
 

YANGA YAICHAPA AFRICAIN 1-0 NA KUTINGA MAKUNDI SHIRIKISHO

Image
KLABU ya Yanga imefanikiwa kwenda Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Club Africain usiku huu Uwanja wa Olimpiki mjini Rades nchini Morocco. Bao pekee la Yanga leo limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 79 kwa shuti akimalizia pasi ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele. Yanga wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 1-0 kufuatia sare ya bila kufungana Jumatano iliyopita Jijini Dar es Salaam.

AZAM FC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 NA KUIFIKIA YANGA POINTI

Image
WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo mzawa, Ismail kader dakika ya 38 na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 90 na ushei kwa pelnati, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na mshambuliaji Mkenya, Collins Opare dakika ya 41. Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao wana mechi mbili mkononi, wakati Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao sita za mechi 10 sasa nafasi ya 14.

SINGIDA BIG STARS NA SIMBA SARE 1-1 LITI

Image
WENYEJI, Singida Big Stars wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa LITI mjini Singida. Kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke alianza kuifungia bao Singida Big Stars dakika ya 11, kabla ya winga Mmalawi, Peter Banda kuisawazishia Simba SC dakika ya 79. Kwa sare timu zote zimafikisha pointi 18, Simba ikibaki nafasi ya pili katika mchezo wa tisa na Singida nafasi ya nne katika mchezo 10.

BODI YA LIGI YAUFUNGULIA UWANJA WA USHIRIKA

Image
BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeufungulia Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro ambao hutumiwa na klabu ya Polisi Tanzania.

CHAMA NA AZIZ KI WAFUNGIWA, YANGA FAINI, FLORENTINA...

Image
VIUNGO washambuliaji, Mzambia Clatous Chota Chama wa Simba Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso wamefungiwa mechi tatu kila mmoja kwa makosa yanayofanana.