Posts

Showing posts from December, 2018

VIDEO: ILE ISHU YA YANGA KUTAJWA INA MATATIZO YA PESA, MSIKILIZE ZAHERA AKIFUNGUKA

Image
KOCHA wa Yanhga Mwinyi Zahera amesema kuwa Kikosi chake cha Yanga kimefanya vizuri katika mzunguko wa kwanza kwa kumaliza ikiwa imecheza mechi 18 na wakiwa pointi 50 jambo ambalo limewafanya kuaminiwa na mashabiki pamoja na wanachama wa Yanga. Zahera amesema kuwa moja ya vitu ambavyo vinampa nguvu kuendelea kufanya kazi na viongozi wa Yanga ni waelewa hivyo kutoelewana ni mambo madogo madogo ambayo yanatokea na kumalizwa.

VIDEO: BABA YAKE NA OFISA HABARI SIMBA ATOA MUSTAKABALI WA KIKAO CHA WACHEZAJI YANGA NA ZAHERA

Image
Baba Mzazi wa Msemaji wa Simba Sunday Manara ametoa mustakabali wa kikao walichokutana na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambacho kiliwakutanisha wachezaji wa zamani wa Yanga pamoja na kocha Zahara.

VIDEO: KOCHA YANGA ATOA TAMKO RASMI JUU YA KAKOLANYA KUREJEA KIKOSINI

Image
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ametoa tathmini ya kikao walichokutana pamoja na wachezaji wa zamani wa Yanga ikiwa ni pamoja na sula la Beno Kakolanya ambalo wachezaji hao wa zamani walipanga kumwambia kocha huyo lakini kocha amekana. Kocha Zahera amesema amekutana na wachezaji hao lakini hawajagusia suala la Beno lakini kama yeye ataangalia kwa uapnde wake kama amsamehe Kakolanya au amuache aendelee na mambo yake.

VIDEO - DISMAS TEN "TULIAZIMISHA UBINGWA, TUMEZALIWA KUSHINDA

Image
Msemaji wa Klabu ya Yanga Dismas Ten amesema kuwa wanawashukuru mashabiki wa timu ya Yanga kutokana na hamasa yao waliyoitoa hasa Mikoani ambapo mashabiki wameonyesha moyo kwa kujaza viwanja mkoani. Ten amesema kuwa wanachama na mashabiki wa Yanga wamekuwa wakitoa michango kwa hali na mali ili timu endelee kufanya vizuri huku uongozi wa ukitambua uwepo wao.

NAMNA YANGA ILIVYOWAZIDI MAARIFA SIMBA, LIGI KUU

Image
MABINGWA mara 27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, wameufunga mwaka 2018 kibabe kutokana na kuweka rekodi ya kipekee msimu huu licha ya kupitia katika kipindi kigumu cha uchumi huku kila mchezaji akicheza kwa ushujaa kutafuta matokeo uwanjani. Yanga mpaka sasa wana pointi 50 baada ya kucheza michezo 18 na kushinda 16, wakitoa sare michezo miwili, huku wakiwa bado hawajapoteza hata mechi moja. Rekodi zinaonyesha kwamba, Yanga wanafunga mwaka wakiwa ni vinara katika kila idara kwa kuwa wana mabao ya kufunga 35 na kinara wa kupachika mabao ni mshambuliaji wao, Heritier Makambo mwenye mabao 11, akiwaacha mbali washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wenye mabao saba. Wanaofuatia ni Eliud Ambokile wa Mbeya City na Said Dilunga wenye mabao tisa. Katika mabao hayo 35, wafungaji ni mabeki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (2), Kelvin Yondani (1) na Andrew Vincent ‘Dante’ (1).  Viungo ni Feisal Salum ‘Fei Toto’ (2), Rafael Daud (2), Jaffary Mohamed (1), Deus Kaseke (1) na Mrisho Ngass

