Posts

Showing posts from September, 2019

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA HAMZA MANENO

Image

MAHOJIANO MAALUM BIN ZUBEIRY NA PETER NKWERA

Image

MECHI YA YANGA SC NA POLISI LIGI KUU YASOGEZWA MBELE KWA SIKU MOJA HADI ALHAMISI DAR

Image
Na Saada Salim, DAR ES SALAAM MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Yanga SC na Polisi Tanzania umesogezwa mbele kwa siku moja hadi Alhamisi na utachezwa Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam. Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura Mgoyo amesema hatua imefuatia ombi la Yanga wamerejea jana mjini Dar es Salaam kutoka Zambia walipokwenda kucheza na wenyeji, Zesco Unted. Wambura amesema walipokea barua ya Yanga Septembaa 27 wakiomba mechi isogezwe mbele ili kuwapa fursa wachezaji wao waondoe uchovu wa safari ya Zamba ambako walifungwa 2-1 na Zesco United Jumamosi mjini Ndola na kukosa nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Aidha, Wambura amesema mchezo mwingine pia dhidi ya Coastal Union uliokuwa uchezwe Oktoba 5 na umesogezwa mbeke kwa siku moja kwa sababu Uwanja wa Uhuru utakuwa na matumizi mengine ya kijamii siku hiyo. Lakini Wambura amewaambia Yanga SC kwamba ahueni hiyo ni ya mwisho

TIMU TISA ZILIZOWAHI KUTWAA TAJI ZAFUZU HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

Image
WANAUME wametenganishwa na wavulana, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya kukamilika kwa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki. Na sasa upangaji wa makundi manne ya timu nne kila moja kwa ajili ya hatua hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 16 utafuatia Jumatano ya Oktoba 9 mjini Cairo, Misri. Miongoni mwa timu zilizofuzu hatua hyo ni pamoja tisa zilizowahi kubeba taji hilo kubwa la klabu Afrika angalau mara moja, wakiwemo mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia.  ‘Damu na Dhahabu’ wamefuzu baada ya kuitoa Elect Sport ya Chad, wakitoka nyuma kwa mabao 2-1 na kushinda 3-2 jumla na kupata tiketi ya kucheza kwa mara ya nne mfululizo hatua ya makundi. Wanaungana na ndugu zao, Etoile du Sahel, ambao licha ya kumaliza na wachezaji 10 walipindua kipigo cha 2-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana kwa kushinda 3-0 mjini Monastir na kufuzu. Mabingwa wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns, washindi wa mwaka 2016 walipata ushi

MALINDI YAUNGANA NA AZAM, SIMBA, KMC NA KMKM KUAGA MAPEMA MICHUANO YA AFRIKA

Image
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya Malindi SC imeungana na KMKM, zote za Zanzibar na KMC, Azam FC na Simba SC kuaga mapema michuano ya Afrika msimu kufuata jana kuchapwa 3-1 na wenyeji, Al Masry kwenye mchezo wa marudano Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrka Uwanja wa Borg El-Arab mjini Alexandria, Misri. Matokeo hayo yanamaanisha Malindi inatupwa nje kwa jumla ya mabao ya 7-2, kufuata kufungwa 4-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita. Katika mchezo wa jana ambao kocha Ehab Galal aliwapumzisha wachezaji wake muhimu kufuata ushind mnono kwenye mechi ya kwanza, mabao ya Al Masry yalifungwa na Ahmed Yasser dakika ya nne na 55 na Austin Amutu dakika ya 60, wakati la Malindi lilifungwa na Ibrahim Ali dakika ya 10. KMC ilitolewa na AS Kigali ya Rwanda Raundi ya kwanza, Azam FC imetolewa na Triangle United ya Zimbabwe Raundi ya Pili, Kombe la Shirikisho pia, KMKM ilitolewa na Primiero de Agosto ya Angola na Simba SC ili

BIASHARA UNITED 0-2 SIMBA SC (LIGI KUU TANZANIA BARA)

