Posts

Showing posts from March, 2025

SIMBA SC 2-1 BIG MAN FC (KOMBE LA TFF)

Image
 

PAMBA JIJI NAYO YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB

Image
TIMU ya Pamba Jiji FC ya Mwanza imefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa FC. Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, bao pekee la Pamba Jiji limefungwa na kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Alain Mukeya dakika ya 45’+2. Pamba inakamilisha idadi ya timu nane zilizofuzu Robo Fainali za Kombe la TFF katika mwaka wa pili tu wa udhamini was CRDB — nyingine ni mabingwa watetezi, Yanga, Simba, Singida Black Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, JKT Tanzania na Kagera Sugar.

MABINGWA WATETEZI, YANGA NAO WATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB

Image
MABINGWA watetezi, Yanga wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Songea United jioni ya Leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mkenya, Duke Ooga Abuya dakika ya 22 na winga Mkongo, Jonathan Ikangalombo dakika ya 54 wote wakimalizia kazi nzuri za kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua.

KAGERA SUGAR YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB

Image
TIMU ya Kagera Sugar imefanikiwa kutinga Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa penalti 5-3 dhidi ya wenyeji, Tabora United kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Katika dakika 90 za mchezo huo, Tabora United ilitangulia kwa bao la beki wake Mkongo, Andy Bikoko dakika ya tatu, kabla ya kiungo mzawa, Joseph Mahundi kuisawazishia Kagera Sugar dakika ya 28.

SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF

Image
TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Big Man FC ya Tanga leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB, mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mzambia, Joshua Mutale dakika ya 16 na mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida kwa penalti dakika ya 31, wakati bao pekee la Big Man FC limefungwa na Joseph Henock dakika ya 45.

STAND UNITED YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB

Image
TIMU ya Stand United imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB, baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Giraffe Academy leo Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga. Mabao ya Stand United yamefungwa na Khalid Jaffary dakika ya 59, Msenda Senga dakika ya 70 na Omary Ramadhani dakika ya 84, wakati bao pekee la Giraffe Academy limefumgwa na Zelfin Malima dakika ya 73.

TAIFA STARS YACHAPWA 2-0 NA MOROCCO KIFUZU KOMBE LA DUNIA

Image
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania usiku wa kuamkia leo imechapwa mabao 2-0 na wenyeji, Morocco katika mchezo wa Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico. Mabao ya Simba wa Atlasi yaliyoizamisha Taifa Stars yamefumgwa na beki wa Real Sociedad, Nayef Aguerd dakika ya 51' na kiungo wa Real Madrid, Brahim Díaz kwa Penalti dakika ya 58 Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Oujda. Kwa matokeo hayo, Morocco inafikisha pointi 15 katika mchezo wa tano, ikiendelea kuongoza Kundi E, wakati Tanzania inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake sita ikizidiwa tu wastani wa mabao na Niger baada ya wote kucheza mechi nne. Timu nyingine kwenye Kundi hilo, Zambia inashika mkia kwa pointi zake Tatu za mechi nne pia. Timu nyingine mbili zilizopangwa katika Kundi hilo, Eritrea ilijitoa na Kongo - Brazzaville imeenguliwa baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ikiwa tayari imecheza mechi tatu na kufungwa zote.

MVUA YAVUNJA MECHI YA SINGIDA NA YANGA UWANJA MPYA

Image
MCHEZO wa kirafiki baina ya wenyeji, Singida Black Stars na Yanga ya Dar es Salaam imechezwa kwa dakika 57 tu, kabla ya kusitishwa kutokana na mvua kali iliyokuwa inanyesha Uwanja wa Airtel mjini Singida. Hadi mchezo huo unasitishwa timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, Yanga wakitangulia na bao la winga Mkongo, Jonathan Ikangalombo dakika ya 19, kabla ya kiungo Mtogo, Marouf Tchakei kuisawazishia Singida Black Stars dakika ya 55. Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa maalum kuuzindua Uwanja wa huo mpya wa Airtel uliopo eneo la Mtipa ambao utakuwa wa nyumbani wa Singida Black Stars ambayo awali ilikuwa inatumia Uwanja wa CCM LITI uliopo Singida mjini. Yanga wanaweza kurejea Dar es Salaam kesho kuendelea na maandalizi ya mchezo wao wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na benki ya CRDB dhidi ya Songea United Jumamosi Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge.