HII HAPA REKODI YA MAKAMBO INAYOWATESA SIMBA

Image
MAMBO ni moto! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya mshambuliaji wa Yanga, raia wa DR Congo, Heritier Makambo, kuandika rekodi ya pekee hivi karibuni katika michuano ya Ligi Kuu Bara ambayo ilimshinda mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi msimu uliopita. Rekodi hiyo si nyingine bali ni ile ya kupachika mabao mengi katika mechi za mikoani ambazo Yanga imecheza mpaka sasa dhidi ya Mwadui FC, Kagera Sugar, Prisons, African Lyon pamoja na Mbeya City. Katika mechi hizo, Yanga imefanikiwa kushinda zote huku ikijipatia mabao 10 ya kufunga lakini pia ikifungwa manne. Katika mechi dhidi ya Mwadui FC ilishinda 2-1, ikaichapa Kagera Sugar 2-1, ikaifunga Prisons 3-1, kisha ikaichapa 1-0 Afican Lyon na juzi Jumamosi kifanya tena hivyo dhidi ya Mbeya City kwa kuifunga mabao 2-1. Katika mabao hayo 10 ambayo Yanga imefunga mikoani, manne kati ya hayo yamefungwa na Makambo na kufanikiwa kuandika rekodi ya pekee ambayo msimu uliopita licha ya Okwi kuibuka mfungaji bora wa Ligi

SIMBA SC YAPELEKA KIKOSI KAMILI MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KLABU bingwa ya soka Tanzania Bara, Simba SC itaondoka Jumatano ya Januari 2, mwakani kwenda Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, ikiwa na kikosi chake kamili. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amewaambia Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba watakwenda na kikosi kamili ili kufanya vizuri kwenye mashindano hayo. Manara, mtoto wa mchezaji nyota wa zamani wa Yanga, Sunday Manara ‘Computer’ amesema pamoja na dhamira ya kufanya vizuri, lakini pia wanataka kutumia michuano hiyo kuipa mazoezi timu yao ambayo inajiaanda na mechi yake ya kwanza ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria. Amesema kwamba mechi dhidi ya timu hiyo mpya ya mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu itapigwa Jumamosi ya Januari 12, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kuanzia Saa 10:00 jioni. Manara amesema kwamba kikosi cha kwanza kitarejea Dar es Salaam mapema hata Simba ikifuzu ku

YANGA SC YAAMUA KUWEKEZA NGUVU ZAIDI KWENYE LIGI KUU YA NA KOMBE LA TFF

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KLABU ya Yanga SC ya Dar es Salaam imesema kwamba haitapeleka kikosi chake kamili kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, ili kuwapa mapumziko baadhi ya wachezaji wake. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kwamba wanalazimika kuwapumzisha baadhi ya wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC). Zahera, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), amesema kwamba, Yanga kama klabu inatakiwa kuweka malengo kwenye vitu vyenye manufaa kwake, kwani wakiamua kutaka mataji yote wanaweza kujikuta wanakosa yote. Kocha wa Yanga SC, Mwinyi Zahera (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo    “Kufuatana na nguvu yetu tulionayo (wachezaji) inatubidi tuangalie wapi tutapata faida, tupo na Ligi Kuu, tupo na Azam Federation Cup, Mapinduzi Cup na Sport Pesa, inabidi

PRISONS WATAFUTA MBINU KUREJEA KWENYE UBORA

Image
REKODI ya kikosi cha Tanzania Prisons msimu huu inawaumiza mashabiki na viongozi kutokana na kushindwa kufurukuta kwa michezo ambayo wamecheza Ligi Kuu. Prisons walimaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya nne huku Kocha wao Mkuu, Mohamed Abdallah akipewa tuzo ya Kocha Bora wa msimu uliopita. Kwa sasa Prisons wamecheza michezo 18 wameshinda mchezo mmoja pekee na kutoa sare michezo 9, wamepoteza michezo 8 na kujikusanyia pointi 12 wakiwa nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi hali iliyofanya wamtimue kazi kocha wao.  Beki wa kikosi hicho Salum Kimenya amesema kuwa wanatambua kazi kubwa waliyonayo katika kupata matokeo hivyo wataongeza juhudi kuweza kujinasua katika nafasi waliyopo kwa sasa. "Hatupo sehemu nzuri, tuna kazi kubwa kutoka hapa tulipo na njia ni moja tu kupata matokeo mazuri katika michezo yetu mashabiki watupe sapoti," alisema.

