Posts

Showing posts from April, 2024

REAL MADRID YATOA SARE 2-2 NA BAYERN MUNICH UJERUMANI

Image
WENYEJI, Bayern Munich wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani. Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na winga Mjerumani mwenye asili ya Senegal, Leroy Aziz Sané dakika ya 53 na mshambuliaji Muingereza, Harry Kane kwa penalti dakika ya 57, wakati ya Real Madrid yote yamefungwa na mshambuliaji Mbrazil, Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior dakika ya 24 na 83 kwa penalti. Sasa Real Madrid itatakiwa kushinda nyumbani kwenye mchezo wa marudiano au sare si za ya bao 1-1 ili kwenda Fainali kwa faida ya mabao ya ugenini. Na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Borussia Dortmund ya Ujerumani pia na PSG ya Ufaransa.

SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA NAMUNGO FC 2-2 RUANGWA

Image
WENYEJI, Namungo FC wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Simba walitangulia kwa bao la mshambuliaji Mcameroon, Leandre Willy Essomba Onana dakika ya 34, kabla ya mshambuliaji mzawa, Kelvin Sabato Kiduku kuisawazishia Namungo FC dakika ya 39. Kipindi cha pili tena Simba walitangulia kwa bao la kiungo Edwin Balua dakika ya 70, kabla ya beki Kennedy Wilson Juma kujifunga dakika ya 90 kuisawazishia Namungo FC. Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 24 nafasi ya tisa, wakati Simba SC inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 22 nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 54 na Yanga 62 baada ya wote kucheza mechi 24.

FIFA YAIFUNGIA YANGA KUSAJILI HADI IMLIPE KAMBOLE

Image
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifungia klabu ya Yanga kusajili mchezaji mpya hadi hapo itakapomlipa aliyekuwa mshambuliaji wake, Mzambia Lazarous Kambole msimu uliopita.

KLABU YA SWEDEN YAWASILI NCHINI KWA MWALIKO WA AZAM FC

Image
KLABU AIK Stockholm ya Sweden imewasili nchini usiku huu kwa mwaliko wa Azam FC kwa ajili ya kujenga mahusiano na wenyeji wao hao. Ugeni huo umeongozwa na mtendaji mkuu wa club hiyo (CEO), Fredrik Söderberg, Mkurugenzi wa Ufundi,(Technical Director)Peter Wennberg, na msaka vipaji mkuu, (Chief Scout)Tobias Ackerman. Baada ya kuwasili nchini walipokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Omary Kuwe, wawakilishi hawa wa klabu hiyo watapata nafasi ya kushuhudia mashindano ya kusaka vipaji yaliyoandaliwa Azam FC. Timu zaidi ya 10 kutoka akademi mbali mbali za mikoa tofauti hapa nchini zitashiriki, ambazo zina ushirikiano nazo Azam FC kufuatia makubaliano yaliyoingiwa mapema mwezi uliopita. Mashindano hayo yatashirikisha  wachezaji wa chini ya miaka 15, 17 na 20, umri chini ya na chini ya miaka 15 na yataanza Aprili 30 na kumalizika Mei 4. Dhumuni la ujio huo ni kusimika mahusiano ya klabu hizo mbili katika biashara ya mpira ikiwa ni pamoja na kusaka vipaji katika mashindano hayo. AI

JKT TANZANIA YAICHIMBIA KABURI MTIBWA SUGAR, YAICHAPA 2-1 MBWENI

Image
WENYEJI, JKT Tanzania wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam. Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na Edson Katanga dakika ya saba na Sixtus Sabilo dakika ya 90, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Charles Ilamfya dakika ya 22. Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 24 na kusogea nafasi ya 10, wakati Mtibwa Sugar inabaki nafasi ya mwisho kwenye Ligi ya timu 16 ikiwa na pointi 17 za mechi 23 sasa.

