Posts

Showing posts from January, 2019

ALLIANCE FC WAITANGAZIA VITA LIPULI YA MATOLA

Image
UONGOZI wa Alliance FC umesema kuwa kesho itakuwa ngumu kwa kikosi cha Lipuli ya Matola kupenya kwenye machinjio ya Uwanja wa Nyamagana mkoni Mwanza kwa kuwa tayari wamepata mbinu za kuingamiza pamoja na uzoefu kwa michezo yao iliyopita. Alliance ambao wamepanda daraja msimu huu wameanza kurejea kwenye ushindani licha ya kufungwa na timu zote kubwa ikiwa ni pamoja na Simba na Yanga. Ofisa Habari wa Alliance, James Mwafulango amesema mwendo walionao Alliance sasa ni kusambaza misumari ya moto hivyo Lipuli wajiandae kisaikolojia kupokea wanachokitaka. "Kwa sasa naweza kusema kwetu sisi gari limewaka tutatumia vema Uwanja wa nyumbani kupata matokeo kwenye mchezo wetu wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli. "Tunaiheshimu timu ya Lipuli tunaiheshimu, mchezo utakuwa mkubwa ila kikubwa hesabu zetu ni kupata matokeo kwenye uwanja wetu wa nyumbani, mashabiki watupe sapoti," alisema Mwafulango. Alliance inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo

HIZI HAPA TIMU NANE KAZINI LIGI KUU BARA MZUNGUKO WA PILI

Image
LIGI Kuu Bara leo inaendelea kwa timu nane kutimua vumbi kwenye viwanja vinne kutafuta pointi tatu ikiwa ni mzunguko wa pili. Kagera Sugar watacheza leo na kikosi cha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, KMC wapo mkoani Shinyanga watacheza na Stand United uwanja wa Kambarage. JKT Tanzania wataikaribisha Mwadui uwanja wa Isamuhyo na Ruvu Shooting leo atakuwa kazini kumenyana na Mbeya City uwanja wa Mabatini.

MWAMUZI OTHMAN KAZI ALIVYOCHAMBUA SUALA LA KIPA AZAM KUPOTEZA MUDA OVYO UWANJANI

Image

DUH! ZAHERA AWAKA TENA KWA MAKAMBO, AMCHANA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI

Image
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa katika mechi yao ya kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Biashara United imekosa nafasi nyingi ambazo wameshindwa kuzitumia. Zahera amezungumzia kiwango cha mshambuliaji wake Herieter Makambo kuwa kimerudi nyuma kama hapo awali alivyokuwa akicheza na kufanya vitu vya onyo pindi anapokuwa uwanjani.

VIDEO: GOLIKIPA ANAYEDAIWA HUENDA AKASAINI YANGA, APISHANA KAULI NA KOCHA WAKE

Image

VIDEO: HAJI MANARA ATAJA MAAMUZI MAGUMU ALIYOWAHI KUMFANYIA BABA YAKE

Image
Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ametoa wito kwa wasanii kutumia vizuri fursa wanazozipata huku akimtolea mfano mwanamuziki Diamond Platnumz ambaye kwa sasa ndiye anavuma sana na kumkumbusha kuwa ipo siku hatavuma tena kwahiyo ni vyema kutumia muda huu ipasavyo. Aidha Manara amefunguka kuhusiana na kuwahi kumkatalia Baba yake kuingia uwanjani bure siku za nyuma. Msikilize vizuri hapa

VIDEO: MAKONDA AWAPIGWA MKWARA WASANII, JB

Image
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, jana Januari 31, amekutana na wasanii kutoka katika tasnia zote nchini ikiwemo Muvi, Bongo Fleva, Muziki wa asili, wacheza mpira, kwa ajili ya kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali yanayohusu sanaa nchini. Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa Leaders Club Kinondoni jijini Dar. Akizungumza katika kikao hicho, RC Makonda amesema ni mkutano wa wazi ambao wasanii wote walipaswa kutoa mawazo yao ili Serikali imeze kuwasaidia na ambaye anataka mkutano wa privacy kama alivyoomba msanii JB, basi akafanye mkutano wake au akazungumze na mkewe kwani kinachojadiriwa hakina usiri wowote. Awali, JB alimwomba mkuu huyo wa mkoa kuunda kamati maalum kwa ajili ya kwenda kujadili kwa kina yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutanio huo akidai kuna baadhi ya vitu haviwezi kusemwa hadharani.

MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO IJUMAA

Image
Muonekano wa gazeti la Championi katika ukurasa wa mbele leo Ijumaa

YANGA SC YAITOA BIASHARA UNITED KWA MATUTA TAIFA, YATINGA 16 BORA ASFC

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM YANGA SC imefanikiwa kwenda hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90. Waliofunga penalti za Yanga SC ni Heritier Makambo, Paul Godfrey, Ibrahim Ajibu, Thabani Kamusoko na Matheo Anthony, za Biashara United zilifungwa na Lenny Kissu, George Makang’a, Derick Mussa, Kauswa Bernard, wakati Tariq Seif akapaisha ya nne. Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Rashid Zongo, Biashara United ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza 2-1. Waziri Junior alianza kuifungia Biashara United kwa penalti dakika ya pili tu kufuatia beki Andrew Vincent ‘Dabte’ kumuangusha kwenye boksi George Makang’a. Yanga SC wakasawazisha kwa penalti pia iliyopogwa na mshambuliaji wake Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe dakika ya saba kufuatia Frank Sekule wa Biashara United kumuangusha Nahodha, Ibrahim Ajibu. Na Biashara United wakapata bao la pili

KICHUYA AKAMILISHA UHAMISHO WAKE MISRI, ATOLEWA KWA MKOPO ENPPI YA LIGI KUU

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Shiza Ramadhani Kichuya amekamilisha uhamisho wake kujiunga na klabu ya Pharco ya mjini Alexandria nchini Misri. Tayari Kichuya yupo mjini Alexandria na taratibu za kumpeleka kwa mkopo klabu ya ENPPI zimekamilika na kesho ataanza mazoezi na timu yake hiyo mpya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Jumanne Februari 5. Pharco imeamua kumtoa kwa mkopo Kichuya ENNPI kwa sababu Ligi Daraja la Pili Misri imemalizika kwa sasa. Shiza Kichuya amekamilisha uhamisho wake kujiunga na Pharco ya Misri  Pharco iliyoanzishwa mwaka 2010 inapigana kujaribu kupanda Ligi Kuu ya Misri na msimu huu imezidiwa kete na Al Nasr Lel Taa'en, El Sharkia na Tanta zilizofanikiwa kupanda. Kocha wa timu hiyo, Mreno Jose Rui Lopes Aguas ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Cape Verde, amevutiwa mno na Kichuya baada ya kuonyeshwa uwezo wake kupitia DVD. Na akiwa ana umri wa miaka 22, Kichuya aliyejunga na Sim

TAIFA STARS KUMENYANA NA SUDAN KUWANIA TIKETI YA CHAN YA 2020 ETHIOPIA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TANZANIA itaanza na Sudan katika mechi za kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ethiopia. Katika droo iliyopangwa jana makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjin Cairo, Misri kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Kenya itamenyana na Burundi, Sudan Kusini na Uganda na Somalia dhidi ya Rwanda. Tanzania imeshiriki fainali moja tu za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast tena baada ya kuitoa Sudan katika hatua ya mwisho ya mchujo. Ibrahim Ajibu mmoja wa nyota wanaotarajiwa kuunda kikosi cha Tanzania cha CHAN Baada ya kumaliza nafasi tatu katika Kundi A mwaka 2009 mjini Abidjan nyuma ya Zambia na Senegal zilizokwenda Nusu Fainali, Tanzania imeshindwa kurudia mafanikio hayo kwenye michuano hiyo. Ikiwa chini ya kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kwa sasa, Taifa Stars itakuwa na wakati mgumu mbele ya Sudan ambayo ni moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufuzu AFCON ya Ethiopia 2020.

AZAM FC U20 YAWACHAPA VIJANA WENZAO WA YANGA 2-1 CHAMAZI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya vijana ya Azam FC chini ya umri wa miaka 20 (Azam U-20) usiku wa jana iliwachapa vijana wenzao wa Yanga mabao 2-1, katika mchezo wa kirafiki uliomalizika Uwanja wa Azam Complex, dar es Salaam. Azam U-20 imekuwa na utamaduni wa kucheza mechi mbalimbali za kirafiki ikiwa chini ya Kocha Mkuu wake, Meja Mstaafu Abdul Mingange, lengo likiwa ni kujiweka sawa kwa ajili ya ligi ya vijana na michuano mingine iliyopo mbele yao. Mchezo huo ulikuwa ni wa upinzani mkubwa kwa pande zote mbili, jambo ambalo liliwavutia watazamaji waliojitokeza kutazama burudani ya vijana hao, lakini Azam U-20 ikionekana kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha pili. Vijana wa Azam FC walianza kutangulia dakika ya tatu tu ya mchezo, kwa bao safi la umbali lililofungwa na mshambuliaji wake hatari, Abadi Kawambwa kwa shuti zuri lililomshinda kipa. Yanga inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Said Maulid ‘SMG’, ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika chache baadaye k

