Posts

Showing posts from October, 2024

TANZANIA PRISONS YAICHAPA FOUNTAIN GATE 3-2 SOKOINE

Image
TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Nurdin Chona kwa penalti dakika ya 25, Ezekia Mwashilindi dakika ya 48 na Vedastus Mwihambi dakika ya 50, wakati ya Fountain Gate yamefungwa na Suleiman Mwalimu dakika ya 12 na Kassim Suleiman dakika ya 37. Kwa ushindi huo wa kwanza wa msimu, Tanzania Prisons inafikisha pointi saba katika mchezo wa sita, wakati Fountain Gate inabaki na pointi zake 13 za mechi saba sasa.

SAMATTA AREJESHWA TAIFA STARS KWA AJILI YA MECHI DRC KUFUZU AFCON

Image
KAIMU Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco amefanikiwa kumrejesha kikosini Nahodha Mbwana Ally Samatta ambaye alidhamiriwa kustaafu. Morocco amemjumuisha kwenye kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 nchini Morocco. Taifa Stars watakuwa wageni wa DRC Alhamisi ya Oktoba 10 Uwanja wa Martyrs de la PentecĂ´te Jijini Kinshasa, kabla ya timu hizo kurudiana siku tano baadaye, Oktoba 15 Uwanja Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mara ya mwisho Samatta aliichezea Taifa Stars Januari 24, mwaka huu kwenye mechi ya Kundi F Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 dhidi ya DRC Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo timu hizo zikitoka suluhu, 0-0 ambayo Samatta alimpisha Kokola Charles William M'Mombwa dakika ya 86. Makipa; Ally Salim (Simba), Zuberi Foba (Azam FC), Yona Amos (Pamba), Mohamed Hussein (Pamba FC). Mabeki; Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Pascla Msindo (Azam FC), Mohamed Hussein (Simb