SINGIDA UNITED KUMALIZA HASIRA ZAO KWA KIKOSI HIKI LIGI KUU

Image
Baada ya kukubali kupoteza mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 3-0 Uwanja wa Taifa, Singida United wameanza kujipanga kufuta machozi kwa Coastal Union. Mchezo wa Singida United na Coastal Union ya Tanga unatarajiwa kuchezwa Januari 2 katika uwanja wa Namfua, Singinda. Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema wametambua makosa yao na wamepokea matokeo kinachofuata ni maumivu kwa wapinzani wao Coastal Union. "Tumepoteza mchezo wetu hilo tunaachana nalo na kuwekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Coastal Union ambao tutakuwa nyumbani, ni muda wetu kutumia vizuri Uwanja wa nyumbani kupata matokeo chanya," alisema. Singida United wana pointi 19 wakiwa wamecheza michezo 17 wanashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.  

SIMBA HUKU MLIPOFIKIA, NI VITENDO ZAIDI BADALA YA MANENO

Image
Na Saleh Ally KAMA tungesikiliza maneno, basi Simba isingepiga hatua na kufikia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Hii si hatua ndogo hata kidogo kwa klabu za Afrika.   Kuna klabu nyingi kubwa ambazo haujaziona katika hatua hii, angalia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Al Hilal (Sudan), Zamalek (Misri), CS Sfaxien (Tunisia), Asante Kotoko (Ghana), Enugu Rangers (Nigeria) na nyingine nyingi ambazo pia zina utajiri mkubwa lakini zimeshindwa kufikia hatua hii. Tukitaka kuwa waungwana, kwanza ni kuwapongeza Simba kufikia hatua hii ngumu ambayo itakuwa changamoto na itazaa mafundisho mengi katika soka nchini. Pamoja na hivyo, tukitaka kuwa waungwana zaidi, kinachotakiwa ni kuwaambia Simba ukweli na si kuangalia ushabiki. Inawezekana wako wanaopenda ushabiki tunaweza kuwaachia nafasi ya kile wanachokifurahia na sisi tukaangalia njia nyingine sahihi kama wataalamu au wanataaluma ambao tungependa Simba ifanye vizuri zaidi. Makundi manne ya Ligi ya Mabingwa Afrika yam

WASHAMBULIAJI HAWA NA REKODI ZAO ZA MWAKA KOMBE LA FA

Image
WASHAMBULIAJI watatu wanafanikiwa kufunga mwaka wakiwa na mabao matatu 'hat trick' katika kombe la FA, Eliud Ambokile anafanikiwa kufunga mwaka 2019 akiwa na zawadi yake ya mpira ambao aliupata baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Mgambo Shooting katika Uwanja wa Sokoine. Katika mchezo huo wa FA, Mbeya City walishinda kwa mabao 4-0 huku mfungaji akiwa ni Ambokile ambaye kwa sasa anaongoza kwenye orodha ya wafungaji FA. Hat trick nyingine iliyoshuhudiwa msimu huu wa FA ni ile ya Seif Karihe, aliyefunga dhidi ya Laela FC katika mchezo ambao Lipuli waliibuka na ushindi wa mabao 9-0 Uwanja wa Samora. Amiss Tambwe wa Yanga alifunga 'hat trick' katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa dhidi ya Tukuyu Stars ambao waliibuka na ushindi wa mabao 4-0. Hatua ya tatu ya kombe la FA imekuwa na ushindani msimu huu ambapo timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu zimetolewa katika hatua hiyo, gumzo kubwa mwaka huu limekuwa ni kwa Simba ambayo ilito