LIVE: WEMA, SHETA, TALE, DIAMOND KWENYE MKUTANO NA MAKONDA

Image

LIVE: MWAMUZI FIFA: NIYONZIMA ALISABABISHA NIKAPIGWA

Image

ALIYEACHIWA NA CHELSEA KUANZA NA REAL MADRID

Image
ALVARO Morata, ambaye amejiunga na Atletico Madrid kwa mkopo, ataanza kuonyesha cheche zake dhidi ya timu yake ya zamani, Real Madrid. Atletico itavaana na wapinzani wao wa jadi, Real Madrid kwenye mechi ya La Liga itakayopigwa Februari 9, kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano. Ni wazi kuwa jambo hilo litampa presha kubwa Morata kwani alikulia Real Madrid ambao ndio wamemsaidia kumpa jina lakini sasa atavaana nao akiwa na wabaya wao, Atletico Madrid. Morata, ambaye inadaiwa ana mapenzi ya tangu utotoni na Atletico, bila shaka atapata wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa Real Madrid, ambao watamwona kama msaliti. Morata, ambaye amejiunga na Atletico akitokea Chelsea, alipoulizwa kama atashangilia kama akifunga, aligoma kujibu swali hilo. Aliwahi kuchezea kwa mkopo, Juventus hatakuwemo kwenye kikosi kitakachoivaa Real Betis, Jumapili ijayo. Morata sasa ana nafasi ya kuonyesha makali yake baada ya kuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Chelsea

KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA BIASHARA UNITED

Image
Kikosi cha Yanga kitakachoanza leo dhidi ya Biashara United Uwanja wa taifa. 1.Ramadhan Kabwili 2.Paul Godfrey 3.Gadiel Michael 4.Andrew Vincent 5.Kelvin Yondan 6.Feisal Salum 7.Mrisho Ngassa 8.Pius Buswita 9.Heritier Makambo 10.Ibrahim Ajibu 11.Amiss Tambwe Kikosi cha akiba 1.Klaus Kindoki 2.Juma Abdul 3.Papy Tshishimbi 4.Thaban Kamusoko 5.Deus Kaseke 6.Matheo Anthony

MITAMBO HII MIPYA KWA BIASHARA UNITED KUIBUKA TAIFA LEO

Image
BIASHARA United ya Mara leo watakuwa wageni mbele ya Yanga uwanja wa Taifa wakicheza mchezo wa shirikisho ikiwa ni hatua ya nne kwa mujibu wa Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji wote wana morali na wapo sawa. Mchezo wa leo Biashara United kwa mara ya kwanza tangu wapande Ligi Kuu Bara watakuna na mtambo wa kutengeneza mabao Yanga, Ibrahim Ajibu mwenye mabao 6 na pasi za mabao 14 kwenye Ligi Kuu Bara. Kwenye mchezo wao wa kwanza waliokutana nao ambao ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Taifa, Ajibu aliwakosa Biashara kutokana na matatizo ya kifamilia licha ya kutokuwepo walishinda mabao 2-1. Pia kiungo mwenye uzoefu na Ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa, Mrisho Ngasa naye pia leo atakutana na Biashara kwa mara ya kwanza kwani walipokutana kwenye Ligi Kuu alikuwa anatumikia kadi nyekundu aliwakosa Biashara United. Biashara United wao wana kocha mzoefu Amri Said ambaye alikuwa wa kwanza kuitungua Simba alipokuwa Mbao na sasa yupo na kikosi cha Biashara hivyo ana

