Posts

Showing posts from August, 2022

TUISILA KISINDA AREJEA YANGA SIKU YA MWISHO YA USAJILI

Image
WAKATI dirisha la usajili la Ligi Kuu ya Tanzania Bara limefungwa usiku huu, klabu ya Yanga imehitimisha usajili wake kwa kumrejesha winga wake Mkongo, Tuisila Kisinda kutoka RSB Berkane ya Morocco baada ya msimu moja tu tangu imuuze.

SIMBA SC YACHAPWA 1-0 NA EL HILAL SUDAN

Image
KLABU ya Simba imekamilisha mechi zake za kirafiki nchini Sudan kwa kuchapwa 1-0 na wenyeji, El Hilal usiku huu Uwanja wa El Hilal mjini Khartoum. Bao pekee la El Hilal limefungwa na John Mano dakika ya 62 na kwa matokeo hayo wanamaliza na pointi sita, baada ya kuifunga na Asante Kotoko ya Ghana 5-0, timu ambayo ilifungwa 4-2 na Simba.

BOCCO AONGEZWA TAIFA STARS KUIVAA THE CRANES JUMAMOSI

Image
MSHAMBULIAJI wa mkongwe wa Simba SC, John Raphael Bocco ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kuelekea mchezo wa marudiano na Uganda kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Jumamosi Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe. Uteuzi huo umefanywa na makocha wapya wa muda, Mzambia Hanoor Janza na Msaidizi wake, Mecky Mexime na kocha wa makipa, Juma Kaseja siku mbili tu tangu wapewe jukumu hilo. Ikumbukwe juzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimuondoa kazini kocha Mdenmark, Kim Poulsen na wasaidizi wake kufuatia Taifa Stars kuchapwa 1-0 na Uganda katika mechi ya kwanza ya hatua hiyo ya mwisho ya mchujo wa kuwania  tiketi ya CHAN Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mshindi wa  jumla atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.

AZAM FC 3-0 ARTA SOLAR (MECHI YA KIRAFIKI)

Image
 

DUBE, EDINHO NA MBOMBO WAFUNGA AZAM YAWAPIGA WADJIBOUTI 3-0

Image
WENYEJI, Azam FC jana waliichapa Arta Solar ya Djibouti mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo Muivory Coast, Tape Edinho dakika ya pili na washambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube dakika ya 62 na Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 83.

USHINDI DABO DABO NA PARIMATCH

Image
KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha  Parimatch  mara baada ya kumaliza kufanya uzinduzi mkubwa wa kuidhamini Klabu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara katika siku chache zilizopita, sasa imewageukia wateja wao kwa kuwamwagia fursa kemkem za kujipatia mamilioni ya pesa kiulani wakati wakiwa  wanasajili akaunti  zao mpya za ubashiri wa michezo. Hayo yamebainishwa na Afisa Habari na Mawasiliano ya Umma wa Parimatch Tanzania, Ismail Mohamed wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa ofa hiyo ni halali tu kwa wale wateja watakaoweka pesa kwa mara ya kwanza katika akaunti zao, bofya hapa kujipatia  ofa yako “ Ofa hii  inapatikana kwa wateja wapya pekee wa Parimatch na inaweza kutumika wakati wowote baada ya tarehe ta usajili, katika bonasi hii mteja anahitajika kuweka pesa katika akaunti  yake  na kiasi cha juu cha bonasi ni Milioni 1 kwa upande wa Sports na Kasino Milioni 3 na Laki 5 za kitanzania”,   alisema Ismail Mohamed.  

SIMBA SC 4-2 ASANTE KOTOKO (MECHI YA KIRAFIKI SUDAN)

Image
 

TANZANIA 0-1 UGANDA (KUFUZU CHAN)

Image
 

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA MRISHO NGASSA

Image
 

REFA WA YANGA NA COASTAL ARUSHA AFUNGIWA

Image
REFA Raphael Ikambi wa Morogoro ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mizinguko mitatu kufuatia kushindwa kutafsiri kanuni kwenye kati ya Coastal Union na Yanga Agosti 21, Uwanja wa Sheikh Amri Abied Jijini Arusha. 