KMC YAICHAPA AZAM FC 4-2 PALE PALE CHAMAZI

Image
TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Azam FC katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Mabao ya KMC leo yamefungwa na Deusdedit Cosmas Okoyo dakika ya 19, Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 48, Redemtus Mussa dakika ya 56 na Akram Muhina Omar dakika ya 82, wakati ya Azam FC yamefungwa na Zidane Sereri dakika ya 13 na Tepsi Evans dakika ya 89.

RAYVANNY AZINDUA KULA SHAVU YA PIGABET

Image
MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya, Raymond Shaban Mwakyusa maarufu Rayvanny ametangazwa kuwa balozi wa kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Pigabet. Mkurugenzi mkuu wa Pigabet,  Panayiotis Giannakopoulos amesema wameingia mkataba wa Rayvanny kutokana na kuvutiwa na kazi zake mbalimbali za muziki na kuwa na chapa kubwa katika fani hiyo. Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Kula Shavu uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam, Giannakopoulos amesema mwanamuziki huyo atakuwa balozi wa kampeni hiyo ambayo inakwenda kutoa fursa kwa wananchi kuibuka na ushindi kila siku. Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Pigabet,  Panayiotis Giannakopoulos  (kushoto) akimkabidhi jezi balozi wao mpya, mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Raymond Shaban Mwakyusa maarufu kwa jina la Rayvanny wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni ya “Kula Shavu” uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. “Mkataba wetu na Rayvanny ni wa muda mrefu, ambao  umezingatia vigezo, ...

SIMBA QUEENS 0-1 YANGA PRINCESS (LIGI KUU YA WANAWAKE TZ BARA)

Image
 

YANGA PRINCESS YAICHAPA SIMBA QUEENS 1-0 MWENGE

Image
TIMU ya Yanga Princess imeibuka na ushindi wa bao 1-0 na watani wao, Simba Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Jeannine Mukandayisenga dakika ya 49 akimchambua kipa wa Kimataifa wa Kenya,  Winfrida Seda Ouko. Kwa ushindi huo, Yanga Princess inafikisha pointi 27, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi saba na vinara, Simba Queens ambao pia ni mabingwa watetezi baada ya wote kucheza mechi 12. JKT Queens ipo katikati yao, Simba Queens na Yanga Princess ikiwa na pointi 32 katika nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 12 — na kesho inacheza na Mashujaa Queens Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. 

SASA NI SAJENTI IBRAHIM ABDALLAH HAMAD, BACCA APANDISHWA CHEO KMKM

Image
BEKI wa Yanga, Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ amepandishwa cheo kazini kwake, Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM), kutoka Koplo na kuwa Sajenti. Hatua hiyo ya KMKM kumpandisha cheo Bacca ni taratibu za kawaida kulingana na muda na ufanisi wake kazini — huku akiendelea kufanya vyema kisoka katika klabu yake na timu ya taifa, Taifa Stars.

SERENGETI GIRLS YATOLEWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KWA VIPIGO ‘DABO’

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2025 baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Zambia ‘Copper Princesses jioni ya leo Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola. Bao la Copper Princesses leo limefungwa na Natasha Nkaka dakika ya 53, hivyo wanasonga mbele Raundi ya Tatu na ya mwisho ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ushindi wa jumla 4-0 na watakutana na mshindi wa jumla kati ya Benin na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Ikumbukwe mechi ya kwanza Serengeti Girls ilifungwa 3-0 na Zambia Jumapili iliyopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam — mabao ya Copper Princesses yakifungwa na Grace Phiri dakika ya 64 na Mercy Chipasula mawili, dakika ya 80 na 89  kwa penalti. Mwaka jana Serengeti Girs ilitolewa na pia na Copper Princesses katika hatua kama hii ya kufuzu Kombe la Dunia kwa...

SIMBA SC 6-0 DODOMA JIJI FC (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)

Image
 

KIBU NA AHOUA KILA MMOJA AFUNGA MAWILI, SIMBA YAITANDIKA DODOMA JIJI 6-0 MWENGE

Image
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo a Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mkongo, Elie Mpanzu Kibisawala dakika ya 16, kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua mawili, dakika ya 21 na 45’+1, mshambuliaji Mganda, Steven  Dese Mukwala dakika ya 46 na kiungo Mtanzania mwenye asili ya Kongo, Kibu Dennis Prosper mawili pia, dakika ya 54 na 69. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 57, ingawa  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 57, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 22, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 27 za mechi 23 sasa nafasi ya nane. 