STRAIKA HUYU AWEKA REKODI YAKE BONGO KWA MAKIPA WOTE WA SIMBA

Image
MSHAMBULIAJI wa Mbao FC, Said Khamis ameweka rekodi yake kwa sasa Bongo akiwa ni mchezaji wa kwanza kuwatungua magolikipa ghali Ligi Kuu Bara, Aishi Manula na Deogratius Munish wote wa Simba. Khamisi alianza kumtungua Aishi Manula kwenye Uwanja  wa CCM Kirumba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulikuwa wa kwanza kwa Simba kupoteza msimu huu ukiwa ni mchezo wao wa nne. Manula alitunguliwa na Khamis kwa mkwaju wa Penalti na kuifanya Simba kuwa timu ya kwanza kubwa kupoteza mchezo wake mapema kwenye Ligi Kuu Bara kabla ya Azam FC na Yanga kupoteza. Hivi karibuni kwenye michuano ya SportPesa Cup ambayo Simba walikuwa washindi wa tatu, Khamis alimtungua tena mlinda mlango Deogratius Munish kwa penalti yake ya kwanza Uwanja wa Taifa. Khamis anaweka rekodi yake Bongo kuweza kuwafunga magolikipa wote wa timu moja kwa aina moja ya ufungaji wa bao la penalti akiwa kwenye viwanja viwili tofauti na mashindano tofauti.

SIKU YA KWANZA MISRI, KICHUYA ATOLEWA MKOPO....

Image
Siku moja baada ya kuuzwa Misri, kiungo Shiza Kichuya ametolewa kwa mkopo. Kichuya ameuzwa na Simba katika klabu ya Pharco ya Misri ambayo imeamua kumtoa kwa mkopo Enppi inayoshiriki Ligi Kuu Misri. Kiungo huyo tayari ni mali ya Mafarao hao na atamalizana na Simba wikiendi hii katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba iko nchini Misri kuwavaa wababe wa Afrika, Al Ahly

SIKU YA KWANZA MISRI, KICHUYA ATOLEWA MKOPO....

Siku moja baada ya kuuzwa Misri, kiungo Shiza Kichuya ametolewa kwa mkopo. Kichuya ameuzwa na Simba katika klabu ya Pakho ya Misri ambayo imeamua kumtoa kwa mkopo Enppi inayoshiriki Ligi Kuu Misri. Kiungo huyo tayari ni mali ya Mafarao hao na atamalizana na Simba wikiendi hii katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba iko nchini Misri kuwavaa wababe wa Afrika, Al Ahly

AUSSEMS AMTUMIA MESEJI ZAHERA

Image
KOCHA mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ya ameweka wazi kuwa akili yake ipo kwenye mambo mawili tu kwa sasa ambayo ndiyo anayapa kipaumbele zaidi kwenye timu yake. Aussems amesema kuwa licha ya kukabiliwa na mchezo mgumu wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly lakini anachotakiwa ni kuhakikisha anachukua ubingwa wa msimu huu. Simba imeondoka jana jioni kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wake wa huo wa hatua ya makundi utakaopigwa Februari 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Borg El Arab uliopo Alexandaria, Misri. Mbali ya Simba kushiriki Ligi Mabingwa Afrika inakabiliwa na mechi sita za viporo katika Ligi Kuu Bara huku nyuma kwa pointi 20 mbele ya Yanga wanaongoza ligi wakifuatiwa na Azam wenye poi nti 47. Aussems ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Tuna mechi ngumu Misri lakini b ado haiwezi kuwa kigezo cha kutufanya tuache kuangalia ligi ya kuu kwa sababu tunataka kutetea ubingwa wetu bila ya kuangalia nani yupo juu, tutashinda mechi zetu ili kufikia ma

ZAHERA ALETA BONGE LA KIUNGO YANGA

Image
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa ili kumfanya kiungo wake, Feisal Salum ‘Fei Toto’ awe na uwezo wa hali ya juu, atamletea kiungo mpya ambaye atampa changamoto ya kugombania namba. Fei Toto aliyetua Yanga msimu huu akitokea JKU ya Zanzibar, kwa kiasi kikubwa ndiye ambaye amekuwa akitumika kama kiungo mkabaji ndani ya kikosi hicho cha Yanga. Viungo wengine ambao wanacheza sambamba na Fei ni pamoja na Papy Tshishimbi, Raphael Daud na Maka Edward. Zahera amesema kwamba anatarajia kumpa ushindani Fei kwa kumleta kiungo Gustapha Simon kwenye timu ya wakubwa ili kutoa changamoto ya namba kwa wachezaji waliokuwepo. “Yule mtoto (Gustapha) anajua sana na naamini akija huku timu ya wakubwa basi ataleta changamoto ya hali ya juu sana. Hawa kina Fei Toto na Tshishimbi watakuwa na kazi kubwa sana ya kugombania naye namba. “Nilimuona alichofanya katika Kombe la Mapinduzi, ana uwezo wa hali ya juu katika kuendesha timu lakini pia kuichezesha timu, akija timu ya wakubwa basi ataf