TWIGA STARS WAENDA AFRIKA KUSINI KUTETEA KOMBE LA COSAFA

Image
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kimeondoka leo kuelekea Afrika Kusini kwenye mashindano ya COSAFA, wao wakiwa ni mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kulitwaa 2021.

TFF YAMFUTA KAZI KIM POULSEN TAIFA STARS

Image
SHIRIKISHO la Soka la Tanzania (TFF) limemuondoa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen kufuatia matokeo mabaya. Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Taifa Stars kuchapwa 1-0 na Uganda katika mechi ya kwanza Hatua ya mwisho ya mchujo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la The Cranes lililoizamisha Taifa Stars jana lilifungwa na Travis Mutyaba dakika ya 87 na sasa timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31. Sasa kikosi kitakuwa chini ya kocha wa Namungo FC, Mzambia Hanoor Janza ambaye atasaidiwa na mzawa, Mecky Mexime huku Juma Kaseja akiwa kocha wa makipa.

AZAM FC YAWAONDOA MAKOCHA WASOMALI WOTE WAWILI

Image
KLABU ya Azam FC imeondoa kazi makocha wake wawili, Wamarakani wenye asili ya Somalia, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser. Taarifa ya Azam FC imesema; “Tumefikia makubaliano ya pande mbili na kocha wetu, Abdihamid Moallin, na msaidizi wake, Omary Nasser, kuachia ngazi kama kocha mkuu na msaidizi mtawalia. Hata hivyo, Azam imesema makocha hao wataendelea kubaki kama sehemu ya idara ya ufundi klabuni kwetu katika nafasi nyingine ambazo tutazitangaza hapo baadaye. Sasa Azam FC inabaki chini ya makocha Waspaniola, Dani Cadena kocha wa makipa, Mikel Guillen kocha wa Fiziki  na mtaalamu wa tiba za wanamichezo (physio), Mreno Joao Rodrigues.

SIMBA SC YAITANDIKA ASANTE KOTOKO 4-2 SUDAN

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Al Hilal mjini Khartoum nchini Sudan. Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Mghana Augustine Okrah dakika ya 19, Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 26 na Mzambia Clatous Chama mawili, moja kwa penalti dakika ya 42 na lingine dakika ya 55, wakati ya Kotoko yamefungwa na Steven Mukwala dakika ya tisa na Stephen Amankona dakika ya 79 kwa penalti. Simba itashuka tena dimbani Jumatano kumenyana na wenyeji, Al Hila kabla ya kurejea nyumbani kwa ajili ya mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya AS Arta Solar ya Djibouti Septemba 3.

TAIFA STARS MGUU NJE CHAN, YACHAPWA 1-0 NA UGANDA DAR

Image
TANZANIA imejiweka kwenye nafasi ngumu ya kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya kuchapwa 1-0 na Uganda jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Bao pekee la The Cranes lililoizamisha Taifa Stars leo limefungwa na Travis Mutyaba dakika ya 87 na sasa timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.

RAIS SAMIA AIPONGEZA SIMBA QUEENS KUTWAA UBINGWA CECAFA

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Simba Queens kwa kutwaa taji la Klabu ya Wanawake Afrika Mashariki na Kati jana. "Nawapongeza wanangu Simba Qeens SC kwa ubingwa wa Afrika Mashariki wa CECAFA 2022 kwa Wanawake (SAMIA CUP). “Mmejenga heshima kwa soka la Tanzania na nchi kwa ujumla. Nawatakia kheri katika Ligi ya Mabingwa Afrika (2022 CAF Women's Champions League ) itakayofanyika nchini Morocco," amesema Rais Samia kupitia ukurasa wake wa Instagram. Simba ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya She Corporate ya Uganda jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Na sasa Simba Queens imejikatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika ya Wanawake Oktoba mwaka huu nchini Morocco.