Image

TANZANIA BARA YAIPIGA UGANDA 4-2, KUIVAA TENA KENYA NUSU FAINALI CECAFA U20

Image
Na Mwandishi Wetu, GULU TIMU ya Tanzania Bara imefanikiwa kuingia Nusu Fanali ya michuano ya Kombe la Matafa ya Afrika Masharki na Kati (CECAFA Challenge U20) baada ya ushind wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Uganda jioni Uwanja wa Kumbukumbu wa Gulu. Mabao ya Tanzania Bara leo yamefungwa na washambuliaji wake hodari, Andrew Albert Simchimba dakika za 25 na 62 na Kelvin Pius John ‘Mbappe’ dakika za 89 na 90 na ushe, wakati ya Uganda yamefungwa na Aziz Kayondo dakika ya 46 na 76.  Robo Fainali nyingine Sudan imefunga 1-0 Sudan Kusini Uwanja wa Gulu pia, Kenya imefunga Burundi 2-1 na Eritrea imeiadhibu 5-0 Zanzibar Uwanja wa Njeru. Sasa Tanzania Bara itamenyana na Kenya katika Nusu Fainali Jumanne yakiwa ni marudio ya mchezo wa Kundi B ulioisha kwa sare ya 2-2 na Ertrea itamenyana na Sudan, wakati Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itapigwa Oktoba 5.

ZESCO UNITED 2-1 YANGA SC (LIGI YA MABINGWA AFRIKA)

Image

KAGERE AENDELEZA MOTO WA MABAO SIMBA SC YAICHAPA BIASHARA UNITED 2-0 MUSOMA

Image
Na Mwandishi Wetu, MUSOMA MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyej, Biashara United 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara. Ushindi huo uliotokana na mabao ya washambuliaji wake hatari, Mnyarwanda Meddie Kagere na mzawa, Miraj Athumani ‘Madenge’ unaifanya Simba SC inayofundishwa na Mbelgiji, Patrick Aussems ifikishe pointi 12 baada ya kushinda mechi zake zote nne za mwanzo, mbili ugenini. Kagere aliye katika msimu wake wa pili Msimbazi tangu awasili kutoka Gor Mahia ya Kenya alifunga bao lake la kwanza dakika ya 22 akimalizia kwa shuri la chini kros ya Miraji Madenge kutoka upande wa kulia. Miraj Athumani anayefahamika pia kama Shevchenko ambaye amerejeshwa Msimbaz msimu huu baada ya kuachwa miaka minne iliyopita alifunga bao lake dakika ya 53 kwa kchwa akimalizia mpira wa adhabu wa Ibrahim Ajibu. Kikosi cha Biashara United kilikuwa; Daniel Mgoke, Innocent Edwin, Victor Hangaya/Lambak

SAID ALMASI ENZI ZAKE AKIWA NA HAMOUD NA LWIZA KIRUMBA

Image
REFA Said Almasi (katikati) akiwa na waamuzi wenzake, Alfred Lwiza (kulia), wote wa Mwanza na Nassor Hamdoun (kushoto) wa Kigoma Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza mwanzoni mwa miaka ya 1990 kabla ya moja ya mechi alizowahi kuchezesha enzi za uhai wake. Almasi alfariki dunia nyumbani kwake Jumanne wiki hii na kuzikwa Nyamanoro mjni Mwanza.

LUIS SUAREZ AFUNGA BARCELONA YAICHAPA GETAFE 2-0 LA LIGA

Image
Luis Suarez akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la kwanza dakika ya 41 kabla ya Junior Firpo kufunga la pli dakika ya 49 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Getafe kwenye mchezo wa La Liga usiku huu Uwanja wa Coliseum Alfonso Perez   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MAHREZ, JESUS NA STERLING WAFUNGA MAN CTY YAIPIGA EVERTON 3-1

Image
Riyad Mahrez akishanglia baada ya kuifungia Manchester City bao la pili dakika ya 71 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Goodison Park. Mabao mengine ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Gabriel Jesus dakika ya 24 na Raheem Sterling dakika ya 84, wakati la Everton limefungwa na Dominic Calvert-Lewin dakika ya 33.   PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