PARIMATCH YAZINDUA PROMOSHENI YA TWENZETU DUBAI ZAYLISSA, KIREDIO WAULA

Image
MASHABIKI wa soka, tenisi, UFC, Kriketi, baseball na michezo mingine sawa wanaweza kushinda tiketi ya kwenda Dubai kwa kubashiri na kampuni ya Parimatch Tanzania. Pia kampuni hiyo imeingia mkataba na muigizaji nyota, Zainabu Saidi Bakari maarufu kwa jina la Zaylissa kuwa balozi wa chapa yao, “Brand Ambassodor”. Mbali ya Zaylissa, pia mchekeshaji maarufu nchini, Vincent Njau “Kiredio” naye ametangazwa kuwa balozi chapa wa Parimatch wakiungana na meneja wa habari wa zamani wa Yanga, Haji Manara. Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa Parimatch, Levis Paul, jumla ya mashabiki nane (8) watashinda tiketi hiyo kupitia promosheni hiyo ya Twenzetu Dubai na Parimatch ambayo imezinduliwa jana kwenye hotel ya Serena. Paul alisema kuwa kutakuwa na droo ya kutangaza washindi kila Alhamis na dhumuni kubwa la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwawezesha wateja wao kuendelea kufurahia ushindi. Alisema kuwa mbali ya zawadi ya kwenda Dubai, pia kutakuwa na bonasi ya Sh5,000 kwa yeyote atakayejisajili na Parim

HATIMAYE PAMBA FC YAREJEA LIGI KUU, BIASHARA NA MBEYA KWANZA KUJARIBU ‘MLANGO WA UANI’

Image
HATIMAYE timu ya Pamba ya Mwanza imefanikiwa kurejea Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mbuni FC leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Ushindi huo unaifanya Pamba FC imalize Ligi ya NBC Championship na pointi 67, nyuma ya mabingwa, Ken Gold ya Mbeya iliyomaliza na pointi 70 na wote wanapanda Ligi Kuu moja kwa moja. Timu ya Mbeya Kwanza ya Mbeya inayotumia Uwanja wa Nangwanda Sijaona wa Mtwara iliyomaliza na pointi 65 nafasi ya tatu itamenyana na Biashara United ya Mara iliyomaliza na pointi 62 na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na timu iliyoporomoka kutoka Ligi Kuu kujaribu kupanda kupitia mchujo huo. GONGA KUTAZAMA MATOKEO MECHI ZOTE ZA MWISHO LIGI YA CHAMPIONSHIP LEO

RAIS WA YANGA HERSI AMKABIDHI JEZI WAZIRI WA MICHEZO IVORY COAST

Image
RAIS wa Young Africans SC na Mwenyekiti wa Shirikisho la Klabu Afrika (ACA) Hersi Ally Said akimkabidhi jezi ya klabu hiyo Waziri wa Michezo wa Ivory Coast, Adjé Silas baada ya kukutana Jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo.  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 

MASHABIKI SIMBA WALIVYOJITOKEZA KUPOKEA KOMBE LA MUUNGANO

Image
MASHABIKI wa Simba SC waliojitokeza kuwapokea wachezaji wao baada ya kurejea kutoka Zanzíbar ambako jana walitwaa Kombe la Muungano kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

RAIS WA ZANZIBAR DK MWINYI ALIVYOWAKABIDHI SIMBA KOMBE NA ‘MAHELA’ YA MUUNGANO JANA

Image
RAIS wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Kombe la Muungano Nahodha wa Simba SC, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ baada ya ushindi wa 1-0 jana dhidi ya Azam FC Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. RAIS wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Nahodha wa Simba SC Fedha Taslimu Sh. Milioni 50 kwa kutwaa Kombe la Muungano jana Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. RAIS wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Tuzo ya Kipa wa michuano ya Kombe la Muungano kipa wa Simba SC, Mmorocco Ayoub Lakred jana Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. RAIS wa Zanzíbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Tuzo ya Mchezaji Bora wa michuano ya Kombe la Muungano kiung Mkongo wa Simba SC, Fabrice Luamba Ngoma jana Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar.