TAIFA STARS KUIVAA MOROCCO BILA SAMATTA NI MAJERUHI

Image
KOCHA Hemed Suleiman ‘Morocco’ amemrejesha kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars mshambuliaji Kelvin Pius John wa Aalborg BK ya Denmark kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji Morocco Machi 25 Uwanja wa Honor mjini Oujda. Kuelekea mchezo huo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico — Kocha Morocco hajamjumuisha Nahodha, Mbwana Ally Samatta wa PAOK ya Ugiriki kwa sababu ni majeruhi. Lakini pia hajawaita makipa wazoefu Aishi Salum Manula wa Simba SC na Metacha Boniphace Mnata wa Singida Black Stars ambao wamepoteza nafasi kwenye klabu zao. Badala yake amewateua Yakoub Suleiman wa JKT Tanzania, Hussein Masaranga wa Singida Black Stars na Ally Salim wa Simba SC, huku pia  akiendelea kumfumbia macho beki na Nahodha wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto. Hajamuita pia mfungaji wa bao la Taifa Stars kwenye ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Zambia, Waziri Junior Shentembo anayechezea Al-Minaa ya Iraq kwa sasa. Katika mechi zake tat...

JKT TANZANIA, SINGIDA NA MBEYA KWANZA ZATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB

Image
TIMU ya JKT Tanzania imefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya Kwanza jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Beki Ibrahim Ngecha alijifunga dakika ya 10 tu kuipatia bao la kuongoza JKT Tanzania, kabla ya mshambuliaji Edward Songo kufunga mawili dakika ya 14 na 17 kuhitimisha shangwe za mabao za timu ya Jeshi la Kujenga Taifa. Nayo Singida Black Stars imetinga Robo Fainali pia baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara. Mechi nyingine ya 16 Bora Kombe la CRDB leo Mbeya City imeitupa nje Mtibwa Sugar kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

YANGA SC 3-1 COASTAL UNION (KOMBE LA TFF)

Image
 

SIMBA SC 3-0 TMA STARS (KOMBE LA TFF)

Image
 

MAXI APIGA MBILI YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 3-1 KOMBE LA CRDB

Image
MABINGWA watetezi, Yanga  wamefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli, mawili dakika ya pili na 15, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Clement Francis Mzize kufunga la tatu dakika ya 21, wakati bao pekee la Coastal Union limefungwa na Miraj Abdallah dakika ya 18. Yanga sasa itakutana na Songea United iliyotoa Polisi Tanzania kwa kuichapa bao 1-0 Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

PRINCE DUBE MCHEZAJI BORA LIGI KUU FEBRUARI, HAMDI KOCHA BORA

Image
KLABU ya Yanga imeshinda Tuzo za Kocha Bora na Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Februari mwaka huu. Mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo amewashinda mchezaji mwenzake wa Yanga, kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki na mshambuliaji wa Kengold, Suleiman Salim Rashid 'Bwenzi' kutwaa Tuzo hiyo. Kwa upande wake Kocha Mualgeria wa Yanga, Miloud Hamdi amewashinda Muafrika Kusini, Fadlu Davids wa Simba na mzawa, Freddy Felix Minziro wa Pamba Jiji.

SIMBA SC YAWAPIGA TMA STARS 3-0 NA KUTINGA 16 BORA KOMBE LA CRDB

Image
TIMU ya Simba imefanikiwa kuingia Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TMA Stars ya Arusha leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC katika mchezo huo wa mkondo mmoja wa Hatua ya 32 Bora Kombe la CRDB yamefungwa na beki Mburkinabe, Valentin Nouma dakika ya 17, mshambuliaji Sixtus Robert Sabilo aliyejifunga dakika ya 19 na mshambuliaji Mcameroon, Christian Leonel Ateba Mbida dakika ya 76. Simba SC sasa itakutana na Big Man FC ya Tanga iliyoitoa Tanzania Prisons kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Ikumbukwe jana Fountain Gate iliingia kwenye orodha ya timu za Ligi Kuu zilitupwa nje na timu za madaraja ya chini katika hatua hii baada ya kutolewa na Stand United kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara....