KIGOGO KIBOKO YA WAARABU ANG’ATUKA SIMBA

Image
KIGOGO wa Simba ambaye aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji ambaye amewahi kuwa mbabe katika mechi za Waarabu ameamua k u j i w e k a pembeni na soka kwa sasa. Dewji ni miongoni mwa wadau wakubwa wa mpira hapa nchini ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi la Friends of Simba akiwa pamoja na aliyekuwa Rais wa Simba, Evance Aveva ambaye kwa sasa yupo rumande. Kigogo huyo wa Simba alikuwa akihusika kwa kiasi kikubwa katika kuiwezesha timu hiyo pamoja na kutoa uhamasishaji kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi mbalimbali zikiwemo zile ambazo zilikuwa zikiwahusisha Waarabu. Dewji alihusika kwa sehemu kubwa kuipa heshima Simba baada ya kuwa kiongozi wa mstari wa mbele kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Zamalek mwaka 2003, mchezo ambao Simba walishinda na kuingia hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika. Hata hivyo katika siku za hivi karibuni kigogo huyo amekuwa haonekani uwanjani kama ilivyokuwa huko nyuma wakati Simba ikicheza. Championi Jumatan

HIZI HAPA LEO TIMU NANE LIGI YA WANAWAKE KUINGIA KAZINI

Image
LIGI ya wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League inaenelea kwa timu nane kushuka Uwanjani kumtafuta mbabe wa pointi tatu. Viwanja vinne leo vumbi litatimka kushuhudia msisimko wa Ligi hii ambayo bingwa mtetezi ni JKT Queens. Evergreen Queens kazini leo uwanja wa Karume kumenyana na Baobab Princess, JKT Queens mzigoni kumenyana na Sisterz FC uwanja wa Mej.Gen.Isamuhyo. Marsh Queens watamenyana na Mlandizi Queens uwanja wa Nyamagana na Mapinduzi Queens mzigoni leo uwanja wa Sabasaba dhidi ya Simba Queens, mechi zote hizi zitaanza saa 10:00 jioni.

MAPINDUZI QUEENS WANAPATA TAABU SANA LIGI YA WANAWAKE, UONGOZI WASHTUKA

Image
TIMU ya Mapinduzi Queens ambayo inashiriki Ligi ya Wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League inapata taabu kutokana na safu yake ya ushambuliaji kushindwa kuwa na makali huku safu ya ulinzi ikiwa ni butu. Mapinduzi Queens yenye maskani yake mkoani Njombe mpaka sasa imecheza michezo tisa na imefungwa michezo saba huku ikitoka suluhu michezo miwili na ina pointi mbili ikiwa nafasi ya 12 kwenye Ligi yenye timu 12. Ofisa Habari wa Mapinduzi Queens, Njenjema Barnabas amesema uongozi umeshtukia hilo kutokana na timu kuwa na mwenendo wa kusuasua dawa ya kuwa na matokeo bora inachemka. "Kwa sasa hatuna namna zaidi ya kupambana kwa hali na mali tupate matokeo Uwanjani, imani yetu ni kwamba tutawapa mashabiki kile ambacho wanakitarajia nacho ni matokeo mazuri. "Tunashindwa kuleta ushindani kutokana na wachezaji wetu kushindwa kuhimili mikikimiki ya ligi kwa sasa ila hali hii ni ya muda tu tayari dawa ipo jikoni ni suala la muda, mashabiki watupe sapoti,"

SUALA LA VIPORO LITAZAMWE UPYA, LIGI KUU INAANZA TUISAHAU SPORTPESA CUP

Image
BAADA ya mashindano ya SportPesa Cup kukamilika wikiendi iliyopita,  Ligi Kuu Bara ambayo ilisimama kwa muda inatarajiwa kuendelea wikiendi hii. Kwa kilichotokea SportPesa Cup ni aibu kiujumla kwa Taifa hivyo timu zote za Tanzania zitambue kwamba zimeshindwa kwa mara ya pili nyumbani kuonyesha ukomavu wao hivyo wachukue kama funzo . Turudi kwenye Bodi ya Ligi Kuu Bara Tanzania (TBLB) inayofanya kazi sambamba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itazame kwa umakini namna ya kupanga ratiba ya Ligi Kuu Bara. Katika ratiba hiyo inaonyesha kuna baadhi ya mechi za viporo kwa baadhi ya timu zitachezwa  Aprili mwaka huu kitu ambacho naona ni mbali wakati hapa kati kuikuwa na uwezekano wa mechi hizo kuchezwa. Uwepo wa viporo kwa timu unaua msisimko wa Ligi Kuu Bara ni lazima kuwe na uwiano wa michezo hata kama kuna viporo basi visizidi sana. Katika jambo ambalo linavuruga ratiba ni pamoja na viporo maana kuna wakati timu zina nafasi ila hakuna mchezo unaochezwa kwa kile kinachoelezwa ni