SIMBA QUEENS MABINGWA WA CECAFA 2022

Image
TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya She Corporates ya Uganda usiku wa jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa kimataifa wa Kenya, Vivian Corazone Aquino Odhiambo dakika ya 49 kwa penalti baada ya Asha Djafar kuangushwa kwenye boksi na Simba Queen itauwakilisha ukanda wa CECAFA kwenye Ligi ya mabingwa ya wanawake Oktoba mwaka huu nchini Morocco. Pamoja na ushindi huo, Simba Queens pia wametoa kipa Bora wa mashindano, mzawa Gelwa Yona na Mchezaji Bora wa Mashindano, ambaye ni Vivian Corazone Aquino Odhiambo, huku Abela Roza wa Commercial Bank ya Ethiopia akiwa Mfungaji Bora.

HAALAND APIGA HAT-TRICK MAN CITY YAICHAPA CRYSTAL PALACE 4-2

Image
WENYEJI, Manchester City wametoka nyuma na kuichapa Crystal Palace mabao 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester. Pongezi kwa mshambuliaji mpya, Erling Haaland aliyefunga ambao matatu dakika za 62, 70 na 81 baada ya Bernardo Silva kufunga la kwanza dakika ya 53, kufuatia Eagles kutangulia kwa mabao ya John Stone aliyejifunga dakiia ya nne na eJoachim Andersen dakika ya 21.

LIVERPOOL YAIKANDAMIZA BOURNEMOUTH 9-0 ANFIELD

Image
WENYEJI, Liverpool wameibamiza AFC Bournemouth mabao 9-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield na kupoza machungu ya kichapo cha 2-1 kutoka kwa mahasimu, Manchester United. Ushindi huo mnono umeifanya Liverpool ifikie rekodi ya kushinda mabao mengi kwenye mechi moja katika Ligi Kuu ya England iliyowekwa na Man United dhidi ya Ipswich mwaka 1994, Southampton mwaka 2021 na Leicester City kwa hao hao The Saints mwaka uliotangulia. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino na Luis Diaz mawili kila mmoja, Trent Alexander-Arnold, Harvey Elliott, Virgil van Dijk, Christopher Mepham aliyejifunga na Fabio Carvalho.

STERLING APIGA MBILI CHELSEA PUNGUFU YASHINDA 2-1

Image
WENYEJI, Chelsea wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Pongezi kwa mfungaji wa mabao yote hayo, mchezaji mpya, Raheem Sterling dakika ya 47 akimalizia pasi ya Marc Cucurella na 63 akimalizia pasi ya Reece James. Katika mchezo huo, Chelsea ilicheza pungufu tangu dakika ya 28 baada ya kiungo wake Conor John Gallagher kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano. Bao la kufutia machozi la Leicester City limefungwa na Harvey Lewis Barnes dakika ya 66 akimalizia pasi ya mkongwe, Jamie Richard Vardy.

MAN UNITED YASHINDA TENA, YAICHAPA SOUTHAMPTON 1-0

Image
BAO pekee la Bruno Fernandes dakika ya 55, limeipa Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Southampton Uwanja wa St. Mary's, Southampton, Hampshir. Ni ushindi wa pili mfululizo kwa kocha mpya, Mholanzi Erik ten Hag katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya England, baada ya mwanzo mbaya wakipoteza mechi mbili mfulullizo.

SINGIDA BIG STARS YASHUSHA MCHEZAJI MUARGENTINA

Image
KLABU ya Singida Big Stars imejiimarisha kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa kusajili mchezaji mpya, Muargentina, Miguel Escobar.