SAMATTA APAMBANA HADI MWISHO KRC GENK YAPOKONYWA USHINDI MWISHONI UBELGIJI

Image
Na Mwandishi Wetu, TRUIDEN  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku huu amecheza kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikitoa sare ya 3-3 na Sint-Truiden katika mchezo wa ugenini wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji usiku Uwanja wa Stayen. KRC Genk ilikaribia kuondoka na ushindi mnono baada ya kuongoza kwa 3-0 hadi baada ya saa moja kwa mabao ya mshambuliaji mpya chipukizi, Mbelgiji Theo Bongonda Mbul'Ofeko Batombo dakika ya 15 akimalizia pasi ya kiungo Mromania mzaliwa wa Uturuki, Ianis Hagi aliyefunga mabao mengine mawli yote kwa penalti dakika za 48 na 60. Lakini Sint-Truiden wakazinduka na kusawazisha mabao yote nusu saa ya mwisho, mshambuliaji Muivory Coast mzaliwa wa Ufaransa, Yohan Boli akifunga mawli dakika ya 63 na 87 na lingine beki Mspaniola Pol Garcia dakika ya 80. Matokeo hayo yanawaacha Genk, mabingwa watetezi nafasi ya sita wakiwa na ponti 14 baada ya kucheza mechi tisa, wakizidiwa pointi sita na vinara, Club Brugge wenye pointi 20 za m

RONALDO AFUNGA LA PLI JUVENTUS YAICHAPA SPAL 2-0 SERIE A

Image
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Juventus bao la pili dakika ya 78 ikiilaza SPAL 2-0 kufuatia Miralem Pjanic kufunga la kwanza dakika ya 45 katika mchezo wa Serie A leo Uwanja wa Allianz mjini Torino   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

CHELSEA YANG'ARA DARAJANI, YAICHAPA BRIGHTON & HOVE ALBION 2-0

Image
Willian akishangilia kishujaa baada ya kuifungia Chelsea bao la pili dakika ya 76 kufuatia Jorginho kufunga la kwanza kwa penalti dakika ya 50 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo huo ukiwa ni ushindi wa kwanza kwa kocha Frank Lampard Uwanja wa Stamford Bridge kwenye ligi hiyo   PICHA ZADI GONGA HAPA

LIVERPOOL YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI ENGLAND, YAIPIGA 1-0 SHEFFIELD

Image
Kiungo Mholanzi, Georginio Wijnaldum akishangilia na mchezaji mwenzake, Mbrazil Roberto Firmino baada ya kuifungia Liverpool bao pekee dakika ya 79 ikiwalaza wenyeji, Sheffield United 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Bramall Lane huo ukiwa ushindi wa saba mfululizo tangu msimu uanze   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

ALLIANCE FC YAZINDUKA NA KUWACHAPA SINGIDA UNITED 1-0 NAMFUA, RUVU NAYO YANG’ARA

Image
Na Mwandishi Wetuk SINGIDA TIMU ya Alliance FC imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Singida United jioni ya leo Uwanja wa Namfua mjini Singida. Bao hilo pekee limefungwa na Sameer Vincent dakika ya 16 na kwa ushindi huo wa kwanza wa msimu katika mechi ya mechi nne, Alliance FC inafikisha pointi tano kufuatia sare mbili awali na kufungwa mchezo mmoja. Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania bao pekee la Yassin Salum aliyejifunga dakika ya tano Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Nayo Mwadui FC imelazimishwa sare ya 1-1 na jirani zao, Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga. Gerald Mathias alianza kuifungia Mwadui FC dakika ya 58 kabla Chilo Mkama kuisawazishia Mbao FC dakika ya 90. Ligi Kuu ya Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi tano kupigwa kwenye viwanja tofauti, ikiwemo mabingwa watetezi, Simba SC kuwa wageni wa Biashara United Uwanja wa Ka

TRIANGLE UNITED YAIGONGA 1-0 TENA AZAM FC NA KUITUPA NJE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Image
Kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya Abbas akimlamba chenga mchezaji wa Triangle United jioni ya leo Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo, Zimbabwe katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika.  Triangle United imeshinda 1-0 na kusonga mbele kwa ushindi wa 2-0 baada ya kushinda 1-0 pia ugenini wiki mbili zilizopita mjini Dar es Salaam