JKT QUEENS WALITAKA KOMBE HILI LIGI YA WANAWAKE, WAANZA KWA MKWARA MZITO

Image
MABINGWA watetezi wa Ligi ya wanawake Tanzania maarufu kama 'Serengeti Lite Women's Premier League' JKT Queens wamepania kufanikiwa kulitetea kombe lao msimu huu baada ya kuanza kwa ushindi wa mabao 9-0 dhidi ya Evergreen Queens. Mchezo huo uliokuwa na msimsimko kwa kuwa ulikuwa ni wa ufunguzi ulifanyika katika uwanja wa Karume, ulikuwa ni wa ushindani mkubwa kwa kila timu kupania kupata pointi tatu muhimu. Mabao ya JKT Queen yalifungwa na Fatuma Mustapha aliyefunga mabao 5, Stumai Abdallah aliyefunga mabao 2 na Asha Rashid alifunga mabao 2 na kukamilisha jumla ya mabao 9. Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Cliford Ndimbo amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia msisimko wa ligi hiyo yenye ushindani mkubwa. "Ushindani ni mkubwa na tunahitaji mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa hamasa wanawake hali itakayosaidia kuweza kuwapa hamasa zaidi wachezaji wakiwa uwanjani," alisema Ndimbo. Kutoka Championi

HIVI UMEWAHI KUJIULIZA HASA KILE ANACHOKITAKA ZAHERA YANGA!

Image
TAARIFA

HIVI UMEWAHI KUJIULIZA HASA KILE ANACHOKITAKA ZAHERA YANGA!

Image
NA SALEH ALLY UNAPOITAJA Klabu ya Yanga kuhusiana na wafanyakazi wake wa kigeni, Wakongo watatu ni gumzo na kila mmoja ana la kwake ambalo halifanani na mwenzake. Mmoja ni Klaus Kindoki ambaye ni kipa namba tatu wa Yanga kwa sasa. Mgeni ambaye ni kipa namba tatu, jambo halijawahi kutokea katika nchi yoyote. Kindoki amekuwa gumzo kubwa sana kutokana na hilo, lakini bado benchi la ufundi limeendelea kumuamini, jambo ambalo binafsi napingana nao. Yanga haiwezi kusajili kipa wa kimataifa aje akuze kiwango wakati akilipwa fedha nyingi kuliko wazawa ambao Yanga ina uwezo wa kuwalipa nafuu na kuwakuza. Wa tatu ni Heritier Makambo. Huyu jamaa ni mshambuliaji na sasa ameanza kuudhihirishia umma wa wapenda mpira kwamba yeye ni hatari sana tofauti na wengi walivyokuwa wakiamini kwamba hawezi. Makambo hana nyota ya karibu kuwavutia mashabiki. Huenda ni kwa kuwa si mtu mwenye mbwembwe sana. Lakini unapozungumzia kazi yake, ni bora na anaijua. Kutofunga kwa muda kwa mshambuliaji, inat

TFF YATOA SHUKRANI KWA SERIKALI, YATAJA MAFANIKIO HAYA

Image
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa shukrani kwa Serikali, wadau pamoja na wanafamilia ya Mpira wa miguu kwa ushirikiano walioonyesha kwa mwaka 2018 ikiwa ni muda mchache kuweza kufunga mwaka na kuingia mwaka 2019. Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo, amesema wanaaga mwaka 2018 kwa mafanikio makubwa na wanaukaribisha mwaka 2019 huku imani ikiwa ni kufikia malengo makubwa. "Tumechukua matajji mbalimbali 2018 ikiwa ni pamoja na lile la Ubingwa wa CECAFA na ubingwa wa COSAFA kwa kikosi cha miaka chini ya 17, Serengeti Boys, Timu ya wanawake ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Queens' ubingwa wa CECAFA, timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' ubingwa wa jumuiya ya Afrika Mashariki kwa wanawake. "Timu ya Azam FC ubingwa wa Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati 'Kagame' na klabu ya Simba imefanikiwa kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema.