MAN UNITED YAAMBULIA SARE 1-1 KWA BURNLEY

Image
WENYEJI, Manchester United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Burnley FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester/ Mshambuliaji Mbrazil, Antony Matheus dos Santos alianza kuifungia Manchester United dakika ya 79, kabla ya mshambuliaji Mswisi mwenye asili ya Tunisia, Mohamed Zeki Amdouni kuisawazishia Burnley kwa penalti dakika ya 87. Kwa matokeo hayo, Manchester United inafikisha pointi 54 katika nafasi ya sita ikiizidi tu pointi moja Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 34, wakati Burnley inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 35 nafasi ya 19.

NI AL AHLY NA ESPERANCE FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Image
MABINGWA watetezi, Al Ahly wamefanikiwa kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) usiku wa jana Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo. Mabao ya Al Ahly jana yalifungwa na Mohamed Abdelmonem dakika ya 68, Wessam Haissam Abou Ali dakika ya 83 na Akram Tawfik dakika ya 90'+12 na kwa ushindi huo mnono wa nyumbani wanakwenda Faniali baada ya kulazimisha sare ya bila mabao kwenye mechi ya kwanza Lubumbashi. Al Ahly itakutana na Espérance Sportive de Tunis ambayo jana nayo iliitoa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa kuichapa 1-0, bao pekee la beki Raed Bouchniba dakika ya 57 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mbrazil, Rodrigo Rodrigues Uwanja wa Loftus Versfeld Jijini Pretoria. Espérance inakwenda Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-0 kufuatia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita bao la mshambuliaji mwingine Mbrazil, Yan Medeiros Sasse dakika ya 41 Uwanja wa Ol

STRAIKA MRUNDI AIPONZA TABORA UNITED YAFUNGIWA TENA KUSAJILI

Image
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifungia klabu ya Tabora United kufanya usajili wa mchezaji mpya hadi hapo itakapomlipa madai yake mshambuliaji Mrundi, Jean Didier Touya.

MAN CITY YAICHAPA 4-0 BRIGHTON & HOVE ALBION

Image
MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Brighton & Hove Albion Uwanja wa The Amex, Falmer, East Sussex. Mabao ya Manchester City yamefungwa na kiungo mkongwe Mbelgiji, Kevin De Bruyne dakika ya 17 na washambuliaji Muingereza, Philip Foden mawili dakika ya 26 na 34 na' Muargentina, Julián Álvarez dakika ya 62. Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 76 katika mchezo wa 33 ikizidiwa pointi moja na vinara, Arsenal ambao pia wamecheza mechi moja zaidi, wakati Brighton & Hove Albion inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 33 nafasi ya 11.

AZAM YAICHAPA KMKM 5-2 NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA MUUNGANO

Image
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Muungano baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya KMKM katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ mawili, dakika ya saba na 42, Nathaniel Chilambo dakika ya tisa, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 49 na Iddi Kichindo dakika ya 74, wakati ya KMKM yamefungwa na Abrahman Ali yote kwa penalti dakika ya 38 na. Azam FC sasa itakutana na Simba SC katika Fainali hapo hapo Uwanja wa New Amaan Complex kuhitimisha sherehe za miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzíbar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Simba SC ilikata tiketi ya Fainali jana kwa ushindi wa mabao 2-0, mabao ya Muivory Coast Freddy Michael Koublan na mzawa, Israel Patrick Mwenda dhidi ya wenyeji wengine, KVZ hapo hapo New Amaan Complex.

SIMBA QUEENS YAIKANYAGA YANGA PRINCESS 3-1 CHAMAZI

Image
TIMU ya Simba Queens imeendeleza ubabe kwa watani wao, Yanga Princess baada ya kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba Queens leo yamefungwa na kiungo Aisha Juma Mnunka mawili dakika ya 49 na 90’+2 na mshambuliaji Mkenya, Jentrix Shikangwa Milimu dakika ya 66, wakati bao pekee la Yanga Princess limefungwa na kiungo Mmarekani, Kaeda Wilson dakika ya 90’+5.

