Posts

Showing posts from February, 2025

KOCHA MPYA YANGA AMEFUNDISHA UFARANSA, KUWAIT, SAUDI ARABIA, MOROCCO NA KLABU KUBWA ALGERIA

Image
KOCHA mpya wa Yanga, Miloud Hamdi (53), Mualgeria mwenye uraia wa Ufaransa ana uzoefu wa kufundisha soka tangu mwaka 2004 alipoanza na timu ya vijana nchini Ufaransa, ES Vitrolles, kabla ya kuhamia GS Consolat mwaka 2009 hadi 2012 . Baada ya hapo akaenda Ettifaq U21 ya Saudi Arabia hadi mwaka 2015 USM Alger akaajiriwa kama Kocha Msaidizi wa USM Alger ya Algeria, kabla ya kupewa Ukocha Mkuu mwaka 2016. Baadaye mwaka 2016 akaenda Nahdat Berkane ya Morocco, kabla ya kurejea USM Alger mwaka 2017 hadi 2018 akaenda Al-Salmiya SC ya  Kuwaiti, kabla ya kurejea Algeria mwaka 2021 kufundisha CS Constantine hadi 2022 alipohamia JS Kabylie hadi mwaka jana. Anajiunga na Wananchi kuchukua nafasi ya Siad Ramovic mwenye uraia wa Ujerumani aliyeondoka ghafla jana.

YANGA SC YAACHANA NA RAMOVIC, YALETA KOCHA WA USM ALGER

Image
KLABU ya Yanga imeachana na kocha Siad Ramovic mwenye uraia wa Ujerumani na kumtambulisha, Miloud Hamdi, Mualgeria mwenye uraia wa Ufaransa pia kuwa Kocha wake Mkuu ambaye anaungana na timu mara moja.

MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA ABEID KASABALALA ALIYETAMBA MECCO NA RELI

Image
 

TABORA UNITED 0-3 SIMBA SC (LIGI KUU YA NBCA TZ BARA)

Image
 

ATEBA APIGA MBILI SIMBA SC YAITANDIKA TABORA UNITED 3-0

Image
TIMU ya Simba SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Chachu ya ushindi wa leo ni winga Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala aliyesaidia upatikanaji wa mabao yote, mawili yakifungwa na mshambuliaji Mcameroon, Leonel Christian Ateba Mbida na lingine beki, Shomari Salum Kapombe. Bao la kwanza Ateba alipokea pasi ya Mpanzu na kufunga dakika ya 12 na la pili akafunga kwa penalti dakika ya 34 kufuatia Mkongo huyo kuangushwa na beki Mkongo-Brazzaville, Faria Jobel Ondongo.  Bao la tatu Ateba alipokea pasi ya Mpanzu tena akiwa kwenye nafasi ya kufunga, lakini akamsetia Kapombe aliyekuwa anatokea nyuma  na kufumua shuti lililotinga nyavuni. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 43 na kurejea kileleni ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 16. Tabora United kwa upande wao wan...

YANGA SC 4-0 KAGERA SUGAR (LIGI KUU YA NBZ TZ BARA)

Image
 

YANGA SC YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA KAGERA SUGAR 4-0

Image
MABINGWA watetezi, Yanga SC wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na nyota wazawa, mshambuliaji Clement Francis Mzize dakika ya 32, kiungo Mudathir Yahya Abbas dakika ya 60, kiungo Muivory Coast, Pacome Zouzoua Peodoh kwa penalti dakika ya 78 na mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda dakika ya 86. Yanga ingeweza kuondoka na ushindi wa mabao 5-0 leo kama kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 16 na kupanda juu ya msimamo, ikiizidi pointi mbili Simba ambayo pia ina mechi moja mkononi na kesho inacheza na Tabora United mjini Tabora. Kwa upande wao Kagera Sugar baada ya kipigo cha leo 11 za mechi 16 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 — mbele ya Ken Gold yenye pointi sita za mechi 16 pia.