UHONDO WA FA CUP SASA KWA KISWAHILI NDANI YA AZAM TV

Image
Kampuni ya Azam Media Group kupitia Azam TV, imetangaza kuwa itaonyesha matangazo ya mechi zote za michuano ya The Emirates FA Cup ya nchini England kwa Lugha ya Kiswahili. Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni hiyo kupata kibali cha kuonyesha michuano hiyo mikongwe na yenye historia kubwa nchini England. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, juzi Jumatatu, Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group, Tido Mhando, alisema: “Desemba 2018, tumefikisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Azam Media Group, hivyo tunafarijika kwa muda wote huo kuwa sehemu ya kuwapa burudani watazamaji wetu hususan wale wanaofuatilia soka. “Kupitia chaneli zetu zilizopo Azam TV, tunapenda kuwaambia kuwa tutaonyesha michuano ya The Emirates FA Cup ambayo ina takribani miaka 150 tangu kuanzishwa kwake, tunaamini watazamaji wetu wataendelea kufurahia kile ambacho tumekuwa tukiwapa. “Kikubwa ambacho naweza kuwaambia ni kwamba, matangazo haya yatawajia kwa Lugha ya Kiswahili tena yenye vikorombwez

KMC WAPANIA KUFUNGUA MWAKA 2019 KIBABE

Image
KIKOSI cha Halmashauri ya Kinodoni KMC kimepania kufungua mwaka kibabe kwa kubeba pointi tatu za mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon. KMC watakuwa Uwanjani kesho Uwanja wa KMC dhidi ya Lyon ikiwa ni mchezo wao wa kwanza kwa mwaka mpya 2019. Ofisa habari wa KMC, Anwari Binde amesema wanaendelea kujiweka sawa katika maandalizi ya mwisho ili kufungua mwaka kwa staili ya kipekee kutokana na timu zote kuhitaji kupata matokeo. "Tumejipanga vizuri kuchukua pointi tatu na tunatambua kwamba haitakuwa rahisi kubeba pointi tatu mbele ya wapinzani wetu ila hamna namna wachezaji watapambana kupata matokeo," alisema. KMC wanafunga mwaka wakiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 18 wana pointi 22, huku Lyon wanashika nafasi ya 18 wakiwa wamecheza michezo 18 na pointi 13.

YANGA YAMPA ULAJI MSHAMBULIAJI HUYU, ATUA CHINA KIBABE

Image
MSHAMBULIAJI wa Stand United, Alex Kitenge raia wa Burundi ambaye alijizolea umaarufu baada ya kuwafunga Yanga mabao matatu 'hat trick' na kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kumtungua mabao hayo kipa namba mbili Klaus Kindoki amepata dili nchini China. Kitenge ambaye amesema kwamba kwa sasa hana hesabu za kurejea bongo kuichezea Stand United mpaka watakapomkamilishia malipo yake, kwa sasa amepata fursa nchini China. "Nimepata timu nchini China, inaitwa Maccau Club ambayo nitakuwa huko kwa muda wa mwezi mmoja kwa majaribio nikitafuta nafasi ya kusajiliwa moja kwa moja. "Kuna wakala aliniona kupitia kanda ya video ambapo alinifuata na kunitafutia timu huko, hivyo nitafanya jitihada kupata nafasi ya kusajiliwa jumlajumla," alisema. Kwa hatua hiyo ni kama amepata ulaji kupitia timu ya Yanga kwa kuwa ni mchezo mmoja tu alionyesh uwezo wake na baada ya hapo hajafanikiwa kufunga hata bao moja katika michezo yake mingine Ligi Kuu Bara.