RONALDO NA JUVENTUS YAKE WACHAPWA 3-0 NA KUTOLEWA COPPA ITALIA

Image
Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo akiudhibiti mpira mbele ya beki wa Atalanta katika mchezo wa Robo Fainali Coppa Italia usiku wa jana Uwanja wa Atleti Azzurri d'Italia mjini Bergamo. Atalanta ilishinda 3-0, mabao yake yakifungwa na Timothy Castagne dakika ya 37 na Duvan Zapata mawili dakika za 39 na 86   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

CHIESA APIGA HAT TRICK FIORENTINA YAICHAPA 7-1 AS ROMA

Image
Federico Chiesa akiwa ameshika mpira wake baada ya kupiga hat-trick kwa mabao yake ya dakika za saba, 18 na 74 katika ushindi wa 7-1 wa Fiorentina dhidi ya AS Roma kwenue mchezo wa Robo Fainali Coppa Italia usiku wa jana Uwanja wa Artemio Franchi mjini Firenze. Mabao mengine ya Fiorentina yalifungwa na Giovanni Simeone mawili dakika za 79 na 89, Luis Muriel dakika ya 33 na Marco Bennassi dakika ya 66, wakati la AS Roma  iliyompoteza mchezaji wake, Edin Dzeko aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 72 tena baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Javier Pastore kipindi cha pili lilifungwa na Aleksandar Kolarov dakika ya 28   PICHA ZAIDI GONGA HAPA    

COUTINHO AFUNGA MAWILI BARCELONA IKIICHAPA SEVILLA 6-1 KOMBE LA MFALME

Image
Mbrazil Philippe Coutinho akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Barcelona katika ushindi wa 6-1 wa Barcelona dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Kombe la Mfalme Hispania usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Mabao mengine ya Barca yalifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 31, Sergi Roberto dakika ya 54, Luis Suarez dakika ya 89 na Lionel Messi dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Sevilla lilifungwa na Guilherme Arana dakika ya 67. Barcelona inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-3 kufuatia kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza   PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA LEICESTER CITY ANFIELD

Image
Mshambuliaji Sadio Mane akishangilia baada ya kuifungia Liverpool bao la kuongoza dakika ya tatu 1-1 kabla ya Harry Maguire kuisawazishia Leicester City katika sare ya 1-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Anfield. Liverpool inafikisha pointi 61 baada ya sare ya jana katika mechi ya 24, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

CHELSEA YAFUMULIWA 4-0 NA BOURNEMOUTH NA KUONDOLEWA 'TOP FOUR

Image
Mshambuliaji wa AFC Bournemouth, Joshua King akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili timu yake dakika za 47 na 74 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vitality mjini Bournemouth, Dorset. Mabao mengine ya Bournemouth yamefungwa na David Brooks dakika ya 63 na Charlie Daniels dakika ya 90 na ushei katika siku ambayo mchezaji mpya Gonzalo Higuain alianza vibaya urejeo wake ligi ya England klabu ya Chelsea ikipigwa na kutolewa kwenye nne Bora ya msimamo wa ligi. Kipigo hicho kinaifanya Chelsea sasa ilingane kwa kila kitu na Arsenal, idadi ya mechi za kucheza wote 24, wastani wa mabao wote jumlisha 17 na pointi wote 47, wakati Bournemouth inafikisha pointi 33 katika mechi ya 24 na kupanda kutoka nafasi ya 12 hadi ya 10   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