SERENGETI GIRLS YATANDIKWA 3-0 NA ZAMBIA KIFUZU KOMBE LA DUNIA U17

Image
KIKOSI cha timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imefungwa mabao 3-0 na Zambia katika mchezo wa kwanza Raundui ya Pili kufuzu Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Zambia jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.   Mabao ya Zambia ‘Copper Princesses’ yamefungwa na Grace Phiri dakika ya 64 na Mercy Chipasula mawili, dakika ya 80 na 89  kwa penalti. Timu hizo zitarudiana Machi 15 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Benin na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika raundi ya Tatu na ya mwisho ya kuwania tiketi ya Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 hadi Novemba 8, mwaka huu. Mwaka jana Serengeti Girs ilitolewa na pia na Copper Princesses katika hatua kama hii ya kufuzu Kombe la Dunia kwa kuchapwa 5-0 Lusaka Februari 3, kabla ya kushinda 1-0 Dar es Salaam hapo hapo Chamazi Februari 11. Ikumbukwe Serengeti Girls ni timu pekee ya soka ...

MECHI YA SIMBA NA YANGA YAAHIRISHWA RASMI KUPISHA UCHUNGUZI

Image
MCHEZO wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Yanga na Simba uliopangwa kufanyika leo kuanzia Saa 1:15 usiku umeahirishwa rasmi hadi hapo utakapopangiwa tarehe nyingine.

SIMBA SC YATISHIA KUTOINGIZA TIMU KWA MKAPA LEO DHIDI YA YANGA

Image
KLABU ya Simba imetishia kutocheza mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Yanga leo baada ya usiku wa jana kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kwa mujibu wa kanuni.

DODOMA JIJI NA COASTAL UNION HAKUNA MBABE, ZATOKA SULUHU JAMHURI

Image
TIMU za Dodoma Jiji na Coastal Union ya Tanga zimegawana pointi baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 22, ikiendelea kukamata nafasi ya nane kwa kuizidi pointi mbili Coastal Union ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.

KAGERA SUGAR YAICHAPA PAMBA JIJI 2-1 KAITABA

Image
WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na kiungo Mkenya,  Shaphan Oyugi Siwa dakika ya 42 na mshambuliaji Mganda, Peter Lwasa dakika ya 63, wakati bao pekee la Pamba Jiji limefungwa na mshambuliaji Mkenya, Mathew Tegisi Momanyi dakika ya 17. Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 14, ikizidiwa pointi tatu na Pamba iliyopo nafasi ya 13 katika ligi ya timu 16. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

JKT TANZANIA YAWAPIGA TABORA UNITED 2-1 PALE PALE MWINYI

Image
TIMU ya JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mabao ya JKT Tanzania yamefungwa na viungo Ally Hussein Msengi dakika ya 32 na Najim Magulu dakika ya 75, wakati la Tabora United limefungwa na winga Offen Francis Chikola dakika ya 64. Kwa ushindi huo, JKT Tanzania inafikisha pointi 30 na kurejea nafasi ya sita, ikizidiwa pointi saba na Tabora United wanaobaki nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 23.

MSINDO APIGA MBILI AZAM FC YAICHARAZA PRISONS 4-0 CHAMAZI

Image
WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao yote ya Azam FC leo yamefungwa na wazawa, kiungo mshambuliaji Nassor Saadun Hamoud dakika ya tano na mabeki, Pascal Gaudence Msindo, mawili dakika ya 45’+2 na 57 na Lusajo Elukaga Mwaikenda dakika ya 68. Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 48, ingawa inabaki nafasi ya tatu na Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 18, nayo inabaki nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 23. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

SINGIDA BLACK STARS YAICHAPA NAMUNGO 1-0 PALE PALE RUANGWA

Image
BAO pekee la mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah dakika ya 79 limeipa Singida Black Stars ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Kwa ushindi huo, Singida Black Stars inafikisha pointi 44, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 23, nayo inabaki nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 23 sasa. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili nyingine zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu, wakati timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Championship kujaribu tena kubaki Ligi Kuu.