HAJI MANARA AWAPA TAHADHARI WACHEZAJI SIMBA 'UMMA UNAHITAJI FURAHA'

Image
Na Haji S Manara Wachezaji wetu wapendwa mtambue huu Umma unataka furaha tu, unawapenda na kuwathamini sana! Nendeni kwenye shindano hili kuthibitisha ukubwa wenu na b inafsi nna imani kubwa sana na nyie. Dharau na kejeli za baadhi ya watu mzimalize uwanjani. Kajengeni historia yenu ktk maisha ,tulikuwa wa kwanza na wa mwisho kuingia fainali ya CAF na sasa mnayo fursa ya kuifikia rekodi hiyo. Mimi nitajitahidi kutimiza wajibu wangu wa kuhamasisha na kujuza umma wa watanzania na nyie katimizeni wajibu kwa kuweka rekodi nyingine .

BIASHARA UNITED WAFUNGA MWAKA NA REKODI YAO, KUPELEKWA FIFA

Image
BIASHARA United ya Mara ambayo imepanda Ligi Kuu msimu huu inafunga mwaka kwa rekodi ya kipekee ikiwa nafasi ya 20 kwenye msimamo wa ligi Kuu Tanzania Bara. Biashara United wamekusanya pointi 10 kwenye michezo 17 waliyocheza huku wakishinda mchezo mmoja ugenini dhidi ya Singida United na wamepoteza michezo 9 na kutoa sare michezo 7 na kufanikiwa kufunga mabao 6. Matokeo hayo yaliwafanya viongozi wa Biashara United kumpiga chini kocha wao Thiery Hitimana raia wa Rwanda ambaye amepata kibarua timu ya Ligi Daraja la Kwanza Namungo. Hitimana ametishia kuipeleka Biashara United Shirikisho la Soka la Kimataifa 'Fifa" endapo hatalipwa stahiki zake pamoja na malimbikizo ya mshahara. "Tumefikia maamuzi ya kuvunja mkataba lakini sijalipwa stahiki zangu, nitapeleka barua yangu TFF wakishindwa kunisaidia kudai basi nitakwenda Fifa," alisema. Mwenyekiti wa timu hiyo Sulemani Mataso amesema watamlipa taratibu malimbikizo yake huku aliyekuwa kocha msaidizi Omary Madenge aki

KUELEKEA MAPINDUZI CUP, KOCHA YANGA AAMUA KUWAPUMZISHA WACHEZAJI WAKE

Image
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema watawapumzisha wachezaji baadhi ya wachezaji wake kutokana na kukabiliwa na mashindano mengi msimu huu. Zahera ameeleza kuwa kufuatana na uwepo wa mashindano hayo ni vema wakawapumzisha wachezaji kadhaa kwa ajili ya kuweka nguvu katika Ligi Kuu Bara. "Kufuatana na nguvu yetu tulionayo (wachezaji) inatubidi tuangalie wapi tutapata faida, tupo na ligi kuu, tupo na Azam federation cup , mapinduzi cup na Sport Pesa. "Inabidi sisi kama Yanga tuwe na malengo kwenye kitu chenye manufaa kwetu tukiamua kuyataka makombe yote tunaweza kosa yote ivyo lazima baadhi ya wachezaji wapumzike kwaajili ya ligi na ASFC", amesema Zahera.

KINGWENDU AWAPA NENO WANAOMZUSHIA KIFO

Image
Muigizaji maarufu wa vichekesho Bongo, Rashidi Mwinshehe ‘Kingwendu’ ameyatolea ufafanuzi madai ya kuwa ni mgonjwa wa kufa wakati wowote huku wengine wakizusha kuwa amekufa. Akizungumza na Showbiz, Kingwendu alisema yeye si mgonjwa kama watu wanavyomzushia kwani anaendelea vizuri na sanaa yake hasa ya muziki kwa sababu amekuwa akipiga shoo zake kama kawaida mikoani. “Unajua watu wanaonizushia habari za ugonjwa, mara oo… nimekufa ni wale ambao hawajaniona muda mrefu kwani nafanya kazi zangu binafsi na shoo mbalimbali za muziki huko mikoani, ingawa mimi sishtuki kwani wananitabiria umri mrefu,” alisema Kingwendu. Kingwendu alisema kuwa, ana miaka mingi hajaugua hata malaria na mpaka sasa anapiga shoo mkoani Mwanza katika kuufunga mwaka wa 2018. CHANZO: SHOWBIZ - GLOBAL PUBLISHERS