SIMBA SC WAENDA SUDAN KUCHEZA NA KOTOKO NA HILAL

Image
KIKOSI cha Simba SC kimendoka Ijumaa Alfajiri ya leo kwenda Sudan kushiriki michuano maalum ya timu tatu, kwa mwaliko wa wenyeji, El Hilal. Wakiwa huko, Simba watamenyana na Asante Kotoko ya Ghana Jumapili kabla ya kumalizana na wenyeji, El Hial Jumatano ijayo, Agosti 31 kisha watarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Djibouti, AS Arta Solar.

ZANZIBAR HEROES YAICHAPA THE CRANES 1-0 AMAAN

Image
BAO pekee la Ibrahim Mkoko limeipa Zanzibar Heroes ushindi wa 1-0 dhidi ya Uganda, The Cranes katika mchezo wa kirafiki usiku wa Jumatano Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mkoko alifunga bao hilo dakika ya 76 akimalizia pasi ya Abdulnasir Hassan Amal kutoka upande wa kulia. Uganda iliutumia mchezo huo kujiandaa na mechi dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kufuzu Fainali za CHAN Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi wa jumla atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.

SIMBA QUEENS YATINGA FAINALI, KUKUTANA NA WAGANDA JUMAMOSI

Image
TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kwenda Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake baada ya ushindi wa 5-1 dhidi ya AS Kigali ya Rwanda usiku wa Jumatano Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Vivian Aquino Corazone dakika ya 14, Opa Clement Tukumbuke dakika ya 30, Aisha Juma Mnunka dakika ya 38 na Diana William Mnally dakika ya 84, wakati la AS Kigali limefungwa na Mukeshimana Dorothee dakika ya 28. Fainali ni Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Na Simba Queens itakutana na She Corporate ya Uganda ambayo imeitoa Commercial Bank ya Ethiopia kwa kuichapa 2-1 pia Jumatano jioni. Simba Queens na She Corporate ni marudio ya mchezo baina yao wa Kundi B ambao Malkia hao wa Msimbazi waliibuka na ushindi wa 2-0.

GEIT GOLD YAWASAJILI NTIBANZOKIZA NA LUIZIO

Image
  KLABU ya Geita Gold imejiimarisha kwa kusajili wachezaji wawili wazoefu, kiungo Mrundi Saido Ntabanzokiza na mshambuliaji mzawa, Juma Luizio. Ntibanzokiza anajiunga na Geita Gold baada ya misimu miwili ya kuichezea Yanga, wakati Luizio anatokea Mbeya City.

YANGA WAHAMASISHA WATU KUSHIRIKI SENSA KESHO

Image
WACHEZAJI wa Yanga wakiwa na bango la kuhamasisha Watanzania kushiriki zoezi la kuhesabiwa, Sensa kesho nchini kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union Jumamosi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha ambao walishinda 2-0.

AZAM FC KUCHEZA NA TIMU YA KALOU, SONG CHAMAZI

Image
TIMU ya Azam FC itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Djibout, AS Arta Solar 7 Agosti 30 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Arta Solar imesajili nyota wa zamani waliowika kwenye Ligi Kuu England, Mcameroon Alex Song aliyewika Arsenal na Muivory Coast, Solomon Kalou aliyetamba Chelsea.

SIMBA KUCHEZA NA ASANTE KOTOKO NA EL HILAL

Image
KLABU ya Simba itacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana, El Hial ya Sudan na AS Arta Solar ya Djibouti kujiweka sawa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

MAN UNITED YAIPIGA LIVERPOOL 2-1 OLD TRAFFORD

Image
WENYEJI, Manchester United wamepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya England msimu huu baada ya kuichapa Liverpool mabao 2-1 Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester. Mabao ya Manchester United yamefungwa na Jadon Sancho dakika ya 16 akimalizia pasi ya Malacia na Marcus Rashford dakika ya 53 akimalizia pasi nzuri ya Anthony Martial. Nyota wa Misri, Mohamed Salah akaifungia bao la kufutia machozi dakika ya 82 akimalizia mpira uliookolewa na kipa David De Gea kufuatia pigo la Carvalho. Mechi mbili za mwanzo za United chini ya kocha mpya, Eric ten Hag ilifungwa 2-1 na Brighton & Hove Albion hapo hapo Old Trafford Agosti 7 na 4-0 na Brentford ugenini Agosti 13, wakati Liverpool ilitoa sare zote, 2-2 na Fulham ugenini Agosti 6 na 1-1 na Crystal Palace nyumbani.