ZESCO UNITED YAIHAMISHIA YANGA SC KOMBE LA SHIRIKISHO BAADA YA KUICHAPA 2-1 LEO NDOLA

Image
Na Mwandishi Wetu, NDOLA BAO la kujifunga la kiungo Mzanzibari, Abdulaziz Makame dakika za mwishoni limeiondoa Yanga SC kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa 2-1 na wenyeji, Zesco United jioni ya leo Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia. Kwa matokeo hayo, Yanga inatolewa kwa jumla ya mabao 3-2, kufuatia sare ya 1-1 baina ya timu hizo kwenye mchezo wa kwanza Septemba 14 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Zesco United inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Mzambia George Lwandamina inaingia hatua ya makundi inayoshirikisha timu 16, wakati timu ya Tanzania itamenyana na moja ya timu zilizovuka Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo mingine ya CAF.  Mshambuliaji Mnamibia, Sadney Urikhob ameifungia Yanga leo ikichapowa 2-1 na Zesco mjini Ndola Makame, mchezaji aliyeibukia kikosi cha vijana cha mahasimu, Simba B kabla ya kwenda kujiendeleza zaidi kisoka kwao, Zanzibar alijifunga dakika ya 79 alipoja

SIMBA SC WALIVYOJIFUA JANA MWANZA KUJIANDA NA MECHI DHIDI YA BIASHARA UNITED KESHO MUSOMA

Image
Mshambuliaji Mbrazil wa Simba SC, Wilker Da Silva akijifua na wenzake jana Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Biashara United mjini Musoma mkoani Mara Beki wa Simba SC, Kennedy Wilson akijifua na wenzake jana Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kujiandaa kuwavaa Biashara United kesho Uwanja wa Karume mjini Musoma  Kiungo Mkenya wa Simba SC, Francis Kahata akijifua na wenzake jana Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza     Beki wa Simba SC, Ramadhani Haruna Shamte akijifua na wenzake jana CCM Kirumba  Wachezaji wa Simba SC, Kennedy Wilson wakiwa mazoezini jana Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza    Wachezaji wa Simba SC wakijifua jana CCM Kirumba tayari kuwavaa Biashara United kesho mjini Musoma 

BOSI WA AZAM TV, TIDO MHANDO ALIVYOWAKABIDHI VYETI WAANDISHI WALIOPIGWA MSASA NA TFF

Image
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited, Dunstan Tido Mhando (wa kushoto), akimkabidhi cheti cha uhitimu mafunzo maalum ya wiki moja ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwandishi wa habari Ramadhani Mwelendo jana hoteli ya Serene mjini Dar es Salaam. Wengine kulia ni Rais wa TFF,. Wallace Karia na Katibu wake, Wilfred Kidau. CEO wa Azam Media, Tido Mhando akimkabidhi cheti, mwandishi wa habari, Charles Abel  CEO wa Azam Media, Tido Mhando akimkabidhi cheti, mwandishi wa habari jana hoteli ya Serene   CEO wa Azam Media, Tido Mhando akimkabidhi cheti, mhitimu wa mafundisho hayo jana Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu pamoja na vigogo wa TFF

YANGA SC WAKIJIFUA KUPINDUA MEZA LEO DHIDI YA ZESCO UNITED NDOLA

Image
Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini mjini Ndola jana asubuhi kuelekea mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Zesco United leo jioni Uwanja wa Levy Mwanawasa. Yanga inatakiwa kushinda ugenini leo baada ya sare ya 1-1 nyumbani wiki mbili zilizopita 

MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUWAVAA TRIANGLE UNITED LEO BULAWAYO

Image
Mshambuliaji Mzambia wa Azam FC, Obrey Chirwa akijifua Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo jana kuelekea mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Triangle United. Azam FC inatakiwa kushindia kuanzia 2-0 ili isonge mbele, baada ya kufungwa 1-0 Azam Complex Septemba 15. Mshambuliaji Richard Ella D'jodi kutoka Ivory Coast akijifua Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo jana  Kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' mazoezini jana Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo   Beki Mghana, Yakubu Mohamed akipiga shuti katika mazoezi ya penalti jana Bulawayo   Beki Mganda, Nicolas Wadada mazoezini jana mjini Bulawayo tayari kwa mchezo dhidi ya Triangle leo   Mshambuliaji Shaaban Iddi 'Chilunda' akipiga penalti mazoezini jana  Beki Mzimbabwe, Bruce Kangwa akiwa mazozini jana mjini Bulawayo  Mshambuliaji Iddi Suleiman 'Nado' akijifua jana Uwanja wa Barbourfields mjini Bulawayo   Kipa Mghana, Razack Abalora akiokoa