KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amekutana na Marais wa Mashirikisho ya Mpira wa Miguu ya nchi wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambapo amewaomba kuiunga mkono Tanzania, Kenya na Uganda ambazo zinaomba kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) 2027. Marais walioshiriki kikao hicho ni Wales Karia, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambaye ni Rais wa CECAFA sasa, Augustino Maduot, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Sudan Kusini, Paulos Andromariam, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Eritrea, Isayas Jiral, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ethiopia, Doris Petra Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya pamoja na watendaji wakuu wa CECAFA Bw. Mossi Yusuf Meneja wa Mashindano CECAFA na Auka Gocheo Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA. Kikao hicho kimefanyika kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Tanzania na Burundi ambayo imechezwa Julai 25, 2023 k