SERIKALI YASAINI MKATABA WA BILIONI 19.7 KUKARABATI UWANJA WA UHURU

Image
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini mkataba na Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ndiye aliyesaini kwa niaba ya Serikali leo Aprili 25, 2024 Jijini Dar es Salaam na unatarajiwa kufanyika kwa muda wa miezi 12 na ukigharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 19.7. Katika hatua nyingine, Katibu huyo Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Msigwa aalizindua toleo Maalum la Mafanikio ya Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

YANGA SC YATOKA PATUPU ISAMUHYO, 0-0 NA JKT TANZANIA

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam. Kwa sare hiyo, Yanga SC inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 23 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi tano zaidi ya Azam FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati JKT Tanzania inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16. Ikumbukwe timu mbili za mwisho zitashuka Daraja mwisho wa msimu na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini ili mshindi wa jumla asalie Ligi Kuu wakati timu itakayofungwa itakwenda kucheza na timu kutoka Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

ARAJIGA AIFUATA SIMBA SC KOMBE LA MUUNGANO ZANZIBAR

Image
REFA Ahmed Arajiga wa Manyara ni miongoni mwa waamuzi watatu wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara walioteuliwa kuchezesha Kombe la Muungnao, michuano inayotarajiwa kuanza leo usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar. Wengine kutoka Bara ni Frank John Komba na Amina Samuel Kyando wakati wa Ligi Kuu ya PBZ Zanzíbar ni wanne, Al Ahmada Mbwana, Ali Ramadhani Ibada, Nasir Siyah ‘Msomali’ na Mohamed Simba Khamis. Simba itafungua dimba Kombe la Muungano michuano inayorejea baada ya miaka 20 kwa kumenyana na wenyeji, KVZ katika Nusu Fainali leo kuanzia Saa 2:15 usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzíbar wakati Azam FC kesho Azam FC itaumana na KMKM. Washindi wa mechi za Nusu Fainali watakutana katika Fainali Aprili 27 hapo hapo Amaan Complex.

YANGA NA TABORA MEI MOSI CRDB BANK FEDERATION CUP

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC watamenyana na Tabora United Mei 1 katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia Saa 2:30 usiku. Mchezo huo utatanguliwa na michezo miwili siku hiyo ya Robo Fainali ya CRDB Bank Federation Cup kati ya Ihefu SC na Mashujaa Saa 10:00 jioni Uwanja wa LITI mjini Singida na Coastal Unión dhidi ya Geita Gold Saa 12:15 jioni Uwanja wa  Mkwakwani Jijini Tanga. Hatua ya Robó Fainali ya CRDB Bank Federation Cup  itakamilishwa Mei 3 kwa mchezo kati ya Azam FC na Namungo FC Saa 1:00 usiku Uwanja Azam Complex.

YANGA YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKA NA ATCL

Image
KLABU ya Yanga leo imeingia makubaliano ya ushirika na Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) ambapo utazinufaisha pande zote mbili. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Yanga wataitangaza biashara ya ATCL na wao watapatiwa punguzo la bei kwenye safari zao mbalimbali ndani na nje ya nchi.  “Hatuwezi kuona huduma ya Air Tanzania inafanyika bila sisi kuitangaza. Kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali yetu," amesema Rais wa Yanga SC, Hersi Said.

KAI APIGA MBILI ARSENAL YAICHAPA CHELSEA 5-0

Image
WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi mnono dhidi ya Chelsea wa mabao 5-0 usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London. Mabao ya Arsenal yamefungwa na mshambuliaji, Mbelgiji Leandro Trossard dakika ya nne, beki Muingereza Benjamin White dakika ya 52 na 70 na kiungo Mjerumani, Kai Havertz dakika ya 57 na 65. Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 77 katika mchezo wa 34 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi tatu zaidi ya Liverpool iliyocheza mechi 33 na wote wakiwa mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 73 za mechi 32. Kwa upande wao Chelsea waliokuwa wanacheza mechi ya 32 ya msimu wanabaki na pointi zao 47 katika nafasi ya tisa baada ya kupoteza mchezo wa leo dhidi ya mahasimu wao wa London.