KINDA WA AZAM, TEPSIE EVANS AONGEZWA TAIFA STARS

Image
KOCHA Mdenmark, Kim Poulsen amemuongeza kiungo Tepsi Evans wa Azam FC kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mchezo wa kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Uganda Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Timu hizo zitarudiana Septemba 3 Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe na mshindi atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.

AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA GEITA GOLD CHAMAZI

Image
WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Azam FC ilitangulia kwa bao la chipukizi wake mwenye kipaji, Tepsie Evans dakika ya 41, kabla ya beki Adeyoum Ahmed kuisawazishia Geita Gold dakika ya 54. Ni sare ya kwanza kwa timu zote katika mechi mbili za mwanzo za msimu kufuatia Azam FC kushinda 2-1 dhidi ya Kagera Sugar hapo hapo Chamazi na Geita Gold kufungwa 3-0 na Simba Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

COASTAL UNION 0-2 YANGA SC (LIGI KUU TZ BARA)

Image
 

USYK AMSNHINDA TENA JOSHUA KWA POINTI

Image
BONDIA Oleksandr Usyk amefanikiwa kutetea mataji yake ya  WBA, IBO, WBO na IBF uzito wa juu baada ya kumshinda tena kwa pointi, Muingereza Anthony Joshua usiku wa jana mjini Jeddah, Saudi Arabia. Majaji wawili walimpa ushindi Usky, Ukraine alimpa pointi 116-112, Muingereza akampa 115-113 huku Mmarekani akimpa ushindi Joshua wa pointi 115-113. Baada ya pambano, Joshua alipiga goti kumpongeza Usky, ingawa baadaye alimwaga machozi alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari. Baada ya ushindi huo, Usyk mwenye umri wa miaka, 35 alisema anataka kuongeza taji la WBC analoshikilia Muingereza mwingine, Tyson Fury zaidi ya hapo hatapigana tena akifikisha rekodi ya kushinda mapambano yake yote 20, kati ya hayo 13 kwa Knockout (KO). Hili ni pambano la tatu Joshua mwenye umri wa miaka 32 anapoteza, mawili akipigwa na Usyk pamoja na lile la Septemba 25 mwaka jana na moja na Mmexico Andy Ruiz Desemba 7, mwaka 2019 pambano pekee alilopigwa KO, raundi ya saba ukumbi wa Madison Square Garden, New

DEJAN APIGA LA PILI SIMBA YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0

Image
VIGOGO, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Kagera Sugar ya Bukoba mabao 2-0 usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa washambuliaji wake wapya, Mzambia Moses Phiri dakika ya 42 na Mserbia Dejan Geirgejevic dakika ya 81. Ni ushindi wa pili kwa Simba SC baada ya awali kuichapa Geita Gold 3-0 na kipigo cha pili kwa Kagera Sugar kufuatia kufungwa 2-1 na Azam kwenye mechi za kwanza zote zikichezwa Dar es Salaam. Mzambia, Moses Phiri leo amefunga bao lake la pili baada ya kufunga pia kwenye mechi na Geita Gold, wakati Dejan ndio anafungua akaunti yake ya mabao Tanzania.