ALICHOKIANDIKA BEN POL BAADA YA KUKUTANA NA MCHOMA NYAMA MKUBWA DUNIANI

Image
Msanii wa Bongo Flava maarufu kama, ‘Ben Pol’ akutana na mchoma nyama mkubwa duniani  ‘Salt Bae’ alipokuwa Dubai katika matembezi ya sikukuu akila bata na mwanadada toka Kenya Aner Lisa. Kupitia akaunti yake ya instagram Ben Pol baada ya kukutana na mchoma nyama huyo aliweka video na picha huku zikiambatana jina, na maneno yaliyosomeka, ‘#SaltBae @nusr_et mwenyewe ..!” Salt Bae ndyo mchoma nyama anayefanya kazi ya kuwauzia na kuwachomea nyama mastaa wakubwa duniani akiwemo, P Diddy, French Montana, Cristian Ronaldo, Messi, Dj Khaled, David Bekham, Pogba na wengineo.

KAMATI YA RUFAA KUAMUA HATMA WAGOMBEA YANGA

Image
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Yanga, Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inatarajiwa kukutana Januari 4, kusikiliza rufaa za wagombea wawili kisha baada ya hapo kubandika majina rasmi ya wagombea. Wagombea wawili katika nafasi mbili tofauti wamekata rufaa kutokana na kuenguliwa ambao ni Yona Kevela ambaye alichukua fomu ya kugombea nafasi mbili tofauti, ya uenyekiti na makamu pamoja na Leonard Marango aliyekuwa akiwania nafasi ya ujumbe. Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliwaengua wagombea hao kutokana na kushindwa kutimiza vigezo wakati wa kipindi cha usajili. Akizungumza na Championi Jumatatu, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela, alisema baada ya kusikiliza rufaa hizo, majina yatawekwa hadharani. “Januari 4 tutakuwa tunasikiliza rufaa za wagombea wawili ambao walikata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa wa wao kuenguliwa, baada ya kila kitu kukamilika hapo basi ndiyo tutabandika rasmi majina ya wagombea. “Uchaguzi unatarajiwa kufanyika Januari 13 na b

TAMKO JINGINE LA ZAHERA KUHUSIANA NA WACHEZAJI YANGA HILI HAPA

Image
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kuwa kasi ya kikosi chake na matokeo wanayoyapata ni kutokana na namna ya hamasa ya hali ya juu anayowapa wachezaji wake kabla ya mechi, kuhakikisha kwamba wanapambana na kuipatia timu hiyo matokeo mazuri. Yanga wameendelea na wimbi lao la ushindi baada ya juzi Jumamosi kuwabutua Mbeya City kwa mabao 2-1 kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Baada ya ushindi huo, Yanga wamefikisha pointi 50 wakiwa vinara wa ligi hadi sasa wakiwa pointi 10 mbele ya wanaowafuatia Azam FC. Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera amesema kwamba matokeo wanayoyapata ni kutokana na hamasa kubwa ambayo anawapa kabla ya mechi na matokeo yake ndiyo yamekuwa yakizaa matunda na kupata ushindi. “Ninawaomba wachezaji wangu wawe na morali ya juu na wapambane kwa kila hali kuona kwamba tunapata ushindi kwenye kila mechi na ndiyo maana tunapata ushindi hadi sasa,” alisema Zahera