MECHI YA JKT TANZANIA NA YANGA YAAHIRISHWA UWANJA MAJI MENGI

Image
MCHEZO wa l Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya mabingwa watetezi, Yanga SC na wenyeji, JKT Tanzania uliopangwa kufanyika jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam umeahirishwa kwa sababu ya maji kujaa kwenye eneo la kuchezea. VÍDEO: ALLY KAMWE AKIZUNGUMZA BAADA YA MECHI KUAHIRISHWA ISAMUHYO 

BODI YAAHIRISHA MECHI ZA SIMBA NA YANGA, YAZIADHIBU TABORA, JKT NA KMC

Image
BODI ya Ligi Kuu (TPLB) imeahirisha mechi kadhaa za Azam na Simba ili kuzipa fursa ya kushiriki michuano ya Kombe la Muungano inayotarajiwa kuanza keshokutwa visiwani Zanzíbar. Simba itamenyana na wenyeji, KVZ katika Nusu Fainali ya Kombe la Muungano Jumatano ya Aprili 24 Uwanja wa New Amaan Complex visiwani, Zanzíbar wakati Azam FC itaanza na KMKM Alhamisi. Washindi wa mechi za Nusu Fainali watakutana katika Fainali Aprili 27 hapo hapo Amaan Complex. Katika hatua nyingine, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imezitoza faini klabu za Tabora United, JKT Tanzania na KMC kwa makosa tofauti ya kikanuni kwenye mechi zao za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. GONGA KUSOMA ZAIDI ADHABU ZILIZOTOLEWA NA TPLB GONGA KUTAZAMA MECHI ZA LIGI KUU ZILIZOAHIRISHWA 

MABINGWA 56 WADONDOSHEWA BATA LA KUFA MTU MTOKO WA KIBINGWA NA BETIKA

Image
MABINGWA wa Promosheni  Kubwa ya Mtoko wa Kibingwa msimu wa 07 waandika historia wakongwa nyoyo kwa burudani ya aina yake zakiem  na Kushuhudia derby ya kariakoo Jukwaa la VIP dimba la Mkapa. Aidha shamramshara hizo za Mtoko wa Kibingwa zilipambwa na burudani ya aina yake kuanzia mabingwa hao kusafiri na Mwewe (Ndege) na Kupokelewa na Kampuni hiyo ya Betika akianziwa na Meneja Mahusiano Juvenalius Rugambwa pamoja na balozi wa Kampeni ya Mtoko wa Kibingwa Mtangazaji wa derby ya Kariakoo kutoka Azam tv Baraka Mpenja. Aidha baada ya hapo Mabingwa hao walipelekwa kwenye hoteli ya hadhi ya Nyota tano kupata chakula cha Mchana na baadae kuelekea Mbagala zakiem  kushuhudia wasanii kibao wakitoa burudani za Kimuziki hasa mziki wa Singeli . Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja Sholo Mwamba,Pk Mr Konki, Mczo,Chino Wanaman,Mzee wa Bwax ,platform pamoja na dj Ommy crazy walihakikisha Mabingwa wanapata burudani ya kuikaribisha derby hiyo. Pia Meneja Masoko alitoa zawadi mbalimbali ikiwem

SIMBA SC KUSHIRIKI KOMBE LA MUUNGANO ZANZIBAR

Image
TIMU ya Simba SC itashiriki michuano ya Kombe la Muungano inayoandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Zanzíbar (ZFF) kuazimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzíbar.

BERNARDO SILVA AIPELEKA MAN CITY FAINALI KOMBE LA FA ENGLAND

Image
TIMU ya Manchester City imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea FC usiku wa jana Uwanja wa Wembley Jijini London. Bao pekee la Mancester City jana lilifungwa na kiungo Mreno, Bernardo Silva dakika ya 84 na sasa watakutana na mshindi kati ya Coventry City na Manchester United zinazomenyana leo katika Nusu Fainali ya pili leo. Fainali itachezwa Mei 25 Uwanja wa Wembley.

ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND

Image
TIMU ya Arsenal jana imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands. Mabao ya mshambuliaji Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 45 na kiungo Mnorway, Martin Ødegaard dakika ya 90'+5 na kwa ushindi huo, Arsenal wanafikisha pointi 74 katika mchezo wa 33 na kurejea kileleni wakiwazidi pointi moja tu mabingwa watetezi,  Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi. Kwa upande wao  Wolverhampton Wanderers baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao43 za mechi 33 nafasi ya 11.

YANGA SC 2-1 SIMBA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

YANGA YAICHAPA SIMBA SC 2-1 NA KUZIDI KUUKARIBIA UBINGWA MWINGINE LIGI KUU

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi watani wao, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 58 katika mchezo wa 22 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi saba zaidi ya Azam FC inayofuatia ikiwa pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Simba SC inabaki na pointi zake 46 za mechi 21 nafasi ya tatu.   Ilikuwa siku nzuri kwa wanasoka kutoka Afrika Magharibi, washambuliaji Joseph Guédé Gnadou (29) na Freddy Michael Kouablan (25) wote kutoka Ivory Coast na kiungo Stephane Aziz Ki (28) kutoka Burkina Faso waliofunga mabao kwenye mechi hiyo ya mahasimu wa Tanzania. Aziz Ki alianza kuifungia Yanga dakika ya 20 kwa mkwaju wa penalti uliotolewa na refa Ahmed Arajiga wa Manyara kufuatia Mburkinabe huyo kuangushwa kwenye boksi na beki mzawa Hussein Kazi ambaye aliingia dakika ya 11 kuchukua nafasi ya beki Mkongo, Henock Inoga Baka aliyeumia. Guede akai

YANGA WAKUTANA NA CSKA MOSCOW KWA LENGO LA USHIRIKIANO

Image
UONGOZI wa klabu ya Yanga SC umekutana na Uongozi wa CSKA Moscow ya Urusi kwa lengo la kutengeneza mahusiano ya kukuza vipaji kwa soka la vijana na kubadilishana taaluma mbalimbali za kimichezo na utawala.  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

AZAM FC YASAJILI BEKI WA MALI YORO MAMADOU DIABY

Image
KLABU ya Azam FC imefikia makubaliano na akademi ya Yeleen Olympique ya Mali kwa ajili ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa nchi hiyo, Yoro Mamadou Diaby. Taarifa ya Azam FC imesema kwamba beki huyo wa kati ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Stade Malien de Bamako, atajiunga nao rasmi kuanzia msimu ujao wa 2024/25. Akiwa klabuni Stade Malien de Bamako, Yoro aliisadia klabu hiyo kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho, akiifungia timu yake mabao katika mechi zote mbili za robo fainali dhidi ya Dreams FC ya Ghana. Yoro amezichezea timu zote za vijana za taifa za Mali, kuanzia ile ya chini ya 17, chini ya miaka 20 na chini ya miaka 23. Yoro pia alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Mali kilichoshiriki CHAN, mwaka 2022 nchini Algeria.

WASHINDI 56 MTOKO WA KIBINGWA BETIKA KUSHUHUDIA DERBY KWA MKAPA KESHO

Image
WASHINDI 56 Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu wa 07 kuitazama Derby ya Kariakoo kati Simba na Yanga itakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Wanahabari mapema Leo Aprili 19,2024 Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Tanzania Juvenalius Rugambwa wakati akiwapokea Washindi Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere amesema washindi hao wamepatikana kupitia droo ya mtoko Kibingwa iliyoanza Mapema Februari 2024. "Kama mnavyowaona hawa ni washindi ambao wamepatikana kupitia kampeni yetu ya mtoko kibingwa na hawa washindi waliowasili Leo wataenda kuungana na wenzao wa Dar es Salaam nakukamilisha idadi kamili ya washindi 56 na wote watakwenda kulala kwenye hoteli yenye hadhi ya nyota tano wakifatiwa na bata la Mbagala zakiem kushuhudia burudani ya Muziki wa Bongofleva itakayodondoshwa na chino Wana Man, Mczo, platform, sholo Mwamba na wengine kibao.". Jevenalius ameongeza kuwa Msimu huu wa mtok