SHIZA KICHUYA AKARIBIA KUJIUNGA NA KLABU YA LIGI DARAJA LA PILI MISRI

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Shiza Ramadhani Kichuya yuko mbioni kujiunga na klabu ya Pharco ya mjini Alexandria nchini Misri. Taarifa ya Simba SC imesema kwamba klabu ipo kwenye mazungumzo na Pharco inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri ambayo yanaendelea vizuri. Pharco iliyoanzishwa mwaka 2010 inapigana kujaribu kupanda Ligi Kuu ya Misri na msimu huu imezidiwa kete na Al Nasr Lel Taa'en, El Sharkia na Tanta zilizofanikiwa kupanda. Shiza Kichuya yuko mbioni kujiunga na Pharco FC ya mjini Alexandria nchini Misri Kocha wa timu hiyo, Mreno Jose Rui Lopes Aguas ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Cape Verde, amevutiwa mno na Kichuya baada ya kuonyeshwa uwezo wake kupitia DVD. Na akiwa ana umri wa miaka 22, Kichuya aliyejunga na Simba SC mwaka 2016 akitokea timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro anapata nafasi ya kwenda kujaribu bahati yake nje. Tayari kuna wachezaji wawili wa Tanzania wanaocheza Ligi Kuu ya Misri ambao ni kiungo Himid M

MUONEKANO WA GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO ALHAMIS

Image

VIDEO: VIONGOZI YANGA WALIODAIWA KULA MAMILIONI WATAJWA, HAWA HAPA

Image
Klabu ya yanga imesema kuwa kuna waandishi ambao wanapotosha watu kuwa Yanga imeingiza kiasi kikubwa cha fedha ambacho baadhi wa viongozi wa Yanga wanatumia kwa matumizi yao binafsi bila kujali klabu.

VIDEO: MAMILIONI YANAYODAIWA KUINGIA YANGA, UONGOZI WALIA NA UPOTOSHAJI

Image

UCHAGUZI WA YANGA GIZA NENE, SIMBA KAZI IPO

Image
Unaweza kusema kwa sasa kuna wingu zito kuhusiana na hatma ya uchaguzi wa Klabu ya Yanga kutokana na kwamba haijfahamika ni lini utafanyika. Uchaguzi huo ni kwa ajili ya kujaza nafasi ya mwenyekiti ambaye awali alikuwa Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe watatu ambao wote walijiuzulu. Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Januari 13, mwaka huu, lakini ukasogezwa mbele kutokana na baadhi ya wanachama wa Yanga kufungua kesi mahakamani kupinga kufanyika kwake. Kitendo cha wanachama hao kufungua kesi katika mikoa zaidi ya mitano kilisababisha Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuahirisha tarehe ya awali ya kufanyika kwa uchaguzi huo mpaka itakapotangazwa tena. Kamati hiyo iliyopo chini ya mwenyekiti wake, Malangwe Mchungahela, walitangaza kuwa baada ya siku saba kuanzia Januari 14, wangeweka hadharani hatma ya uchaguzi lakini mambo yamekuwa tofauti na kamati imekuwa kimya. Siku zinazidi kusonga, bado Yanga haijafahamu uchaguzi wake na kujua ha

KISA JEZI YA BIKO KUVALISHWA MAKAMBO, YANGA WAWAKA BALAA, TAMKO LAO HILI HAPA

Image
Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Ofisa Habari wake, Dismas Ten, umeitaka kampuni ya bahati nasibu 'Biko' kuacha mara moja kuwavalisha wachezaji wake jezi zao kwa kuwa hawajafanya nao mazungumzo.

STRAIKA MPYA SIMBA ASEPA KWAO

Image
Mshambuliaji Sadney Urikhob aliyekuja kwa majaribio Simba ameondoka nchini kurejea kwao Namibia. Urikhob alikuja nchini kufanya majaribio hayo huku kocha Patrick Aussems akiwa ameonyesha kuridhishwa na kiwango chake.  Imeelezwa sraika huyo alitua nchini akitokea Indonesia na alicheza mechi 2 za michuano ya Sportpesa Cup.  Taarifa imesema Kocha Aussems ameahidi kushughulikia suala lake baada ya mechi ya dhidi ya Al Ahly huku Hunlede Kisimbo amefeli majaribio. Taarifa za chini ya kapeti zinasema Mnamibia huyo akisharejea na mipango ya Aussems kishafanikisha juu ya usajili wake anaweza akasini mkataba wa mwaka mmoja au miwili.