JOHN BOCCO AWATISHA WAARABU

Image
Nahodha wa Simba, John Bocco, ameweka wazi licha ya kupangwa na timu mbili kutoka mataifa ya Uarabuni katika Ligi ya Mabingwa Afrika, wamejipanga kuweka rekodi kuhakikisha wanawafunga kila watakapokutana nao na kusonga mbele katika hatua hiyo. Bocco ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliosaidia kikosi hicho kutinga hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika ambapo wamepangwa katika Kundi D. Kundi hilo lina timu za Al Ahly ya Misri, JS Saoura ya Algeria pamoja na AS Vita ya DR Congo huku mechi yao ya kwanza ya hatua hiyo wakitarajia kucheza Januari 11 mwakani. Bocco ameliambia Championi Jumatatu, kuwa wameona kundi ambalo wamepangwa na tayari wameanza kujiandaa kikamilifu kuhakikisha wanazifunga timu zote ambazo watacheza nazo katika Uwanja wa Taifa zikiwemo Al Ahly na JS Saoura. “Mashindano haya ni magumu na kundi tayari tumeliona, kwetu hili ni kundi zuri na tutapambana kwa ajili ya kusonga mbele katika kundi kwa kushika nafasi za juu. “Watu wamekuwa wakiona tukipoteza mara nyingi

CHANGAMOTO NYINGINE KWA SIMBA, YANGA MAPINDUZI CUP HII HAPA ZANZIBAR

Image
Patashika ya Mapinduzi Cup kuanza kutimua vumbi kesho, January 01, 2019, visiwani Zanzibar.

AZAM FC YAFICHUA KILICHOWAFANYA WAKATIBUA REKODI YAO

Image
BAADA ya Mtibwa Sugar kufanikiwa kutibua rekodi ya Azam FC kuwafanya washindwe kufunga mwaka bila kupoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi Kuu, Kocha msaidizi wa Azam FC, Juma Mwambusi amefichua siri ya kushindwa kulinda rekodi yao. Azam FC walifanikiwa kucheza michezo 16 bila kufungwa ila walipoteza mchezo wao wa 17 ambao walicheza dhidi ya Mtibwa wakiwa ugenini katika uwanja wa Manungu mkoani Morogoro kwa kufungwa mabao 2-0.  Mwambusi amesema wapinzani wao walitambua aina ya timu watakayokutana nayo kutokana na rekodi nzuri kwenye michezo ya nyuma waliyocheza hali iliyowafanya wabadili mbinu mara kwa mara uwanjani kutafuta matokeo na wakafanikiwa. "Wapinzani wetu walikuwa makini katika kumaliza makosa ambayo tuliyafanya kwa kuwa mpira ni mchezo wa makosa ila tumejipanga na tumegundua tulipokosea hivyo wachezaji tutawapa mbinu mpya kutafuta ushindi. "Tuna kazi kubwa ya kuendela kupata matokeo, kushindwa ni sehemu ya mchezo hali itakayotufanya tuzidi kuwa imara zaidi, ma

KAGERE AFUNGUKA YA MOYONI KUHUSU LIGI KUU BONGO

Image
MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere ambaye alikosekana kwenye kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United kutokana na kusumbuliwa na majeraha, amewataka mashabiki wa Simba kutokuwa na hofu juu yake. Kagere alipata majeraha hayo katika mchezo wa kimataifa waliocheza dhidi ya Nkana FC ya Zambia amesema kwa sasa anaendelea vizuri hivyo atarejea uwanjani muda wowote akipangwa. Kagere amesema ushindani ni mkubwa ndani ya Ligi na kila mmoja anatafuta matokeo hivyo wataendelea kupambana kutafuta matokeo. "Nilishindwa kuanza kucheza dhidi ya Singida United kwa kuwa bado sikuwa fiti kuanza kupambana ila kwa sasa nipo vizuri nipo tayari kwa ajili ya mapambano. "Mashabiki natambua wanahitaji ushindi ila tumefanikiwa kupata kutokana na wachezaji kucheza kwa kushirikiana, bado kazi inaendelea ili kufikia malengo yetu muhimu sapoti yao," alisema Kagere. Kutoka Championi