SIMBA QUEENS YATINGA NUSU FAINALI KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI

Image
TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Wanawake Afrika Mashariki na Kati baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Yei Joint Stars ya Sudan Kusini katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Vivian Aquino Corazone dakika ya 15, Philemena Abakah mawili, dakika ya 22 na 63 na Opa Clement dakika ya 32. Simba inakamilisha pointi tisa baada ya kushinda mechi zake zote za Kundi B, 6-0 dhidi ya Garde Republicane ya Djibouti na 2-0 dhidi ya She Corporates ya Uganda na kutinga Nusu Fainali kama kinara wa Kundi.

YANGA YAENDELEZA UBABE LIGI KUU, YAICHAPA COASTAL 2-0 ARUSHA

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wameendeleza mwanzo mzuri katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Mabao ya Yanga yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison dakika ya nne na mtokea benchi, mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele dakika ya 68. Ni ushindi wa pili kwa Yanga baada ya kuichapa Polisi Tanzania 2-1 na kipigo cha kwanza kwa Coastal Union kufuatia kushinda 1-0 dhidi ya KMC kwenye mechi za kwanza hapo hapo Sheikh Amri Abeid.

TFF YAWAPA POLE YANGA KWA MSIBA WA SHABIKI WAO

Image
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa pole kwa klabu ya Yanga kufuatia kifo cha shabiki wake mmoja kwenye ajali ya gari akiwa safarini na wenzake kwenda Arusha kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union.

PRISONS YAZINDUKA NA KUICHAPA DODOMA JIJI 2-1 LITI

Image
TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa LITI, zamani Namfua mjini Singida. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Ismail Mgunda dakika ya pili kwa penalti na Jeremiah Juma dakika ya sita, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 18. Ni ushindi wa kwanza kwa Prisons baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Singida Big Stars kwenye mechi ya kwanza, wakati kwa Dodoma Jiji ni kipigo cha pili baada ya kuchapwa 3-1 na Mbeya City hapo hapo LITI.

AZAM FC YASHUSHA PHYSIO MPYA KUTOKA URENO

Image
MTAALAMU wa tiba za wanamichezo, Joao Rodrigues amewasili usiku wa kuamkia leo kutoka kwao, Ureno kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Azam FC. Rodrigues ni physiotherapist wa viwango vya juu kwenye tiba za wachezaji, akiwahi kufanya kazi na mabingwa wa Ureno, FC Porto. Mkurugenzi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa, kabla ya kuanza msimu huu aliahidi atawapa furaha mashabiki wa timu hiyo kwa kuleta wachezaji wa hali ya juu, kocha wa viungo, kocha wa makipa na sasa amemaliza kwa kushusha 'physio' wa viwango.

SHABIKI WA YANGA AFARIKI AJALINI AKIENDA ARUSHA KWENYE MECHI

Image
UONGOZI wa Yanga umetoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha shabiki wake ajalini jana akiwa safarini kuelekea Arusha kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya timu hiyo na Coastal Union leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

NAMUNGO FC YAICHAPA IHEFU 1-0 UHURU BAO LA LUSAJO

Image
BAO pekee la mshambuliaji Relliant Lusajo dakika ya 45 limeipa Namungo FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Ni ushindi wa kwanza kwa Namungo baada ya sare ya 2-2 na Mtibwa Sugar kwenye mechi ya kwanza na kipigo cha pili kwa Ihefu iliyorejea Ligi Kuu msimu huu baada ya kuchapwa 1-0 na Ruvu Shooting kwenye mechi ya kwanza.

YANGA YAINGIA MKATABA WA MASOKO NA JACKSON GROUP LTD

Image
RAIS wa Yanga SC, Mhandisi Hersi Said na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jackson Group Limited, Kelvin Twisa baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano kwenye Idara ya Masoko kwa miaka miwili leo Jijini Dar es Salaam. Katika mkataba huo, Jackson Group itakuwa na jukumu la kuitafutia Yanga wadau na makampuni ya kuwekeza kwenye klabu hiyo kongwe nchini.