MOKONO APIGA ZOTE MBILI FOUNTAIN GATE YAICHAPA KMC 2-1 MWENGE

Image
TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na kiungo Mrundi mzaliwa wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Elie Mokono dakika ya 77 na 90’+4, wakati la KMC limefungwa na Oscar Paul kwa penalti dakika ya 45. Kwa ushindi huo, Fountain Gate wanafikisha pointi 28 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya sita, wakati KMC wanabaki na pointi zao 24 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 23.

PROFESA PHILEMON MIKOL SARUNGI HATUNAYE, AFARIKI DUNIA LEO DAR

Image
ALIYEWAHI kuwa Daktari wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, baadaye Waziri wa Michezo, Profesa Philemon Mikol Sarungi (89) amefariki dunia leo Jijini Dar es Salaam. Sarungi alikuwa Daktati wa timu za taifa kuanzia miaka ya 1970 hadi 1980 mwanzoni, kabla ya kugeukia siasa na kuwa Mbunge wa jimbo la Rorya na kuteuliwa Waziri wa Michezo. Sarungi ni mpenzi na mwanachama wa klabu ya Simba SC. Mungu ampumzishe kwa amani. 

NI AHMED ARAJIGA PILATO WA PAMBANO LA WATANI JUMAMOSI

Image
REFA Ahmed Arajiga ndiye atakayepuliza kipyenga kwenye mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Yanga na Simba Jumamosi wiki hii Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Arajiga, Refa Bora wa nchi katika mchezo atasaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga na Kassim Mpanga wa Dar es Salaam watakaokuwa wakikimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja, wakati mezani atakuwepo Amina Kyando wa Morogoro.

JKT TANZANIA, TABORA UNITED NA MTIBWA SUGAR ZATINGA 16 BORA KOMBE LA CRDB

Image
WENYEJI, JKT Tanzania jana walifanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United ya Mara Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam. Mabao ya JKT Tanzania yalifungwa na Shiza Kichuya dakika ya 19 na Najim Magulu dakika ya 47, wakati bao pekee la Biashara United lilifungwa na Freddy Kiwale dakika ya 82. Nayo Tabora United ikaitupa nje Transit Camp kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Mtibwa Sugar wakaitupa nje Town Stars kwa kuichapa mabao 5-3 Uwanja w Manungu Complex, Morogoro. Mechi nyingine za Hatua ya 32 Bora jana Mbeya Kwanza iliichapa Mambali Ushirikiano mabao 3-0 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Nao Songea United wakapata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, wakati Giraffe Acade...

AZAM FC, TANZANIA PRISONS ZATOLEWA NA TIMU ZA CHAMPIONSHIP KOMBE LA CRDB

Image
TIMU ya Azam FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na benki ya CRDB baada ya kufungwa na Mbeya City kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. Katika mchezo huo wa Hatua ya 32 Bora — Mbeya walianza kupata bao kupitia bao kupitia kwa Daniel William dakika ya 64, kabla ya kiungo Yahya Zaid kuisawazishia Azam FC dakika ya 90’+5. Kwenye mikwaju ya penalti waliofunga kwa upande Mbeya City ni Adili Buha, Baraka Philemon, David Mwasa na Riffat Msuya, wakati Kilaza Mazoea alikosa. Kwa upande wa Azam FC ni beki Lusajo Mwaikenda na kiungo Mghana, James Akaminko pekee waliofunga, huku winga Mgambia, Gibril Sillah na beki Nathaniel Chilambo wakikosa. Mechi nyingine za 32 Bora leo, Singida Black Stars wameitupa nje Leo Tena kwa kuichapa 4-0 Uwanja wa CCM LITI mjini Singida, KMC wameichapa Cosmopolitan 2-0 Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam na Big Man FC wameitoa Tanzania Prisons kwa penalti 3-2 baada ya sare...

COASTAL UNION 0-3 SIMBA SC (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)

Image
 

MUKWALA APIGA HAT TRICK SIMBA YAICHAPA COASTAL UNION 3-0 ARUSHA

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Imekuwa siku nzuri kwa mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala aliyefunga mabao yote matatu ya Wekundu wa Msimbazi leo, dakika za 30, 45’+2 na 56. Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi. Kwa upande wao Coastal Union baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao 24 za mechi 22 sasa nafasi ya tisa katika ligi ya timu 16.