KAKOLANYA AFUNGUKA UPYA JUU YA SUALA LAKE NA YANGA

Image
Baada ya kuomba kuvunjiwa mkataba wake na uongozi wa klabu ya Yanga, mlinda mlango, Beno Kakolanya, amesema hawezi kuzungumza lolote kwa sasa bali anamwachia Wakili wake. Kakolanya ambaye alitua Yanga akitokea Tanzania Prisons, amesema tayari Wakili wake ameshakamilisha kupeleka barua Yanga na kilichobaki kitasimamiwa na Mwanasheria huyo. Kakolanya na Wakala wake waliamua kukaa chini na kuamua kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba kutokana na timu yake kushindwa kumlipa stahiki ikiwemo mshahara. Tayari Yanga imekiri kupokea barua hiyo ambayo wamesema nao wataijibu kisheria, ambapo wamemtaka Kakolanya na Wakili wake wasubirie majibu hayo ya kisheria. Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti, Samuel Lukumay, amefunguka kwa kukiri kuipokea barua hiyo ambayo wataitolea majibu siku yoyote kuanzia leo.

AJIBU AIBUKA NA KALI JUU YA MKATABA WAKE NA YANGA, ANAONDOKA?

Image
Nahodha wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajibu, amesema hawezi kuondoka ndani ya timu hiyo hivi sasa kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kuitimizia kile alichonacho, imeelezwa. Ajibu ambaye alichukua kitambaa cha unahodha kutoka kwa Kelvin Yondani aliyevuliwa na Kocha Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa ni ngumu kuondoka kwake hivi sasa. Mshambuliaji huyo ameibuka na kali kwa kusema hajui mkataba wake umebakiza muda gani lakini anachoangalia ni namna atakavyokuwa na wachezaji wenzake kama nahodha. Aidha, taarifa imesema Ajibu ameeleza kuwa anacheza na wachezaji wenzake ndani ya Yanga hivyo itakuwa si rahisi kuwaacha kwa maana ana majukumu ya kuwaongoza kama Kapteni. Wakati Ajibu akifunguka hayo, kikosi cha Yanga hivi sasa kipo katika maandalizi ya kucheza na Biashara kesho Jumamosi, mechi itakayokuwa ya Kombe la FA.

AMBOKILE WA MBEYA CITY AJIUNGA NA BLACK LEOPARDS YA AFRIKA KUSINI KWA MKOPO

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Eliud Ambokile amejiunga na klabu ya Black Leopards FC ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu. Taarifa iliyotolewa na Mbeya City leo imesema kwamba Ambokile anajiunga Black Leopards FC  iliyoanzishwa mwaka 1983 katika mji wa Venda uliopo kaskazini mwa Afrika Kusini baada ya mpango wa awali wa kujiunga na El Gounah kushindikana. Ambokile wiki iliyopita nchini kutoka Misri baada ya wiki moja ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu huyo ya Ligi Kuu ya nchini humo. Eliud Ambokile amejiunga na Black Leopards FC ya Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu Na Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe alisema kwamba Ambokile alorejea baada ya kufanya vizuri katika majaribio yake El Gounah, lakini klabu hiyo haikufikia makubaliano na Mbeya City. “Hawa mabwana (El Gounah) baada ya kumjairbu kwa siku sita, wakataka kumchukua kwa mkopo, au acheze kwanza kwa miezi sita ndiyo waaamue kumnunua m

SIMBA SAWA AL AHLY WAGUMU, ILA MKIJARIBU INAWEZEKANA

Image
NDANI ya wiki iliyopita, kulikuwa na mambo mengi kwelikweli kwenye medani ya soka ambayo yalitokea. Ndani ya siku saba tu, kuna matukio ya Kombe la SportPesa ambalo kama ilivyo ada Watanzania tumeshindwa kufua dafu kwa kuruhusu ubingwa uende Kenya. Pia siku hizo kukaibuka hoja ya wachezaji wa Simba kutoroka kambini na mwishowe kabisa tukamaliza kuhusiana na Kombe la Shirikisho (FA) ambalo liliendelea kwa mechi kadhaa. Yote hayo yameenda na hii ni wiki nyingine, kwa hiyo tunayaweka pembeni. Baada ya kuanza na mambo hayo, sasa narudi kwenye mada yangu. Msafara wa Simba jana jioni uliondoka nchini na kwenda Misri kwa ajili ya mechi yake nyingine ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameenda Misri kucheza na vigogo Al Ahly katika mechi nyingine ngumu ya ugenini itakayofanyika Jumamosi hii. Mechi hii imekuja ikiwa ni wiki chache baada ya kikosi hicho kutoka DR Congo ambapo kilipoteza kwa mabao 5-0, hoja yangu ya msingi ipo hapa. Natambua hali n